Ikulu yamtaka Askofu Kakobe aache porojo!

Ikulu yamtaka Askofu Kakobe aache porojo!

All this because of allowance of 300,000 wampe yaishe aaakh

Kakobe hapiganii posho ya Sh 300,000 ingekuwa hekima na akili iliyo bora kwa waliopewa onyo hilo kuomba Mungu aepushe hayo kuliko kuingia kwenye malumbano na Kakobe, hata mlevi(simfananishi Kakobe na mlevi) akikukuta njiani akukuambia kesho muda kama huu nyumba yako itavunjwa na wezi utamtukana na kusema hizo ni porojo wakati hiyo kesho haijafika au utachukua tahadhari na kujilinda ili kuzuia lisitokee!?, Hekima inanifundisha hivyo
 
Kakobe Ana hekalu wapi?
Aliwai sema mtu yeyote anayeijua nyumba yake zaidi ya Ile kijitonyama.Aseme.
Mty yeyote anayejua ac ktk benk yeyote duniani kwa jina lake Au Mke wake Au watoto wake aseme.
Kakobe siyo kama wahuni mliowazoea.
We subiri yatakapoanza kutimia Yale aliyoyanena

mwizi tu hakuna lolote
 
ili neno la jah litimie ilitegemewa ikulu adharau na kudhihaki waraka wa kakobe.

sellasie majesty, a king of da king all over da world!

Jah ill show dem why second freedom struggle is coming soon through chadem's party.
The party which's under jah's power!

'can we do this'
"chadema's social networks movement" (chasonemo).
 
Siku zote mpuuzi ni mtu wa kupuuzwa tu.

Naipongeza Ikulu kwa kusikia maombi yetu Watanzania ya kupuuzwa kwa Kakobe.

Kwa sasa Ikulu ina simamia mambo ya maendeleo ya umma, leo mpuuzi mmoja (Kakobe) anataka asumbue serikali?

Aende zake huko na ndoto zake za vitisho. Mungu wa Abrahamu ni mwenye huruma kwa wanaadamu.

Hayupo kutufanyia visasi, bali kutulea watu wake. I doubt kama Kakobe ana Mungu wa Abrahamu.
 
Njaa za maaskofu ndio zinazowaponza. Posho inamtoa roho kakobe na wachungaji wenzake. Kazoea kutapeli waumini wake kanisani mpaka kajenga na mahekalu sasa mradi umeota mbawa na unazidi kudorora anaona atunge njia nyingine itayompatia pesa. Huyu askofu ni mganga njaa sana hata hivyo na abuni mradi mwingine kuliko utapeli wake anaotaka ufike mpaka serikalini.

can you prove it? Hebu walete waumini wake hapa kama uthibitisho kwamba anawatapeli waumini wake ili nikuamini vinginevyo ni ule 'udini' wako wa siku zote unakusumbua kwa kusema "...njaa za maaskofu ndio zinawaponza...", acha udini
 
2.jpg


kurugenzi ya mawasiliano ikulu imesema haina muda wa kujibu porojo zilizotolewa na askofu wa kanisa la full gospel fellowship, zachary kakobe kwani ina kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania.

imesisitiza kuwa ofisi ya kurugenzi ya mawasiliano ikulu haifanyi kazi za porojo kama sehemu ya kuendesha utawala wake, badala yake iko makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa kulinda na kuheshimu demokrasia na kufuata katiba ya nchi.

kauli hiyo inatokana na waraka maalumu unaodaiwa kutolewa na askofu kakobe na kisha kupelekwa ikulu.hata hivyo, kurugenzi ya mawasiliano ikulu imesema haijathibitisha rasmi kama waraka huo umefika katika ofisi hiyo.

Akizungumza juzi na gazeti la jambo leo kwa njia ya simu,mkurugenzi wa idara ya mawasiliano ikulu, salvatory rweyemamu alisema serikali si lazima ijibu porojo zilizotolewa na kakobe, kwani ikulu ni sehemu nyeti ya kutumikia wananchi katika maswala ya msingi na yenye tija kwa taifa.

yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",

alisema na kuongeza kuwa swala hilo lilishajibiwa na kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, dr florence turuku ambapo alilitolea ufafanuzi wa kutosha.

Waraka huo uliotolewa kwenye vyombo vya habari na askofu kakobe ulikuwa ukieleza namna ikulu "ilivyotupa kapuni" majina yote ya wapentekoste waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, hivyo kuwafanya wapentekoste takribani milioni 10 kukosa mwakilishi hata mmoja.

Pia waraka huo ulidai kuwa baada ya kukosa uwakilishi, ikulu ilitoa kauli za kejeli kuwa, haijawahi kupokea jina hata moja la mpentekoste.

"ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti la jambo leo walisema askofu kakobe amezoea kulumbana na serikali, hivyo uamuzi wake hauna mashiko.

"tunajua ana waumini wengi wanaomsikiliza, lakini kwa maswala ya kiserikali ambayo inaaminika haina dini ni vigumu kuitabiria mabaya, kwani yeye kama mchungaji alistahili kukaa pamoja na ofisi husika na si kwenda kunukuu vitabu vitakatifu kwa kuitabiria mabaya serikali",
alisema patrick haule ambaye ni mwinjilisti.

chanzo: gazeti la jambo leo, tarehe 13 march 2014

kweli ikulu ya magogoni kituko duuh teh teh teh....
 
porojo ziko ikilu kakobe anaporojo gani??? uchumi mbaya ni kakobe au ikilu???
 
Njaa za maaskofu ndio zinazowaponza. Posho inamtoa roho kakobe na wachungaji wenzake. Kazoea kutapeli waumini wake kanisani mpaka kajenga na mahekalu sasa mradi umeota mbawa na unazidi kudorora anaona atunge njia nyingine itayompatia pesa. Huyu askofu ni mganga njaa sana hata hivyo na abuni mradi mwingine kuliko utapeli wake anaotaka ufike mpaka serikalini.

Hivi jamani tuongee ukweli nani kati ya maaskofu na wale wenzetu wa upande wa pili wana njaa? we kwa akili yako kweli utasema kakobe ana njaa ya kulilia posho ya laki3 kwa siku?
 
Unauhakika na usemalo kaka!kumbuka ni madai ya msingi hayo sasa haiingii akilini wewe unapoamua kuwasemea ikulu
 
safi sana serikali ifike mahali hawa wachunga kondoo wa bwana wafanye kazi ya kuchunga kondoo..

habari za siasa wawaachie wanasiasa au kama wanatamani kazi ya siasa wavue majoho wafanye siasa...

CC: Ntuzu
 
Last edited by a moderator:
Hivi kakobe alishatoka canada??-atuletee cd na tape za mahubiri tumtukuze mungu bhana.
 
Siku zote mpuuzi ni mtu wa kupuuzwa tu.

Naipongeza Ikulu kwa kusikia maombi yetu Watanzania ya kupuuzwa kwa Kakobe.

Kwa sasa Ikulu ina simamia mambo ya maendeleo ya umma, leo mpuuzi mmoja (Kakobe) anataka asumbue serikali?

Aende zake huko na ndoto zake za vitisho. Mungu wa Abrahamu ni mwenye huruma kwa wanaadamu.

Hayupo kutufanyia visasi, bali kutulea watu wake. I doubt kama Kakobe ana Mungu wa Abrahamu.

Ongelea nafsi yako Ikulu imesikia kilio cha watanzania? Je wewe umekuwa msemaji wa watanzania wote zaidi ya mil 40? Kama ndivyo nani waliokuchagua na kura walikupigia lini na kwa mfumo upi? Unadai Mungu wa Abrahamu siyo Mungu wa visasi? Sasa mimi kuna mahali nimesoma hivi "....usilipize kisasi maana kisasi ni juu yangu mimi Mungu...",tena anena ".........nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu...."-Kutoka 20:5-6
 
Gazeti lenyewe Jambo leo , Mtu mwenyewe Salva . Jamaa kanjanja sana huyo hapo amejidhalilisha na pia amedhalilisha state house.
 
safi sana serikali ifike mahali hawa wachunga kondoo wa bwana wafanye kazi ya kuchunga kondoo..

habari za siasa wawaachie wanasiasa au kama wanatamani kazi ya siasa wavue majoho wafanye siasa...

CC: Ntuzu

Sasa ulimwengu hauna kondoo tu una mbuzi pia hivyo siyo kosa kuchunga mbuzi wakati wako zizini
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom