Ikulu yamtaka Askofu Kakobe aache porojo!

Ikulu yamtaka Askofu Kakobe aache porojo!

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
2,412
Reaction score
1,928
2.jpg


Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema haina muda wa kujibu porojo zilizotolewa na Askofu wa kanisa la Full Gospel Fellowship, Zachary Kakobe kwani ina kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Imesisitiza kuwa ofisi ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu haifanyi kazi za porojo kama sehemu ya kuendesha utawala wake, badala yake iko makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa kulinda na kuheshimu demokrasia na kufuata katiba ya nchi.

Kauli hiyo inatokana na waraka maalumu unaodaiwa kutolewa na Askofu Kakobe na kisha kupelekwa Ikulu.Hata hivyo, kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema haijathibitisha rasmi kama waraka huo umefika katika ofisi hiyo.

Akizungumza juzi na gazeti la Jambo Leo kwa njia ya simu,Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu alisema serikali si lazima ijibu Porojo zilizotolewa na Kakobe, kwani Ikulu ni sehemu nyeti ya kutumikia wananchi katika maswala ya msingi na yenye tija kwa taifa.

"Yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",

alisema na kuongeza kuwa swala hilo lilishajibiwa na kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, Dr Florence Turuku ambapo alilitolea ufafanuzi wa kutosha.

Waraka huo uliotolewa kwenye vyombo vya habari na Askofu Kakobe ulikuwa ukieleza namna Ikulu "ilivyotupa kapuni" majina yote ya wapentekoste waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, hivyo kuwafanya wapentekoste takribani milioni 10 kukosa mwakilishi hata mmoja.

Pia waraka huo ulidai kuwa baada ya kukosa uwakilishi, Ikulu ilitoa kauli za kejeli kuwa, haijawahi kupokea jina hata moja la mpentekoste.

"Ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti la Jambo Leo walisema Askofu Kakobe amezoea kulumbana na Serikali, hivyo uamuzi wake hauna mashiko.

"Tunajua ana waumini wengi wanaomsikiliza, lakini kwa maswala ya kiserikali ambayo inaaminika haina dini ni vigumu kuitabiria mabaya, kwani yeye kama mchungaji alistahili kukaa pamoja na ofisi husika na si kwenda kunukuu vitabu vitakatifu kwa kuitabiria mabaya serikali",
Alisema Patrick Haule ambaye ni Mwinjilisti.

Chanzo: Gazeti la Jambo leo, tarehe 13 march 2014
 
Njaa za maaskofu ndio zinazowaponza. Posho inamtoa roho kakobe na wachungaji wenzake. Kazoea kutapeli waumini wake kanisani mpaka kajenga na mahekalu sasa mradi umeota mbawa na unazidi kudorora anaona atunge njia nyingine itayompatia pesa. Huyu askofu ni mganga njaa sana hata hivyo na abuni mradi mwingine kuliko utapeli wake anaotaka ufike mpaka serikalini.
 
eti oooh hawana haja ya kumjibu huku wakimjibu, mbona wanajikanyaga

mara nyingi sana kama si mara zote hilo kurugenz hujibu mambo yasiyo ya msingi,huwa hawajibu mambo ya msingi hata siku moja,tumesoma press release zao nyingi sana hapa,me nadhan kukaa kimya kungekua jambo jema,ila sasa wao wanalinda vibarua vyao hawawez kukaa kimya,ndo huhorojoka hivi,any way mambo ya ngoswe hayo,mwachie mzee NGENGEMKENI MITOMINGI anayaweza
 
"Ikulu iko makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi"
Ikuuuulu!!! Ikulu ipi hiyo?? Itakuwa ni white house ya USA.
Nasema hivii "Ikulu ya Magogoni iache POROJO"

yaani wananchekesha tu,,,,,eti wapo makini kutatua matatizo ya watanzania,wa wapi????
 
Kazi ipo,Mzee kakobe endelea na manyanga yako waisome hawa magamba maana wamepuuza wito wako.
 
2.jpg


kurugenzi ya mawasiliano ikulu imesema haina muda wa kujibu porojo zilizotolewa na askofu wa kanisa la full gospel fellowship, zachary kakobe kwani ina kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Imesisitiza kuwa ofisi ya kurugenzi ya mawasiliano ikulu haifanyi kazi za porojo kama sehemu ya kuendesha utawala wake, badala yake iko makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa kulinda na kuheshimu demokrasia na kufuata katiba ya nchi.

Kauli hiyo inatokana na waraka maalumu unaodaiwa kutolewa na askofu kakobe na kisha kupelekwa ikulu.hata hivyo, kurugenzi ya mawasiliano ikulu imesema haijathibitisha rasmi kama waraka huo umefika katika ofisi hiyo.

Akizungumza juzi na gazeti la jambo leo kwa njia ya simu,mkurugenzi wa idara ya mawasiliano ikulu, salvatory rweyemamu alisema serikali si lazima ijibu porojo zilizotolewa na kakobe, kwani ikulu ni sehemu nyeti ya kutumikia wananchi katika maswala ya msingi na yenye tija kwa taifa.

"yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",

alisema na kuongeza kuwa swala hilo lilishajibiwa na kaimu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, dr florence turuku ambapo alilitolea ufafanuzi wa kutosha.

Waraka huo uliotolewa kwenye vyombo vya habari na askofu kakobe ulikuwa ukieleza namna ikulu "ilivyotupa kapuni" majina yote ya wapentekoste waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, hivyo kuwafanya wapentekoste takribani milioni 10 kukosa mwakilishi hata mmoja.

Pia waraka huo ulidai kuwa baada ya kukosa uwakilishi, ikulu ilitoa kauli za kejeli kuwa, haijawahi kupokea jina hata moja la mpentekoste.

"ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti la jambo leo walisema askofu kakobe amezoea kulumbana na serikali, hivyo uamuzi wake hauna mashiko.

"tunajua ana waumini wengi wanaomsikiliza, lakini kwa maswala ya kiserikali ambayo inaaminika haina dini ni vigumu kuitabiria mabaya, kwani yeye kama mchungaji alistahili kukaa pamoja na ofisi husika na si kwenda kunukuu vitabu vitakatifu kwa kuitabiria mabaya serikali",
alisema patrick haule ambaye ni mwinjilisti.

chanzo: gazeti la jambo leo, tarehe 13 march 2014

huyu anayesema kuwa serikali haina dini hajui tafsiri yake maana hata yeye ni serikali je hana dini? Mungu hadhihakiwi tuache mzaha na kujibu mambo magumu kilaini
 
Huyu anayesema serikali haina dini anatafsiri tofauti maana yeye mwenyewe serikali je hana dini? Mungu hadhihakiwi tuache kujibu mambo magumu kilaini
 
Njaa za maaskofu ndio zinazowaponza. Posho inamtoa roho kakobe na wachungaji wenzake. Kazoea kutapeli waumini wake kanisani mpaka kajenga na mahekalu sasa mradi umeota mbawa na unazidi kudorora anaona atunge njia nyingine itayompatia pesa. Huyu askofu ni mganga njaa sana hata hivyo na abuni mradi mwingine kuliko utapeli wake anaotaka ufike mpaka serikalini.

Kakobe Ana hekalu wapi?
Aliwai sema mtu yeyote anayeijua nyumba yake zaidi ya Ile kijitonyama.Aseme.
Mty yeyote anayejua ac ktk benk yeyote duniani kwa jina lake Au Mke wake Au watoto wake aseme.
Kakobe siyo kama wahuni mliowazoea.
We subiri yatakapoanza kutimia Yale aliyoyanena
 
waiache ikulu yetu itatue matatizo yetu, imetujengea barabara, shule nk. Inaendelea kuhudumia wananchi wake sio kujibu porojo
 
Mwikulu lya magogoni ina ongozwa na dhaifu, wasaidizi wake ni dhaifu ,wanamajibu yaliyo dhaifu !
Duh! Watanzania tumkatae jei kei na udhaifu wake ili nasisi tusije onekana dhaifu katika jumuiya za kimataifa !
Aiiiseeeeeeee! Kweli c.c.yem na jei kei ni urojo.
 
hivi kuna mtu aliyewahi kuwaza au kufikiri Muamari Gaddaf siku moja angejificha chini ya karavati la maji taka kujaribu kukwepa asiuliwe na kuburuzwa barabarani kama kibaka. wakati mwingine tusifanye vitu kwa kujaribu ili kuona kama kweli kitatokea kwani matokeo yake huwa ni mabaya sana.
 
kama ni porojo wasingehangaika kujibu, mbona wamejibu? inamaana ikulu yetu iko busy kujibu hata porojo.
 
Back
Top Bottom