Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
IKULU YA MASHETANI.
1)tutauteka Dunia,milele tutatawala.
Nyote mtaangamia,kila kona kila pala.
Sana tutawachukia,wale wafanyao sala.
ikulu ya mashetani,tutaiteka Dunia.
2)mbona hofu wanatia,kwa hadithi ya kutisha.
Yote unayonambia,moyo unapukutisha.
Mbona unalojambia,mkononi lang'arisha.
Ikulu ya mashetani,nini unamaanisha.
3)kwa makini we sikia,kitoto mwanamkiwa.
Asikize ka mkia,kwanza wachanganyikiwa
Anza sasa kutambua,kama ulivyoambiwa.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
4)naanza kukutambua,wewe bwana wa mapembe
Naona wajisumbua,ewe mwana wa mirembe
Wewe mlavitumbua, kulikoni si mzembe
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
5)tulikwisha fafanua,kwa kondoi mwenye pembe
Tamaa mkafunua,tukawalisha maembe.
Tulokwisha yachubua,kwa kisima cha ngarambe.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
6)kama vile naumia,kwa ngumu yako mafumbo.
Ulokwisha angamia,zamani toka kitambo.
Kwa pigo lake Ramia,kama ulienda ng'ambo.
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
7)lile hukuzingatia,kutoka kwa madhabahu.
Kwanza ukapuuzia,hukuiona suluhu
Mikononi takishika,kafiri ulokubuhu.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
8)mbona nayoulizia, unataka kuyachenga.
Ama unanitania,nianze piga kipenga.
Jibu kulitagutia,kwenye anga la malenga.
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
9)mwezi nyota tazamia,ishata utaziona
Zote nilikutajia,karibu zitakubana.
Pingu tutawafungia,tuwapige danadana.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
10)naijua asilia,lile tunda ulokula.
Roho linakumizia,unapofanya chakula.
Akili inasinzia,kama tunda amarula.
Ikulu ya mashetani,nini unamaanisha.
11)nimeandila barua,mateka kuwakusanya
Mtakufa kwa halua,tulo wazi nakukanya.
Machoni unamafua,kama pua naifinya.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
Shairi:IKULU YA MASHETANI.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382486.
1)tutauteka Dunia,milele tutatawala.
Nyote mtaangamia,kila kona kila pala.
Sana tutawachukia,wale wafanyao sala.
ikulu ya mashetani,tutaiteka Dunia.
2)mbona hofu wanatia,kwa hadithi ya kutisha.
Yote unayonambia,moyo unapukutisha.
Mbona unalojambia,mkononi lang'arisha.
Ikulu ya mashetani,nini unamaanisha.
3)kwa makini we sikia,kitoto mwanamkiwa.
Asikize ka mkia,kwanza wachanganyikiwa
Anza sasa kutambua,kama ulivyoambiwa.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
4)naanza kukutambua,wewe bwana wa mapembe
Naona wajisumbua,ewe mwana wa mirembe
Wewe mlavitumbua, kulikoni si mzembe
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
5)tulikwisha fafanua,kwa kondoi mwenye pembe
Tamaa mkafunua,tukawalisha maembe.
Tulokwisha yachubua,kwa kisima cha ngarambe.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
6)kama vile naumia,kwa ngumu yako mafumbo.
Ulokwisha angamia,zamani toka kitambo.
Kwa pigo lake Ramia,kama ulienda ng'ambo.
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
7)lile hukuzingatia,kutoka kwa madhabahu.
Kwanza ukapuuzia,hukuiona suluhu
Mikononi takishika,kafiri ulokubuhu.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
8)mbona nayoulizia, unataka kuyachenga.
Ama unanitania,nianze piga kipenga.
Jibu kulitagutia,kwenye anga la malenga.
Ikulu ya mashetani,kipi unamaanisha.
9)mwezi nyota tazamia,ishata utaziona
Zote nilikutajia,karibu zitakubana.
Pingu tutawafungia,tuwapige danadana.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
10)naijua asilia,lile tunda ulokula.
Roho linakumizia,unapofanya chakula.
Akili inasinzia,kama tunda amarula.
Ikulu ya mashetani,nini unamaanisha.
11)nimeandila barua,mateka kuwakusanya
Mtakufa kwa halua,tulo wazi nakukanya.
Machoni unamafua,kama pua naifinya.
Ikulu ya mashetani,tutaiteka dunia.
Shairi:IKULU YA MASHETANI.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382486.