Ikulu Vs gazeti la Mwananchi!

Bora wameacha kutumia ki email cha Yahoo. Lakini naona Kiswahili bado kinawapiga chenga.
 
Bora wameacha kutumia ki email cha Yahoo. Lakini naona Kiswahili bado kinawapiga chenga.

Hata hivyo bado mawasiliano ya ikulu ya TZ hayajawa encripted na hii sijui wanafanya makusudi au ni kutokujua. Email za ikulu, mambo ya ndani, ulinzi na jkt zinakuwa intercepted bila hata kutumia akili nyingi. Mfano kuna server mbili za mambo ya ndani ziko wazi hata kwa wapita njia wenye high-tech-wifi.
 
Hivyo, Ikulu inapenda kuwaambia wananchi kuwa kama ilivyokuwa kwenye habari ile ya Mei 21, habari ya jana ya gazeti hilo pia siyo ya kweli na ni ya kufitinisha watu na inastahili kudharauliwa na kupuuzwa.

Mmh, sasa wananchi watawezeje kudharau na kupuuza kitu ambacho Ikulu imeshindwa si tu kudharau bali hata kukipuuza na imebidi itumie rasilimali za taifa kupinga? Si vyema na wananchi wakapewa haki ya kupima na kuamua kwa hiyari yao kama habari ya Mwananchi ina ukweli au la, badala ya kuamuriwa kudharau na kupuuza? Maana lugha iliyotumika sio hata ya kushauri wananchi wadharau na kupuuzia, bali wananchi wanaambiwa na kurugenzi ya mawasiliano kuwa habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi siyo ya kweli na inastahili kudharauliwa na kupuuzwa!

Annina
 
Houseboy uliyemtoa bush ataanzaje kukuletea umwamba??
Afate unayotaka au apotee kwako...
 
Serikali ya JK imekuwa kama mtu aliyeshika chungu cha moto. Inatapapata kujaribu kuweka sawa mambo katika mazingira tata na ambayo haiingii akilini kwa wajuzi wa mambo.

Inajibu hoja kwa kwa kujichanganya. Kama Mwaziri hawatumwi na mtu yeyote huko mikoani, huu Waraka wa kuwazuia kusafiri nje ulitolewa kwa madhumuni gani??.


Katika kile kinachoonekana ni kujipanga vema na kujihami kwa maswali magumu wakati wa kampeni za uchaguzi, Ikulu imetoa waraka wa kuzuia mawaziri kusafiri nje na badala yake kuwaagiza kuzunguka mikoani kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne.

Waraka huo, ambao umepewa jina la "Mlitutuma, Tumetekeleza, Tumerudi Kuwaelezeni Tulivyotekeleza na Kuwasikilizeni", pia unawaagiza mawaziri kukutana na watu wa aina mbalimbali kwenye ziara hizo, wakiwemo viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Ikulu kutoa maagizo kama hayo baada ya ziara ya kwanza iliyofanywa mwaka 2007 ya kutetea na kuelezea bajeti ya mwaka 2007/08, ambayo ilikuwa ya kwanza kwa serikali ya awamu ya nne, kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za walipakodi na kampeni za mawaziri kupata ujumbe kwenye halmashauri kuu ya CCM, chombo ambacho ni cha pili kimamlaka kwenye chama hicho kikongwe baada ya mkutano mkuu. Pia katika ziara hizo, mawaziri walijikuta wakiishia kufanya vikao vya ndani ya chama kutokana na wananchi kuwazomea kila walipotaka kufanya mikutano. "Huko nyuma, tumepata kuwaandalia Outreach Programmes angalau mara mbili. Zote mbili zilianza vizuri lakini zikaishia njiani kabla ya kumalizika," inasema sehemu ya waraka huo. "Ili kuhakikisha kila waziri anatekeleza wajibu wake katika hili, tunashauri ziara zote za mawaziri za nje ya nchi zisimamishwe hadi kila waziri atakapokuwa amefanya ziara yake."

Waraka huo umetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa amewatangazia vijana, viongozi na wana CCM wote kujiandaa kujibu tuhuma za ufisadi ambazo zitaibuliwa na wapinzani kama silaha kwenye kampeni za uchaguzi wa Oktoba. Agizo hilo la Kikwete alilolitoa juzi mjini Iringa wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), limedhihirishwa na waraka huo ambao umeambatana na ratiba ambayo inaonyesha ziara za mawaziri hao mikoani kueleza wananchi mafanikio ya serikali katika kutatua kile walichoituma.

Katika waraka huo wa Mei 11, Ikulu imeelekeza na kutoa mapendekezo ya wadau husika ambao kila waziri atapaswa kukutana nao katika mikutano yake mikoani kwa mujibu wa ratiba.

Waraka huo, ambao Mwananchi imeona nakala yake, umeelekeza kwamba katika mkutano wa kwanza waziri atapaswa kukutana na wafanyakazi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, madiwani, wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa CCM.

Agizo hilo la waraka limetaja wadau wengine wakuu wanaopaswa kukutana na mawaziri kuwa ni pamoja na wajumbe wa nyumba kumi, wawakilishi wa sekta za wizara zilizopo mkoani humo, wawakilishi kutoka sekta ya biashara mkoani na wawakilishi wa sekta nyingine za uchumi.

Sehemu ya waraka huo ambao unatokana na maamuzi kati ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu) na wasemaji wa wizara za serikali, imetoa pia ratiba ambayo kila waziri atapaswa kutembelea mkoa mmoja kwa tarehe maalum iliyopangwa. "Inapendekezwa katika programu hii kila waziri atembelee mkoa mmoja kwa tarehe zilizopangwa...," inaeleza sehemu ya waraka huo.

Waraka huo umeelekeza madhumuni mawili ya ziara hizo ambayo ni pamoja na kila waziri kueleza mafanikio ya wizara yake katika miaka mitano ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne na kusikiliza kero na shida za wananchi katika maeneo wanayotembelea na kujibu hoja.

Ikulu imeeleza katika waraka huo ikisema: "Kabla na baada ya ziara ya waziri, kila wizara itatakiwa kufanya mambo yafuatayo, kutengeneza vipindi maalumu viwili in the form of Documentaries (katika mfumo wa vipindi vya makala (redio na TV))."

Kazi nyingine kwa mujibu wa waraka huo ni pamoja na "kuandaa tangazo fupi (public service announcement) kutangaza mafanikio ya wizara katika miaka hiyo mitano kwa ajili ya redio na televisheni na matangazo hayo yaanze kutumika mara moja".

Pia wametakiwa "kuandaa retreat na wahariri wakuu na wahariri waandamizi wa vyombo vya habari nchini kwa nia ya kujenga uhusiano na vyombo hivyo na pia kuwaelezea wahariri hao mafanikio ya serikali ya awamu ya nne". "Kabla ya kuanza ziara, kila waziri aandae mkutano mkubwa wa waandishi wa habari kuelezea mafanikio na shabaha ya ziara yake," unaeleza waraka huo. "Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inapendekeza kuwa ofisi zote za wakuu wa mikoa zifuatilie ratiba hiyo ili kuandaa na kufanikisha mikutano hii na waziri husika. "Pia taarifa kwa vyombo vya habari iandaliwe kabla ya kuanza na ratiba nzima ya waziri na mkoa itolewe kwa wana habari."

Ratiba ya ziara iyo inaonyesha, mawaziri Muhammad Seif Khatibu (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Mei 13 hadi 16, 2010, William Ngeleja (Waziri wa Nishati na Madini) alipaswa kuanza ziara mkoa wa Shinyanga (Ziara ya kwanza) kuanzia tarehe hiyo, Profesa David Mwakyusa (Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) naye alipaswa kuanza ziara mkoani Arusha katika muda huo (ziara ya kwanza).

Waziri mwingine ambaye alipaswa kuanza ziara katika tarehe hiyo ni Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha na Uchumi), ambaye alipaswa kuwa mkoani Lindi.

Kundi la pili ambalo limetajwa katika ratiba hiyo linajumuisha mawaziri John Magufuli (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) ambaye alipaswa kuanza ziara mkoani Mara kuanzia Mei 17 hadi 20, 2010.

Wengine ambao wamepangiwa katika tarehe hiyo ni Dk Diodaurs Kamala (Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki) ambaye alipaswa kuwa mkoani Ruvuma, Sophia Simba (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora) ambaye alipaswa kuwa mkoani Tanga na Profesa Jumanne Mghembe (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi) ambaye alipaswa kuwa mkoani Iringa, katika tarehe hiyo.

Kundi la tatu ambalo limetajwa kwenye ratiba ya waraka huo linahusisha mawaziri Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) ambaye kuanzia Mei 21 hadi 24, 2010 atapaswa kuwa mkoani Morogoro, Mathias Chikawe ( Waziri wa Sheria na Katiba) ambaye atapaswa kuwa mkoani Rukwa, Philip Marmo (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge) atapaswa kuwa mkoani Singida.

Waraka huo umeeleza kuwa kundi la nne litamjumuisha Profesa Juma Kapuya (Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana), ambaye kuanzia Mei 25 hadi 28, atapaswa kuwa mkoani Mwanza, wengine ni Stephen Wassira (Kilimo, Chakula na Ushirika) ambaye atapaswa kuwa mkoani Tabora.

Katika ratiba ya tarehe hiyo, Lawrence Masha (Mambo ya Ndani) atapaswa kuwa mkoani Kagera na Shamsa Mwangunga (Maliasili na Utalii) atapaswa kuwa mkoani Arusha (mara ya pili).

Kundi la tano, kwa mujibu wa ratiba hiyo, litamuhusisha Profesa Mwandosya (Waziri wa Maji na Umwagiliaji) kuanzia Mei 29 hadi Juni mosi, atapaswa kuwa mkoani Dodoma, Celina Kombani (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi) atapaswa kuwa mkoani Shinyanga (mara ya pili), Prof Peter Msolla (Mawailiano, Sayansi na Teknolojia) atapaswa kuwa mkoani Kilimanjaro.

Kundi la sita ambalo limetajwa katika ratiba hiyo, litahusisha mawaziri, Dk Hussein Mwinyi (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mtwara kuanzia Juni 2-5, George Mkuchika (Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo) ambaye atapaswa kuwa mkoani Mwanza, Dk Shukuru Kawambwa (Miundombinu) atapaswa kuwa mkoani Manyara, Magaret Sitta (Maendeleo ya Jamii, Jinsi na Watoto) atapaswa kuwa mkoani Mbeya na John Chilligati (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) atapaswa kuwa mkoani Kigoma.

Utaratibu huu uliwahi pia kutumiwa wakati wa bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne, ambayo mawaziri walitawanywa mikoani kuinadi na kuitetea.
http://www.wavuti.com/4/post/2010/05/mawaziri-wastopishwa-safari-za-nje-kwa-sasa.html
 
Kwa hiyo Mawaziri wanaweza kukurupuka tu bila kumuaga Bosi wao? Halafu wote wanaondoka kwa kujituma katika ziara zenye mtazamo mmoja? Kweli upambe ni kazi ngumu, I am lcky siko kama Salva.

Afadhali nile dona yangu kwa amani kuliko kugeuka kijibwa cha Wakubwa!

Napata tabu sana na uelewa wa huyu mtu anaeitwa Salva Rweyemamu hapa IKULU. Siku zote kazi yake imekuwa ni propaganda za kupotosha mambo na wamekuwa wakimpotosha hata JK katika mengi na ndio maana mpaka leo IKULU haina vyombo vya hakika vya mawasiliano ikiwemo tovuti na hata hizo tovuti zao za Serikali ni utumbo mtupu kutokana na huyu kilaza kuwa pale. Huu Waraka niliwahi kuupost hapa kuhusu safari za watumishi wa UMMA wakiwemo mawaziri ambazo zinahitaji vibali vya wakubwa wao. Sasa akisema Mawaziri hawatumwi na yeyote..haiingii akilini kabisa kama si kujikangaya na kutapatapa.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS


Anwani ya Simu: "UTUMISHI", DSM. Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Simu Nambari: 2118531-4 S.L.P. 2483,
Fax: 2131365 Dar es Salaam,


Barua Pepe: permsec@estabs.go.tz

TANZANIA.


Unapojibu tafadhali taja:


Kumb. Na: EA 45/257/01 Tarehe: 27 Agosti, 2004





WARAKA WA UTUMISHI NA.7 WA MWAKA 2004



KIKOMO CHA SIKU ZA KUWA NJE YA KITUO CHA KAZI




KWA WATUMISHI WA UMMA




1:0. UTANGULIZI:


1:1. Wakati huu ambapo mchango wa Utumishi wa Umma unatambuliwa
kuwa muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii, Serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika vituo vyao vya kazi kwa sehemu kubwa ya muda wao wa kazi. Hapo hapo Serikali inatambua umuhimu wa watumishi wa umma kujiongezea ujuzi wa kazi kwa kushiriki katika kongamano za kitaaluma.



1:2. Pia Serikali imeweka viwango vya posho za safari za nje ya vituo vya
kazi kwa siku vinavyokidhi gharama za kujikimu ambavyo ni vya kiwango cha juu na vinavyoongeza matumizi ya Serikali.


1:3. Nyaraka za Rais Na.1 wa mwaka 1992 na Na.1 wa mwaka 1998 zimesisitiza kupunguza safari za watumishi ili kupunguza matumizi ya Serikali.


2:0. MADHUMUNI YA WARAKA


2:1. Ili kuhakikisha maelekezo haya yanatekelezwa ipasavyo sasa inaagizwa kwamba mtumishi hataruhusiwa kuwa nje ya kituo chake cha kazi kwa sababu za kikazi, mafunzo mafupi, kuhudhuria warsha, kongamano na mengineyo kwa zaidi ya siku za kazi sitini (60) kwa kila mwaka wa fedha.



2:2. Pale inapobidi kuzidisha siku sitini itabidi yatolewe maelezo ya kina
yatakayomridhisha msimamizi wa kazi.


2:3. Pamoja na Waraka huu tumeanzisha fomu maalum – (TFN 856 &
856A) za kujazwa na mtumishi na kuidhinishwa na msimamizi wake wa
kazi.
3:0. UTARATIBU UTAKAOTUMIKA KUANZIA TAREHE YA KUANZA
KUTUMIKA KWA WARAKA HUU


Utaratibu ufuatao utatumika kwa watumishi wa umma wanaosafiri nje ya
kituo cha kazi.


3:1. Kiwango cha juu cha muda wa kusafiri nje ya kituo cha kazi kitakuwa
siku SITINI (60) KWA MWAKA WA FEDHA.


3:2. Kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma safari zote kwa madhumuni tajwa zitaidhinishwa kwa kuzingatia utaratibu ufuatao:-
3:2:1. Makatibu Wakuu na Wakuu wa Idara za Serikali Zinazojitegemea safari zitaidhinishwa na Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kushauriana na Waziri wa Wizara/Idara inayohusika.
3:2:2. Makatibu Tawala wa Mikoa safari zitaidhinishwa na Wakuu wa
Mikoa.


3:2:3. Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Serikali za Mitaa, safari hizo zitaidhinishwa na Wakuu wa Wilaya.


3:3. Kwa Watumishi wengine wote, safari hizo zitaidhinishwa na Watendaji
Wakuu wa sehemu zao za kazi.


3:4. Inashauriwa kuwa Mikutano, Semina, Jopo na Makongamano ipunguzwe sana na kubakia ile ya muhimu tu ambayo ina mwelekeo wa mafunzo muhimu kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.


3:5. Pia Watendaji Wakuu wasiende safari na Wasaidizi wao Wakuu kwa wakati mmoja na kuacha eneo lao la kazi bila kiongozi mwenye uwezo wa kutoa maamuzi au ufafanuzi wa mambo muhimu yanayoihusu Taasisi yao.


3:6. Mtumishi yeyote aliyepata kibali cha kusafiri, akisharudi kutoka safari lazima athibitishe kwamba alikaa huko alikokwenda kwa muda wa siku



alizoomba au alizoruhusiwa kwa kuandika ripoti ya kazi ya safari yake
na kumkabidhi kiongozi wake wa kazi.


4. TAREHE YA KUANZA KUTUMIKA
Waraka huu unaanza kutumika tarehe 1 Septemba, 2004.





Joseph A. M. Rugumyamheto



KATIBU MKUU (UTUMISHI)



 
Nilikuwa Sifahamu kumbe moja ya Job Description za Mawaziri ni Kufafanua Mafanikio ya Serikali kwa Wananchi.

Hii ni failuire ya ku-compose watu wanaofaa kuwa ikulu. Hao mawaziri wana umoja gani huo unaowafanya wote kwa pamoja waamuwe kwenda mikoani bila kutumwa? Au sasa ndo wanaonyesha kihelehele cha uongozi wao?

Hiyo kurugenzi lazima ikubali kwamba boss wao ni mzigo na kila wakati ni mihangaiko ya kumusafisha. Eti mazungumzo na TUCTA! Si mpangaji wetu alisema hahitaji kura za wafanyakazi?
 
Duuuu!!!!!!.Kwakweli Sijui jamii tunafundishwa nini katika hili? Mungu ibariki Tanzania.Tusioweza kuwa Vubaraka Tuna wakati Mgumu sana,Na mambo haya hayapo Serikalini tu,hata katika mashirika Binafsi,Usipokuwa kibaraka hupati haki zako za msingi.Wajameni?????Kweli kazi ipo.
 
Back
Top Bottom