Ikulu Vs gazeti la Mwananchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu Vs gazeti la Mwananchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AK-47, Jun 3, 2010.

 1. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [FONT=Century Gothic, sans-serif]DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS[/FONT]
  [FONT=Century Gothic, sans-serif]UNITED REPUBLIC OF TANZANIA[/FONT]​


  [FONT=Book Antiqua, serif]Telephone: 255-22-2114512, 2116898 [/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]E-mail: press@ikulu.go.tz[/FONT]
  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.  [FONT=Book Antiqua, serif]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]​


  [FONT=Book Antiqua, serif]Gazeti la kila siku la Mwananchi la jana, Jumanne, Juni Mosi, 2010, lilichapisha habari kwenye ukurasa wake wa kwanza chini ya kichwa cha habari, “Waziri Amuumbua Msemaji wa Rais”.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Katika habari hiyo, gazeti hilo lilidai kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Mheshimiwa Philip Marmo alikuwa amepingana na maelezo yaliyotolewa Mei 21, mwaka huu, 2010, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu, kuhusiana na ziara za mawaziri nje ya nchi na katika mikoa mbali mbali nchini.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Katika taarifa yake ya Mei 21, mwaka huu, kwa vyombo vya habari, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilikuwa imekanusha habari zilizokuwa zimeandikwa na gazeti hilo hilo la Mwananchi chini ya kichwa cha habari, “Serikali Yahaha Uchaguzi Mkuu: Ikulu yazuia mawaziri kwenda nje, yawatuma mikoani kukutana na viongozi wa Dini na TUCTA’.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Ikulu imeshangazwa na kusikitishwa sana na kiwango cha juu cha jitihada na juhudi kubwa zinazofanywa na gazeti hili kufitinisha watu na kupotosha umma kwa jambo ambalo halipo, na inapenda kurudia na kusisitiza kama ifuatavyo:[/FONT]
  1. [FONT=Book Antiqua, serif]Siyo Ikulu wala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewakataza mawaziri kusafiri nje ya nchi kama linavyodai gazeti hili. Hakuna waziri aliyezuiwa kusafiri nje.[/FONT]
  2. [FONT=Book Antiqua, serif]Siyo Ikulu wala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza mawaziri kusambaa katika mikoa mbali mbali kukutana na viongozi wa Dini na TUCTA kama linavyodai gazeti hili.[/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]Kama mawaziri wanakwenda mikoani kuelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya Awamu ya Nne ya uongozi wa Tanzania ni jambo jema. Na hiyo ni sehemu ya wajibu wao na kazi zao kama mawaziri wa Serikali. Na wala siyo wafanye hivyo kwa kutumwa ama kuagizwa na yoyote. Ni wajibu wao wa kikazi na uwajibikaji.[/FONT] [FONT=Book Antiqua, serif]Kama tulivyoelezea katika taarifa ya Mei 21, hakuna haja wala hoja ya msingi kwa Serikali kuwatuma Mawaziri ama hata watu wengine wowote kwenda mikoani kuzungumza na viongozi wa kiroho ama wale wa TUCTA. [/FONT] [FONT=Book Antiqua, serif]Kama wananchi watakavyokuwa wanakumbuka, mazungumzo kati ya viongozi wa dini na Serikali yamemalizika majuzi. Yalifanyika rasmi na hadharani pale Hoteli ya White Sands, mjini Dar es Salaam. Tena mazungumzo hayo yalikwenda vizuri na yalimalizika vizuri. Viongozi wa dini walifurahi sana. [/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Mazungumzo yenyewe yalifungwa na Mheshimiwa Rais Kikwete, na viongozi wa roho walifurahi kiasi cha kwamba wamependekeza kuwa utaratibu wa kuwa na mazungumzo ya namna hiyo liwe ni jambo la kudumu na yafanyike kila mwaka. [/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Na Mheshimiwa Rais Kikwete amekubali pendekezo hilo ambako sasa itafanyika mikutano miwili kati ya viongozi wa kiroho na wale wa Serikali kila mwaka. Mkutano mmoja utakuwa kati ya Serikali na kila dhehebu, na ule wa pili utakuwa kama ule uliomalizika White Sands yaani kati ya Serikali na viongozi wote wa kiroho.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Hivyo, kwa sasa Serikali haina sababu ya kuwatuma mawaziri wake kwenda kuzungumza na viongozi wa dini wakati mkutano kati ya pande hizo mbili umemalizika majuzi tu, tena vizuri, kwa kushirikisha viongozi wa kiroho kutoka mikoa yote.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Aidha, mazungumzo kati ya Serikali na TUCTA pia yamemalizika. Mazungumzo hayo yalimalizika Mei 8, mwaka huu, 2010, mjini Dar es Salaam. Haya nayo yalimalizika vizuri na pande hizo mbili zilikubaliana. Lililobakia sasa ni Serikali kuyafanyia kazi makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo kupitia taratibu na michakato mbalimbali ya Kiserikali ukiwamo mchakato wa Bajeti.[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Sasa, kama mazungumzo kati ya Serikali na TUCTA yamefanyika vizuri na pande hizo mbili zimekubaliana, Serikali ama Ikulu, ina sababu gani ya kutuma mawaziri kwenda kuzungumza na viongozi wa TUCTA mikoani? Wanazungumza nini tena?[/FONT]

  [FONT=Book Antiqua, serif]Hivyo, Ikulu inapenda kuwaambia wananchi kuwa kama ilivyokuwa kwenye habari ile ya Mei 21, habari ya jana ya gazeti hilo pia siyo ya kweli na ni ya kufitinisha watu na inastahili kudharauliwa na kupuuzwa.[/FONT]


  [FONT=Book Antiqua, serif]Imetolewa na:[/FONT]


  [FONT=Book Antiqua, serif]Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,[/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]Ikulu,[/FONT]
  [FONT=Book Antiqua, serif]DAR ES SALAAM[/FONT][FONT=Book Antiqua, serif].[/FONT]


  [FONT=Book Antiqua, serif]02 Juni, 2010[/FONT]
   
 2. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Salva Rweyemamu @ Work
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Salva, mbona ni wewe tu unayepelekeshwa kasi?
  Habib halahala na wasemaji na waandishi wengine wa marais waliokutangulia wamekufundisha nini kwa matendo yao?
   
 4. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa kazi ipo wajamene!!!!!!!!
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa Sifahamu kumbe moja ya Job Description za Mawaziri ni Kufafanua Mafanikio ya Serikali kwa Wananchi.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  BTW: Wanaposema wanaenda kufafanua wanenda kufanya nini hasa?
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  what is the difference between cabinet of ministers and the president? uelewa wa huyu salva ni mdogo sana...anajichanganya
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ngoma nzitoooo. Sasa nini kitafuata kwa gazeti la Mwananchi! Hivi ni nani share holders pale Mwananchi Communication Ltd. Maana RA alishaondoa zile za kwake!!!Je aliziondoa ki amani au ni kwa mikiki??!! Salva ni kibaraka wa nani Vile!!! usikute ni anguko la Mwananchi linaandaliwa maana na uchanguzi u karibu, ni lazima yabaki magazeti yale ambayo yanapigia filimbi au vibaraka wa.... malizia. Connect the dot.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  inawezekana mpaka leo hajui kwanini yupo pale Ikulu, yeye na premi Kibanga ni waropokaji tu, ni sawa na vijana wa kijiweni.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hao mawaziri wanakuja mikoani kueleza mafanikio gani? Au ndio kampeni zimeanza!
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Lilipokua linaanza liliitikisa Serikali, hadi kufikia kutumika kwa sheria ya kazi plus zile za uhamiaji kuwatimua Wahariri na management ya wale Wakenya, hahaha.

  Ukweli hauzimwi kwa vitisho, Salva anasema uwongo, jamaa wametumwa kuandaa uwanja wa kampeni za Kikwete kwa kisingizio cha mafanikio, yeye anahubiri uongo kuwa si kweli hakuna kitu kama hicho, sijui sasa anapinga nini.
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kurugenzi ya mawasiliano ikulu imeendeleaa kuonyeshaa uwezo mdogo katika kuratibu mawasiliano kati ya ikulu na umma wa watanzania! hivi ningependaa kuuliza, je sifa muhimu ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano kwa umma ni kufahamu/kusomea uandishi wa HABARI???

  uzoefu unaonyesha kwamba hapa nchini tasnia ya habari sio career of choice!!! hii ni kutokana na mfumo wetu wa kielimu ambao wachahce hapo nyuma (waliochaguliwa kwa kufauluu) hupenda zaidi kujiunga na tasnia nyingine kama sheria, uchumi,uhandisi, udaktari, na biashara kwa maana ya chagua la kwanza zaidi. Tasnia nyingine huafuatie kwa maana ya kupata nafasi ya kujiunga elimu ya juu. Uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma ni tasnia muhimu iliyopaswaa kuwa na wajiungajii wengi wenye uwezoo wa kutathiminii na kuchambuaa mambo kwa upanaa kwa kuelewaa vema tasniaa nyingine zote.

  Inasikitishaa ikulu kama ofisi ya juu katika taifa letu inakuwaa na kitengo muhimu kama mawasiliano kwa umma chenye watendaji wavivuu kufikiri wanojivikaa ubabe, ukada na itikadii zenyee porojooo rahisii katikaa kuelimishaa umma masualaa muhimu ya Taifa letu.

  Salva Rweyemamu nasikia ni mmoja wa wakongwe wa tasnia ya habari nchini, lakini kwa kipindi chake kuongoza kurugenzi hii ya mawasiliano amejipambanuaa vizuri alivyoo na upeoo mdogoo katika utendajii wake. Je kama huyu ni mmoja wa wakongwe katika tasnia hii, waliobakiaa hali ikojee?

  Napenda kuchukua fursa hii kutoa ushauri kwa wale wote walio kwenye tasnia ya habari kurejeaa tena katika misingi ya taaluma yao na kujielekezaa kuwa na upeoo wa mbelee wenye kujenga umma ikitegemewaa umuhimu wa vyombo vya habari nchini.

  LEO YUKO SALVA IKULU, HUENDA KESHO AKATEULIWA MWINGINE MIONGONI MWAO (KWANI INAAMINIKA TANZANIA UTAALAMU WA MAWASILIANO KWA UMMA SIFA NI KUWA MWANDISHI WA HABARI) Mwalimu hakuwa na taaluma ya uandishi wa habari ila ni mmoja kati ya waandishi mahiri duniani iwe majarida, vitabu hata makala.
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani natamani 1995 ingerudi. Wakati ule kiongozi wa serikali mpaka rais akipita tulikuwa tunamuonyesha alama ya vidole viwil yaani ''V'' kiasi kwamba walikuwa wanakosa hata comfidence ya kusimamisha gari. Si mnajua wadau wakatu ule Lyatonga alikuwa na nguvu kiasi kwamba wadau wengi walimpa matumaini?. Sasa hawa mawaziri wakija; maana najua ni kampeni tu. TUWANYOOSHEE alama ya '' V ''
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Si mchezo... :smile-big:
   
 15. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  Habari hii ya Ikulu inazidi kujichanganya kuliko kutoa majibu toshelevu, bado nakubaliana na Mwananchi kwani wametoa vielelezo ikiwa ni pamoja na ratiba ya mawaziri. Ni kweli kuwa Salva alisema mawaziri hawajatumwa mikoani wakati huo huo Marmo akakiri Je, huko si kupingana?

  Taarifa hii inajichanganya kwa kupiga ziara za mawaziri mikoani wakati huo huo inakubali kuwa wameenda kueleza mafanikio ya Serikali, kipi sahihi sasa? this kurugenzi is very low, nashangaa vitu vinavyotoka ikulu vipo low sana. Pale magogoni pamevamiwa!
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ikulu inatapa tapa sasa.

  Ninavyoifahamu mimi Ikulu ,laiti kama Mwananchi waliandika habari za kupotosha na za uongo ni lazima wangechukua hatua za gazeti hilo kufungiwa.

  Mnakumbuka gazeti la Mwana Halisi?

  Wasitudanganye, ni swala ambalo lipo wazi Mawazili wanazunguka mikoani kufanya kampeni za kijanja kijanja.

  Hilo hata Rais mwenyewe akilikanusha haisadii kwani wananchi wana akili timamu.
   
 17. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kwa hiyo Mawaziri wanaweza kukurupuka tu bila kumuaga Bosi wao? Halafu wote wanaondoka kwa kujituma katika ziara zenye mtazamo mmoja? Kweli upambe ni kazi ngumu, I am lcky siko kama Salva.

  Afadhali nile dona yangu kwa amani kuliko kugeuka kijibwa cha Wakubwa!
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jamani haya ni mambo ya mfa maji haishi kutapatapa. mbona hawajalichukulia hatua kama limekosa?
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  NYAUBA, haya uliyoyasema yamenigusa sana, kwa sababu nilishapitia fani ya habari, na kujisomea mawasiliano ya umma. Ni kweli uandishi wa habari ni sehemu ya mawasiano ya umma, ila mawasiliano ya umma ni more than uandishi wa habari.

  Kumlinganisha Salva na watangulizi wake ni kumuonea bure, Salva ameingia Ikulu wakati media imepanuka zaidi na demands ni kubwa zaidi kuliko waliomtangulia. Nakumbuka vizuri kipindi cha Mwinyi, hakuwahi kuzungumza chochote na waandishi wa habari wowote kipindi chake chote cha miaka 10 madarakani. Balozi Choks, alimaliza kila kitu.

  Kwa maoni yangu, majukumu ya mawasiliano ya Ikulu ni more than what Salva na timu yake can do. Kwa vile Salva alikuwa ni Mhariri, kuandika Press Release ndio the best he can do, nothing more, nothing less; wakati Kazi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu is more than kutoa Press Release. Hawa jamaa wakijibu kitu, majibu yawe yenye substance. Mbona Salva na Premmy were dam good newsroom, wana uwezo na elimu nzuri tuu, lakini hapo Ikulu bado hawa-fit vizuri. Kuna Nini?

  Tukubali tusikubali, umefika wakati, sio Salva hawezi kazi, bali lazima ajenge capable team. Yeye aendelee kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, awe na wasaidizi wafuatao:

  1. Press Secretary wa Rais -
  2. Spokesperson wa Rais - Premmy?.
  3. Presidential Producer/Mtangazaji wa Ikulu - Wapate mtu toka TBC
  4. Presdential Photographer - Wapate Mtu toka Daily News/Maelezo
  5. Presidential Videographer - Wapate mtu toka Audio Visual.

  NB- Nimesuggest watu toka sehemu hizo ili wewe rahisi kuwa vetted kwa sababu ukiingia tuu ikulu lazima ama tayari ulikuwa nyoka ana lazima ugeuzwe nyoka ndio Ikulu yenyewe.
   
 20. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Baada ya hapo kichwa cha habari kinachopaswa kufuatia ni "Msemaji wa Rais amuumbua Waziri", maana nilidhani huyu jamaa atafafanua Marmo alimaanisha nini, kama alikuwa anatania tu au vipi.

  Sasa kwa kuwa kauli za Marmo hazijazungumziwa, sijui naye atalichukuliaje hili, kwamba alikurupuka?
   
Loading...