Ikulu: Rais Magufuli awaapisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala, awaasa wakatende haki na kutatua migogoro

Djif3mPW0AA9Fzh.jpeg

Ninayatafakari maneno ya JPM kuhusu utendaji kazi wa RAIS WA MKOA WA DSM kwamba hauridhishi.
Halikadhalika kwa Aly Happi.

Je Anguko lao liko njiani? Au JPM amewapa nafasi nyingine ya kujirekebisha??
Au ameshindwa kuwatumbua sababu hakuna watu wengine ndani ya chama/circle yake ambao wataziweza kazi zao?
MUDA UTAONGEA
 
Mbona ndio wamepandishwa vyeo? Kutoa DC hadi RC si bonge la promotion haijalishi mkoa gani ni sawa kutoka "CLASS MONTA" hadi "HEDI PRIFEKTI."
 
Last edited:
Vigezo vya utendaji bora ni mapato?

Mmhh mitaala ya utawala bora vyuoni na semina elekezi zimekaa ki mwendo kasi hivi!
 
kwa nini iwe Makonda na Hapi tu?mikoa mingine wanafanya vyema au ndo chuki na husda za kibongo as usual.
 
Atawazungungumza vibaya wote ila kwa Paulo ni full stop, hapo amezungumza mambo ya jumla ya hii wiki na kuwatisha wakuu wengine wa mikoa
 
Vigezo vya utendaji bora ni mapato?

Mmhh mitaala ya utawala bora vyuoni na semina elekezi zimekaa ki mwendo kasi hivi!

hujamuelewa,sio mapato...ni usimamizi wa hayo mapato kwenye miradi mingine,inaelekea Rais wa Dar alikua anafuja
 
Anachagua boguses kisa tu ni makada watiifu harafu anataka wakaboost ukusanyaji wa mapato? Hivi mtu kama Muro au Jokate wanaanzaje kwa mfano kuimarisha ukusanyaji mapato? Hizi kelele za JPM saa zigine bora akazipigie chumbani kwake na mkewe
 
View attachment 824728
Ninayatafakari maneno ya JPM kuhusu utendaji kazi wa RAIS WA MKOA WA DSM kwamba hauridhishi.
Halikadhalika kwa Aly Happi.

Je Anguko lao liko njiani? Au JPM amewapa nafasi nyingine ya kujirekebisha??
Au ameshindwa kuwatumbua sababu hakuna watu wengine ndani ya chama/circle yake ambao wataziweza kazi zao?
MUDA UTAONGEA

Mkuu hili lilikuwa dongo lililoelekezwa upande wa pili na sio kama wewe ulivyoelewa, jiulize kitu gani kimempandisha Hapi kuwa mkuu wa Mkoa?
 
Mkuu hili lilikuwa dongo lililoelekezwa upande wa pili na sio kama wewe ulivyoelewa, jiulize kitu gani kimempandisha Hapi kuwa mkuu wa Mkoa?
Kwa hiyo kauli ya mapato na ufujaji alizotoa raisi sio za kweli???
 
Back
Top Bottom