Ikulu: Rais Magufuli awaapisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala, awaasa wakatende haki na kutatua migogoro

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Shughuli ya uapishwaji wa Viongozi wapya walioteuliwa na Rais John Pombe Magufuli mnamo tarehe 28.07.2018 inaendelea Ikulu, Dar es Salaam. Shughuli iko live TBC.

IMG_5688.JPG


====

Alichoongea rais Magufuli kwa ufupi...

=> Niungane na wenzangu waliotanguliwa kuwapongeza ninyi. Hongereni sana.

=> Kikubwa ambacho ninaweza nikasema, kazi ya kuwapata ninyi haikuwa rahisi, nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne. Wapo waliopungua na wapo waliongezeka.

=> Tanzania tupo zaidi ya Mil 55. Mimi nliyesimama mbele yenu sio kwamba mimi nasitahili kuwa rais au mimi ndo nafaa, bali Mungu ndo alitaka. Siwezi jisifu mimi bali ni Mungu.

=> Waziri mkuu hata sijui nlimchaguaje, wapo watu walioenda Dodoma wakiwa wamevaa na suti wakijua wanakuwa mawaziri wakuu. Na sio kwamba Waziri Majaliwa anafaa sana bali Mungu ndo aliamua na vivo hivyo katika nafasi zenu, Uwe mkuu wa mkoa, jeshi, Magereza. Nafasi hizi zimepangwa na Mungu alitaka tuzipate. Tukijua hilo, tutafanya mema sana. Usipojua hilo, hutatenda haki kwa wale unao waongoza.

=> Hii Tanzania ni yetu. Nani mpinzani wa Tanzania? Eti nimechagua Wapinzani. Kafulila alipigania APTL, kuna mtu anaipenda IPTL aliitwa majina yote hadi tumbili lakini hajawa tumbili. Huyu utasema ni Mpinzani wa Tanzania?

=> Mkuu wa mkoa Hapi alikuwa Kinondoni, alianzia CCM pale makao makuu, Utamsema wa Chama gani? RAS ambaye ametoka chama kingine ni mmoja tu kafulila. Kumi na watatu wote. Makatibu wakuu, MaDC simuoni ambaye ametoka chama kingine ukiacha huyu wa Longido, Dodoma Mjini, Nanyumbu Machali na Bukombe Nkumba.

=> Hata hivyo ndugu zangu mkiwa mnapigana kwenye vita mkateka vifaru mnavuiweka kwenye stoo? Si unarudi kuwapigia hao hao?

=> Kwa tanzaia tunayoijenga tukiangalia mambo ya vyama hatutafika. Tunataka kwenda mbele, yule anayetaka kuchirikiana mshirikishe. Mkumbo alikuwa ACT akawa katibu mkuu.

=> Nachotaka kuwaambia ninyi mlioteuliwa, Msikilize mlioambiwa na viongozi wa dini, mumeteuliwa sababu mna uwezo. Mnaenda kufanya kazi za watanzania sio kazi zenu.

=> Unakuta migogoro Mingine ni midogo ya kutatua kwa siku moja lakini haitatuliwi. Sisi tukawe viongozi wa kutatua matatizo ya wananchi wetu

=> Juzi nlikuwa naongea na mabalozi bil 24.5 imekusanywa dodoma. Sasa unaweza kujiuliza dodoma kuna nini? Viongozi wa Dodoma wana nini ukilinganisha na Dar ambayo malengo yake ilikuwa bil12 ambayo nayo haijafikia. Unaweza ukajua kwamba hapa Dar kuna upigaji tena wa Nguvu. Kinondoni ambayo alikuwa anaiongoza Hapi ndo ilikuwa ya Mwisho. Nikaona ni wilaya iliyokuwa na Upinzania.

=> Kwanini katika majijij ambayo yapo Sita, mbeya iwe ya Mwisho? why? Yaani Jiji ambayo nmelitangaza limekuwa la kwanza lakini ya zamani yapo. Utaitwaje jiji wakati hukusanyi?

=> Halmashauri iliyokuwa ya Mwisho Mbulu na Mbinga why? Sasa haya sisi kama viongozi Hasa wakuu wa Mikoa, nyie ni kila kitu. Wewe rais wa Mkoa umeshindwa kusimamia mapato, kwanini nisiseme kwamba haufai? Hii nchi ili iendelee ni mapato.

=> Hapa Dar madiwani wakikutana siku moja wanalipana siku nne. Ndo maana hata mamachinga wamekosa hata sehemu ya kufanyia biashara. Hadi wamsubiri rais au makamu wa rais. Kimgogoro kidogo cha ardhi kutakua hakuna. Hizi kazi wote tumepewa dhamana. Hakuna mwenye garantii wa kazi hizi. hata mimi kwamba ntakuwa rais wa kudumu hapa. Kazi ya kukesha kwenye mafile mengine unaweka hadi kitandani. Siku moja nlimpeleka Waziri ninapolala Nikasema hata mimi sikujua, ningejua nisingeuomba huu urais.

=> Nawaomba, kazi hizi ni kazi za watu. Leo nmeamka nafikiri ni saa nane IGP kule ananipigia watu wamepata ajali.

Nanyi teseka kidogo, Machozi yao tutakuja kuyalipa. Kama mabaya yamefanyika katika mkoa wako razima malipo utayapata

Kuna alifanya mambo ya ovyo, waziri akaja kuniambia mimi wakati yeye ndo anataka atengue.

-=> iwaombe ndugu zangu wateuliwa wote kila mmoja akatimize wajibu wake. Kashirikianeni. Unakuta RC haongei na RAS, hizi kazi ni za muda, mkawashirikishe watu. Sisi huku tunaongea, nafahamu makamu wa rais anafanya nini, nafahamu Waziri anafanya nini kasulu.

Mimi nina hakika ninyi mna uwezo, wote mna uwezo na ndio maana. MSijihusishe na mabaya.

=> Mawaziri kafanyeni kazi kila mmoja akailewe kazi zake. wapo watu hawajazielewa wizara zao.

=> Tuna wajibu wa kutekeleza Ilani ya CCM hakuna jinsi ya kukwepa hili.

=> Mtu unamteua, halafu anafika kule ansema yeye ni neutral mtendaji wa serikali..hakuna kitu kama hicho. Umeteuliwa na CCM halafu unafika hapa unasema upo neutral wakati umeteuliwa na CCM, Mimi ni CCM, Kamamu wa Rais CCM, Waziri Mkuu CCM halafu wewe eti huna chama. Kafanyeni kazi.

=> Wote nliowateuwa wanafanya kazi vizuri. Ukimtanguliza Mungu hata wachawi hawakuwezi, mtafanikiwa.

=> Nawashukuru sana Mashehe, Maasikofu na Wachungaji wameendelea kuweka taifa hili kwenye maombi, na niniyi jiombee.

=> Mengi nimechomekea lakini kubwa lilikuwa ni kuwapongeza. Asanteni sana

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 01 Agosti, 2018 amewaapisha Wakuu wa Mikoa 4, Makatibu Wakuu 2, Makatibu Tawala wa Mikoa 13 na Naibu Makatibu Wakuu 2 aliowateua tarehe 28 Julai, 2018.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Dkt. Elieza Feleshi, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Wakuu wa Mikoa wote wa Tanzania Bara, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wakuu wa Mikoa walioapishwa ni Brig. Jen. Nicodemus Elias Mwangela (Songwe), Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti (Kagera), Ali Salum Hapi (Iringa) na Albert John Chalamila (Mbeya), wakati Makatibu Wakuu walioapishwa ni Prof. Joseph Rwegasira Buchweishaija (Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji) na Andrew Wilson Massawe (Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu).

Makatibu Tawala wa Mikoa walioapishwa ni Eric Katemansimba Shitindi (Njombe), Maduka Paul Kessy (Dodoma), Dr. Jilly Elibariki Maleko (Mtwara), Abubakar Mussa Kunenge (Dar es Salaam), Happiness William Seneda (Iringa), Karolina Albert Mthapula (Mara) na David Zacharia Kafulila (Songwe),

Wengine ni Denis Isidory Bandisa (Geita), Abdalla Mohamed Malela (Katavi), Rashid Kassim Mchatta (Kigoma), Missaile Raymond Musa (Manyara), Christopher Derek Kadio (Mwanza) na Prof. Riziki Silas Shemdoe (Ruvuma).

Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa ni Dkt. Jim James Yonazi (Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano {Mawasiliano}) na Edwin Paul Mhede (Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji).

Akizungumza baada ya kuwaapisha Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa katika maeneo waliyopangiwa kwa kushirikiana na viongozi na wafanyakazi wengine waliopo katika maeneo hayo.

Mhe. Rais Magufuli amesema amechukua muda mrefu kufanya uteuzi wa viongozi hao pamoja na Wakuu wa Wilaya ambao wanaapishwa na Wakuu wa Mikoa katika mikoa waliyopangiwa, ili kujiridhisha juu ya uwezo wao na kwamba anaamini aliowateua watafanya kazi ya kutatua kero za wananchi na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenda kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na ameelezea kutoridhishwa na ukusanyaji wa kiwango cha chini wa mapato hasa katika Majiji ya Dar es Salaam na Mbeya ambayo yana vyanzo vingi na vikubwa lakini yanakusanya kiasi kidogo huku yakizidiwa na Jiji jipya la Dodoma.

“Mkuu wa Mkoa wewe ndio Rais wa mkoa huo, sasa mkoa wako unapokuwa haukusanyi mapato huwa najiuliza sana kuna sababu gani ya kuendelea na Mkuu wa Mkoa ambaye hasimamii ukusanyaji wa mapato?” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amewaonya viongozi wa mikoa wasiokuwa na uhusiano mzuri miongoni mwao na amewataka viongozi hao kuwajibika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mapema kabla ya hotuba ya Mhe. Rais, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya uteuzi wa viongozi hao na wamewataka viongozi hao kuzingatia viapo vyao, kujifunza kwa umakini yaliyopo katika ofisi zao na kusimamia kwa tija shughuli za Serikali.

Viongozi walioapishwa na Mhe. Rais Magufuli pia wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

01 Agosti, 2018
 
Last edited by a moderator:
Hebu tumsubiri Mkulu tuone Leo atatema cheche gani??

Usije shangaa akaleta "nitaanzai kupiga shangazi zao" part 2
 
Ngoja tusubiri mipasho
Maana kwenye haya mambo ndo huwa anaona pakutolea Upepo wake
Ndiyo njia bora ya Rais kuongea na umma wa Watanzania kwani ujumbe unakuwa mahususi kwa mazingira ya wakati huo badala ya Rais kukaa na mapovu muda mrefu eti anasubiri hotuba ya mwisho wa mwezi.
 
Rais John Pombe Magufuli amesema yeye kuchaguliwa kuwa Rais siyo kwa kuwa yeye ni mzuri sana kuliko Watanzania wote bali ni Mungu ndiye aliyeamua. Hivyo akawaasa Viongozi hao kuwa katika nafasi zao, ni Mungu ndiye aliyeamua kuwapa nafasi zao ili kuwatumikia Watanzania.
 

MaCCM muacheni Magu ateue wapinzani,ndio anawaamini maana nyie ni wanafiki mno.

Hivi CCM mliomtukana Kafulila mnajisikiaje rais akimsifu?
 
Rais Magufuli amewauliza wanaodai kuwa, ameteua Wapinzani, mbona katika makatibu wakuu 13 ni mmoja David Kafulila pekee aliyetoka upinzani?
 
Hivi ni sawa kumtoa Mkuu intelijensia ya jeshi (MI) kumfanya Mkuu wa Mkoa?

Halafu kutoa na siri kuwa alikuwa Mkuu wa Military Intelligency si kunaweza kumfanya awe target ukizingatia anaenda mpakani
 
Last edited:
Rais Magufuli amewaonya Wakuu wa Mikoa watakaokuwa wakijidai kuwa wako neutral katika utendaji kazi wa majukumu yao kwa kuwa yeye ni CCM, Makamu wa Rais ni CCM na Waziri Mkuu pia ni CCM.
 
Back
Top Bottom