IKULU, Rais Magufuli akutana na Wakuu wa Mikoa na kuwaagiza wagawe mashamba yasiyoendelezwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na wakuu wa mikoa wote nchini,, kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, leo Jumanne Juni 13.

Katika kikao hicho pia Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan, naye alihudhuria pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi John Kijazi na baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.

Rais amewapa maagizo wakuu wa mikoa kukamata mashamba ambayo hayajaendelezwa na kuyagawa kwa wananchi

View attachment 523342

View attachment 523346

View attachment 523345
Ila Mama Samia Suluhu atakuwa na wakati mgumu sana kwa staili ya uongozi wa huyu jamaa. Maana amemfanya kama msaidizi wake anampangia ratiba kila siku. Hivi huyu mama kuna siku anaweza kujipangia majukumu yake ya kiofisi kweli? Au ndo namna ya kumfanya asifurukute? Kazi za raisi kila siku???
 
Hawa wakuu Wa mikoa waanze kuamsha moto wa maendeleo kwenye mikoa yao. Kuna mikoa tajiri lakini umaskini wa kutupwa. Mazao ya biashara na chakula hayawasaidii wananchi. Siasa n.a. maendeleo
 
Kumbe hata ikulu wanatumia notebooks za kawaida kama zetu huku uswahilini?? Af sijaziona vizuri hzo bites, sijui itakua ni korosho vile, maana zinanywewa na maji
 
Kugawa shamba ni jambo moja ila kuliendeleza ndio shughuli. Maeneo yenye mashamba wangepeleka matractor hapo ingekuwa poa sana. Ni jambo jema lakini tujiulize mbona watu wanakimbia huko mashambani wanakwenda mijini huku wakiacha mashamba? Sera ya kilimo ni mbovu ndio maana watu wanakimbia kilimo.
 
Ila Mama Samia Suluhu atakuwa na wakati mgumu sana kwa staili ya uongozi wa huyu jamaa. Maana amemfanya kama msaidizi wake anampangia ratiba kila siku. Hivi huyu mama kuna siku anaweza kujipangia majukumu yake ya kiofisi kweli? Au ndo namna ya kumfanya asifurukute? Kazi za raisi kila siku???
Makamu wa rais kwa Tanzania kwani ana nguvu gani?mimi naona ni cheo cha kufutwa tu, tuna waziri mkuu
 
naomba mwenyenamba za mrisho gambo kunamishamba pale Meru inarutuba na maji télé imeshikwa na wazungu mikataba ya miaka 99 na ushee...
mi naomba ka hekari pale Doli estate kabla hawajajenga vibanda kuzuga kuwa wanayaendeleza
 
Yaleyaleee, ya operesheni vijiji na baadaye hujumu uchumi. Kukamata na kugawa ardhi kwa mwingine unaweza kuwa na nia nzuri lakini utekelezaji wake utaleta shida na kubwa sana. Nini maana ya kutoyaendeleza? Ni kipindi gani hilo shamba litahesabika kama halijaendelezwa? Je huyo mtu atakaepewa naye asipoliendeleza in another next period nini kitafuata? Wananchi hasa vijijini waliorithi maeneo yao enzi na enzi wameshirikishwa kwa kiasi gani? Hili jambo kama lisipowekewa mfumo mzuri litakuja kuleta migogoro isiyomithilika katika histoia.
 
Wahimizwe kuzingatia sheria ktk kuyapokonya hayo madhamba maana ma-RC wengine mihemuko mingi.

Kumpokonya umiliki mtu mwenye umiliki halali lakini aliyetelekeza ama kushindwa kuendelezwa eneo lake kuna utaratibu wa kufuata unaoelekezwa na sheria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom