IKULU, Rais Magufuli akutana na Wakuu wa Mikoa na kuwaagiza wagawe mashamba yasiyoendelezwa

what will happen if ardhi yote itagawanywa kwa watu bila kubakiza reserve ya ardhi? Future generation itaishi wapi...vp kuhusu mipango ya baadae ya serikali.
 
Kama ni kweli kasema hayo maneno basi asiwe anamtaja Mungu maana afanyayo hajatumwa na Mungu labda mungu
 
Mmhhh, haya mazingaombwe mengine. Inawezekana mkuu anajiweka karibu na masikini walio wengi ili hata akiharibu kwa wale watu ambao wanatumia bongo zao kufikiria upande wa pili wa shilingi wasiweze kugonga ngome yake kwani tayari kajenga ukuta wa waliowengi na waliozibwa masikio na kiongozi wao mkuu. Hapa nakumbuka neno lile kuwa watakuja kwa ngozi ya kondoo ilihali kwandani ni wanyama mwitu. Mfano wake ni Pablo Escobar, Idi Amin nk nk nk.
 
Hao ambao wengine hata kusoma hawajui, inabidi wakae wanarudia haya maneno vizuri "lakini fanyeni jambo hili kwa kufuata utaratibu" maana hawa jamaa kwa kukurupuka, wanaweza anza kunyang'anya ovyo tu hadi kwa watu ambao hawana makosa.
 
Bashite aonyeshe cheti, hatujasahau kabisa.Juhudi zake za makinikia zitakua na mashiko Bashite atakapoonyesha vyeti vyake.
waliokuwa na phd wameisaidia nini hii nchi! hebu muacheni bashite apige kazi, kipaji cha uongozi anacho, kuliko hao mnaowaita wasomi wa vyeti!
 
Chonde chonde wasije wakakamata vieka kamoja tuwili eti nayo ni mashamba, wataumiza watu, na watu watajenga chuki dhidi ya serikali iwapo zoezi hilo litafanyika kimabavu na kiuonevu!.

Wajue tu kwamba hali ya maisha imebana kidogo ndiyo maana watu hawaendelezi lakini watu wanahitaji mashamba yao, hatuwezi kuibadiri jamii kwa haraka, twende taratibu!!!!
 
Lengo kuu lilikuwa ni Kupokonya Mashamba ya kamanda wa Mbowe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom