Ikulu na Rais Kikwete: Wanaingiaje Skendo ya Msanii Davido?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Juzi (Jumapili), Novemba 16, mwaka huu, niliandika makala nikichambua maeneo mbalimbali yenye mshangao kuhusiana na ukimya uliopo baada ya Davido kuja Tanzania, kupanda jukwaa la Fiesta 2014 kinyume na zuio la Baraza la Sanaa la Taifa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Unaweza Kuisoma Hapa;
Davido 'kapafom' na Kuondoka: BASATA, Mahakama Kimya

BASATA liliinyima kibali Prime Time Promotion cha kumtumia Davido kwenye Fiesta 2014. Vilevile Mahakama ya Kisutu ilitoa Amri ya Zuio (Court Injunction Order), ikikataza Davido kutumika kwenye Tamasha la Fiesta 2014. Maagizo ya mamlaka hizo hayakufua dafu, Davido alipanda jukwaani, akafanya kazi yake na kuondoka.

Baada ya mwezi mmoja kupita, ndipo nikaandika kuhoji kwa nini ukimya umetamalaki katika suala la Davido? Basata hawana nguvu? Mahakama ya Kisutu makali yake yamekwenda wapi? Na je, tunaona sawa Davido kwenda kwao Nigeria kuwasimulia Wanigeria wenzake kwamba mamlaka za nchi yetu zipo mikononi mwa watu?

Nasisitiza, suala la Davido kupanda jukwaani pamoja na makatazo yote siyo tu kwamba ni aibu kwa sanaa ya Tanzania, bali pia ni matusi makubwa dhidi ya Basata na Mahakama. Basata kimya, Mahakama ya Kisutu imenyamaza, wanahabari hatuandiki chochote, mwezi mzima ukapita, nikashangaa!

Kilichonirejesha leo ni baada ya kuona watu wengi wakiitaja Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete katika sakata la Davido. Leo tujadili, kwa nini Ikulu, kwa nini Rais Kikwete? Ukizingatia katika makala yangu kuhusu Davido na ukimya wa Basata na Mahakama, nilieleza kuwa yapo madai kwamba kuna wakubwa wanawalinda wahusika.

Nitangulie kumtakia nafuu ya haraka Dk. Kikwete ambaye yupo nchini Marekani kwenye matibabu. Bila shaka atarudi akiwa mzima kabisa aweze kumalizia ngwe yake. Binafsi kutoka moyoni, namkubali sana JK kwa mambo mengi. Mwakani atakapokuwa anakabidhi kijiti, ataondoka na rekodi ya kuwa rais aliyetekeleza miradi mingi ya maendeleo kuwahi kutokea.

Kwa vile namkubali, inaniuma sana kuona anachafuliwa na skendo zinazodhalilisha nchi. Hivi ni kweli JK anaweza kuweka sahihi mamlaka za nchi zivunjwe na kudhalilishwa? Mbona siamini! Watu wanapoitaja Ikulu wanamaanisha nini katika suala hili?

Je, ni nani Ikulu anayempenda sana Davido kiasi kwamba akaruhusu Basata lidhalilishwe? Maana kama ni JK, mbona hata siku ile Leaders Club hakwenda kuangalia shoo? Sasa Basata imedhalilishwa kwa masilahi ya nani? Mahakama imepuuzwa kwa ulinzi wa nani? Inatupasa kama taifa tujue!

Yapo maelezo kuwa JK na menejimenti ya Prime Time Promotion ni damdamu. Uswahiba haukatazwi, maana siwezi kujua wala kujadili walipotokea. Ila kwa hili la Davido, naamini watakuwa wanamsingizia, Rais wa Nchi hawezi kuruhusu mamlaka zake zivunjwe.

Kama kweli ni marafiki na wanatumia kiburi cha Ikulu, hapa pia ninalo swali; Prime Time wanawezaje kuhatarisha uswahiba wao na JK kwa kuvunja mamlaka za nchi? Maana kudharau Basata na Mahakama ni sawa na kumsaliti JK. Na kama kweli ni marafiki, basi wanasaliti pia urafiki wao.

Mzalendo wa kweli wa nchi hii, anayeamini kwamba maisha bora yanapatikana ukiishi kama raia mwema, huwezi kuchekelea kuvunja mamlaka za nchi. Prime Time walitoa wapi kiburi cha kukaidi katazo la Basata pamoja na Amri ya Zuio la Mahakama ya Kisutu?

Davido ni nani hasa mpaka wewe Mtanzania ukubali kudhalilisha mamlaka za nchi yako kwa kumpandisha jukwaani kinyume na katazo la Basata na Amri ya Zuio la Mahakama ya Kisutu? Kulikuwa kuna ulazima gani wa kumtumia ikiwa chombo kinachohusika na usimamizi wa sanaa kwa jumla nchini kimekataza? Chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki kimezuia?

Je, ni ubabe? Hapa pia siamini, yaani waliovunja sheria wana nguvu kuliko Basata (chombo cha serikali) na mahakama (mhimili huru namba tatu wa dola). Kama haya siyo sahihi, kwa nini hatua hazijachukuliwa mpaka leo. Au ndiyo ule msemo kuwa wanaokwenda jela wanaangaliwa kwanza usoni?

Mpaka hapo tuweke nukta kwamba Basata wana nguvu za kutosha ila hawajaamua kuzitumia. Mahakama kwa kawaida haichezewi, sijui kuna nini hapa? Au ndiyo upo ukweli kuwa kuna mkubwa anaagiza mambo yaachwe, huyo naye nani anayekuwa mtovu wa nidhamu kwa mamlaka halali za nchi yetu?

Hapa nikumbushe kuwa mtu ambaye anaruhusu uvunjaji wa misingi ya mamlaka za nchi, huyo ni adui mkubwa sana. Ni adui wa haki, maendeleo na amani yetu. Mataifa mengi yaliingia kwenye machafuko na damu ikamwagika kutokana na mamlaka za nchi zao kushindwa kutimiza wajibu.

Anayejiona amedhulumiwa au kuonewa naye anakuwa na akili ya pili. Kwa sababu tatizo linakuwa la kimfumo, husababisha wadhulumiwa na waonewa wawe wengi. Hali hiyo husababisha ujenzi wa kundi kubwa lisilokuwa na imani na mamlaka za nchi.

Watu ambao hawana imani na mamlaka za nchi hugawanyika katika makundi matatu . La kwanza, huishi kwa unyonge kwa kuamini kuwa hawana kitu cha kufanya kwa sababu walioshikilia mpini ni wazito na kwamba wao wakibisha makali yatawakata.

Kundi hili linaitwa "hewala" au "tutafanyaje". Maana huona hawana kitu cha kufanya kuwasaidia. Badala yake hujikunyata na kutamka "sasa tutafanyaje ikiwa wameshaamua" na wanapoambiwa hujibu "hewala", maana hawana cha kupinga. Hili ni kundi baya kwa maendeleo ya taifa japo halivunji amani. Hili ni kundi la wakata tamaa!

Kundi la pili ni lile ambalo huyatazama yatokeayo sasa kama muongozo wa namna ambavyo nao wanapaswa kuishi miaka ijayo. Mtu anakosa haki yake leo kwa sababu mamlaka za nchi zinamkandamiza, naye anajiapiza kuwa atalipa kisasi. Anaamua kutafuta fedha kwa bidii.

Mtu huyu akishafikia kiwango kizuri cha kiuchumi huanza kujipendekeza kwa wakubwa akitumia fedha zake. Anayetumia fedha kuwa karibu na viongozi hawezi kuwa raia mwema. Lengo lake la juu linakuwa ni kutafuta ulinzi katika kazi zake.

Ndiyo hao ambao wanavunja sheria, mamlaka zikitaka kuchukua hatua, wanapiga simu kwa mawaziri kuomba ulinzi. Viongozi ambao wananunuliwa na wafanyabiashara ni hatari mno. Kwanza wanakuwa hawajiheshimu, pia wao ni sababu ya mmomonyoko mkubwa wa maadili katika taifa letu. Ndiyo chanzo cha mamlaka za nchi kupuuzwa na kuvunjwa.

Hulka hii ilianza kwa wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Asia. Wao imani yao ni kwamba ukishawaweka viongozi mifukoni hakuna tatizo. Matokeo yake hata maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakitaka kuwakamata wanapobaini wanakwepa kodi, wanajikuta wanafungwa ‘pingu' na simu za viongozi.

Tabia hiyo imesababisha viongozi wengi wenye nafasi katika mamlaka za umma, hasa mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi, makamishna na kadhalika, kuona ni haki yao kupokea bahasha za takrima kutoka kwa wafanyabiashara na malipo yake ni kumsaidia mfanyabiashara husika anapoingia kwenye matatizo ya kisheria.

Hiyo tabia, imerithiwa na wafanyabiashara wenye weusi asilia. Nao wakipata visenti vyao wananunua viongozi taratibu. Hajaombwa msaada katoa. Siku naye akipata matatizo ya kisheria, anapiga simu tu kwa mkubwa mmoja, mambo yanaisha haraka.

Unakutana na mtu anamtishia yule anayefanya kazi yake kwa kumwambia "kaa mbali na mimi nitakupoteza!" Kumbe ukifanya kazi yako vizuri unapotezwa na wafanyabiashara watoa rushwa kwa msaada wa viongozi wa juu wala rushwa.

Mfanyabiashara wa aina hiyo anaweza kufanya chochote kwa kiburi kwamba ana fedha, vilevile viongozi walio mamlakani wanamuona na wanamlinda. Akitaka kitu lazima kifanyike, hata kama sheria inatakaza atalazimisha. Atavunja sheria na atakumbatiwa! Taifa linaingia kwenye dhoruba taratibu!

Kundi la tatu ni lile la watu wasio na uvumilivu, ambao wakishaona wanaonewa wanakuwa hawana cha kufanya zaidi ya kuwa wakaidi kwa mamlaka za nchi, tena ni rahisi kwao kuchukua sheria mkononi. Mara nyingi hawa hutazamwa kwa vitendo vya baadaye, hawafikiriwi kwa walivyoumizwa kabla.

Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema; mlango wa uhuru unapokuwa umefungwa, halafu walinzi wa mlango hawataki kufungua, hapo kinachobaki ni kwa wanaotaka uhuru kuamua ama kuendelea kukosa uhuru wao au kuvunja mlango ili wapate uhuru wao.

Watu wanaona wanaonewa na mamlaka za nchi hazioneshi utayari wa kukomesha uonevu huo, unatarajia waonewa wasio na subira wafanye nini kama siyo kuvunja sheria za nchi waziwazi? Kwa maana hiyo tukubali kwamba mamlaka za nchi zinaposhindwa kutenda kazi yake ipasavyo zinakuwa zinaweka rehani amani yetu.

Nini matarajio ya wasanii kama Basata linapuuzwa na kudharauliwa kwa kiwango ambacho Prime Time wamefanya kwa Davido. Mtanzania wa kawaida anaitazama vipi Mahakama leo kama Amri ya Zuio la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipuuzwa na hakuna hatua iliyochukuliwa?

Ni mkubwa gani katika nchi hii mwenye nguvu kuliko mahakama? Je, ndiye huyo ambaye anazuia rungu stahiki lisiwabutue wahusika? Kweli, hata Mahakama ya Kisutu ambayo ina rekodi ya kupeleka jela watu wazito, tena inaongoza kwa ‘unoko' leo imenyamaza na amri yake ya zuio!

MSISITIZO
: Makala haya na yaliyopita pamoja na maswali yangu, kesho nitawasilisha Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu (inijibu kuhusu kutajwa kwa JK katika skendo hii), vilevile BASATA, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamanaduni na Michezo.

Nitaendelea kuandika.

By Luqman Maloto
 
Tunahitaji waandishi wa namna hii tz wasio waoga kuhoji,wenye kushupalia mambo yanaotakwa kuzimwa
nitachangia haraka haraka maana nin dk chache,mi nadhani wewe kama mwandishi ungekamilisha uchunguzi wako kwa kwenda basata kuhoji iweje davido alitumbuiza wakati walimwekea pingamizi na pia mahakama ungefatilia ilikuwaje davido akadharau agizo lao?
tetesi za kuihusisha ikulu ni mapema mno,anzia basata na pia mahakamani ndio utajua nani alitoa maagizo.
Nasi wadau wa burudani tutafatilia kujua ilikuwaje,kama davido alikiuka maagizo ikibainika.Adhabu yake ni kupigwa marufuku kazi zake kupigwa nchini na apigwe marufuku kuja tz tena iwe fundisho kwa watu wa nnje wanaodhani watanzania tumelala.Umoja wa kitaifa unahitajika katika hili.
 
Duh Hii sasa nouma aiseeeee. haya ngoja nikae kimya
 
wewe unganisha hilo tukio na THT pamoja na clouds pia unganisha sugu na Ruge unganisha times fm na Gardener zidi ya clouds kisha toa jibu ndiyo utajua ukweli upo wapi wala hapaitaji uwe na shahada ya chuo kikuu.
 
Tatizo la nchi yetu kwa sasa ni kila jambo kuchukuliwa juu juu na rahisi, pia mtu au watu wanavunja sheria kwa kujiamini sana. Hatuna tena misingi ya kufuata sheria kwani inachukulia kama kitabu au muongozo wa mfano tu.
 
Ndo akili mgando za watanzania... sasa yeye vita ya wafanyabiashara inamuusu nini?

Aiseee wewe ndo mwenye akili mgando hapa..! Umesoma kulikuwa na zuio toka kwa Basata na mahakama vile vile.. Na tuhuma zinaigusa ikulu so lazima majibu yapatikane..
 
unalia lia lia nini unazunguka tu. we unamjua JK.aka ------, waulize walowahi kukatiza kwenye anga zake kama warioba, costa mahalu, lowasa, babu seya, unayoyahoji yanawezekana kabisa ni amri ya mkulu wa ofisi kuu, sisi tunaosoma uzi wako huu ndo tunakushangaa, labda nikukumbushe kidogo, JK aliwahi kuwasamehe wezi wa EPA akaamuru warudishe hela tu waendelee kupeta uswahilini, wengi hawajarudisha n tunao kitaa wanakula bata, sasa huyo sijui davido nonino hiyi issue ndogo sana, mwisho laujilaumu mwenyewe na nduguzu kuchagua chama cha majambazi na raisi wao hewa,
 
Skendo zote nchi hii umeona ya Davido tu ndio ikufanye uandike gazeti lote hilo!!! Yaani ikulu ishughulike na akina Davido kweli !!??? we utakuwa umetumwa au unafikiri kwa kutumia kichwa!!!
 
Luqman maloto ametumia weledi wa hali ya juu kufikisha ujumbe kwa watawala na watawaliwa wakata tamaa, nampa nyota 5 huyu mwandishi.
 
Juzi (Jumapili), Novemba 16, mwaka huu, niliandika makala nikichambua maeneo mbalimbali yenye mshangao kuhusiana na ukimya uliopo baada ya Davido kuja Tanzania, kupanda jukwaa la Fiesta 2014 kinyume na zuio la Baraza la Sanaa la Taifa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Unaweza Kuisoma Hapa;
Davido 'kapafom' na Kuondoka: BASATA, Mahakama Kimya

BASATA liliinyima kibali Prime Time Promotion cha kumtumia Davido kwenye Fiesta 2014. Vilevile Mahakama ya Kisutu ilitoa Amri ya Zuio (Court Injunction Order), ikikataza Davido kutumika kwenye Tamasha la Fiesta 2014. Maagizo ya mamlaka hizo hayakufua dafu, Davido alipanda jukwaani, akafanya kazi yake na kuondoka.

Baada ya mwezi mmoja kupita, ndipo nikaandika kuhoji kwa nini ukimya umetamalaki katika suala la Davido? Basata hawana nguvu? Mahakama ya Kisutu makali yake yamekwenda wapi? Na je, tunaona sawa Davido kwenda kwao Nigeria kuwasimulia Wanigeria wenzake kwamba mamlaka za nchi yetu zipo mikononi mwa watu?

Nasisitiza, suala la Davido kupanda jukwaani pamoja na makatazo yote siyo tu kwamba ni aibu kwa sanaa ya Tanzania, bali pia ni matusi makubwa dhidi ya Basata na Mahakama. Basata kimya, Mahakama ya Kisutu imenyamaza, wanahabari hatuandiki chochote, mwezi mzima ukapita, nikashangaa!

Kilichonirejesha leo ni baada ya kuona watu wengi wakiitaja Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete katika sakata la Davido. Leo tujadili, kwa nini Ikulu, kwa nini Rais Kikwete? Ukizingatia katika makala yangu kuhusu Davido na ukimya wa Basata na Mahakama, nilieleza kuwa yapo madai kwamba kuna wakubwa wanawalinda wahusika.

Nitangulie kumtakia nafuu ya haraka Dk. Kikwete ambaye yupo nchini Marekani kwenye matibabu. Bila shaka atarudi akiwa mzima kabisa aweze kumalizia ngwe yake. Binafsi kutoka moyoni, namkubali sana JK kwa mambo mengi. Mwakani atakapokuwa anakabidhi kijiti, ataondoka na rekodi ya kuwa rais aliyetekeleza miradi mingi ya maendeleo kuwahi kutokea.

Kwa vile namkubali, inaniuma sana kuona anachafuliwa na skendo zinazodhalilisha nchi. Hivi ni kweli JK anaweza kuweka sahihi mamlaka za nchi zivunjwe na kudhalilishwa? Mbona siamini! Watu wanapoitaja Ikulu wanamaanisha nini katika suala hili?

Je, ni nani Ikulu anayempenda sana Davido kiasi kwamba akaruhusu Basata lidhalilishwe? Maana kama ni JK, mbona hata siku ile Leaders Club hakwenda kuangalia shoo? Sasa Basata imedhalilishwa kwa masilahi ya nani? Mahakama imepuuzwa kwa ulinzi wa nani? Inatupasa kama taifa tujue!

Yapo maelezo kuwa JK na menejimenti ya Prime Time Promotion ni damdamu. Uswahiba haukatazwi, maana siwezi kujua wala kujadili walipotokea. Ila kwa hili la Davido, naamini watakuwa wanamsingizia, Rais wa Nchi hawezi kuruhusu mamlaka zake zivunjwe.

Kama kweli ni marafiki na wanatumia kiburi cha Ikulu, hapa pia ninalo swali; Prime Time wanawezaje kuhatarisha uswahiba wao na JK kwa kuvunja mamlaka za nchi? Maana kudharau Basata na Mahakama ni sawa na kumsaliti JK. Na kama kweli ni marafiki, basi wanasaliti pia urafiki wao.

Mzalendo wa kweli wa nchi hii, anayeamini kwamba maisha bora yanapatikana ukiishi kama raia mwema, huwezi kuchekelea kuvunja mamlaka za nchi. Prime Time walitoa wapi kiburi cha kukaidi katazo la Basata pamoja na Amri ya Zuio la Mahakama ya Kisutu?

Davido ni nani hasa mpaka wewe Mtanzania ukubali kudhalilisha mamlaka za nchi yako kwa kumpandisha jukwaani kinyume na katazo la Basata na Amri ya Zuio la Mahakama ya Kisutu? Kulikuwa kuna ulazima gani wa kumtumia ikiwa chombo kinachohusika na usimamizi wa sanaa kwa jumla nchini kimekataza? Chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki kimezuia?

Je, ni ubabe? Hapa pia siamini, yaani waliovunja sheria wana nguvu kuliko Basata (chombo cha serikali) na mahakama (mhimili huru namba tatu wa dola). Kama haya siyo sahihi, kwa nini hatua hazijachukuliwa mpaka leo. Au ndiyo ule msemo kuwa wanaokwenda jela wanaangaliwa kwanza usoni?

Mpaka hapo tuweke nukta kwamba Basata wana nguvu za kutosha ila hawajaamua kuzitumia. Mahakama kwa kawaida haichezewi, sijui kuna nini hapa? Au ndiyo upo ukweli kuwa kuna mkubwa anaagiza mambo yaachwe, huyo naye nani anayekuwa mtovu wa nidhamu kwa mamlaka halali za nchi yetu?

Hapa nikumbushe kuwa mtu ambaye anaruhusu uvunjaji wa misingi ya mamlaka za nchi, huyo ni adui mkubwa sana. Ni adui wa haki, maendeleo na amani yetu. Mataifa mengi yaliingia kwenye machafuko na damu ikamwagika kutokana na mamlaka za nchi zao kushindwa kutimiza wajibu.

Anayejiona amedhulumiwa au kuonewa naye anakuwa na akili ya pili. Kwa sababu tatizo linakuwa la kimfumo, husababisha wadhulumiwa na waonewa wawe wengi. Hali hiyo husababisha ujenzi wa kundi kubwa lisilokuwa na imani na mamlaka za nchi.

Watu ambao hawana imani na mamlaka za nchi hugawanyika katika makundi matatu . La kwanza, huishi kwa unyonge kwa kuamini kuwa hawana kitu cha kufanya kwa sababu walioshikilia mpini ni wazito na kwamba wao wakibisha makali yatawakata.

Kundi hili linaitwa “hewala” au “tutafanyaje”. Maana huona hawana kitu cha kufanya kuwasaidia. Badala yake hujikunyata na kutamka “sasa tutafanyaje ikiwa wameshaamua” na wanapoambiwa hujibu “hewala”, maana hawana cha kupinga. Hili ni kundi baya kwa maendeleo ya taifa japo halivunji amani. Hili ni kundi la wakata tamaa!

Kundi la pili ni lile ambalo huyatazama yatokeayo sasa kama muongozo wa namna ambavyo nao wanapaswa kuishi miaka ijayo. Mtu anakosa haki yake leo kwa sababu mamlaka za nchi zinamkandamiza, naye anajiapiza kuwa atalipa kisasi. Anaamua kutafuta fedha kwa bidii.

Mtu huyu akishafikia kiwango kizuri cha kiuchumi huanza kujipendekeza kwa wakubwa akitumia fedha zake. Anayetumia fedha kuwa karibu na viongozi hawezi kuwa raia mwema. Lengo lake la juu linakuwa ni kutafuta ulinzi katika kazi zake.

Ndiyo hao ambao wanavunja sheria, mamlaka zikitaka kuchukua hatua, wanapiga simu kwa mawaziri kuomba ulinzi. Viongozi ambao wananunuliwa na wafanyabiashara ni hatari mno. Kwanza wanakuwa hawajiheshimu, pia wao ni sababu ya mmomonyoko mkubwa wa maadili katika taifa letu. Ndiyo chanzo cha mamlaka za nchi kupuuzwa na kuvunjwa.

Hulka hii ilianza kwa wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Asia. Wao imani yao ni kwamba ukishawaweka viongozi mifukoni hakuna tatizo. Matokeo yake hata maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakitaka kuwakamata wanapobaini wanakwepa kodi, wanajikuta wanafungwa ‘pingu’ na simu za viongozi.

Tabia hiyo imesababisha viongozi wengi wenye nafasi katika mamlaka za umma, hasa mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi, makamishna na kadhalika, kuona ni haki yao kupokea bahasha za takrima kutoka kwa wafanyabiashara na malipo yake ni kumsaidia mfanyabiashara husika anapoingia kwenye matatizo ya kisheria.

Hiyo tabia, imerithiwa na wafanyabiashara wenye weusi asilia. Nao wakipata visenti vyao wananunua viongozi taratibu. Hajaombwa msaada katoa. Siku naye akipata matatizo ya kisheria, anapiga simu tu kwa mkubwa mmoja, mambo yanaisha haraka.

Unakutana na mtu anamtishia yule anayefanya kazi yake kwa kumwambia “kaa mbali na mimi nitakupoteza!” Kumbe ukifanya kazi yako vizuri unapotezwa na wafanyabiashara watoa rushwa kwa msaada wa viongozi wa juu wala rushwa.

Mfanyabiashara wa aina hiyo anaweza kufanya chochote kwa kiburi kwamba ana fedha, vilevile viongozi walio mamlakani wanamuona na wanamlinda. Akitaka kitu lazima kifanyike, hata kama sheria inatakaza atalazimisha. Atavunja sheria na atakumbatiwa! Taifa linaingia kwenye dhoruba taratibu!

Kundi la tatu ni lile la watu wasio na uvumilivu, ambao wakishaona wanaonewa wanakuwa hawana cha kufanya zaidi ya kuwa wakaidi kwa mamlaka za nchi, tena ni rahisi kwao kuchukua sheria mkononi. Mara nyingi hawa hutazamwa kwa vitendo vya baadaye, hawafikiriwi kwa walivyoumizwa kabla.

Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema; mlango wa uhuru unapokuwa umefungwa, halafu walinzi wa mlango hawataki kufungua, hapo kinachobaki ni kwa wanaotaka uhuru kuamua ama kuendelea kukosa uhuru wao au kuvunja mlango ili wapate uhuru wao.

Watu wanaona wanaonewa na mamlaka za nchi hazioneshi utayari wa kukomesha uonevu huo, unatarajia waonewa wasio na subira wafanye nini kama siyo kuvunja sheria za nchi waziwazi? Kwa maana hiyo tukubali kwamba mamlaka za nchi zinaposhindwa kutenda kazi yake ipasavyo zinakuwa zinaweka rehani amani yetu.

Nini matarajio ya wasanii kama Basata linapuuzwa na kudharauliwa kwa kiwango ambacho Prime Time wamefanya kwa Davido. Mtanzania wa kawaida anaitazama vipi Mahakama leo kama Amri ya Zuio la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipuuzwa na hakuna hatua iliyochukuliwa?

Ni mkubwa gani katika nchi hii mwenye nguvu kuliko mahakama? Je, ndiye huyo ambaye anazuia rungu stahiki lisiwabutue wahusika? Kweli, hata Mahakama ya Kisutu ambayo ina rekodi ya kupeleka jela watu wazito, tena inaongoza kwa ‘unoko’ leo imenyamaza na amri yake ya zuio!

MSISITIZO
: Makala haya na yaliyopita pamoja na maswali yangu, kesho nitawasilisha Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu (inijibu kuhusu kutajwa kwa JK katika skendo hii), vilevile BASATA, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamanaduni na Michezo.

Nitaendelea kuandika.

By Luqman Maloto

Mkuu hongera kwa kazi nzuri, usiishie hapo, naomba ufatilie ktk siku hiyohiyo pale leaders Diamond alivaa uniform za JWTZ, idara husika zikaanza mchakato na hatua za kumchukulia Diamond kwa kushirukiana na jeshi la polisi....je nini kilifuata?
 
Hizi tuhuma ni nzito sana tunahitaji ufafanuzi kutoka mahakama ya hakimu mkazi kisutu na pia Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu waje kufafanua hili jambo laa sivyo kutakua na kaufisadai kapo nyuma ya pazia
 
Mkuu hongera kwa kazi nzuri, usiishie hapo, naomba ufatilie ktk siku hiyohiyo pale leaders Diamond alivaa uniform za JWTZ, idara husika zikaanza mchakato na hatua za kumchukulia Diamond kwa kushirukiana na jeshi la polisi....je nini kilifuata?

Siku nyingine usirudie kucopy ligazeti lote unatusumbua wenye vitecno.
 
Acha kelele wewe! Nenda kashitaki Polisi.
 
Back
Top Bottom