Huyu dogo anajitahidi sana na akiendelea na hizi juhudi zake atafika mbali sana. Ila anapaswa either kufundishwa mambo fulani fulani ya jinsi unapokuwa maarufu unapaswa kuongea na kubehave au kupata mshauri mzuri zaidi kwenye team ya wapambe wake atakayekuwa anamuandaa before interviews. Mfano nilibahatika kuangalia moja ya clips za interview yake ya few days ago but kuna vitu viwili havikukaa vizuri na ni vema wapambe wake humu ndani wamshauri:
1. Kuweka mguu juu ya meza ya watu ya kioo (coffee table) wakati anakuwa interviewed; it was bad even though atazuga kuwa alikuwa free..
2. Kutangaza kuwa demu wake alitoa mimba mbili. Huu ni ujinga, huwezi kwenda kuongea mambo yenu ya ndani kwenye public tena kama msanii.. Si-support abortion but mtu anapaswa kufundishwa cha kuongea na kisicho cha kuongea kwenye public hasa unapokuwa una umaarufu fulani.. Yule binti ana wazazi, ndugu, na si ajabu sasa hivi mume au mchumba.. Kwa nchi za wenzetu ingekuwa jambo la kawaida, ila kwa tamaduni zetu sidhani kama sahihi hata kidogo...
Ni mtazamo tu...