Ikulu kuwafutia posho Wabunge!

Ikulu kuwafutia posho Wabunge!

Labda ataliongea pale atakapopata nafas ya kuzungumza na wazee
 
RAIS KIKWETE SWALA LA POSHO LISIZUNGUMZWE VICHOCHORONI KWENYE MI-FASIBUKU, TUNAHITAJI JUHUDI KWENDA MBELE ZAIDI NA KUPUNGUZA ZAIDI 'GHARAMA ZA UTAWALA' KWENYE BAJETI YA KILA WIZARA NA 'KUONGEZA ZAIDI BAJETI ZA MAENDELEAO' KUANZIA HAPO MWAKA WA FEDHA UJAO BUNGENI!

Kwa nini anapata kigugumizi kiasi hicho na kuanza kupitapita huko vichochoroni na taarifa nyeti kma hiyo.

Kusema tu kwa POSHO sasa basi peke yake haitoshi; tunahitaji suluhisho la kudumu juu ya ufujaji wa kodi zetu kupitia malipo yote holela nchini.

Kila siku tunaona BAJETI ya gharama za utawala zikiwa ni kubwa mno kuliko fedha zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo.

This time around, macho yote Dodoma kupembua kila wizara inavyojipanga na bajeti yake; tutapenda sana kujua kwamba jumla ya FEDHA ZA MAENDELEO ni kiasi gani ukilinganisha na zile zitakazopangwa kama gharama ya utawala.
 
TANAPA tena!!!!!!! imekuwaje kikwete ameona TANAPA kabla wabunge hawajaliona hilo a TANAPA. Because TANAPA=BUNGE

Ni pale amabpo anayetakiwa kuwa mlinzi anapoanza kuwa mdokozi. atawazuiaje wadokozi wengine......

Je kamati ya Bunge inayohusika na maliasili iko wapi imjibu Kikwete kuhusu TANAPA. AU hawalijui hilo lol hizi movie si mchezo.
 
Labda umeanza na TANAPA

Hahaha, never trust a smiling face!
Kama kawa kama dawa! Hongera facebook!
 
Kwa nini rais asiandike waraka wa kusitisha posho rasmi badala ya kulalamika kwenye social media kama mwanachi wa kawaida? Anakumbuka ni kitu gani kimeandikwa kwenye ule mpango wa maendeleo wa taifa aliuzindua kwa mbwembwe Dodoma? Ashindwe kusamamia chama hata hili la posho nalo?
 
Hizi ni SIHASA za Tanzania, mambo muhimu hayapewi umuhimu. yasiyo ya muhimu ndo anayavalia njuga
 
Kumbuka mkuu hilo ni changa la macho ndio maana mh amelizungumzia vichochoroni na kwake hilo si tatizo kwani amelipitisha ndipo wakaanza kupeana tangu bunge lililopita.
 
Angalau AMESEMA! Atoke sasa ASIMAMIE HOJA yake! Safari tungependa aongee na waandishi wa Habari ama wahariri, ili wamwulize maswali. Aseme yooote yaliyomo moyoni mwake, yaani aende hatua moja mbele, zaii ya yale anayoandaliwa na Salva pamoja na January!
 
Thubutuuu
hilo sahau
Angalau AMESEMA! Atoke sasa ASIMAMIE HOJA yake! Safari tungependa aongee na waandishi wa Habari ama wahariri, ili wamwulize maswali. Aseme yooote yaliyomo moyoni mwake, yaani aende hatua moja mbele, zaii ya yale anayoandaliwa na Salva pamoja na January!
 
Kwa nini rais asiandike waraka wa kusitisha posho rasmi badala ya kulalamika kwenye social media kama mwanachi wa kawaida? Anakumbuka ni kitu gani kimeandikwa kwenye ule mpango wa maendeleo wa taifa aliuzindua kwa mbwembwe Dodoma? Ashindwe kusamamia chama hata hili la posho nalo?
Mwacheni mwenzenu anaogopa ivoo
 
yeye analipwa tsh ngapi? Aweke wazi marupurupu yake hapa.. ..wabunge nao vipi? Anawasainia lini?
 
Hana Jipya kwanini asitoe kauli kwenye vyombo vya Habari.
 
Wabunge wanaonewa bureee! Vikao kama tender boards kwenye taasisi za umma wajumbe hulipwa posho ya laki 2 per sitting ndani masaa yasiyozidi 4. Vikao vya board za wakurugenzi za mashirika wajumbe hulipwa kuanzia laki 4 na kuendelea. Vikao vingine vyote katika taasisi za umma wajumbe hulipwa kati ya elfu 50000 hadi laki 2 kutegemeana na uwezo wa taasisi. Semina, workshops, trainings etc zote wahusika hujilipa kati ya 50000 hadi laki 2. Sijui kwa nini tunakomalia posho za wabunge tu
 
Back
Top Bottom