Wabunge wanaonewa bureee! Vikao kama tender boards kwenye taasisi za umma wajumbe hulipwa posho ya laki 2 per sitting ndani masaa yasiyozidi 4. Vikao vya board za wakurugenzi za mashirika wajumbe hulipwa kuanzia laki 4 na kuendelea. Vikao vingine vyote katika taasisi za umma wajumbe hulipwa kati ya elfu 50000 hadi laki 2 kutegemeana na uwezo wa taasisi. Semina, workshops, trainings etc zote wahusika hujilipa kati ya 50000 hadi laki 2. Sijui kwa nini tunakomalia posho za wabunge tu
Kwenye ukurasa wake wa fb rais Kikwete amekemea matumizi ya posho kwenye taasis za umma,ametolea mfano TANAPA
Wabunge wanaonewa bureee! Vikao kama tender boards kwenye taasisi za umma wajumbe hulipwa posho ya laki 2 per sitting ndani masaa yasiyozidi 4. Vikao vya board za wakurugenzi za mashirika wajumbe hulipwa kuanzia laki 4 na kuendelea. Vikao vingine vyote katika taasisi za umma wajumbe hulipwa kati ya elfu 50000 hadi laki 2 kutegemeana na uwezo wa taasisi. Semina, workshops, trainings etc zote wahusika hujilipa kati ya 50000 hadi laki 2. Sijui kwa nini tunakomalia posho za wabunge tu
Hoja imepotoshwa. JK alitoa changamoto kwa TANAPA kutangaza vivutio vya Utalii wa Tanzania hadi Far East na kutobaki maofisini (nchini) wakigawana Posho. Kwa maoni yangu hakutoa kauli ya maana ya kupinga posho hizo na wala hakugusa kiivo Taasisi za Umma, ameisaidia TANAPA kubaini maeneo mengine ya posho (kwa ruksa ya Rais mwenyewe). Kwani ziara za kutangaza vivutio nje ya nchi hufanyika bila watu kulipwa posho?
muoga ni muoga tu.......
Mbona asijitambulishe huku JF na kutoa hayo maona yake huku?
Rais tumempa mamlaka atekeleze mambo, nasikitika nae analalamika sasa nani atatenda?. Soma hapa kwenye FB yake
![]()
Hatuwezi kuvumilia kuona taasisi za umma zikitumia mamilioni ya fedha kwa ajili tu ya posho kwa watumishi wake. Taasisi hizi kwa mfano Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambazo ni mali ya umma zinapaswa kutumia fedha hizi kwa ajili ya kukuza na kujiboresha zenyewe na sekta husika zaidi na zaidi na si vingineyo.