Ikulu ifafanue: Safari za nje zilizofadhiliwa kwa kila gharama nazo marufuku?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Tunahitaji ufafanuzi wa Ikulu ili mambo yote yafanyike kwa utaratibu mzuri badala ya mikurupuko ya amri na utekelezaji usio na lojiki.

Kumekuwa na mkanganyiko katika ofisi za serikali na taasisi za umma juu ya kusafiri nje. Kila ombi la kusafiri nje sasa linakataliwa kwa sababu kwamba rais Magufuli kapiga marufuku wafanyakazi kusafiri nje ya nchi. Wakuu makazini hawakubali kuipitisha safari hata zile zilizofadhiliwa (full sponsored trips) kwa kuogopa Magufuli atawatumbua majipu!

Katika hali hii, ni vema Ikilu wakatoa ufafanuzi. Je, marufuku ya safari za nje, kama lengo ni kubana gharama za serikali, yanahusu pia safari zilizofadhiliwa kwa kila gharama ya safari? Na kama safari hizo hazihusiki, nazo zinahitai kibali cha ikulu ili mfanyakazi aweze kusafiri?

Waandishi wa habari tunaomba msaada katika kufikisha ujumbe huu Ikulu.
 
Lazima mtumbuliwe tu kwani mnasafiri kwenda nje ya nchi
kama vile nchi yenu ina waka moto ...
 
Kaa chini ufanye kazi!!!! Katibu mkuu kiongozi alishatoa utaratibu wa kufwatwa ii upate kibali

Kwanza kiongozi wa taasisi, anapitia akiona unastahili kusafiri, anapeleka kwa msajili hazina, akiridhika nae ana foward ikulu?

Na logically hata kama una lipiwa ukiondoka ofisi wafunga ka,i zetu hazifanyiki? Una sababu gani ya kwenda??

Ila kasome tena taarifa ya katibu mkuu kiongozi ilieleza vizuri sana
 
Ikulu ilifafanua kuwa, safari za nje kwa watumishi wa umma zitaruhusiwa iwapo ikulu itajiridhisha kuwa kwa safari hiyo kuna manufaa kwa taifa! Hata kwa sponsorship ni lazima ujulikane safari hiyo inamanufaa kwa taifa maana pindi mtumishi wa umma akisafiri nje pasipo manufaa ya taifa kazi za mtumishi huyo nchini zitafanywa na nani wakati mtumishi huyo analipwa kwa kazi hiyo! Kwa hiyo mtumishi wa umma atasafiri nje kwa manufaa ya taifa mkuu!
 
Kaa chini ufanye kazi!!!! Katibu mkuu kiongozi alishatoa utaratibu wa kufwatwa ii upate kibali

Kwanza kiongozi wa taasisi, anapitia akiona unastahili kusafiri, anapeleka kwa msajili hazina, akiridhika nae ana foward ikulu?

Na logically hata kama una lipiwa ukiondoka ofisi wafunga ka,i zetu hazifanyiki? Una sababu gani ya kwenda??

Ila kasome tena taarifa ya katibu mkuu kiongozi ilieleza vizuri sana

Wallahi tena unatumia kinywaji gani mpwa ...utokapo kazini agiza mie nitalipia
 
mi niko hapa tunduma ndo nimeajiliwa...Je nikikatiza mpaka nikaenda Zambia mara moja nayo inaweza kuwa kesi?!
 
Hili lilishajadiliwa kwa kina hapa (tafuta thread) na kuna watu wakapuuza sasa moto ushaanza kuwawakia miguuni.
 
Watendaji wakuu hawana maamuzi ya mwisho kwenye safari ya mwajiriwa, jukumu lao ni kujaza part yao kwenye fomu vile wanaona inafaa na kuhakikisha fomu ya mwajiriwa ya kuomba idhini ya safari inafika Ikulu. Katibu mkuu kiongozi ndio ataamua uende au usiende.
 
Kaeni nchini muwahudumie wananchi, mnapoteza muda kwa safari zisizo na tija, zinawanufaisha binafsi tu
 
Hapa si rahisi kupata jibu. Humu wamejaa watu wasio watumishi wa umma na wana wivu kweli kweli. Swali lina mantiki lakini utaona yanavyokuja kujibu majitu yaliyoajiriwa kwa wahindi. Kuna safari nyingi tu zina ufadhili wote kila mwaka kwa watumishi wa umma wa nchi za Africa na Asia. Hizo hazihitaji hela ya serikali, tena kuipata nafasi ilikuwa lazima Utumishi wakuidhinishe. Sasa tunawaachia Wakenya na Wanigeria wakaongezewe uwezo wa kiutendaji wakati sisi tunaziachia nafasi kwa kisingizio cha amri ya rais. Ni kupoteza opportunity za bure kabisa. Hao wenzetu wanaenda kuongezewa maarifa halafu wanakuja kukamata soko, wakati tungekuja kuwapa maujanja ndugu zetu nao wapambane nao kwenye sekta binafsi. Acheni hizo mlioajiriwa kwa wadosi
 
kaeni nchini muwahudumie wananchi, mnapoteza muda kwa safari zisizo na tija, zinawanufaisha binafsi tu
Sawa tu, tutakaa kukuhudumia. Lakini ukija tukakuambia system imeharibika, inasubiri mtaalamu aje kutoka South Africa, usilalamike na wewe uwe mpole tu. Kama una haraka zako ndo hivyo tena, sisi hatujajengewa uwezo, tusubiri waliotuletea teknolojia waje kutengeneza, sisi tuendelee kuwa operators. Tumezuiwa kwenda kujifunza nje ya nchi BURE
 
Hapa si rahisi kupata jibu. Humu wamejaa watu wasio watumishi wa umma na wana wivu kweli kweli. Swali lina mantiki lakini utaona yanavyokuja kujibu majitu yaliyoajiriwa kwa wahindi. Kuna safari nyingi tu zina ufadhili wote kila mwaka kwa watumishi wa umma wa nchi za Africa na Asia. Hizo hazihitaji hela ya serikali, tena kuipata nafasi ilikuwa lazima Utumishi wakuidhinishe. Sasa tunawaachia Wakenya na Wanigeria wakaongezewe uwezo wa kiutendaji wakati sisi tunaziachia nafasi kwa kisingizio cha amri ya rais. Ni kupoteza opportunity za bure kabisa. Hao wenzetu wanaenda kuongezewa maarifa halafu wanakuja kukamata soko, wakati tungekuja kuwapa maujanja ndugu zetu nao wapambane nao kwenye sekta binafsi. Acheni hizo mlioajiriwa kwa wadosi

Kwa kipindi chote ambacho mmekuwa mkienda taifa na wananchi wamefaidika na nini. Sasa tulieni muone zuoi hilo litakavyoleta tija.

Lakini mmeshaambiwa ukiomba ruhusa wataangalia tija ya safari hiyo kwa umma. Ukiona umezuiliwa basi ujue safari yako haina tija.
 
Sawa tu, tutakaa kukuhudumia. Lakini ukija tukakuambia system imeharibika, inasubiri mtaalamu aje kutoka South Africa, usilalamike na wewe uwe mpole tu. Kama una haraka zako ndo hivyo tena, sisi hatujajengewa uwezo, tusubiri waliotuletea teknolojia waje kutengeneza, sisi tuendelee kuwa operators. Tumezuiwa kwenda kujifunza nje ya nchi BURE

Mbona kwa kipindi hiki still wataalam wanatoka nje ?
 
Sawa tu, tutakaa kukuhudumia. Lakini ukija tukakuambia system imeharibika, inasubiri mtaalamu aje kutoka South Africa, usilalamike na wewe uwe mpole tu. Kama una haraka zako ndo hivyo tena, sisi hatujajengewa uwezo, tusubiri waliotuletea teknolojia waje kutengeneza, sisi tuendelee kuwa operators. Tumezuiwa kwenda kujifunza nje ya nchi BURE

Ninayofahamu kuna vyuo vya kukidhi haja hapa nchini, nendeni mkasome au agizeni hao wataalamu waje kuwafundisha hapa hapa. Gharama ya kuleta mtaalam mmoja au wawili ni nafuu kuliko kubeba lundo la watu kumi hadi ishirini kwenda nje.

Lakini mmeshaambiwa ukiomba kibali uinyeshe umuhimu wa safari yako ka taifa ili upewe kibali, sasa hapo tatizo liko wapi.

Kama mtu umashindwa presentation ya faida ya safari yako basi hata hicho unachoenda kujifunza hakitaingia kichwani maana uwezo wako utakuwa mdogo tu !
 
Back
Top Bottom