Ikulu ifafanue: Safari za nje zilizofadhiliwa kwa kila gharama nazo marufuku?

Mleta mada namshauri angeacha kabisa kufikiria safari,kina magufuli wana hasira,utaharobu kibarua,kama una mfadhili subiri wakati wa likizo ndipo usafiri
 
Ha ha ha ha,walimwita jk vasco dagama kwa kupinga safari,halafu wanaanza kulaumu safari za nje kufutwa,
mtakoma
 
Ikulu ilifafanua kuwa, safari za nje kwa watumishi wa umma zitaruhusiwa iwapo ikulu itajiridhisha kuwa kwa safari hiyo kuna manufaa kwa taifa! Hata kwa sponsorship ni lazima ujulikane safari hiyo inamanufaa kwa taifa maana pindi mtumishi wa umma akisafiri nje pasipo manufaa ya taifa kazi za mtumishi huyo nchini zitafanywa na nani wakati mtumishi huyo analipwa kwa kazi hiyo! Kwa hiyo mtumishi wa umma atasafiri nje kwa manufaa ya taifa mkuu!

Umeeleweka vizuri sana.
 
Umejibu vyema
 
Tatizo kubwa hapa ni kwamba; baada ya Mhe. Rais kukataza safari za nje ya nchi kwa kubana matumizi; sasa imekuwa deal kutafuta safari zenye ufadhili. Kama mtumishi wa Serikali unatakiwa ufanye kazi, na siyo kutafuta safari zenye ufadhili ili mradi tu, usafiri nje ya nchi na kuacha kazi zinadorora! "HAPA KAZI TU".
 
Tunahitaji ufafanuzi wa Ikulu ili mambo yote yafanyike kwa uratatibu mzuri badala ya mikurupuko ya amri na utekelezaji usio na lojiki. Kumekuwa na mkanganyiko katika ofisi za serikali na taasisi za umma juu ya kusafiri nje. Kila ombi la kusafiri nje sasa linakataliwa kwa sababu kwamba Raisi Magufuli kapiga marufuku wafanyakazi kusafiri nje ya nchi. Wakuu makazini hawkubali kuipitisha safari hata zile zilizofadhiriwa (full sponsored trips) kwa kuogopa Magufuli atawatumbua majipu!

Katika hali hii ni vema Ikilu wakatoa ufafanuzi. Je, marufuku ya safari za nje, kama lengo ni kubana gharama za serikali, yanahusu pia safari zilizofadhiriwa kwa kila gharama ya safari? Na kama safari hizo hazihusiki, nazo zinahitai kibali cha Ikulu ili mfanyakazi aweze kusafiri?

Waandishi wa habari tunaomba msaada katika kufikisha ujumbe huu Ikulu.

Safari za nje badala ya kuwatumikia watz??Ukienda huko mshahara unalipwa nusu??kama ni kwa manufaa ya umma kwa nini ung'ang'ane wakati umma wenyewe umeona haina manufaa!??Mie mwenyewe ni mdau wa katika tafiti mwanzo sikuelewa lakini sasa nimeelewa!Omba kibali utapewa tu ili mradi kuwe na hoja na umuhimu wa safari hata kama unajilipia mwenyewe labda kama uko likizo.
 
Safi sana nafikili ameelewa mmemjibu vzr kama bado amtafute Katibu mkuu kiongozi
 
Tatizo kubwa hapa ni kwamba; baada ya Mhe. Rais kukataza safari za nje ya nchi kwa kubana matumizi; sasa imekuwa deal kutafuta safari zenye ufadhili. Kama mtumishi wa Serikali unatakiwa ufanye kazi, na siyo kutafuta safari zenye ufadhili ili mradi tu, usafiri nje ya nchi na kuacha kazi zinadorora! "HAPA KAZI TU".
 
Naona serikali hii inakimbia majukumu yake na kuwatwisha watumishi mizigo hiyo. Na watumishi wakishindwa ama kuchoka kuibeba mizigo hiyi, atakayeumia ni lofa anayeshabikia game hii bila kujua madhara yake.
 
Sioni hoja ya mleta mada hapa...huko nje mbona wapo watumishi ambao wanaendelea kwenda.

Ishu hapa sio kutoka nje tu, ishu ni kwamba kuna tija yoyote kwa taifa kwa kutoka kwako nje ya nchi. Hilo ndilo la muhimu kuliko hata kubana matumizi kwenyewe.

Ila ukiona Ikulu wamekubania kutoka nje ujue tu kuwa, tathmini ya safari yako imeonyesha haina tija yoyote kwa taifa. Simple logic.

Sasa usipoelewa hili ujue kabisa uwezo wako wa akili ni mdogo na upo hapo ofisini kimakosa. Vilaza mmejazwa kwenye ofisi za umma ndio maana sekta ya umma inakosa ufanisi kulinganisha na sekta binafsi. So sad.
 
Naona serikali hii inakimbia majukumu yake na kuwatwisha watumishi mizigo hiyo. Na watumishi wakishindwa ama kuchoka kuibeba mizigo hiyi, atakayeumia ni lofa anayeshabikia game hii bila kujua madhara yake.

Ukishindwa kazi unatimuliwa tu...Wapo vijana kibao benchi wanasubiri hizo nafasi. By the way, watendaji ndio hawa hawa walikuwepo wakati wa Kikwete (mliuita utawala dhaifu)....Je, sekta ya umma ilikuwa na ufanisi gani zaidi ya kunyanyasa wananchi? Acha kuandika pumba hapa.
 
Hapa si rahisi kupata jibu. Humu wamejaa watu wasio watumishi wa umma na wana wivu kweli kweli. Swali lina mantiki lakini utaona yanavyokuja kujibu majitu yaliyoajiriwa kwa wahindi. Kuna safari nyingi tu zina ufadhili wote kila mwaka kwa watumishi wa umma wa nchi za Africa na Asia. Hizo hazihitaji hela ya serikali, tena kuipata nafasi ilikuwa lazima Utumishi wakuidhinishe. Sasa tunawaachia Wakenya na Wanigeria wakaongezewe uwezo wa kiutendaji wakati sisi tunaziachia nafasi kwa kisingizio cha amri ya rais. Ni kupoteza opportunity za bure kabisa. Hao wenzetu wanaenda kuongezewa maarifa halafu wanakuja kukamata soko, wakati tungekuja kuwapa maujanja ndugu zetu nao wapambane nao kwenye sekta binafsi. Acheni hizo mlioajiriwa kwa wadosi

Mkuu mf mimi, nna safari imefadhiliwa gharama zote na serikali yao, na nimejaza form za kuomba kibali kwa KM, nasubiria kibali na huku tarehe ya safari inakaribia, najiuliza itakuwaje km kibali sintapata mpk siku ya safari?
 
Bila shaka wewe una kichwa kigumu au una masikio mabovu...Serikali ilishatoa ufafanuzi kuwa safari yeyote nje ya nchi kwa mtumishi wa Umma lazima ipate kibali kutoka kwa katibu mkuu kiongozi haijalishi nani anaigharamia!
 
Acha uzembe dogo mbona maelezo yameshatolewa hapo juu? Hata kama ni full sponsored lazima serikali ijiridhishe kuwa safari ina tija kwa taifa
 
Bila shaka wewe una kichwa kigumu au una masikio mabovu...Serikali ilishatoa ufafanuzi kuwa safari yeyote nje ya nchi kwa mtumishi wa Umma lazima ipate kibali kutoka kwa katibu mkuu kiongozi haijalishi nani anaigharamia!

hawa ni wale wanataka kukwapua na kwenda kupotelea huko nchi za watu. kaa tu hiyo itapita tukishajiridhisha kuwa wote tunachapa kazi.

kuna watu wana ajira lakini hawajui wanafanya nini, ili mradi tu wako kazini
 
Kama wewe ni mtumishi wa umma utakapohitaji kwenda safari yeyote nje ya nchi lazima upate kibali. Hivyo hata kama utalipa gharama za safari wewe mwenyewe, bado utahitajika kupata kibali. Utapaje kibali? Mwajiri akuandikie barua ya ruhusa na kusema kwamba umeruhusiwa kwenda nje ya nchi na safari hiyo haitagharimiwa na serikali. Omba kibali na kuambatanisha barua ya mwajiri, basi utapata kibali. Bila kibali watu wa airport hawatakuruhusu, kwa sababu passport yako itaonesha wewe ni mwajiriwa wa serikali.

Watumishi wanaopata full sponsorship ya safari zao wanalipwa na mwajiri asilimia fulani ya stahili ya posho zao. Hivyo kuwa full sponsored sio kigezo kinachokubalika kusafiri bila kibali.
 
Mkuu mf mimi, nna safari imefadhiliwa gharama zote na serikali yao, na nimejaza form za kuomba kibali kwa KM, nasubiria kibali na huku tarehe ya safari inakaribia, najiuliza itakuwaje km kibali sintapata mpk siku ya safari?

Jiulize usipoenda tunapungukiwa nn.Mbona mmeruka sana toka shs 60 zinanunua dola moja hadi sasa tumefikia elfu mbili na ushee.Tija iko wapi.Magu watu huku wanalazimisha kuotesha majipu.Hawa usiwatumbue kwa wembe.Agiza sime nyingine toka masailand.
 
Back
Top Bottom