Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,277
- 4,683
Mnaomtegemea MboweIndependent thinkers hatukosekani!
Mnaomtegemea MboweIndependent thinkers hatukosekani!
kwa mawazo haya nitakwazwa sana na mtu atakaekujibu kwa kutanguliza neno "mkuu"..Ni vyema likatolewa tangazo na Tanesco kama wananunua umeme kutoka kwa local producer.
Sipingani nawewe lakini kuna vitu inabidi tuvifikirie kiundani sana kabla ya kuvichukulia maamuzi..
Newtons, Faraday, Galileo nk walikuwepo kipindi hicho dunia ikiwa haina uelekeo na hakuna teknolojia hivyo wao kanuni zao ndio zikaleta msingi wa kila kitu leo kwa maana ya Meli, Ndege, Rockets, submarines nk, Kifupi kwa sasa hakuna kitu utatengeneza bila kupitia kwenye hiyo misingi. Kinachofanyika duniani kwa sasa ni researches na technology invention zikitumika kanuni ambazo tayari zipo, Mchina akaja kwa kasi na kitu kinaitwa reverse engineering kwa maana ya copy and paste ili naye aingie kwenye soko.
Kama tumeamua kutengeneza hivi vitu lazima pia tujue sababu ni ipi hasa, tutengeneze tuuze au tutengeneze tutumie?
Kama kutengeneza kuuza tunamuuzia nani na soko likoje la bidhaa hiyo maana sokoni tayari wapo wengine, Je tutaweza kushindana kwenye ubora, ufanisi, bei na umadhubuti wa bidhaa yetu?
Kama tutaamua kutengeneza na kutumia wenyewe, Je itatulipa kiuchumi kwa maana ileile ya ufanisi, ubora, gharama za uendeshaji, umadhubuti nk..
Binafsi naamini kuendelea kupoteza muda kwenye hizi local inventions ni kama kuamua kuishi 1800 wakati dunia iko 2019 labda kama tumeamua kuanza mwanzo kujifunza, maana naamini tuko watanzania wengi wenye uwezo wa kudesign na kuendesha hizo local invetions kama Magari ya kienyeji, bunduki, Umeme wa kienyeji, Pombe za kienyeji, Ndege za kienyeji, Meli za kienyeji nk. SERIKALI IKITOA RUHUSU UTAONA MPAKA BUNDUKI ZA KIENYEJI HUKO URAIA, UMEME TUTANGENEZA WENYEWE HUKO URAIANI maana si kweli kutengeneza hivi vitu kunahitaji kipaji au akili sana everybody can do it locally tuwe wakweli..
Serikali iache kukimbia majukumu yake; uwekezaji mkubwa unahitajika kwenye technology ili vijana wengi waweze kuwa na uwezo kwenye ubunifu wa kweli utakaoendana na kasi ya sasa ya dunia ili hizo teknolojia zitakazogunduliwa ziweze kuleta tija kwenye jamii yote kuanzia kwetu hapa na duniani kwa ujumla.
kutengeneza kitu chochote kwa matumizi binafsi kwa maana ya nyumbani kwako changamoto inaweza kuwa ndogo au isiwepo kabisa, Lakini kitu hicho hicho kwa matumizi ya wengi hapo ndipo changamoto zinapoanza na utaalamu ndipo utaanza kuhitajika.. Kuzalisha maji au kufua umeme kutoka kwenye chanzo sio tatizo na maarifa hayo yapo kwa wengi tatizo linaaza pale utapohitaji kupeleka kwenye matumizi ya wengi maana mengi lazima yazingatiwe ili huduma hiyo isiwe namadhara.
Dalili ya dowans hiiHii iwe nafasi ya kuruhusu wazalishaji na wasambazaji binafsi wa umeme Nchini. Biashara bila upinzani hakuna mabadiriko..
Lumpen again!Mnaomtegemea Mbowe
jinga sana wewe na siasa zako mavi na kukosoa kila kitu....Magufuli huwa anapenda sana kukurupuka. Hapa alipaswa kuwatuma kwanza wataalamu wote wahusika wakakae na hao wagunduzi ilii wamletee concrete findings and opinions.
Hapa nao watu wanajikanyaga kanyaga tu kwa kushtukizwa bila hoja zenye msingi na msimamo.
Na Magufuli alivyo usishangae Akaondoka na Mtu hapa!
Acha dharau za kishamba, Kwani Faraday uliyemsoma na laws zake alikuwa na elimu gani? Hayo majenereta si yeye ndiye aliyeyagundua bila hata ya kujua surface integral ni nini?Sileti dharua kwa yeyeto.Napinga layman kujipendekeza ni mtaaalam wa energy systems. Usistajabu mapendekezo ya mashine inayozalisha umeme milele daima bila gharama yeyote-perpetual motion machine.
Heee, unasemaje mkuu. Wamebuni teknologia mpya kabisa, mbali ya hii iliyopo sasa?Ubunifu wa ku supersede technology ya kufua umeme iliyopo kwenye soko?
[/QUOTE]Kama tumeamua kutengeneza hivi vitu lazima pia tujue sababu ni ipi hasa, tutengeneze tuuze au tutengeneze tutumie?
Kama kutengeneza kuuza tunamuuzia nani na soko likoje la bidhaa hiyo maana sokoni tayari wapo wengine, Je tutaweza kushindana kwenye ubora, ufanisi, bei na umadhubuti wa bidhaa yetu?
Kama tutaamua kutengeneza na kutumia wenyewe, Je itatulipa kiuchumi kwa maana ileile ya ufanisi, ubora, gharama za uendeshaji, umadhubuti nk..
Binafsi naamini kuendelea kupoteza muda kwenye hizi local inventions ni kama kuamua kuishi 1800 wakati dunia iko 2019 labda kama tumeamua kuanza mwanzo kujifunza, maana naamini tuko watanzania wengi wenye uwezo wa kudesign na kuendesha hizo local invetions kama Magari ya kienyeji, bunduki, Umeme wa kienyeji, Pombe za kienyeji, Ndege za kienyeji, Meli za kienyeji nk. SERIKALI IKITOA RUHUSU UTAONA MPAKA BUNDUKI ZA KIENYEJI HUKO URAIA, UMEME TUTANGENEZA WENYEWE HUKO URAIANI maana si kweli kutengeneza hivi vitu kunahitaji kipaji au akili sana everybody can do it locally tuwe wakweli..
Serikali iache kukimbia majukumu yake; uwekezaji mkubwa unahitajika kwenye technology ili vijana wengi waweze kuwa na uwezo kwenye ubunifu wa kweli utakaoendana na kasi ya sasa ya dunia ili hizo teknolojia zitakazogunduliwa ziweze kuleta tija kwenye jamii yote kuanzia kwetu hapa na duniani kwa ujumla.
Tunajidharau kwa sababu hatujiheshimu.Tuache kujidharau
Ni vigumu kuelewa kwa nini ililazimu haya yafanyike, kwani yamewaondoa wengi waliotaka kuona haya mengine mazuri yakipewa nguvu zaidi. Wengine roho zilipinda moja kwa moja baada ya matukio hayo yaliyokuwa si ya lazima yafanyike.Ila Ben Saanane angeridishwa na waliompiga risasi Lissu kuchukuliwa hatua, mambo yangekuwa mswanu sana yani.
Rais Magufuli leo 13 Juni, 2019 anakutana na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito
Kuanzia saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es salaam
UPDATE
Rais Magufuli: Nilifikiri kuwa Mkurugenzi wa TANESCO pamoja na Katibu Mkuu wangekuwepo hapa kusikiliza shida zao. Hawa ni mafundi ndiyo maana hawazungumzi sana.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu
Hadi sasa jumla ya wabunifu 60 wameshatambuliwa na kuingizwa katika Kanzidata ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo
Tutawaendeleza wabunifu hawa wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kuwaongezea shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kuendeleza kazi zao
TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo
Rais Magufuli
Tatizo la Watanzania tunajidharau na hatuthamini vya kwetu, hawa wabunifu wa mitambo wangegunduliwa mapema wangepunguza gharama za uzalishaji umeme kwa sababu tayari wana chanzo cha umeme.
Wangekuwa wameshasaidiwa wasingefika hapa. Transfoma zingekuwepo, Mkurugenzi wa TANESCO kwao ni Njombe na nina uhakika huwa anaenda likizo huko lakini hajafanya lolote. Meneja wa TANESCO mkoa (Njombe) nimemsikia akizungumza hawa waje wanione kasha waende Ewura…yeye hakutaka shida.
Hata wangezalisha umeme ukaleta madhara shida isingekuwa kwa watendaji wa TANESCO kwa hiyo Mkurugenzi wa Njombe naye hajaleta taarifa yoyote kuhusiana na wagunduzi hawa tangu mwaka 1980.
Natoa siku saba kwa TANESCO kwenda katika eneo la mradi huo wa kufua umeme uliopo Mkoani Njombe na kuona ni namna gani utafanya kazi vizuri zaidi
Natoa wito kwa viongozi wote kuangalia Televisheni ya Taifa (TBC) ili kila kitakachoonyeshwa kuhusu wizara husika kikashughulikiwe kwa haraka.
Natoa shilingi Milioni Tano kwa wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili kuwaongezea mtaji katika shughuli zao.
Zaidi, soma;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Juni, 2019 amekutana na wabunifu wawili wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya mito kutoka Mkoani Njombe na kuagiza wataalamu wa wizara na taasisi zinazojihusisha na sayansi, teknolojia na uvumbuzi kuwafuatilia na wabunifu na wavumbuzi mbalimbali ili kuwaunga mkono katika kuboresha kazi zao.
Wabunifu waliokutana na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam ni John Akani Fute na Jairos Ngairo ambao wamebuni miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji yanayotiririka mtoni, kusukuma maji kwa kutumia pampu zisizotumia umeme na kusaga nafaka kwa kutumia machine zinazoendeshwa na maji ya mto. Bwana Fute amebuni mradi unaozalisha kilowati 28 na Bw. Ngairo anazalisha kilowati 15 za umeme.
Mkutano huo umewahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye pamoja na viongozi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wabunifu hao kwa kuzalisha umeme wa gharama nafuu unaowanufaisha wananchi na ameagiza TANESCO na COSTECH kuwaunga mkono ambapo TANESCO itatoa shilingi Milioni 30 na COSTECH shilingi Milioni 20 kwa wabunifu hao, na pia timu ya wataalamu itaondoka kesho kwenda Njombe ilipo miradi hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu na kuiboresha.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na vitendo vya wataalamu kuwakatisha tamaa na kuwatisha wabunifu wa vitu mbalimbali vinavyowasaidia wananchi kama ambavyo Bw. John Fute (Pwagu) na Bw. Jairos Ngairo wamekuwa wakifanyiwa na badala yake ametaka wabunifu hao waungwe mkono kwa ushauri wa kitaalamu na kuwawezesha kuongeza tija.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza TBC kwa kufuatilia kazi za ubunifu na uvumbuzi kupitia makala yake ya Hadubini (Habari kwa Kina) ikiwemo makala ya ubunifu wa mradi huo wa umeme iliyoandaliwa na waandishi wa Habari Bi. Tatu Abdallah na Bi. Zaituni Mkwama na ameagiza Wizara na Taasisi za Serikali kufuatilia taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari na kuchukua hatua katika maeneo yanayozihusu.
Ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuatilia jengo la ghorofa 3 linalodaiwa kutelekezwa na raia mmoja wa kigeni huko Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambalo limebaki mikononi mwa mlinzi ambaye anatishwa na wajanja wanaotaka kujimilikisha kwa nguvu. Taarifa hii pia ilitangazwa na TBC kupitia makala ya Hadubini.
“Nakupongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na wafanyakazi wa TBC kwa kazi nzuri mnayoifanya, angalau nyinyi mnathubutu kujituma hadi vijijini kufuatilia mambo haya muhimu kwa jamii, nataka wizara na taasisi ambazo zina wataalamu na wasomi ziigeni mfano huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wakizungumza katika mkutano huo, Bw. Fute na Bw. Ngairo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwapa shilingi Milioni 5 ikiwa ni kutambua ubunifu wao na wameahidi kwenda kuboresha zaidi kwa kushirikiana na wataalamu wa Serikali.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Juni, 2019
View attachment 1126395View attachment 1126396