Wasomi wengi wa nchi hii ni hovyo,huo ndio ukweli japo mchungu 😀.Level yako ya uelewa ndogo. Unaongea topic usiyojua hata basics essentials. Kapige domo vikao vya chama huko mtaelewana vizuri na dropouts wenzako.
Well said👍🏽👏🏽Vyuo vyetu vikuu havifanyi kazi inayotakiwa, watu wanafanya tafiti mbalimbali zinabaki kwenye makabati, kwanini wasomi wasifanye tafiti kulingana na mahitaji yetu ya ndani?
Hawa wenye Phd wengi wameingia kwenye siasa badala yake kutumia ujuzi wao kwenye kuliendeleza taifa mbele wao wamekuwa watu wa maslahi binafsi.
Rais Magufuli leo 13 Juni, 2019 anakutana na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito
Kuanzia saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es salaam
UPDATE
Rais Magufuli: Nilifikiri kuwa Mkurugenzi wa TANESCO pamoja na Katibu Mkuu wangekuwepo hapa kusikiliza shida zao. Hawa ni mafundi ndiyo maana hawazungumzi sana.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu
Hadi sasa jumla ya wabunifu 60 wameshatambuliwa na kuingizwa katika Kanzidata ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo
Tutawaendeleza wabunifu hawa wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kuwaongezea shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kuendeleza kazi zao
TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo
Rais Magufuli
Tatizo la Watanzania tunajidharau na hatuthamini vya kwetu, hawa wabunifu wa mitambo wangegunduliwa mapema wangepunguza gharama za uzalishaji umeme kwa sababu tayari wana chanzo cha umeme.
Wangekuwa wameshasaidiwa wasingefika hapa. Transfoma zingekuwepo, Mkurugenzi wa TANESCO kwao ni Njombe na nina uhakika huwa anaenda likizo huko lakini hajafanya lolote. Meneja wa TANESCO mkoa (Njombe) nimemsikia akizungumza hawa waje wanione kasha waende Ewura…yeye hakutaka shida.
Hata wangezalisha umeme ukaleta madhara shida isingekuwa kwa watendaji wa TANESCO kwa hiyo Mkurugenzi wa Njombe naye hajaleta taarifa yoyote kuhusiana na wagunduzi hawa tangu mwaka 1980.
Natoa siku saba kwa TANESCO kwenda katika eneo la mradi huo wa kufua umeme uliopo Mkoani Njombe na kuona ni namna gani utafanya kazi vizuri zaidi
Natoa wito kwa viongozi wote kuangalia Televisheni ya Taifa (TBC) ili kila kitakachoonyeshwa kuhusu wizara husika kikashughulikiwe kwa haraka.
Natoa shilingi Milioni Tano kwa wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili kuwaongezea mtaji katika shughuli zao.
Zaidi, soma;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Juni, 2019 amekutana na wabunifu wawili wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya mito kutoka Mkoani Njombe na kuagiza wataalamu wa wizara na taasisi zinazojihusisha na sayansi, teknolojia na uvumbuzi kuwafuatilia na wabunifu na wavumbuzi mbalimbali ili kuwaunga mkono katika kuboresha kazi zao.
Wabunifu waliokutana na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam ni John Akani Fute na Jairos Ngairo ambao wamebuni miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji yanayotiririka mtoni, kusukuma maji kwa kutumia pampu zisizotumia umeme na kusaga nafaka kwa kutumia machine zinazoendeshwa na maji ya mto. Bwana Fute amebuni mradi unaozalisha kilowati 28 na Bw. Ngairo anazalisha kilowati 15 za umeme.
Mkutano huo umewahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye pamoja na viongozi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wabunifu hao kwa kuzalisha umeme wa gharama nafuu unaowanufaisha wananchi na ameagiza TANESCO na COSTECH kuwaunga mkono ambapo TANESCO itatoa shilingi Milioni 30 na COSTECH shilingi Milioni 20 kwa wabunifu hao, na pia timu ya wataalamu itaondoka kesho kwenda Njombe ilipo miradi hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu na kuiboresha.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na vitendo vya wataalamu kuwakatisha tamaa na kuwatisha wabunifu wa vitu mbalimbali vinavyowasaidia wananchi kama ambavyo Bw. John Fute (Pwagu) na Bw. Jairos Ngairo wamekuwa wakifanyiwa na badala yake ametaka wabunifu hao waungwe mkono kwa ushauri wa kitaalamu na kuwawezesha kuongeza tija.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza TBC kwa kufuatilia kazi za ubunifu na uvumbuzi kupitia makala yake ya Hadubini (Habari kwa Kina) ikiwemo makala ya ubunifu wa mradi huo wa umeme iliyoandaliwa na waandishi wa Habari Bi. Tatu Abdallah na Bi. Zaituni Mkwama na ameagiza Wizara na Taasisi za Serikali kufuatilia taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari na kuchukua hatua katika maeneo yanayozihusu.
Ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuatilia jengo la ghorofa 3 linalodaiwa kutelekezwa na raia mmoja wa kigeni huko Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambalo limebaki mikononi mwa mlinzi ambaye anatishwa na wajanja wanaotaka kujimilikisha kwa nguvu. Taarifa hii pia ilitangazwa na TBC kupitia makala ya Hadubini.
“Nakupongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na wafanyakazi wa TBC kwa kazi nzuri mnayoifanya, angalau nyinyi mnathubutu kujituma hadi vijijini kufuatilia mambo haya muhimu kwa jamii, nataka wizara na taasisi ambazo zina wataalamu na wasomi ziigeni mfano huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wakizungumza katika mkutano huo, Bw. Fute na Bw. Ngairo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwapa shilingi Milioni 5 ikiwa ni kutambua ubunifu wao na wameahidi kwenda kuboresha zaidi kwa kushirikiana na wataalamu wa Serikali.
Vyombo vya uslama pamoja na baadhi ya wasaidizi wake ndiyo wanaomwaribia. Awasiliane na sisi wananchi moja kwa moja. Vikao kama hivi viendelee bila kukoma, hata ikibidi kila wiki!
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Juni, 2019
View attachment 1126395View attachment 1126396
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Juni, 2019 amekutana na wabunifu wawili wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya mito kutoka Mkoani Njombe na kuagiza wataalamu wa wizara na taasisi zinazojihusisha na sayansi, teknolojia na uvumbuzi kuwafuatilia na wabunifu na wavumbuzi mbalimbali ili kuwaunga mkono katika kuboresha kazi zao.
Wabunifu waliokutana na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam ni John Akani Fute na Jairos Ngairo ambao wamebuni miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji yanayotiririka mtoni, kusukuma maji kwa kutumia pampu zisizotumia umeme na kusaga nafaka kwa kutumia machine zinazoendeshwa na maji ya mto. Bwana Fute amebuni mradi unaozalisha kilowati 28 na Bw. Ngairo anazalisha kilowati 15 za umeme.
Mkutano huo umewahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye pamoja na viongozi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wabunifu hao kwa kuzalisha umeme wa gharama nafuu unaowanufaisha wananchi na ameagiza TANESCO na COSTECH kuwaunga mkono ambapo TANESCO itatoa shilingi Milioni 30 na COSTECH shilingi Milioni 20 kwa wabunifu hao, na pia timu ya wataalamu itaondoka kesho kwenda Njombe ilipo miradi hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu na kuiboresha.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na vitendo vya wataalamu kuwakatisha tamaa na kuwatisha wabunifu wa vitu mbalimbali vinavyowasaidia wananchi kama ambavyo Bw. John Fute (Pwagu) na Bw. Jairos Ngairo wamekuwa wakifanyiwa na badala yake ametaka wabunifu hao waungwe mkono kwa ushauri wa kitaalamu na kuwawezesha kuongeza tija.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza TBC kwa kufuatilia kazi za ubunifu na uvumbuzi kupitia makala yake ya Hadubini (Habari kwa Kina) ikiwemo makala ya ubunifu wa mradi huo wa umeme iliyoandaliwa na waandishi wa Habari Bi. Tatu Abdallah na Bi. Zaituni Mkwama na ameagiza Wizara na Taasisi za Serikali KufuatiliaView attachment 1126406
“Tanesco hakikisheni mnaondoka na hawa waliozalisha umeme kwenda kuangalia hiyo mitambo na kuweka kinga maana mlitakiwa muwape ushirikiano kuanzia mwanzo lakini hamkufanya hivyo, na wasiondoke na basi kama walivyokuja mchukue magari yenu yenye nembo ya Tanesco,” amesema
Wabunifu hao wamekabidhiwa shilingi milioni 7.5 kila mmoja kutoka kwa rais Magufuli huku Tanesco wakiahidi kutoa shilingi milioni 15 kwa kila mmoja, nayo Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) imeahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa kila mmoja kama kianzio cha kuwasaidia wabunifu hao kujiendeleza.
Da, Mwinuka amepata taabu sana!
Viongozi wote kwenye mashirika ya umma hawafai hata kidogo! Ni kufumulia uongozi mbali na kuweka watu ambao ni “proactive”, wasiokaa maofisini, walioelimika, na wenye uchungu na hii nchi.Kwa kweli niliangalia kile kipindi TBC kuhusu hawa jamaa mawili wanaozalisha umeme wa maji huko njombe maeneo ya vijijini na kuugawa bure umeme kwa wananchi.Nilivutiwa sana na ubunifu wao na jitihada zao za kuzalisha umeme na kuwagawia wanavijiji wenzao bure kabisa. Ila kusema ukweli hata mimi binafsi nilishangaa na kukasirika kiasi fulani pale ambapo meneja wa Tanesco Mkoa wa Njombe alipohojiwa na mwandishi wa habari kama anafahamu chochote kuhusu hhawa wabunifu na wazalishaji na meneja kukuri kutofahamu chochote lakini mbaya zaidi ni pale aliposema kwamba wanawasubiri hao wazalishaji waende ofisini (Tanesco) ndio wajadiliane nao.
Nilishangaa sana na kuwaza wamba kama ndio aina ya viongozi tulionao kwenye mashirika yetu basi tuna safari ndefu sana. Na si hili suala la umeme tu kuna wabunifu wengi sana ambao kama ubunifu wao ungethaminiwa na serikali na kuuendeleza uengeleta manufaa makubwa sna kwenye jamii yetu lakini NO BODY CARES!
Well said brother. Pamoja sana kiongozi.👍🏽🙏🏾Kwenye hili nampongeza Raisi Magufuli la kuwatambua wabunifu.
Ujue waafrica tunamtafuta mchawi wa maendeleo lkn kumbe yupo kwenye fikra zetu.Pumbavu kabisa! Eti mapumbavu yanaulizia CV! Yani hiyo habari kidogo initoe machozi ya gadhabu! Miafrika tunakwamishana wenyewe! Rais ajifunze sasa kujaza hao wenye phd si solution kwenye hii nchi! Yani hadi mjerumani ndiyo amekuja kumthamini darasa la saba!
Na hilo jamaa lenye miwani, linalo ile mentality ya kutaka litumikiwe badala lenyewe ndo liwatumikie wananchi, lenyewe kukaa ofisini na kubweka maamuzi tu! ningekuwa rais ningelitimulia mbali. Pambaaf kabisa😡