Ikulu, Dar: Rais Magufuli azungumza na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,317
Rais Magufuli leo 13 Juni, 2019 anakutana na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito

Kuanzia saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es salaam





UPDATE
Rais Magufuli:
Nilifikiri kuwa Mkurugenzi wa TANESCO pamoja na Katibu Mkuu wangekuwepo hapa kusikiliza shida zao. Hawa ni mafundi ndiyo maana hawazungumzi sana.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu
Hadi sasa jumla ya wabunifu 60 wameshatambuliwa na kuingizwa katika Kanzidata ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia

Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo

Tutawaendeleza wabunifu hawa wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kuwaongezea shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kuendeleza kazi zao

TANESCO imejipanga kutoa shilingi Milioni 30 kwa ajili ya wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili waongeze uzalishaji wa umeme huo

Rais Magufuli
Tatizo la Watanzania tunajidharau na hatuthamini vya kwetu, hawa wabunifu wa mitambo wangegunduliwa mapema wangepunguza gharama za uzalishaji umeme kwa sababu tayari wana chanzo cha umeme.

Wangekuwa wameshasaidiwa wasingefika hapa. Transfoma zingekuwepo, Mkurugenzi wa TANESCO kwao ni Njombe na nina uhakika huwa anaenda likizo huko lakini hajafanya lolote. Meneja wa TANESCO mkoa (Njombe) nimemsikia akizungumza hawa waje wanione kasha waende Ewura…yeye hakutaka shida.

Hata wangezalisha umeme ukaleta madhara shida isingekuwa kwa watendaji wa TANESCO kwa hiyo Mkurugenzi wa Njombe naye hajaleta taarifa yoyote kuhusiana na wagunduzi hawa tangu mwaka 1980.

Natoa siku saba kwa TANESCO kwenda katika eneo la mradi huo wa kufua umeme uliopo Mkoani Njombe na kuona ni namna gani utafanya kazi vizuri zaidi

Natoa wito kwa viongozi wote kuangalia Televisheni ya Taifa (TBC) ili kila kitakachoonyeshwa kuhusu wizara husika kikashughulikiwe kwa haraka.

Natoa shilingi Milioni Tano kwa wabunifu wawili wa mitambo midogo ya kufua umeme ili kuwaongezea mtaji katika shughuli zao.

Zaidi, soma;

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Juni, 2019 amekutana na wabunifu wawili wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya mito kutoka Mkoani Njombe na kuagiza wataalamu wa wizara na taasisi zinazojihusisha na sayansi, teknolojia na uvumbuzi kuwafuatilia na wabunifu na wavumbuzi mbalimbali ili kuwaunga mkono katika kuboresha kazi zao.

Wabunifu waliokutana na Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam ni John Akani Fute na Jairos Ngairo ambao wamebuni miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji yanayotiririka mtoni, kusukuma maji kwa kutumia pampu zisizotumia umeme na kusaga nafaka kwa kutumia machine zinazoendeshwa na maji ya mto. Bwana Fute amebuni mradi unaozalisha kilowati 28 na Bw. Ngairo anazalisha kilowati 15 za umeme.

Mkutano huo umewahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye pamoja na viongozi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wabunifu hao kwa kuzalisha umeme wa gharama nafuu unaowanufaisha wananchi na ameagiza TANESCO na COSTECH kuwaunga mkono ambapo TANESCO itatoa shilingi Milioni 30 na COSTECH shilingi Milioni 20 kwa wabunifu hao, na pia timu ya wataalamu itaondoka kesho kwenda Njombe ilipo miradi hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu na kuiboresha.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na vitendo vya wataalamu kuwakatisha tamaa na kuwatisha wabunifu wa vitu mbalimbali vinavyowasaidia wananchi kama ambavyo Bw. John Fute (Pwagu) na Bw. Jairos Ngairo wamekuwa wakifanyiwa na badala yake ametaka wabunifu hao waungwe mkono kwa ushauri wa kitaalamu na kuwawezesha kuongeza tija.

Mhe. Rais Magufuli ameipongeza TBC kwa kufuatilia kazi za ubunifu na uvumbuzi kupitia makala yake ya Hadubini (Habari kwa Kina) ikiwemo makala ya ubunifu wa mradi huo wa umeme iliyoandaliwa na waandishi wa Habari Bi. Tatu Abdallah na Bi. Zaituni Mkwama na ameagiza Wizara na Taasisi za Serikali kufuatilia taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari na kuchukua hatua katika maeneo yanayozihusu.

Ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuatilia jengo la ghorofa 3 linalodaiwa kutelekezwa na raia mmoja wa kigeni huko Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambalo limebaki mikononi mwa mlinzi ambaye anatishwa na wajanja wanaotaka kujimilikisha kwa nguvu. Taarifa hii pia ilitangazwa na TBC kupitia makala ya Hadubini.

“Nakupongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na wafanyakazi wa TBC kwa kazi nzuri mnayoifanya, angalau nyinyi mnathubutu kujituma hadi vijijini kufuatilia mambo haya muhimu kwa jamii, nataka wizara na taasisi ambazo zina wataalamu na wasomi ziigeni mfano huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakizungumza katika mkutano huo, Bw. Fute na Bw. Ngairo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwapa shilingi Milioni 5 ikiwa ni kutambua ubunifu wao na wameahidi kwenda kuboresha zaidi kwa kushirikiana na wataalamu wa Serikali.





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

13 Juni, 2019
IMG_20190613_145503.jpg
IMG_20190613_145509.jpg
 
Wanaotumika na mabeberu watasema umeme wetu utawafukuza wawekezaji.
Inawezekana wewe utakuwa kati ya wale wapumbavu. Anyway hii ni wazo zuri Rais kafikiria maana kuna mito mingi inaweza kuzalisha umeme bila kuharibu vyanzo vya maji na wananchi wakajipatia umeme wa bei rahisi kuliko huu wa Tanesco. Mfano mito kama Ruvuma, Rusumo, etc
 
Magufuli huwa anapenda sana kukurupuka. Hapa alipaswa kuwatuma kwanza wataalamu wote wahusika wakakae na hao wagunduzi ilii wamletee concrete findings and opinions.

Hapa nao watu wanajikanyaga kanyaga tu kwa kushtukizwa bila hoja zenye msingi na msimamo.
Na Magufuli alivyo usishangae Akaondoka na Mtu hapa!
 
Nawaona tu wasaidizi/wataalam wa mkuu wanavyo jichanganya! Kiufupi tu 10% itaitafuna hii nchi mpaka akili zikae sawa. Wapo radhi kununua teknolojia ya gharama kubwa kutoka nje ili tu wapate 10% lakini siyo kuwakuza na kuwaendeleza wazalishaji wa ndani. Kwa hili nikupongeze tu mh. Rais.
 
Hii iwe nafasi ya kuruhusu wazalishaji binafsi wa umeme Nchini. Biashara bila upinzani hakuna mabadiriko..
Kabisa Kuna mapadri wakatoliki wanazalisha umeme hadi unashangaa njombe wanao mwingi waweza uza kwa wananchi .Mapadri sehemu nyingi hujizalishia umeme wao kwa matumizi yao maeneo remote kabisa Lakini huwa mwingi unaoweza uziwa watu
 
Kama Karitas Kyando wa kutoka Njombe hayuko kwenye huo mkutano, akatafutwe. Yeye ndiye mwanzilishi wa kwanza wa huu mradi. Alienda Sido wakamtengenezea Turbine, akaunganisha na altenator akaanza kugenerate umeme. Alivyokuja Dar, alielekezwa kwangu nikamsaidia kupata vifaa vya umeme kwa ajili ya kufanya distribution. Nadhani ni huko Lujewa/ Ludewa...

Baada ya hapo kina Cefa- Ikondo ndio nao waka chip in kuzalisha at larger scale na kusambaza. Wengine ni hawa Rift Valley (Mwenga) nao ni wadau wa kuzalisha.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom