Ikulu, Dar: Rais Magufuli akutana na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka kila Wilaya nchini. Ataja changamoto za biashara kwa Serikali na Wafanyabiashara

Hakuna sehemu ngumu kufanya biashara kama Tanzania. Siku serikali ya Tanzania ikiacha kufanya biashara badaa ya kusimaia biashara tutaendelea sana.
 
Jiwe anawaambia wafanyabiashara wafanye shughuli zao kwa uwazi na uadilifu wakati yeye mwenyewe sio muadilifu serikali yake imepoteza Trilioni kadhaa bila kujulikana zimefanyiwa nini
Hazijapotea.Si umemsikia waziri wa fedha,kasema, fedha za kodi hizo zimenunua ndege (Leo si umesikia Atcl imejaa),flyover nk.Pitia ripoti ya Conroller and Auditor General (CAG 2017/2018) Utaelewa tu.Amini hivyo yaishe
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema rushwa zinazotozwa na maafisa wa serikali na udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara ni baadhi ya vikwazo vikubwa vinavyoandama ukuaji wa biashara na uchumi nchini Tanzania.
Akizungumza katika mkutano maalum alioutishaleo na wafanyabiashara zaidi ya 1,000 kutoka kila kona ya Tanzania Magufuli amesema japo kuna jitihada kubwa zinazofanyika kupambana na rushwa, bado kuna maafisa wa serikali si waaminifu.
amewaasa wafanyabiashara kwenye mkutano huo wasisite kuwaripoti maafisa wanaowaomba rushwa kwa mamlaka ili wachukuliwe hatua.
Magufuli pia amekiri kuwa bado serikali haijaweka mipango endelevu ya kuwaendeleza wafanyabiashara na sekta binafsi kwa ujumla wake ili wachangie zaidi kwenye kuujena uchumi wa nchi yao.
"Hapa kwetu tuna zaidi ya wajasiriamali milioni lakini tumeshindwa kuwa na mipango ya kuwatambua, kuwalinda na kuwaongozea tija," amesema na kuongeza: " Mpaka sasa ni watu milioni 2.7 pekee ambao ndio wanaolipa kodi. Wigo kati ya wanaolipa na wasiolipa kodi ni kubwa sana, njia moja ya uhakika ya kutatua hili ni mipango thabiti ya kurasimisha wajasiriamal ili waendeshe uchumi."
Magufuli pia ametaja utitiri wa kodi na taasisi za udhibiti kama ni chamgamoto nyengine ya kimfumo inayoathiri ukuaji wa biashara nchini Tanzania. Lakini amesema jitihada za kutatua changamoto hiyo zinafanyiwa kazi na wameanza kwa kufuta tozo a ada zaidi ya 100 kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Kwa upande wa wafanyabiashara, Magufuli amesema wapo ambao si waaminifu wanakwepa kodi kwa kutoa rushwa na wengine kufanya udalali na kujihusisha na makundi ya uhalifu wa kibiashara.

Magufuli ameyataja maeneo yanayoongoza kwa rushwa ni bandarini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), barabarani pamoja na mipakani.

"Jitihada kupambana na rushwa zinaendelea...kuna mfanyabiashara alishawahi kusema kuwa ukitaka kuona rushwa bado ipo, toa kontena bandarini hadi Kariakoo. Sijui kama tumeshafanyia kazi kauli ile..." amesema Magufuli.
 
Mtu wa kulaumiwa ni Kikwete kwa kutuletea mrithi asiye na sifa za urais ili akumbukwe yeye kama shujaa na kuficha historia ya udhaifu wake

Sidhani kama maneno yako ni sahihi. Magufuli anayo nia njema sana na Tanzania. Tatzio hatuna systems inayo andaa viongozi. Magu anataka kufanya kila kitu which hataweza. Nashauri afanye kitu kimoja zaidi ya kingine.
Nia njema anayo !
 
Mkuu unadhani hizo serikali za mitaa na hao wengine watakwenda kutoza kodi bila kupewa amri kutoka uko juu? Tatizo linaanzia uko uko juu ndio mana kuna kiongozi alimuambia rais, hatuelewi wewe unatakaje hivo kupelekea sisi kwa sisi kupishana/ kutofautiana kwenye utendaji.
Mkuu kuna kodi zinatozwa na serikali za mitaa hapa ndo shida inaanzia...pia wingi wa mamlaka TFDA, BRELA, TBS na wengineo na tozo si rasmi....
Kazi ya urais ngumu
 
Nina mdogo wangu aliona kwenye simu ya mchumba wake jinsi anavyoongea ujinga kwenye group la whatsap,binti kaaamua kumtupa jamaa,amesema katu hawezi kuolewa na mwanaume anayejipendekeza kwa mwanaume mwenzake kwani huenda hata siku akawa mwanamke mwenzake kwa kuendekeza tumbo.
Hakika mkuu, wanaume wa siku hizi ni shida, walio takiwa wajipendekeze ni wanawake.. Sasa napata ukakasi wa hawa wanaume wa kileo
 
humpendi magufuli..
Unafuatilia kila anchofanya na anachoongea..
una get busy kukosoa, kukashifu na kupinga kila kitu
Love is addiction 😅 😅 😅 😅 😅
 
Ni mawazo yako mkuu
Si mawazo yake tu bali huo ndio ukweli. Hakuna wanaondika mambo ya hovyo, ya uongo na yasiyo na uhalisia kama verified users ndani ya JF. Yawezekana verified users wenye uthubutu wapo lakini ni asilimia ndogo sana kwani wengi ni wanafiki na hawana ujasiri wowote wa kuthubutu kuita koleo kwa jina lake...cheusi wataita cheupe, chungu watadai tamu, udikteta wataita demokrasia, yaani lengo lao kubwa ni kuonekana na hivyo wasisahaulike katika himaya tukufu.
 
Nimeshindwa kuelewa, reaction ya Mh Raisi kwa makosa ya Kichere ni tofauti na wengine!
hakuna mtu anaependa kulipa kodi duniani , hivyo hayo malalamiko lazima yawe mengi.
Kamishana wakodii za ndani ameambiwa akamshushe cheo aliyekuwa manager wa tra ilala mwaka 2017 sasa ukistajabu ya mussa utaona ya firauni,kamishana wa ilala mwaka 2017 alikuwa yeye mwenyewe
Alieambiwa kushushwa cheo ni wa kituo cha kariakoo .
 
Back
Top Bottom