Ikulu, Dar: Rais Magufuli akutana na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka kila Wilaya nchini. Ataja changamoto za biashara kwa Serikali na Wafanyabiashara

Mbona sijasikia hata sioni hata mtu mmoja akiandika kuhusu kucheleweshwa malipo kwa ma kontrakar na wenye tenda za serikalini? Au wao sio wafanya biashara..
 
Unachotaka kutuambia kiongozi akitoa maelekezo leo asifuatilie tena utekelezaji wake sababu akifanya hivyo zitakuwa ni NGONJERA. Magufuli ktk miaka mitatu alifuta zaidi ya kodi 10 zenye kero ktk kilimo, alitakiwa asisikilize kero yoyote baada ya hapo mpaka anapotoka madarakani? Uongozi sio kukaa na kuridhika na uliyoamua ni pamoja na kufuatilia effectiveness ya unayoyaamua.
Hizo ni ngonjera na porojo, hayo matatizo yote ya nayotusibu wafanyabiashara yametengenezwa na serikali halafu leo serikali hiohio inakuja hapa kujifanya inauliza kero za wafanyabiashara, sikulazimishi uamini haya kwa sababu naamini wewe sio muhanga wa kero hizo.
 
Mbona sijasikia hata sioni hata mtu mmoja akiandika kuhusu kucheleweshwa malipo kwa ma kontrakar na wenye tenda za serikalini? Au wao sio wafanya biashara..
Ndio ushangae mkuu, halafu kuna watu humu na akili zao kabisa wanajaribu kusifia sanaa inayofanyika hapo
 
Mna ropoka sana humu ndani, sasa wewe ungefanyaje ktk hili. sema tuuu!
 
Kwa nini una niita poyoyo wakati mimi nimeandika alichokisema mkuu kuwa taasisi ndio tatizo? Kosa langu ni kuwakilisha au nini? Mimi nimedhihaki wapi hapo kwenye nilicho andika? Tumia akili na busara hata kama una mahaba sana kwa mtu sio kijongelea kwa jazba mpaka ulicho andika kina kasoro kwa sababu ya pupa una andika maneno nusu nusu.. Wingi wa taasisi yeye ana uwezo wa kuziondoa kbala ya kulalamika.
Nimeandika kwa sababu umechukua sehemu ndogo ya hotuba yake kuhitimisha hicho ulichoandika.

Makamu wa Rais na Waziri Mkuu walimwelewa na kuahidi kufanyia kazi hayo unayoita "malalamishi ya Rais" mimi nikiyaona kama "maagizo" ili vyombo vinavyohusika vichukue hatua kulingana na Katiba ya nchi, Sheria na Kanuni zilizopo
 


Rais Dkt John Magufuli anaongea na Wafanyabiashara Nchini ambapo katika hotuba yake ametaja vikwazo vikuu vya biashara Nchini kuwa ni Rushwa, utitiri wa kodi na tozo, ukosefu wa mitaji, Mawakala wa TPDF na utitiri wa taasisi zinazosimamia biashara.

Rais Magufuli anaendelea na hotuba na atawakaribisha wafanyabiashara kutoa maoni yao.

MAONI YA WAFANYABIASHARA

Mfanyabiashara(Arusha):
Kwenye sekta ya utalii, wenzangu wamenituma nikuulize “Je, kuna kitu unataka tufanye ili tuendane na kasi yako?”

- Wewe umetufanyia makubwa na tunaridhika na unayotufanyia. Je, wewe unaridhika na tunayoyafanya? Tupo vizuri tunashukuru sana


Mfanyabiashara(Pwani): Ulikuja kufungua kiwanda cha chuma na nilikuomba eneo la kujenga viwanda vingine. Nilikuomba eneo, ukanambia nijaze eneo nililonalo kwanza

- Nilifanya hivyo na nikajenga viwanda 4. Baada ya hapo nikaomba eneo lingine kwa kufuata taratibu


Mfanyabiashara(Pwani): Wakati naendelea kujenga kiwanda cha saruji nikapewa barua kuwa nisimamishe ujenzi pale maana kiwanda kipo chini ya Rais

- Ninaomba uniruhusu kujenga kiwanda kile na ukinipa hata miezi minne, utakuja kufungua viwanda zaidi ya 10 pale


Mfanyabiashara(Rukwa): Tanzania kuna Watu wamesomea hujuma, kuna mradi mkubwa sana ila sitausema kutokana na watu ila nitakupa kitabu cha mradi huo

- Katika mpango wa kuwapata mabilionea uliosema, ni lazima serikali iwe na mpango madhubuti. Urasimu bado ni tatizo


Mfanyabiashara(Rukwa): Mimi ndio mzee hapa kuliko wote na Mwalimu(Nyerere) alitufundisha ukifanya jambo usifanye nusu nusu, fanya kwa asilimia 100

- Wewe unaongoza kwa kutofanya mambo nusu nusu na hawa Mawaziri wako naomba wachague jambo moja wafanye kwa ufanisi


Mfanyabiashara(Rukwa): Mimi ni mkulima na ktk Wizara zote inayotuangusha ni Wizara ya Kilimo. Kilimo si Siasa, huwezi kusema ‘Kilimo hoyee, mahindi yakaota’

- Waziri mpya tunaomba afanye kazi na akubali ushauri. Vijana wako wakubali ushauri, niko tayari kuwashauri.


Mfanyabiashara(Dodoma): Nimewekeza kwenye kilimo ila bado kipo chini sana. Jitihada tulizofanya za kuwekeza ni kubwa, tumeweka fedha. Tunasubiri hati, hadi sasa hazitoki

- Wananchi hawajapimiwa mashamba na kwenye kodi, Watumishi wengi wa TRA hawajui wakifanyacho


Mfanyabiashara(Dodoma): Watumishi wa TRA wanafanya kazi kimazoea na badala yake sasa wanakuwa wao ndio sheria

- Kwa sababu sheria imekaliwa, Wafanyabiashara wanakwepa kulipa kodi hiyo pia kuna utitiri Mkubwa sana wa tozo


Rais Magufuli(Anaingilia kidogo): Tumekuja hapa Serikali nzima, bado mnaongea mambo rahisi rahisi, hebu pigeni vizuri basi. Vinginenvyo kikao hiki tunapoteza muda

- Na hapa nyie tutawapotezea biashara zenu, nataka mseme yale magumu magumu kabisa


Mfanyabiashara(Shinyanga): Sisi wafanyabiashara wa duka, kodi ya Service Levy inatusumbua sana kwa kuwa haiangalii faida inaangalia mauzo. Tunaomba ututolee hii, hailipiki

- Nyingine ni VAT, tunapendekeza kodi hii itoke kabisa kwenye viwanda, sisi tulipe makato


Mfanyabiashara(Simiyu): Kwa wafanyabiashara wadogo anakopa benki, akienda TRA hapo hapo anakadiriwa kodi. Tunaomba kuwe na muda hata miezi 6 ndio aanze kukatwa

- Tunapoagiza mizigo nje tunaomba Serikali tuweze kukopesheka, pale bandarini tulipe 30% na baadaye 70%


Mfanyabiashara(Mtwara): Sisi Wafanyabiashara wa Mtwara tunaomba kitu kimoja, tunaomba meli itakayotusaidia kwa biashara ktk visiwa vya Comoro maana tupo navyo karibu sana

- Pia, tunaomba miundombinu ya mto Ruvuma iboreshwe ili tuweze kuvusha bidhaa kwenda Msumbiji


Mfanyabiashara(Mara): Bado kuna changamoto kufanya Butiama kuwa eneo la Utalii, kuna maeneo mazuri sana. Tunashukuru, barabara nzuri sana hadi Serengeti

- Changamoto kubwa ni uwanja wa ndege wa Musoma na sasa umefungwa, ndege zinazotua ni ndogo zenye bei kubwa

Mfanyabiashara(Mara): Katika utalii pia suala la Afya ni jambo muhimu, tunaomba huduma za afya ziboreshwe katika wilaya yetu

- Katika kilimo umezungumzia mikopo na taasisi. Taasisi ni nyingi lakini hazipo katika Wilaya. Mfano hakuna ‘Business Market Intelligence’


Mfanyabiashara(Mbeya): Umezungumzia taasisi zilivyo nyingi na zinafanya kazi zinazoelekeana. Wafanyabiashara hatupendi usumbufu na hapo ndipo Serikali inapoteza kodi

- TBS na TFDA tunakubaliana nao lakini tunaomba TBS wafanye kama TFDA, wakagulie hapa ndani


Mfanyabiashara(Mbeya): Inauma sana unapochukua Mzigo SADC na kulipa tuu VAT ambapo hatuwezi kusema ni kodi ila ikija TBS unalipa asilimia 50 ya kodi, inauma

- Na kwa namna hiyo lazima vichochoro vya kukwepa kodi viwepo. Kwanini mtu asilipe VAT tuu


Mfanyabiashara(Mwanza): ‘Service Levy’ ina changamoto kutokana na sehemu na sehemu. Kwetu Mwanza inasikitisha sana

- Japo inakatwa 0.03% ya mauzo lakini wanakuja kukusanya na bunduki na Polisi wanatutisha sana. Wanachonganisha Wananchi na Serikali


Mfanyabiashara(Mwanza): Wakija wanaangalia kwenye mfumo wao na kukuambia unadaiwa Milioni 200 na wanakupa siku saba uwe umelipa

- Lakini ukienda mlango wa nyuma unaambia toa milioni 20. Sasa tunaomba utusaidie Rais


Mfanyabiashara(Iringa): Sisi wafanyabiashara wa mbao tuna utitiri mkubwa sana wa kodi (karibia 19) na inashangaza sana maana tunakodi mti ukiwa shambani na ukiwa umevuna. Tunaomba kodi ibaki sehemu moja

- Pia, tunakatwa kodi ya VAT tukiwa bado hatujavuna bidhaa


Mfanyabiashara(Njombe): Naomba kutoa ushauri juu ya mashine za risiti tunazozitumia. Naomba kuwe na usimamizi moja kwa moja kutoka kwa TRA

- Ninaponunua mashine, usumbufu unakuja wakati mashine inaposumbua kwani TRA wanakuambia nenda karekebishe uliponunua


Mfanyabiashara(Kigoma): Sisi watu wa Kigoma tuna mahitaji makubwa sana kutoka Congo lakini changamoto ni wao kuingia nchini ‘Visa’ tu wanalipa elfu 50

- Pia wanapoingia kumekuwa na kamata kamata kubwa sana wakiwa hotelini. Lakini pia usalama wa fedha ni mdogo


Mfanyabiashara(Kigoma): Hakuna Cooperative Bank za Tanzania huko Congo yaani mtu hawezi kuweka hela Congo akaja kutumia Tanzania

- Lakini pia kibali cha usafirishaji lazima ukifuate Dodoma. Maabara ya kupima dagaa ipo Arusha “Kwanini haipo Kigoma?”


Mfanyabiashara(Kigoma): Tulivumbua soko la Madini Kigoma, dhahabu kubwa ilikuwa inatoka Congo kuja Tanzania lakini masharti unayopewa ni makubwa

- Watu hao walikuwa wanatakiwa kulipa ‘Import Fee’ dola 300 haitegemei wala kiasi cha dhahabu. Tunaomba iwe Dola 50


Mfanyabiashara(Katavi): Kwa Katavi suala la kwanza ni kwenye madini, miamba ya Katavi ni migumu sana kuichenjua. Ningeomba tupewe kibali maalumu kusafirisha miamba

- Tunaomba utusaidie kupata bandari ktk mpaka wa Kalema ili tuweze kusafirisha bidhaa kwenda Congo


Mfanyabiashara(Geita): Kuna usiri mkubwa unaoendelea kwa TRA. Kwanini bei za kodi zisiwe wazi?

- Ukwepaji kodi ni kutokana na usiri wa TRA. Mfano, tunaweza kwenda China Wafanyabiashara watano tukiwa na bidhaa sawa ila kila moja akatoa kwa bei yake pale bandarini


Mfanyabiashara(Geita): TRA wasumbufu sana, Waganda wanatumia bandari ya Tanzania lakini bidhaa zao bei ipo chini kuliko za Tanzania

- Kwanini TRA wasiende kujifunza Uganda na kuacha kuwaumiza Wafanyabiashara?


Mfanyabiashara(Manyara): Kiwanda cha Minjingu kinazalisha mbolea tani laki 1.5 kwa mwaka

- Tayari uwezo wetu unakua ila tunaomba iwe kusudio la Serikali kuwa zianze kutumika bidhaa za ndani
- Changamoto mzalishaji wa mbolea anatozwa VAT, ila muagizaji hatozwi


Rais Magufuli: Kuna wakati Wizara ya Kilimo(enzi za Waziri Tizeba) walikuwa wananunua mbolea nje na nikauliza “Kwanini?”
-Lazima niseme ukweli, walinijibu “Umekataa kuuza mbolea mpaka upewe ‘capital’ ya milioni kadhaa” Je, ni kweli?

Mfanyabiashara: Si kweli

Rais Magufuli: Kwa hiyo yalikuwa ni maneno ya kutengeneza. Mimi niliuliza hilo nikajibiwa unataka mamilioni - Nimekuelewa na ndio maana mbolea zako ulikuwa unaandika zinatoka Kenya. Haya asante, nimeelewa


Mfanyabiashara(Songwe): ‘Service Levy’ ambayo ni 0.03% ya mauzo tunayolipa kwa Halmashauri, tunaomba iondolewe maana Halmashauri haijui kama umepata hasara au faida

- Pia biashara ya Hoteli kuna kodi nyingi sana. Kama ulivyosema awali kodi ziwe chini ya mwamvuli 1


Mfanyabiashara(Songwe): Ukitaka kuanzisha kiwanda kwa kweli mlolongo ni mrefu sana. Kazi zinashindikana kutokana na mlolongo mrefu

- Pia, tunaomba BRELA waunganishwe na NIDA ili BRELA wapate taarifa zangu moja kwa moja maana wengi bado hatuna vitambulisho hivyo


Mfanyabiashara(Songwe): Mwisho hapa kuhusu TANESCO, unapotaka kuanzisha kiwanda wanakuambia hakuna umeme wa kutosha mara hakuna ‘Transfoma’

- Na tukinunua ‘Transfoma’ tunatumia na watu wengine bila maelezo yotote yale


Rais Magufuli: Unapokuwa na kiwanda chako wewe jenga halafu subiri hao wenye kodi zao waje wakudai kodi

- Hili nifafanue hapa hapa, ukinunua Transfoma ya umeme wadai TANESCO maana wewe ni Mwekezaji, Transfoma ni ya kwao

RAIS MAGUFULI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI RCO MOROGORO
Amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumsimamisha kazi kutokana na baadhi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Tumbaku kunyanyaswa.

Wanawanyanyasa kwa kukamatwa, kuwekwa ndani na kuachiwa bila kufunguliwa kesi


Mbunge Musukuma: Natoka jamii ya ufugaji na soko kubwa lipo Comoro, ukinunua ng’ombe Geita ili umsafirishe unalipa Tsh. 4,000 na unalipia ng’ombe ‘Permit’ ya Tsh. 2,500‬

‪- Unamsafirisha mpaka Pugu, ili umshushe unalipa Tsh. 6,500. Ukiwa unampeleka Comoro inabidi umpeleke Kwara‬

Musukuma: Ukifika Kwara, pale kusajili ng’ombe mmoja ni Tsh. 1,500 na akilala hapo anachajiwa Tsh. 1,000 na lazima wakae siku 14 pale‬

‪- Kisha unalipa ‘Export Permit’ Dola 30, Tsh. 6,500 ya kupeleka bandarini na siku zote ng’ombe hawa tunanenepesha kwa mashudu‬

Wafanyabiashara wa Comoro wa ng’ombe hawanunui tena huku kwetu wamehamia Madagascar‬

‪- Lakini ili usafirishe ng’ombe kutoka Geita inabidi ulipoe kibali wanaita ‘abnormal’ Dola 10 mtandaoni‬

‪- Wafugaji wa ng’ombe wengi wana simu ya tochi, ‘Wanatoa wapi mtandao?’‬

Kuna biashara ndogo inafanyika bandarini kwa akili zangu ndogo huwa najiuliza sana. Inapoingia meli ya mizigo kuna watu wameshapanga hii inaenda ICD‬

‪- Bandari yetu ipo tupu makontena yanagawanywa kwenda ICD. Nashangaa sana‬


Rais wewe una hoteli kule Chato, kabla hoteli yako haijajaa wakija watu unawaambia “nenda kule”, utakuwa na akili gani wewe!‬

‪- Kwanini tunapeleka makontena yetu kwenye ICD wakati bandari yetu iko tupu? Na kule unalipa $40 kwa siku 7 na ukichelewa unalipa $80‬

Tunakushukuru na Waziri amekuwa msikivu kuhusu dhahabu, ila nilikuwa naangalia tu ile rekodi ya mkoa wangu wa Geita ambao ni kinara wa dhahabu‬

‪- Toka mwezi wa kwanza hadi wa 5 tunaenda kusoma bajeti tumekusanya kilo 600. Niliongea Bungeni na wewe leo nikueleze‬

Ni kwamba hata theluthi ya dhahabu hatujaweza kukusanya maana kwa Geita tunaweza kukusanya tani moja kwa siku‬

‪- Sasa pengine kuna udhaifu kwa wasimamizi, niliomba, nakuomba kama unaweza kutoa kikosi kidogo tu cha Jeshi kizungunge Geita kama utakosa tani 1‬

Kama ukikosa tani hiyo kwa kutumia Jeshi tena hata wakiwa hawana nguo za Jeshi mimi nipo tayari kujiuzulu. Hatuwezi kujisifu tumekusanya kilo 600‬

‪- Jiulize timu yako ya ulinzi ilikamata kilo 300 maana yake alikusanya siku ngapi kama miezi mitano tuna kilo 600‬


Rais Magufuli: Kutokana na kikao hiki yapo mengi sana yatabadilika iwe ni chanya au hasi. Mfano, mwaka jana hapa tuliongea kuhusu taulo za wakina mama

- Serikali ikapunguza bei ila Wafanyabiashara hawakupunguza bei kwenye taulo hizo za mama zetu na watoto wetu

Ndio maana nikawaita hapa tuongee leo, tuelezane ukweli kabisa na katika yote haya inaonekana kuna ‘mnyama’ anaitwa TRA

- Anaonekana ni mnyama mbaya sana...ila labda kuna watu ambao....eenhe ‘anyway’ tuendelee. Najua mnanielewa

Shida kubwa kwenye sekta ya ujenzi ipo kwa Serikali na ‘Contractors’ wenyewe

- Inapokuja ‘Ku-apply’ kazi hamfanyi hivyo kutokana na mahitaji ya mikataba. Pia Contractors hamtaki ushirikiano

- Nilienda Ujerumani mradi 1 wapo Contractors wengi

Hamtaki kufanya kazi moja kwa ushirikiano, kuna kundi fulani tuliliweka pamoja na likafanya kazi, lilipoenda kuomba kazi ya kujenga barabara Butiama likasambaratika

- Kinachosumbua sekta binafsi ni ‘Selfishness’, ila sasa tusaidiane katika haya

Wafanyabiashara malizeni uoga, najua wengi hapa mmefanyiwa mambo na TRA lakini meogopa kuongea kwa kumuona Kamishna wa TRA na Wakurugenzi wake

- Acheni uoga, nilitegemea hata mtataja na majina kabisa ya Makamisha wa huko mikoani


BoT: Serikali haiwezi kukusanya fedha na kuipelekea sekta binafsi, hilo lazima lifanywe na benki zetu

- Tunahitaji benki zinazotanuka na kupeleka huduma hadi vijijini kwa bei zinazostahili

- Tumeona utoaji mikopo kwa sekta binafsi unapanuka na kufikia 12%

Benki lazima ziwe na Ukwasi na ndio maana tunakuwa wakali na kutuma watu kufanya udhibiti ili benki hizo zisitetereke

- Zinapotetereka lazima tutafute nani anaziteteresha. Na sasa zina fedha za kigeni na kwa wiki 3 hazijaja Benki Kuu kuomba fedha za kigeni

Hakuna fedha zilizonyang’anywa kwa watu wenye maduka ya kubadili fedha, fedha zilichukuliwa kama vielelezo kwenye uchunguzi

- Wataanza kupewa majibu ya utafiti uliofanywa na watakaokutwa na shida wanatakiwa kujieleza. Aliyenyang’anywa fedha aje atuambie

Mwanasheria Mkuu: Yote yaliyozungumzwa yanagusa sheria ila sheria hizi zinasimamiwa na Mawaziri. Wakihitaji sheria au marekebisho ya sheria wanatuambia sisi

- Waziri mkuu tayari ametupatia maagizo ya kurejea mamlaka zote na kuangalia wapi kuna haja ya urekebishaji

Waziri Mkuu pia ametupa maagizo ya kupitia sheria ya uwekezaji na kufikia mwezi wa tisa tunaweza kuwa na sheria mpya

- Ametuambia tupitie sheria hiyo na kurekebisha mapungufu yote yanayoonekana


Katibu Mkuu, Wamiliki wa Mabasi: Basi linalotoka Dar kwenda Bukoba kila siku linalipa 140,000/-. Tozo ni nyingi sana, Sekta ya usafirishaji tunaisha

- Sisi tupo chini ya Wizara 3, mwendo tunaokwenda ni Km 80/saa tunaomba tusikaguliwe kila kituo bali sehemu maalumu


Rais Magufuli: Tumelipa ardhi kule Bagamoyo, kilichofanyika ni mambo ya ajabu na ya kipumbavu kabisa. Watu wa Bagamoyo waliolipwa ni wachache, wengi wa mjini huku

- Wawekezaji nao wana masharti ya ajabu sana, hawataki uendeleze Bandari yoyote, uwalipe wakichimba


Waziri Madini: Sehemu kubwa ya mambo yaliyosemwa kwenye madini yamefanyiwa kazi. Januari tulikuwa na mkutano kama huu na Rais ndiye alifungua mkutano

- Matatizo yalikuwa mengi sana ila yamefanyiwa kazi. Wizara kwa sasa imetenga maeneo mbalimbali ya kuwapa watu

Kuhusu Kigoma kwamba ukitaka kuingiza dhahabu lazima ulipe Dola 350. Sisi hatuna shida, na ada hiyo hakuna tena

- Hatujali dhahabu inaingizwa kutoka wapi, kwenye soko letu uza, kuingiza bure ila kutoa lazima ulipie. Chunya kuna soko zuri la dhahabu


Waziri Mkuu: Napenda niwahakikishie Wafanyabiashara kuwa Serikali imeanza kufanyia kazi kero zao ikiwemo ile ‘Blue Print’

- Waziri wa Uwekezaji alipitia na kuongea na Kila Wizara, pia tumeongea na Wakulima, umoja wa wauza bodaboda, Watu wa Utalii na hata TIC

Tumekubaliana kuwa mawaziri wakutane na kuanglia zile tozo zinazojirudia ktk taasisi tofauti. Tunataka ibaki tozo moja na kwenye taasisi moja

- Lakini pia ktk kazi tulizoanza kuzifanyia kazi ni kuziunganisha taasisi ambazo zinafanya kazi zinazofanana

Kwa TRA bado tuna tatizo la kufunga maduka ya watu bila hata elimu na wakati TRA kuna kitengo cha Elimu

- Nimekutana na TRA na nimekutana na Wafanyabiashara wa eneo dogo tuu Kariakoo na wakazungumza mengi sana. Mengi waliyosema hapa na kule yapo

Yupo Mfanyabiashara mmoja alikamatwa na mzigo wake tangu mwaka 2016 kwa sababu tuu aliyemkamata alitaka rushwa ila yeye alikataa

- Mfanyabiashara huyo alikuwa ‘Smart’ aliamua kuacha mzigo uende ili yeye asitoe rushwa na mzigo wake amerudishiwa juzi

Rais Magufuli: Waziri Mkuu, hao waliomuonea Mfanyabiashara si unawajua?

Waziri Mkuu: Alikuwa anasafiri kutoka Zambia, alipita maeneo yote, amekaguliwa yupo sahihi hadi Kimara alipokutwa na tatizo

Tatizo ni kuwa alikataa kutoa rushwa usiku ule


Rais Magufuli: Waziri Mkuu bado usijisahaulishe hapo. Hapo ndio patamu. Kamishna wa TRA unawajua hao waliokuwa wameshika mzigo?

Kamishna TRA: Majina yao nimesahau kidogo naomba nitakupatia

Rais Magufuli: Walikuwa wangapi?

Kamishna TRA: Watatu


Rais Magufuli: Kamishna wa TAKUKURU ukawashike, uwaweke ndani . Halafu wapelekwe Mahakamani na watakapokuwa Mahakamani, Kamishna wa TRA uwe umewasimamisha kazi

- TRA mkapige hesabu ile biashara yake imekaa kwa miaka mitatu, mumlipe fidia

Ninawaomba TRA nao wawe ‘Flexible’. Akija mtu akajieleza kuwa “haya nilifoji zamani kwa kuwa ilikuwa inawezekana”, msikilizeni

- Akija aka-comply kwamba “nisaidie hapa na pale”, msikilizeni. Biashara ni mahusiano

Kwa sababu mmetoka kwenye mikoa 26, mnaporudi nyumbani katafuteni muda hata kaeni Kikanda kama alivyopendekeza Makamu Rais

- Nendeni mkaorodheshe kodi zenu na shida zenu. Hayo mtayokubaliana yaleteni moja kwa moja kwa Waziri Mkuu. Leo nimejifunza sana

Lakini Wafanyabiashara muache kuoneana wivu, mnaoneana ninyi kwa ninyi. Mfanyabiashara huyu wa nondo anampiga vita huyu wa nondo

- Nataka muda wangu ukiisha, tuwe na Mabilionea 100. Na hili linawezekana tukiamua. Tuache kuoneana wivu

Kafanyeni biashara zenu na katika hilo msisahau kumtanguliza Mungu. Serikali iliyopo madarakani inapenda Wafanyabiashara

- Kwenye biashara hakuna chama, chama chake ni pesa. Haijalishi uwe mweusi au chama gani

MWISHO

nilicho gundua wafanya biashara wengi wmemuunga mkono president but kitaani wnsema hali mbaya tunawaelewaje??
 
NUKUU NILIYOIPENDA KWA MMOJA WA WAFANYA BIASHARA "Kilimo si Siasa, huwezi kusema ‘Kilimo hoyee, mahindi yakaota."
 
Sikilizeni porojo za mzee baba baada ya kuangusha uchumi

Hao mabilionea 100 watapatikaneje?
Huyu huyu Magufuli amewahi kusema WALE ALIOWAKUTA MABILIONEA WAKIISHI KAMA Malaika amewashusha chini ILI WAISHI KAMA MASHETANI......!!!
Magufuli kwa kweli ni JIPU!
 
Nukuu kuu kwangu:
Kilimo si Siasa, huwezi kusema ‘Kilimo hoyee, mahindi yakaota’
 
Wadau,

Nimevutiwa na utartibu uliotumiwa na Rais Magufuli leo.

Rais amesema anachofahamu na kile kilichokuwa kwenye flush zake mbili.

Wadau wa biashara wamesema wanachofikiri.

Rais akasikiliza na kujibu.

Kulikwepo na dayalogia.

Rais asiishie hapo, ayaite makundi mengine pia.

Atajifunza sana na kufundisha sana, na kuongeza weledi wake wa kiutawala.

Wote Karibuni Sumbawanga!
Mama Amon Habari Ya Swax
 
Back
Top Bottom