Ikulu, Dar: Rais Magufuli akutana na Wafanyabiashara Wakubwa kutoka kila Wilaya nchini. Ataja changamoto za biashara kwa Serikali na Wafanyabiashara

Wadau,

Nimevutiwa na utartibu uliotumiwa na Rais Magufuli leo.

Rais amesema anachofahamu na kile kilichokuwa kwenye flush zake mbili.

Wadau wa biashara wamesema wanachofikiri.

Rais akasikiliza na kujibu.

Kulikwepo na dayalogia.

Rais asiishie hapo, ayaite makundi mengine pia.

Atajifunza sana na kufundisha sana, na kuongeza weledi wake wa kiutawala.

Wote Karibuni Sumbawanga!
 
Kwa nchi ama yetu idadi hiyo ya makampuni ni ndogo sana. Makampuni nchi hii ni mengi mno na yanayofanya uzalishaji ni mengi sana (zingatia kuwa cgereni tatu nne zinatosha kuwa 'kampuni' ya uzalishaji). 17,000 inayozungumiwa na Rais ni idadi ya makampuni ya ayokwepa kodi!
Ndio maana wafanyabiashara wamemkomalia
 
Amejivua lawama na kusingizia TAASISI za serikali na wingi wa tozo ndio umedumaza biashara, yeye hahusiki...utitiri wa taasisi ni kikwazo anasema mzee baba.
Ni Taasisi ambazo zimekuwepo miaka nenda miaka rudi. Iwapo umwelewa kama popoyo utabaki kulaumu tu, kwa jinsi hivyo.

Ujumbe uliomo kwenye maelezo yako s ilushauri bali AGIZO kwa Tasisi hizo ama kujipanga upya kutimiza malengo ya uanzishwa wake au zifutwe na kuunganishwa.

Naamini utakuwa mkakati wa kiuchumi utakaofuata baada ya kuimarisha nguzo kuu za kuchochea ukuaji wa uchuki, ambazo ni usafiri wa barabara, reli, maji na anga.
 
polisi morogoro ni wanyasaji sana kusimamishwa rco iwe salamu kwa askari wa chini hasa kile kituo chao cha madili kule sua
 
Mtu wa kulaumiwa ni Kikwete kwa kutuletea mrithi asiye na sifa za urais ili akumbukwe yeye kama shujaa na kuficha historia ya udhaifu wake
Jk hana hatia alikijua kikombe toka ndani,na halikuwa chaguo lke,kosa lake ni kutoheshimu makubaliano yao Edo,wa kulaumiwa ni machinga Na lubuva ndo wametuletea shida.
 
Amejivua lawama na kusingizia TAASISI za serikali na wingi wa tozo ndio umedumaza biashara, yeye hahusiki...utitiri wa taasisi ni kikwazo anasema mzee baba.
Ndio ukweli na wanasumbua Sana kuliko kauli zake
 
wengi waliochangia wamechangia internal environment....kwa kuwa ndio wanayoweza kudeal nayo...kama tra natozo...extanal environment ...watu mtaani hawana pesa bidhaa utamuuzia nani...biashara haitoki...ingekuwa inatoka na watu mtaani wana pesa nani angepoteza muda kuzungumza kero za tra...tra wanakuwa wabaya pale wanapofanya mambo kwa mazoea na afisa kupewa uwezo mkubwa wa kupunguza au kuongeza kodi...na unakuta wamepewa target ya kukusanya....sasa unapofika pale wanaangalia watafanyaje target yao ifike ndipo watu wanapoumia na kulalamiaka...hapo magu anamfungulia mbwa tra akukamate akikuuma anakupa pole...
 
Kuwasingizia TRA ni kuwaonea wao wanatii maagizo kama ilivo Kwa matrafiki kugeuza GARI zetu ng'ombe wa maziwa,asipokukuta Na kosa ananuna
 
Rais John Magufuli amesema anatamani atakapomaliza muda wake aache zaidi ya mabilionea 100 nchini. Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini. “Natamani inapoka mwisho wa kipindi changu cha uongozi, niache angalau mabilionea 100 nchini,” amesema.

Rais amesema, amekutana na wafanyabiashara nchini ili wajadili namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara nchini. “Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kushughulikia baadhi ya changamoto zinazokabili sekta hii ya biashara na tumeshaandaa kitabu cha muongozo,” aliongeza. Rais Magufuli pia amebainisha kuwa tangu serikali yake iingie madarakani, miradi mipya iliyosajiliwa katika kituo cha uwekezaji ni 897 ambapo miradi 313 ni Watanzania, 377 ni wageni na 207 ni ubia kati ya Watanzania na wageni.

Miradi hiyo yote ina thamani ya Dola za Marekani Bil. 13.8 na imetoa ajira kwa wananchi 21,390.

Amesema, ana orodha ya kampuni hewa 17, 447 zilizojisajili Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) zinazofanya biashara hewa na kudai kurudishiwa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).

Kutokana na hilo ametoa siku 30 kwa kampuni hizo kulipa fedha wanazodaiwa serikalini. Rais amesema lengo la mkutano huu ni kuzungumzia changamoto, mafanikio na maboresho ya kufanyika ili kuboresha mazingira ya biashara nchini.
 
Sidhani kama maneno yako ni sahihi. Magufuli anayo nia njema sana na Tanzania. Tatzio hatuna systems inayo andaa viongozi. Magu anataka kufanya kila kitu which hataweza. Nashauri afanye kitu kimoja zaidi ya kingine.
Nia njema anayo !
Na njema gani huku anaua, anateka, anatesa wanaomkosoa?
 
Ni Taasisi ambazo zimekuwepo miaka nenda miaka rudi. Iwapo umwelewa kama popoyo utabaki kulaumu tu, kwa jinsi hivyo.

Ujumbe uliomo kwenye maelezo yako s ilushauri bali AGIZO kwa Tasisi hizo ama kujipanga upya kutimiza malengo ya uanzishwa wake au zifutwe na kuunganishwa.

Naamini utakuwa mkakati wa kiuchumi utakaofuata baada ya kuimarisha nguzo kuu za kuchochea ukuaji wa uchuki, ambazo ni usafiri wa barabara, reli, maji na anga.
Kwa nini una niita poyoyo wakati mimi nimeandika alichokisema mkuu kuwa taasisi ndio tatizo? Kosa langu ni kuwakilisha au nini? Mimi nimedhihaki wapi hapo kwenye nilicho andika? Tumia akili na busara hata kama una mahaba sana kwa mtu sio kijongelea kwa jazba mpaka ulicho andika kina kasoro kwa sababu ya pupa una andika maneno nusu nusu.. Wingi wa taasisi yeye ana uwezo wa kuziondoa kbala ya kulalamika.
 
Makampuni hewa 17000 hili ndio lilikuwa lengo la kuwaita wafanyabiashara,walipe kodi
 
Back
Top Bottom