Ikitokea unawaza kwa sauti juu ya mabadiliko yaliyotokea uongozi wa awamu ya tano na ya sita, kwa huu muda mfupi unafikiri tutasikia maneno

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,279
Kwanza natoa pongezi kwa uongozi wote wa awamu ya sita kwa jitihada kubwa inayofanywa hasa ya kuondoa ujinga kwa watoto wetu kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kujenga shule na hospitali kila mahali kwa speed ya hali ya juu na kuendana na mahitaji na muda unaotakiwa, jambo ambalo limelazimika hadi wananchi tuchangie kwa kukatwa tozo za simu na huduma za kifendha lakini zaidi kuiomba dunia zile pesa za korona nazo pia zitusaidie kujenga shule, hali ambayo kwa hakika naamini hadi tarehe 17, January naamini haitakuwa hadi mtoto afaulu ila itakuwa ni kuhamisha darasa la saba lote na kulipeka shule ya upili yaani mtoto ashidwe mwenyewe tu.

lakini pamoja na yote hayo bado kama binadamu tulio hai huwa kuna mda tunafanya tathimini ya wapi tulikotoka na wapi tunaenda na nini kilifanyika na nini kinafanyika na nini kitafanyika.

Ikitokea nafasi ya kuwaza kwa sauti kama hivi, basi mimi nitawaza yafuatayo:

1. Iliwezekana vipi wabunge kuunga juhudi na kurudishiwa nafasi zao kwenye majibo, hali leo aliyekuwa mshawishi mkubwa kwa mujibu wa mchungaji peter msigwa, yeye ndio anaachia nafasi yake kubwa kwa hiari yake mwenyewe.

2. Iliwezekanaje kama taifa kupata vikwazo vidogo vidogo vya kupewa mikopo,lakini leo hii tunapata mkopo hadi wa tirioni saba na waziri wa fedha kuongea na moja ya benki kubwa duniani juu ya mkopo huo.

3. Iliwezekanaje Freeman Mbowe kuwa raia mwema na leo hii anatuhumiwa kuwa ni kama gaidi

4. Ilishindikanaje kipindi kile watu kupangiwa maeneo ya kufanyia biashara kama machinga na leo imewezekana bila shida yoyote ile na kwa upole wa hali ya juu sana. Iliwezekana sababu kuwa inachezea sh. 250 hadi 300 na leo imefika 600,

5. Iliwezekanaje ule msemo wa UNAJUJUA MIMI NANI kuisha na leo umerudi kwa kasi kubwa,

6. Iliwezekaje baadhi ya watu kipindi hicho kuwa hawakamatiki (untouchable) na leo wako jela na wengine kesi zinaendelea juu wa waliyoyafanya naamini kuna mengi ya kufikiria ila kama na wewe unalo la kuwaza kwa sauti basi ongeza hapa ili tufikilie wote tuone tunashaurianaje maana mlango wa kushauri uko wazi na umeshatangazwa
 
Ukiona mtu anatoa pongezi kwa serikali ambayo Rais wake ni fisadi anaehamasisha ufisadi kupitia TV ya Taifa basi jua huyo mtu ni tahira namba moja🤡🤡🤡
 
Back
Top Bottom