Ikitokea umefariki kama "Atheist" hauamini uwepo wa Mungu, Ikienda ukamkuta utamwambia nini?

Deep down, kuna vitu vinakua overrated sana

Wengi huwa wanasema ni bora uamini yupo, uende ukute hayupo. Kuliko uamini hayupo, uende umkute

Ukiwa hauamini uwepo wake, ukaenda ukamkuta, nini jambo gani utalitumia kujitetea
Etheist wanaamini uende wapi wakati ushakua mchanga. Siku ile roho inatoka kwenye mwili ndio imeisha uwepo wake yaani roho haiwezi kuishi nje ya mwili. Kwa hivyo nini kikute eti mungu yupo🤣
 
Nitamuuliza kwa nini duniani maisha hayapo fair kwa binadamu wote ?

Yaani ni kama mbio za marathon ambayo hatuanzi kwenye mstari sawa . Imagine mtoto Mwingine anazaliwa akiwa na virusi vya ukimwi ama kipofu haoni tena anazaliwa na wazazi maskini, walevi , wanatelekeza watoto . Mtoto anajilea mwenyewe akiwa na ukimwi juu.

Mtoto Mwingine anazaliwa akiwa na afya njema na tena anazaliwa na wazazi matajiri, wenye upendo na wanampa elimu nzuri, malezi bora. Na urithi wa mali juu mfano Mo dewji

Hapo nitamuuliza why hajaweka u fair ?
 
Deep down, kuna vitu vinakua overrated sana

Wengi huwa wanasema ni bora uamini yupo, uende ukute hayupo. Kuliko uamini hayupo, uende umkute

Ukiwa hauamini uwepo wake, ukaenda ukamkuta, nini jambo gani utalitumia kujitetea
Utetezi wake ni mdogo sana, kwamba: 'hapakuwepo na chanzo sahihi cha kisayansi kuthibitisha.'

Lakini ambacho najiuliza wale wenye hoja za kukataa uwepo wa Mungu muweza(Lord of the Lords), huwa hawajiulizi 'nidhamu' ya uwepo wa 'vitu', ilijianzia tu yenyewe bila mwasisi?

Mishepu ya binadamu kila mtu na sura yake na finger prints zake kwa mfumo wa password, kwa nini tusiwe na sura moja kama magari ya Land cruiser V8, nani alilisimamia hili nk nk?

Yapo mengi ya kustaajabisha ambayo huonekana kama ni ya kawaida kwa sababu tumezoea kuyaona yapo.

Yaweza kuwa mengi ya kumhusu Mungu ikawa ni 'kamba', lakini haiwezekani ukawepo uwepo wetu bila ya kuwa na mbunifu na muanziishi ambaye ndiye Mungu kweli.
 
Deep down, kuna vitu vinakua overrated sana

Wengi huwa wanasema ni bora uamini yupo, uende ukute hayupo. Kuliko uamini hayupo, uende umkute

Ukiwa hauamini uwepo wake, ukaenda ukamkuta, nini jambo gani utalitumia kujitetea
. ...eti uamini yupo afu ukute hayupo.......huu n upagan kama upagan mwingne ....bora ata atheist
 
Mkuu, kabla ya kutoa hii mada ulijiandaa kisaikolojia kupambana na ma atheist?
Atakuja Kiranga hapa atakushushia nondo unaeza jikuta unaukimbia uzi wako
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, angejidhihirisha kwa wote, bila utata, kwa wakati wote, wamjue, kwa namna ambayo hata mjadala huu usingewezekana. Mjadala huu kuwezekana ni uthibitisho Mungu hayupo.

Kujibu swali la msingi.

Nikikutana na Mungu nitamuuliza kwa nini kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya wakati aliweza kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya? Nitamwambia yeye ndiye chanzo cha ubaya wote na hana haki ya kuhukumu mtu kwa kufanya ubaya, kwa sababu bila ya yeye kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, hakuna mtu ambaye angeweza kufanya ubaya.

Ningemuuliza, kwa nini hakujiweka wazi kwa namna ambayo haiwezi kupingika kwa viumbe wote? Mungu kutoeleweka wazi yukoje ni chanzo cha vita nyingi za kidini na migogoro mingi ya kifalsafa, yeye alipenda hilo litokee? Alichekelea wakati nchi na nchi zinapigana, familia na familia zinauana, kwa sababu ya tofauti za kumuelewa Mungu?

Lakini, yote hayo hayatatokea.

Kwa sababu, Mungu hayupo.

Angekuwapo, hata huu mjadala tusingeweza kuufanya. Wote tungejua yupo bila ya shaka yoyote.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, angejidhihirisha kwa wote, bila utata, kwa wakati wote, wamjue, kwa namna ambayo hata mjadala huu usingewezekana. Mjadala huu kuwezekana ni uthibitisho Mungu hayupo...
umeona gari inatembea barabarani na imeandikwa made in china na ww unaamini yuko designer na maker wa hiyo gari bila hata kumuona lakini unapoangalia universe na mambo yake haumin kuwa yupo designer na maker unasema ulitokea bahati na sibu daah. Mtu wa hivi ata ukimuona utambishia kuwa siye YEYE (BWANA WA WOTE wenye mwili)) ukiwemo ww KIranga)
 
Kiranga akija hapa sijui kama mtaweza kujibu mapigo yake.... nawaambia mtaharibu mjadala wenyewe lakini hamtamuweza kwa hoja
Mjadala wowote, wenye swali lolote, kuhusu Mungu mjuzi wa vyote, mwenye uwezo wote na upendo wote, uwepo wake, kazi zake etc, ni ushahidi kwamba huyo Mungu hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, kwa hizo sifa zake, kimantiki kabisa, mjadala huo usingewezekana kuwapo.

Kwa sababu Mungu huyo, kwa vile ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote, angewapa waja wake ujuzi wote wa kumjua, asibakishe utata wowote kwenye akili zao. Na kama kuna mambo ambayo hawakutakiwa kuyajua, labda kwa faida yao, basi Mungu huyo angewaondolea hata uwezo wa kujiyliza maswali kuhusu hayo mambo.

Matokeo yake, mijadala kama hii ya kuhoji na kuhakiki uwepo wa Mungu huyo, isingewezekana.

Kuwezekana kuwepo kwa mijadala hii ya kuhoji, kuhakiki, kufanya thought experiments etc, inawezekana kwa sababu Mungu huyo hayupo kikweli kama Mungu.

Ni muhusika katika hadithi iliyotungwa na watu tu.
 
Kuna watu wanaodhani kwamba wakishupaa kuamini kwamba Mungu hayupo, ijapokuwa kweli yupo, basi hutoweka asiwepo.

Kuamini kwamba Mungu hayupo ni sawa kabisa na kuamini kwamba hata sie hatupo.

Kama akili za watu haziwezi kuaminika juu ya uwepo wa Mungu, basi haziaminiki kuhusu uwepo wa chochote.

Na hapo sasa ndipo tatizo kubwa huanzia -- kwamba mtu anaweza kudai kwa ujasiri kwamba hata yeye hayupo!
 
umeona gari inatembea barabarani na imeandikwa made in china na ww unaamini yuko designer na maker wa hiyo gar bila hata kumuona lkn unapoangalia universe na mambo yake haumin kuwa yupo designer na maker unasema ulitokea bahati na sibu daah....mtu wa hivi ata ukimuona utambishia kuwa siye YEYE (BWANA WA WOTE wenye mwili)) ukiwemo ww KIranga)
Kwanza kabisa, umefanya logical fallacy ya logical non sequitur.

Gari kuwa imeandikwa "Made in China" haina maana kuwa ni lazima imetengenezwa China na Hua Mulan. Inawezekana gari imeandikwa "Made in China" kwa sababu watu wanajua ikiandikwa hivyo itauzwa sana tu, na halafu Hua Mulan akawa ni muhusika wa hadithi ya kutungwa tu. Prove kwamba gari imetengenezwa na Hua Mulan huko China. Gari kuwa imeandikwa "Made in China" hai prove kuwa imetengenezwa China.

Pili, hoja yako ya msingi hapa ni kwamba, kila chenye order, kilicho complex, ni lazima kimeumbwa. Hakiwezi kutokea tu kuwa hivyo, ni kazima kina muumbaji wake.

Kwa akili ndogo ya kuangalia mambo juu juu tu, hapo unaweza kujiona kuwa umejenga hoja ya kutetea uwepo wa Mungu.

Lakini, kwa mtu anayepima mambo kwa mantiki kubwa, kwa kina, hiyo hoja yako haitetei uwepo wa Mungu. Kwa kweli, hoja hiyo inasema kuwa Mungu muumba vyote hayupo na kamwe hawezi kuwepo.

Tuiangalie tena hoja yako.

Unasema hivi:-

Kila kilicho complex, chenye order, ni lazima kiwe na muumbaji. Na huyo muumbaji ni lazima awe na order na complexity zaidi ya kilichoumbwa (otherwise unaruhusu evolution from less complex things to more complex things, ambayo haimuhitaji Mungu).

Sasa, ukishakubali hii kanuni, sawa, inaweza kukurudisha nyuma na kukuonesha kuwa Mungu ndiye muumbaji wa ulimwengu, watu etc. Lakini, kanuni hii hii bado itakubana.

Na Mungu naye ni complex na ordered. Na yeye atahitaji muumbaji wake. Atahitaji Mungu wake wa kumuumba. Na Mungu wake atahitaji Mungu wake. Hivyo hivyo bila mwisho. Ad nauseam, ad infinitum.

Hapo utaona kuwa hakuna Mungu muumba vyote.

Katika ulimwengu huo, hakuna Mungu muumba vyote.

Hoja yako, ambayo uliiona kama ya kutetea uwapo wa Mungu muumba vyote, kiukweli inatuonesha kuwa Mungu huyo hawezi kuwapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom