SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Simba kucheza mpira usiovutia, au wengine wanaita papatu papatu. Kuna wengine wamekuwa wanasifia uchezaji wa Yanga hivi sasa. Ngoja niwagusie mbinu mojawapo ninayoijua mimi ya kuwajenga wachezaji kuweza kucheza mpira wa umiliki yaani possession football.
Kuna zoezi fulani ambalo wachezaji wanakaa kwenye duara wanapasiana, halafu mchezaji mmoja au zaidi wanakuwa wanapambana kuugusa mpira. Ukiugusa, yule aliyepoteza anaingia kati. Najua wote mnaujua huu mchezo. Zoezi hili linaitwa "Rondo".
Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia jinsi timu za Tanzania zinavyofanya hili zoezi. Ni zoezi ambalo nadhani kwa wachezaji na timu za Tanzania halijaeleweka faida zake, ni kama zoezi ambalo wengi wanafanya kama la kujifurahisha tu kusubiri mazoezi mengine ila lina faida kubwa katika kumjengea mchezaji uwezo wa kutoa pasi za uhakika kwa haraka na uwezo wa kufikiri.
Moja ya kitu nilichogundua kwa Simba ni kuwa hili zoezi wanalifanya sana ila wachezaji hawako vizuri kabisa, wachezaji hawawezi kumiliki mpira bila kuupoteza kwa muda mfupi sana. Huwezi kuona video ya mazoezi ya Simba uwanjani usione wakifanya Rondos. Yanga huwa nikiangalia mazoezi ni nadra sana kuona wakionyesha rondos zao ambalo ni jambo la kushangaza ila nakumbuka kila nikiziona niligundua wachezaji wake wako vizuri sana kwenye hili zoezi. Siri inaanzia hapa.
Hii hapa ni video ya mazoezi ya Simba ya leo tu wakifanya rondo. Ukiingia kwenye channel ya Simba ukatafuta video yoyote wanayofanya mazoezi, utaliona hili ninalolisema. Wachezaji wanakosa umakini wa kukaa na mpira na kutoa pasi bila kupoteza. Sisemi wachezaji wa Simba hawana uwezo, ila nadhani kuna hali fulani ya kurelax na matokeo yake bongo zao zinafubaa inafika kwenye mechi wanakosa ile usharp wa akili unaohitajika.
View: https://www.youtube.com/watch?v=7Dq9cA3oc_c
Linganisha na Rondos za timu zinazojulikana kwa kucheza possession football kama Barcelona au Manchester City.
Hizi hapa Rondos za Barcelona (unaweza kuzipata nyingi Youtube)
View: https://www.youtube.com/watch?v=oofexHQGCbM
View: https://www.youtube.com/watch?v=UUV5gbknTG0
Hii hapa rondo ya Manchester City
View: https://www.youtube.com/watch?v=--cyAUmN85w
Mtu akipata rondo yoyote ya Yanga ya hata kipindi cha Nabi aiweke mtaona ninachokisema ni nini.