Ijue pombe na Hangover kitaalamu

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Kwa lugha za kikemikali pombe ni organic compound iliyo na mchanganyiko wa kemikali za Carbon, hydrogen na oxygen (ROH). Pia ipo kwenye familia moja kikemikali na mafuta (Cholestrol) na wanga (Carbohydrates).

NINI HUTOKEA MWILINI MTU ANAPOKUNYWA POMBE?

Asilimia 10 ya pombe unayokunywa haiendi moja kwa moja kwenye ini bali hutolewa kwa njia ya hewa, mkojo na jasho.

Kiasi kinachobaki yaani asilimia 90 huenda kwenye ini kupitia mishipa ya damu iliyopo tumboni na kumengenywa (Metabolised) kwa kutumia vimengenyo (Enzymes) za aina mpaka tatu zilizopo kwenye ini. Kumbuka kuwa mwili wetu hauhitaji alcohol hivyo pombe inamengenywa ili itolewe mwilini kazi ambayo inafanywa na Ini (Liver) mwilini.

Kwenye ini, kimengenyo kikuu au enzyme inayo process alcohol ni alcohol dehydrogenase (ADH) na huibadili kwenda kwenye kemikali za acetaldehyde baadae acetate na mwisho kwenda kwenye hewa ya carbon dioxide na maji.

Kemikali ya acetaldehyde ni sumu ambayo ni jamii ya formaldehyde na Acetate ni kemikali iliyopo sana kwenye vinegar ambazo ki msingi hizi kemikali huingia kwenye mzunguko wa kutengeneza nguvu (ATP) mwilini ujulikanao kama krebs cycle ambapo mfumo huu huzalisha nguvu (ATP) na hewa ya carbon dioxide pamoja na maji ambavyo vinatolewa mwilini.

Kemikali aina ya formaldehyde ambayo ni zao la mmengenyo wa alcohol mwilini tunasema ni sumu kwa sababu kemikali hii ndio hutengeneza antseptic kama dawa za fungus, bacteria na kemikali kama dettol, spiriti n.k! Acetaldehyde inapokuwa kwa wingi mwilini baada ya kunywa pombe huleta madhara yanayokera kama hangover na hata kifo (Intoxication).

Pia kemikali hii huleta madhara ya mwili na ubongo pindi mtu anapokunywa kupindukia (Chronic effect).

MAHESABU YA KIWANGO CHA POMBE KWENYE VINYWAJI KAMA BIA

Kila kinywaji chenye pombe au alcohol hasa zinazotengenezwa viwandani lazima utakuta kiasi cha pombe kilichomo kwa kuandikwa percentage ya ujazo (v/v) au uzito (w/w)..Kwa mfano chupa ya bia ya Kilimanjaro utaona kwenye lebo imeandikwa 5.5 % alcohol (v/v) maana yake ni kuwa 5.5 mls za alcohol zipo kwenye 100mls za mchanganyiko wa kinywaji husika ambacho ni Kilimanjaro beer kwa huo mfano hapo juu.

Hii hesabu humsaidia mnywaji au mlevi kujua ni kiasi gani cha pombe anaingiza mwilini na hivyo kujikadiria kiasi anachotaka kutumia..Ikumbukwe pia kuwa kadri unavyokunywa kiasi kingi (Consumption) cha alcohol basi na madhara yake huwa makubwa (Acute effect huwa kubwa pia)

Twende vizuri kwenye hili…..

ü Specific gravity ya alcohol ni 79, hivyo basi lita 1 ya alcohol ina uzito wa 790g

ü Kwa Ujazo (V/V), lita 1 ya alcohol ukiongeza lita 1 ya maji ni sawa na 50% (Vol)

ü Kwa uzito (W/W), lita 1 ya alcohol ambayo ni sawa na 790g ukiongeza na 790g za maji ni sawa na 50% (weight)

Maelezo haya ni muhimu ili mtumiaji aweze kujua kipimo cha pombe anachotumia na kiwango kinachokubalika kwenye mwili wa binadamu yaani Blood Aclohol concentration.

Kama nilivyoeleza hapo juu, Blood Alcohol concentration (BAC) ni kipimo ambacho husaidia kujua kiasi cha pombe kilichopo kwenye damu..Baadhi ya vitabu vinaelezea kuwa kiwango cha juu ni 0.004 % ndicho kinachokubalika na hii ina maana kuwa 0.004 gm za alcohol zikiwa kwenye 100 mls za damu mwilini ndio kiwango kinaweza kukubalika kiafya. Kiwango hiki kinapokuwa juu basi na madhara ya pombe ni makubwa mwilini.

Kwa hiyo ili uweze kujua unahitaji bia ngapi za kunywa bila kufikia kiwango kisichoruhusiwa basi unaweza kujua kwa kutumia hiyo calculation.

MADHARA YA POMBE KITAALAMU

Makala nyingi zimeshaelezea madhara ya pombe lakini leo najikita kitaalamu zaidi kuilezea kwa mtiririko wa tofauti..Kiwango cha madhara kinatofautiana na kiasi cha alcohol (Consumption) ambacho kipo kwenye damu (mg per deciliter) hivyo kupelekea madhara kuwa na utofauti pia.

Mifumo ya mwili ambayo huathirika na pombe ni kama ifuatavyo na nitakuja na makala siku nyingine kuelezea kwa kirefu zaidi madhara hayo ya pombe ila leo tujikite kuifahamu ki undani alcohol kitaalamu.

§ Mfumo wa fahamu au Central Nervous System (CNS)

§ Mfumo wa damu na mishipa ya Damu au Cardiovascular system

§ Mfumo wa upumuaji au Respiration

§ Madhara kwenye Damu

§ Mfumo wa Tumbo (GIT)

§ Figo, mfuko wa uzazi (Uterus),Kisukari na hamu ya mapenzi (Aphrodisiac).

AINA ZA VINYWAJI NA KIWANGO CHA ALCOHOL KWENYE VINYWAJI HIVYO

1. Malted liquors- Hizi ni pombe zinazotokana na fermentation ya mbegu za nafaka kama malt cereals (Barley) mfano ni beer (3-6% ya alcohol iliyomo)

2. Wine- hizi hutokana na fermentation ya sukari iliyopo kwenye matunda kama zabibu na apples na ambapo ikiwa hakuna distillation wakati wa kuandaa pombe hutoa asilimia chini ya 15 ya alcohol, ikiwa fortified hupata hadi 22% ya alcohol na champagne 12-16%

3. Spiritis-Rum,Whisky,Brandy na Gin huwa na hadi asilimia 55 na zaidi ya kilevi


HANGOVER INAVYOTOKEA

Kama unavyojua weekend inapofika basi ni jambo la kawaida watu kujivinjari kwa kupiga mitungi ya kutosha lakini hali huwa tofauti siku yake asubuhi na hasa kama ni siku ya kazi hasa Jumatatu.. Watu wengi hukimbilia kwenye supu na kunywa maji mengi na bila shaka utajua kuwa ni pombe ambayo imesababisha mninginio huo. Lakini wengi hawajui kinachotokea mwilini au nyuma ya pazia mpaka kutokea hali hiyo…

Hebu tujiulize ni kipi husababisha hali hiyo?

Hang over mara nyingi hutokea masaa 8 hadi 16 baada ya unywaji wa pombe kwa wingi..Haya matokeo ni mchanganyiko wa mambo kadhaa hasa kwenye mmengenyo (Metabolism) wa pombe na baadhi ya kemikali (Products) zitokanazo na mmengenyo wa pombe.

Ni mambo mengi husababisha hali hii kwa mfano kukojoa sana (Dehydration) , mabadiliko ya homoni baada ya kunywa pombe (ant diuretic hormone alterations), mabadiliko ya kikemikali mwilini (electrolytes imbalance and inflammatory molecules) na mabadiliko ya kiwango cha sukari mwilini (Blood sugar swings).

Ki ufupi ni kuwa unapokunywa pombe sana, mapigo ya moyo huongezeka lakini ubongo una punguza ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kutolewa kidogo kwa homoni ya Ant Diuretic Hormone ambayo kazi yake ni kusaidia kutunza maji mwilini kwa kudhibiti kukojoa hovyo..

Homoni ya ADH inapopungua au kutolewa kidogo maana yake ni kuwa utakojoa sana na kufanya mwili kukosa maji ya kutosha hivyo kupelekea kusikia kiu sana na itakufanya uzidi kupiga mitungi zaidi..Unapozidi kupiga mitungi zaidi ndipo homoni hii muhimu haifanyi kazi yake kabisaa na kukufanya kukojoa sana na maji kupungua mwilini mwishowe kunakuwa hakuna uwiano wa kemikali kabisa (Electrolyte imbalance mwilini)..Kumbuka pombe inapoingia mwilini na kumengenywa kwenye ini hupelekea kiasi cha acetaldehyde huzalishwa kwa wingi na huleta madhara.

Hii kemikali ya Acetaldehyde inapozalishwa kwa wingi mwilini husababisha madhara ya kukera (Flushy syndrome) kama mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kutoka jasho sana (Cold sweating), kichefu chefu na kutapika. Kitaalamu hii kemikali ndio kiini hasa cha hangover kuliko kukosa maji kama nilivyoelezea mwanzo.

Pia unywaji wa pombe hufanya mishipa ya damu hasa inayopeleka damu kwenye ubongo na kichwa kutanuka (Dilation) na hivyo kufanya Kichwa kuuma sana (Headache). Hii pia ni sababu kuu ya hangover na madhara haya yanaweza kutoka kwa kunywa antpain kama aspirin!

TIBA HASA YA HANGOVER NI IPI?

Tiba hasa ya moja kwa moja haipo ila unaweza ku deal na tatizo moja husika (Syndrome) kwa kunywa dawa!Kwa mfano kama kichwa kinauma basi unaweza kunywa dawa za kupunguza maumivu ya kichwa kama Ibuprofen au Aspirin.

Pia inaelezwa kuwa caffeine ambayo hupatikana kwenye kahawa, sukari na vitamin B6 imesaidia kiasi kikubwa kupunguza hangover! Unywaji wa maji hupunguza pia hang over japo wengi hupiga supu kwa wingi hasa mchuzi wa supu kusaidia kupunguza hali hii ya kukera!

HITIMISHO

Lengo la makala hii ni kutoa ufahamu hasa ikizingatiwa kwamba wengi tunatumia vitu bila kujua nini hutokea mwilini. Japo sijaangazia kwa undani madhara ya pombe ila naamini kuifahamu kitaalamu pia utaweza kujua kinachoendelea mwilini baada ya kunywa pombe.

Naamini elimu hii fupi imekupa mwanga kitaalamu jinsi mwili unavyopambana na pombe au kemikali zinazozalishwa baada ya pombe kuwa mwilini. Siku njema!
 
Ibuprofen na aspirin? c'mon man unashauri raia watumie dawa hatari namna hiyo kukata hang over? Soma vizuri kabla ya kupost vitu kama hizi.
 
The issue hapo ni kuondoa maumivu ya kichwa na si kutibu hangover..Hata hivyo inabidi mtu awe mwangalifu..asante kwa umakini
 
Mleta mada naomba kujua ni kwanini kama umeamka na Hangover halafu ukazimua na bia moja unarudi na kuwa fiti?
 
R-OH.

R=alkyl group.

OH=hydroxyl group.

Mkuu mbona hujamuongelea baba wa pombe zote ethyl alcohol(CH3CH2OH) walau kidogo.
 
The issue hapo ni kuondoa maumivu ya kichwa na si kutibu hangover..Hata hivyo inabidi mtu awe mwangalifu..asante kwa umakini
Sonaderm

Umesema hang over inasababishwa na chemical ya acetoldehde kuwa nyingi mwilini,

so nilitegemea main solution hapa iwe ni kupunguza kiwango cha hiyo chemical mwilini

How do we go about
 
Sonaderm

Umesema hang over inasababishwa na chemical ya acetoldehde kuwa nyingi mwilini,

so nilitegemea main solution hapa iwe ni kupunguza kiwango cha hiyo chemical mwilini

How do we go about
Ukipunguza pombe na kiwango cha acetaldehyde kinakuwa kidogo
 
Mleta mada naomba kujua ni kwanini kama umeamka na Hangover halafu ukazimua na bia moja unarudi na kuwa fiti?
Hakuna ukweli kwenye hilo naweza kusema..ila kwa sababu mtu anapokuwa na hangover anakuwa dehydrated na pombe ni kimikinika basi mtu hupata afadhali ila kuna hatari ya kurudi kwenye ulevi au hangover kali..
 
Vipi katika maelezo yako yote sijaona faida ya pombe ina maana pombe haina faida
 
Mleta mada hivi unaongelea pombe ya aina gani? kwakua kila pombe ina Stim yake na madhara yake kwamfano Kiroba! hembu tufafanulie!
 
Back
Top Bottom