Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,196
IJUE MITEGO 3 YA KICHAWI
Wachawi hutumia mbinu mbalimbali katika kufanikisha mipango yao ya kichawi kwa watu walio kusudia kuwadhuru kwa uchawi.
Leo nitaizungumzia mitego mikuu mitatu ambayo watu wengi hawaifahamu.
1.MTEGO WA SHILINGI
Mtego huu wa kichawi ni maarufu sana katika mikoa ya Rukwa/Katavi ,Tabora, Shinyanga/Simiyu na Kigoma pamoja na katika baadhi ya wilaya za mkoa wa Mwanza hususani wilaya za Magu, Kwimba na Ukerewe.
Nchini Tanzania, uchawi huu asili yake ni katika mkoa wa Tabora , wilaya ya Urambo .
Uchawi huu uliingia katika wilaya ya Urambo ukitokea nchini Kongo.
Kutoka wilayani Urambo mkoani Tabora, uchawi huu ulisambaa kwa kasi ya ajabu sana katika mikoa tajwa hapo juu na kwa sasa umesambaa nchi nzima.
UCHAWI WA MTEGO WA SHILINGI NI UPI ?
Uchawi wa mtego wa shilingi ni uchawi unao fanya kazi ya kufunga rizki ya mtu na kumfilisi kabisa.
JINSI INAVYO KUWA :
Ili mchawi afanikiwe kufunga ridhiki ya mtu wake kwa kutumia aina hii ya uchawi ni lazima afanikiwe kupata hela yoyote yenye thamani ya chini sana kutoka kwa mtu wake.
Hela hiyo ni lazima isiwe ya karatasi na ni lazima iwe hela yenye thamani ndogo sana.
Huwa inakuwa hivi, mzee mmoja unae muheshimu sana mtaani kwenu ama kijijini kwenu atakufuata na kukuomba umsaidie shilingi hamsini, au shilingi mia au shilingi mia mbili ( Miaka ya nyuma walikuwa wanaomba shilingi, thumni, sh.kumi au sh.tano au shilingi ishirini zile za chuma,ambazo kwa sasa hazipo tena kwenye mzunguko wa fedha.
Mzee huyo atakwambia anataka kununua kahawa au ugoro na ana shida na shilingi hamsini tu. Kama sio mzee basi anaweza kutumwa hata mtoto mdogo na kukwambia naomba sh. Hamsini nikanunue pipi n.k.
Ukimpa shilingi hamsini, utakuwa umejiroga Shilingi hiyo hamsini itakwenda kufanyiwa uchawi mbaya sana ambao siwezi kuelezea hapa namna unavyo fanyika. Matokeo ya uchawi huo ni kwamba rizki yako itafungwa kabisa, utakuwa unashika shilingi Hamsini hamsini tu, thamani yako itakuwa sawa sawa na thamani ya shilingi hamsini, na mwisho wa siku utafilisika kabisa na kurudia maisha ya chini kabisa.
watu wengi sana wameumizwa bila kujua kwa uchawi huu hatari kabisa.
2. MTEGO WA NYOKA.
Lengo la mtego huu ni kumchukua mtu msukule ama kumuua kabisa kwa njia ya uchawi. Vile vile mtego huu unatumika kuua vitoto vichanga, kumuua mwanamke mjamzito au kunyofoa mimba ya mwanamke mjamzito na kumfanya asizae.
Mtego huu ni wa hatari sana kwani kuubaini ni vigumu sana kama mwili hauko vizuri na kwa jinsi unavyotumwa ni vigumu sana kuchomoka , yaani lazima uingie mtegoni.
JINSI INAVYO KUWA :
Mtego huu mara nyingi huwa unakuja katika sura kuu 5 :
1. Jini aliye vaa sura na umbo la nyoka huingia hadi chumbani kwako, au hukutokea bafuni au chooni . Kwa vyovyote vile lazima utatafuta njia ya kumuua, ukimuua tu huyo nyoka na wewe ndio unakuwa mwisho wako hapo, kwa sababu utakuwa unajiua mwenyewe. Baada ya kumuua nyoka huyo utaugua kwa sana na mwisho wa siku utakufa . Nyoka huyo wa kichawi anakuwa ameunganishwa na nafsi yako mwenyewe , hivyo kitendo cha wewe kumpiga nyoka huyo wa kichawi unakuwa unainyonga nafasi yako mwenyewe bila kujijua. NI HATARI SANA!
2. Ndugu yako ama jirani yako ( ambaye lazima atakuwa mwanamke ) atakuja nyumbani kwako na kukwambia kuwa kuna nyoka mkubwa ameingia nyumbani/chumbani kwake, sasa ameshindwa kumuua au anaogopa kumuua, na nyumbani kwake kuna watoto tu, hivyo anakuomba ukamsaidie kumuua huyo nyoka. Ukienda kumuua huyo nyoka, umejiua mwenyewe. Utaugua sana na mwisho wa siku utakufa.
3. Ukiwa na mgonjwa ambaye amelazwa nyumbani , atatokea nyoka karibu na kitanda chake na wewe ukiwa kama mwanaume katika familia hiyo, utalazimika kwenda kumuua nyoka huyo ili asimdhuru mgonjwa wako...Ukisha muua tu huyo nyoka, mgonjwa wako hatomaliza siku saba atakufa.
4. Mke wako akiwa anakaribia kujifungua, nyoka huyo atajitokeza katika chumba unacholala wewe na mke wako au katika eneo lolote atakalo kuwapo mke wako. Ukiwa kama mwanaume, kwa vyovyote vile utalazima kumuua nyoka huyo. Ukifanya hivyo, mke wako atakufa wakati wa kujifungua. Au atazaa mtoto aliyekufa na yeye ataugua sana na mwisho wa siku atakufa.
5. Mke wako akiwa amejifungua mtoto au watoto, nyoka huyo ataonekana katika chumba ambacho watoto wenu watakuwa wamelala, eidha peke yao au pamoja na mama yao. Kwa vyovyote vile, utalazimika kwenda kumuua huyo nyoka, ukifanya hivyo, watoto wako wataugua sana na mwisho wa siku watakufa.
DAWA YA KUJIKINGA NA NYOKA WA KICHAWI NI NINI ?
Kuna mti mmoja unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe.
Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.
Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi.
Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.
Dawa hii itakupa pia uwezo wa kuwaona misukule.
Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.
Hata ukikaa mahali kama kuna nyoka hawezi kukaa hapo, atakimbia tu.
Ukichanjiwa unga unga wa mti huu pamoja na mafuta ya nyonyo, na mafuta ya samba, nyoka wa kichawi hawawezi kukudhuru .
Ukichukua unga unga wa mti huu, ukachanganya na unga unga wa mti wa mfa usiku, ukaufunga kwenye kitambaa chesi, ukafukia mbele na nyuma ya nyumba yako, nyoka wa kichawi hawawezi kuingia ndani ya nyumba yako. Hata nyoka wa kawaida hawawezi kuingia ndani ya nyumba yako. Wachawi hawawezi kuingia ndani ya nyumba yako.
3. MTEGO WA ULIMI
Wachawi wanapotaka kumuua mtu kichawi hufanya mambo mbalimbali ya kichawi. Baada ya kufanya ulozi wao ,moja kati ya mambo makubwa wanayo yafanya ni kutengeneza hati ya kichawi ya kifo cha mlengwa wa uchawi. Hati hiyo ya kichawi itasainiwa na mlengwa mwenyewe kabla ya kutekelezwa bila ya mlengwa mwenyewe kujijua kama ana saini hati ya kifo chake mwenyewe.
KWA NINI NI LAZIMA MLENGWA ASAINI HATI YA KICHAWI YA KIFO CHAKE MWENYEWE
Kila binadamu anayeishi duniani ameletwa na Mungu kwa ajili ya kutimiza yale aliyokadiriwa mpaka ifike siku yake maalumu. Binadamu huyo hawezi kurudi kwa Mungu bila kutimiza kadari hiyo, hivyo ni vigumu sana kwa wachawi kumuua mtu yoyote maana watakuwa wanaingilia kazi ya Mungu ndyo maana pakasemwa WANA IDHULUMU NAFSI yaani anakufa machoni petu na kutumikishwa na wachawi lakini ikifika siku yake ndyo anakufa kiukweli na roho yake inarudi kwa muumba wake
Hivyo basi wachawi hufanya namna au kutengeneza mtego utakao mfanya mlengwa kutia saini kwenye hati ya kifo chake mwenyewe bila kujua kama anajiua mwenyewe.
JINSI INAVYOFANYWA
Siku saba kabla ya mtu Fulani kuchukuliwa kichawi. Maneno ya kichawi yatakayokuwa yameandikwa kwenye mfano wa sura ya nafsi ya mlengwa huwa kama ifuatavyo
Kwa mfano kama wewe jina lako unaitwa “ ALLY” na imekusudiwa uwe haupo duniani ifikapo siku ijumaa. Maneno yatakayokuwa yameandikwa kwenye mfano wa sura ya nafsi yako ni “ALLY BIN (JINA LA MAMA AKO ) SIKU YA ijumaa HATOKUWEPO DUNIANI “
Ili maneno hayo yakamilike, ni lazima ALLY mwenyewe akiri kwa kinywa chake kuwa siku hiyo hatokuwepo.
HEBU TUONE UCHAWI HUU
Kwa mfano mchawi anajua kuwa , wewe ALLY ambaye una miliki duka la dawa za ASILI pale Tanga, dini yako ni muislam na siku za Ijumaa huwa haufanyi kazi unaenda msikitini
.
Siku moja kabla ya “ kifo” chako, mtu mmoja atakupigia simu na kukwambia kuwa,kesho ijumaa atakuja dukani kwako kuchukua mzigo hapo, halafu atamalizia kwa kukuuliza “ UTAKUWEPO ?” Kwa vyovyote vile lazima utamjibu “ SITAKUWEPO !”. Hapo ndio utakuwa umesaini hati ya kifo chako mwenyewe. Maneno yako yatakwenda kutumika dhidi yako mwenyewe.
Kwa ufupi tu ni kwamba, katika mtego huu, utaulizwa swali “ utakuwepo?” ambalo kwa vyovyote vile majibu yake yatakuwa “ SITOKUWEPO “
KUJIKINGA NA UCHAWI HUU :
Kujikinga na uchawi huu, epuka sana kutumia neno “ SITOKUWEPO!” Badala ya kujibu “Sitokuwepo” jibu kwa kutaja sehemu utakayo kuwepo.
Kwa mfano,hapo Bwana ALLY atatakiwa kujibu “ SIKU YA KESHO NITAKUWA MSIKITINI