Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,109
- 53,626
Jibu lako " mfumo mbovu" hasa ndio tatizo kuu kwa wakulima.
Bila kubadilisha mfumo wetu ( siasa hapa inaingia) benki haitakuwa na manufaa sana. Ngoja nifafanue. Kuna sheria inasema, sijui kifungu chake, " kiongozi wa serikali anaweza kuzuia mkulima asiuze mazao yake kwa sababu tu, kuna dalili ya njaa katika eneo lake la utawala bila kujali gharama alizoingia mkulima husika", utasikia, hakuna kuuza mahindi mabichi, dc kakataza. Haya, kuna wakati serikali inafungulia maghala ya hifadhi ya chakula na kuuza kwa bei ya chini kisiasa. Wakulima wanashindwa kurudisha mikopo.
Nchi yetu haina Bima katika kilimo, sasa mkopaji huyu aliyepitiwa na ukame/mafuriko analipaje mkopo. Mimi nimejikita ktk misitu, lakini serikali hata ktk misitu yake yenyewe ya Sao Hill hawana Bima, ila makampuni ya kigeni kama grl yana Bima. Kuna mchele toka nje, huu umeua soko la wakulima wetu,waulize bonde la Usangu kilicho wapata.
Kyerucu ilikuwa inauza kokoa nje ya nchi kwa Us $, siasa zikaingia Kyerucu ikafa. Huko kwa wenzetu wakulima wanapewa ruzuku ili waweze kulima kwa malengo na faida na hivyo kilimo kwa wenzetu kuwa kazi ya matajiri wenye elimu nzuri.Hapa kwetu kilimo kinaonekana kazi ya laana, angalia graduate wa SUA wako benki wanahudumia wateja,mama zetu na bibi zetu ndio wanalima vijijini.
Hati za kumiliki shamba zinapatikana kwa taabu na gharama kubwa, hivyo wengi wanashindwa kutumia mashamba yao kama dhamana ktk benki, sasa sijui hii benki itatoaje mikopo kama wakulima hawana hati za mashamba yao,maana hata hati za kimila hazikubaliki benki. Ila kama wanalenga wakulima wachache mafisadi basi benki hiyo itakuwa sio yetu.
Sijui wanaposema riba nafuu wanamaanisha nini? au kiasi gani?
Tuje katka bidhaa za ndani kushindana na bidhaa za nje, kuna wakati kuku walitoka SA lakini kuna wakulima pale Singida hawajui wapeleke wapi kuku wao. Kuna apples Njombe,lakini tunakula za SA, mpaka samaki wanatoka Japan wanaliwa Tanga mjini.
Ili benki yetu ifanye kazi, ni lazima kuwe na mazingira rafiki kwa wakulima kuifikia, serikali iangalie sera za kilimo na bishara za mazao za mazao ya kilimo upya kwa kutushirikisha wakulima tulioko shambani kupitia vyama vyetu. Serikali isimamie uboreshaji/usindikaji wa mazao ya wakulima ili tuweze kuingia soko la nje.
Umejibu vyema mkuu.
Kesho nitakujibu vizuri nikitulia.