Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,172
- 133,260
Wanabodi,
Leo ni Tarehe 7 mwezi wa August, kesho ni tarehe 8 August, siku ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane, Tanzania licha ya uchumi wetu kutegemea kilimo, hatujawahi kuwa na Benki mahasusi ya kilimo, CRDB ndio illanzishwa kwa madhumuni hayo akiitwa Cooperative & Rular Development Bank yaani Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijini ikitegemewa itawakopesha wakulima kupitia vyama vya ushirika, it didn't!. Ikabinafsishwa sasa neno CRDB ni synoname tuu!.
Sasa kesho, tarehe 8. August, Tanzania tunakwenda kuzindua benki specific kwa kilimo. Hivyo hii ni makala elimishi kuhusu benki hii.
Karibu.
IJUE BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA [TADB]
1.0 Utangulizi
Katika juhudi za kuinua ukuaji wa uchumi na Kupunguza umaskini nchini Tanzania, Serikali imechukua hatua mbalimbali zikilenga kuharakisha mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo ina ajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya Tanzania.
Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji; ukosefu wa mbinu na teknologia za kisasa; matumizi madogo ya umwagiliaji; ukosefu wa mtaji na upatikanaji wa mikopo kwa wakulima; ukosefu wa masoko ya mazao na yasiyotosheleza; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu ya ya vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo.
Changamoto hizo hapo juu, zikiambatana na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa; mikopo ya muda mfupi mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa; sekta ya kilimo imekuwa ikikosa mikopo ya kutosha kuendeleza kilimo chenye tija kwa mkulima/wakulima nchini.
Kutokana na changamoto tajwa hapo juu, Serikali imeamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuweza kuwezesha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuhamasisha taasisi zingine za fedha nchini kusaidiana na Benki Kuu ya Tanzania kuongeza kiasi cha kutoa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuwezesha mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Kilimo. TADB kwa sasa iko tayari baada ya kukamilisha masharti yanayotakiwa na Benki Kuu ili kupatiwa leseni ya kudumu kuanza shughuli zake rasmi baada ya kuzinduliwa tarehe 8.8.2015.
2.0 Madhumuni ya Kuanzishwa kwa TADB
TADB ilianzishwa kwa madhumuni makuu yafuatayo, pamoja na mengine:
i. Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula nchini, na kuchangamkia fursa zilizopo za uuzaji wa bidhaa za Kilimo nje ya nchi;
ii. Kuchangia ongezeko la uzalishaji kwa njia ya upatikanaji wa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwenye sekta ya Kilimo na kwa riba na masharti nafuu;
iii. Kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya miradi ya umwagiliaji; usafirishaji; uhifadhi; masoko; na usindikaji/utayarishaji wa mazao ya Kilimo;
iv. Kutafuta fedha na rasilimali nyingine ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu ya muda wa kati na mrefu kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo;
v. Kuwa benki kiongozi ya Kilimo yenye kusaidi kujenga uwezo na kuchagiza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye sekta ya Kilimo;
vi. Kuwezesha taasisi za fedha kukopesha zaidi katika sekta ya kilimo kwa kuzipatia mikopo ya riba nafuu kwa njia ya kuzirejeshea fedha zinazokopesha mikopo ya muda mfupi kati na mrefu kwenye Sekta ya Kilimo;
vii. Kuwezesha benki za maendeleo ya jamii, vyama vya kuweka na kukopa, taasisi ndogo za fedha, vyama vya ushirika, kwa kuzipatia mikopo ya riba nafuu kwa njia ya kuzirejeshea fedha zinazokopesha mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu zilizotoa kwenye sekta yakilimo;
viii.Kutoa mikopo ya moja kwa moja kwenye miradi mikubwa ya kilimo ya muda mfupi, wa kati na mrefu yenye masharti nafuu; na
ix. Kushirikiana na benki za maendeleo na za biashara kuwezesha kutoa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwenye miradi mikubwa ya kilimo, miundo mbinu ya kuwezesha kilimo cha kisasa, uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, ununuzi wa zana za kisasa za kilimo na uwekezaji mwingine wowote unaolenga kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo.
3.0 Umuhimu wa TADB kwenye Kilimo cha Tanzania:
Kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), kuna umuhimu ufuatao:
a. Kurahisishwa kwa upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara vilivyo kwenye soko;
b. Kuwepo kwa mfumo mahususi wa uratibu wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mnyororo wa ongezeko la thamani kwa mazao ya Kilimo (yaani kuanzia uzalishaji, hatua mbali mbali za uongezaji wa thamani, hadi masoko ya mwisho ya bidhaa na hatimaye kumfikia mlaji) na kusaidia kuwaunganisha wakulima na masoko.
c. Kuongezeka upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile uandaaji wa andiko la miradi ya ya Kilimo, upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba, na kadhalika;
d. Kuratibu taarifa za utafiti na maendeleo ya Kilimo, hali ya hewa, udongo unaofaa kwa Kilimo, pamoja na hatua nyingine za kuhuisha maendeleo kwenye Kilimo;
e. Kutoa ushauri wa kisera kwa serikali na kujadiliana na serikali na wadau mbali mbali wa Kilimo ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na uendelezaji wa Sekta ya Kilimo;
f. Kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la Taifa kutokana na upatikanaji wa fedha za kutosha kuendeleza kilimo na uzalishaji kwa masharti na riba nafuu;
g. Ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo na ajira nchini;
h. Kuhuishwa kwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miundo mbinu ya Kilimo na Vijiji; i. Mapinduzi ya Kilimo kutoka kile cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara;
j. Kusambaza huduma za Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) hadi kwenye ngazi za Wilaya kupitia wakala mbalimbali kama vile matawi ya benki za biashara, vyombo vidogo vya fedha, Benki za maendeleo ya jamii, na vyama vya ushirika vya kutoa mikopo.
4.0 Bidhaa na Huduma za TADB
Benki imejipanga kutoa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwa njia ya urejeshaji wa fedha, ushirika wa utoaji fedha, na utoaji wa fedha za miundombinu ya Kilimo, hususan kuziba pengo la upatikananji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki) za kipaumbele.
Kwa kuanzia, sekta zitakazopewa kipaumbele ni nafaka hasa mazao ya mahindi na mchele, mifugo hasa maziwa na nyama, ufugaji wa kuku wa kienyeji, uvuvi hasa ufugaji wa samaki, matunda, mboga mboga viungo (spices), na maua, mazao ya viwanda hasa miwa, mbegu za uzalishaji mafuta ya kula, na mazao ya misitu hasa ufugaji wa nyuki na mazao yake. Benki itawezesha upatikaji wa mikopo ya muda mfupi, wa kati na mrefu katika minyororo yote ya ongezeko la thamani katika sekta zilizotajwa hapo juu kwa kuanzia.
Benki itatumia bidhaa mbalimbali zenye ubunifu katika kuwezesha taasisi za fedha na taasisi, benki za maendeleo ya jamii, vyama vya kuweka na kukopa, taasisi ndogo za fedha, vyama vya ushirika na taasisi au vyama vya wakulima kutoa mikopo katika minyororo ya thamani.
Bidhaa hizo ni kama stakabadhi za mazao ghalani, mikopo ya uzalishaji mazao ya kilimo hasa katika kilimo cha mikataba, mikopo ya pembejeo za kilimo, mpango wa mikopo ya dhamana ya vikundi, kutoa mikopo ya riba nafuu kwa taasisi mbalimbali zilizotoa mikopo katika sekta ya kilimo kwa kurejesha fedha za mikopo iliyotolewa kwenye kilimo;
Usimamizi wa Makubaliano ya Dhamana, Mikopo ya vifaa vya Kilimo kwa ajili ya uboreshaji wa mbinu za Kilimo na miradi ya umwagiliaji, na zana za miradi mingine ya uwekezaji. Benki pia itasimamia fedha zinanzoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo na vijiji nchini.
Kwa upande wa masharti ya mikopo, Benki imejipanga kutoa mikopo ya riba nafuu ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwa riba nafuu kwa kupitia taasisi za fedha, benki za maendeleo ya jamii, vyama vya kuweka na kukopa, taasisi ndogo za fedha, vyama vya ushirika na taasisi au vyama vya wakulima.
Kwa miradi mikubwa ya kilimo inayoendeshwa kati ya Serikali, taasisi za serikali na binafsi; mikopo ya moja kwa moja itatolewa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo hasa kuimarisha mifumo ya minyororo ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo.
Source: TADB.
My Take.
Mambo mazuri kama haya yanapoanzishwa sisi media tunaalikwa kutoa coverage, lakini kamwe hatuitwi kupewa feedback ya utekelezaji wa malengo ya kuanzishwa kwake. Tulianzisha Mkukuta, Mkuza, Mkurabita, Mkumbita, Kilimo Kwanza, na miradi mkakati mingi tuu, media tunaitwa wakati wa uzinduzi, lakini hatuitwi tena kupewa feedback, hivyo tunazindua miradi mingine, kama uzinduzi wa hii benki bila kupewa feedback ya Kilimo Kwanza, is not right!.
Na sisi media kwa upande wetu, hatutimizi wajibu wetu kikamilifu, tusibweteke kwa kukaa newsroom kuchangamkia barua za mialiko ya uzinduzi, tujiongeze, baada ya mwaka, tujialike, tuitembelee miradi iliyozinduliwa tupate feedback ya utekelezaji.
Pasco