Nashukuru sana mheshimiwa spika kwa kunipa fursa hii ya kwanza kabisa katika bunge hili la awamu ya nne, niamze kwa kukupongeza wewe kuchaguliwa kuwa spika, pia pongezi zangu zikufikie wewe pia kwa kuwa shemeji naye amekuwa ni waziri, pia nimpongeze rafiki yangu na mshirika wa karibu ndugu edo kwa kuteuliwa na hatimaye kupitishwa na bunge kuwa waziri mkuu, nitoe pongezi na shukrani kwa chama changu kwa ushindi mkubwa kilioupata na natumai wakati wa uchaguzi ujao nitakuwa meneja wa kampeni ili ushindi huu uendelee. Baada hatua hiyo ningependa kutoa pole kwa wabunge familia ndugu na jamaa za wabunge wafuatao waliotangulia mbele za haki:
1,2,3,4,5,6,7,8,9,10, 11,12, na mwenyezi mungu aziweke roho zao mahala pema peponi amina. Nami ningependa kuungana wenzangu kuelezea hisia zangu juu ya kifo kisicho tarajiwa cha mbunge kijana na machachari aliyekuwa imara katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ambaye kuna wakati wanafiki waliwahi kunihusha naye kimapenzi mdogo wa AC. Mheshimiwa spika sitaweza kutoa mchango wangu bila kuelezea mshtuko mkubwa uliotukumba sisi katika CCM kwa kuondokewa na mwenzetu na waziri mchapakazi,dada yetu pia ni mfano wa kuigwa kwa wanawake wote salome mbatia.................hii itakuwa ni hatua ya kwanza
Vilevile mheshimiwa spika ningependa kumpongeza kwa moyo wa kishupavu, ujasiri na uzalendo mhesimiwa waziri mkuu edo kwa kuamua kujiuzuru ilikukinusuru chama na kulinda heshima yake na wapiga kura wake wa monduli, mheshimiwa spika napenda kuelezea nia yangu ya kuleta hoja binafsi juu vitendo vya baadhi ya waheshimiwa wabunge kuendesha kampeni ya kunichafua na siasa chafu juu yangu hii ikiwa ni pamoja na kunihusisha tuhuma za ufisadi..(spika anaingilia Mheshimiwa rost ya hamu hayo hilo tulikwisha liongea mimi, wewe, vasco da gama, edo, maminyororo na wazee kwenye vikao yvetu sasa unapolileta humu utawapa faida akina zitto na huyu mnoko slaa) Sawa mhsimiwa spika sasa nichukue nafasi hii kumpongeza waziri mkuu mteule mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda kwa kuchaguliwa, kama walivyosema wenzangu waliochangia mwaka 2008 mwezi wa pili uchapa kazi wa pinda kila mtu anaujua..........(hii itakuwa ni sehemu pili )
Hapo bado ni mwaka 2008 kwa mtaji huu asiongee tu itabidi atumie siku nzima kupongeza, kushukuru, kulaani, kuungana, kutetea, kuhoji.,,LMAO