Igunga: Kivumbi cha kampeni kuanza leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Kivumbi cha kampeni kuanza leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Sep 7, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CCM WAREJESHA FOMU KIMYAKIMYA, KIVUMBI CHA KAMPENI KUANZA LEO

  CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) vimeingia vitani katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga baada ya kutunishiana misuli wakati wa kurejesha fomu za wagombea wao.Vyama hivyo ambavyo ofisi zao mjini hapa ziko karibu, vilianza kufanya maandalizi majira ya saa nne asubuhi kwa ajili ya kuwasindikiza wagombea wao kurudisha fomu, maandalizi ambayo yalikuwa ya ushindani mkubwa.

  Ubabe ulianza pale CUF walipoanza kupiga muziki kwenye magari yao mawili aina ya Mitsubishi Fuso huku wakiitambia Chadema. Baadaye Chadema nao walijibu mapigo kwa kufungua muziki kwa sauti ya juu kwenye magari yao mawili pia aina ya Mitsubishi Fuso na kusababisha kelele nyingi katika eneo walilokuwapo.

  Misafara yaingiliana
  Wakati muziki ukiendelea, Chadema walitangaza msafara wao utakavyokwenda na kuanza kuwapanga wafuasi wao na magari yao huku CUF nao wakijipanga. Msafara wa Chadema ulipoanza kwenda ofisi za msimamizi wa uchaguzi na wa CUF nao uliingia.

  Msafara wa CUF ulipita katikati ya ule wa Chadema na baada ya kufika mbele ukaziba njia.

  Kitendo hicho kilitafsiriwa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wametanda barabara nzima kuwa ni uchokozi hali iliyosababisha wafuasi wa vyama hivyo kuonyeshana ubabe kwa dakika kadhaa kabla ya Chadema kufanikiwa kupenya na kuendelea na safari ya kwenda Ofisi za Tume ya Uchaguzi.

  Mzozo hadi kwa msimamizi
  Chadema wakiwa na wafuasi wao, walifika katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi saa 8:00 mchana na mgombea wake kukabidhi fomu zake, lakini kabla hawajatoka, CUF nao waliingia na mgombea wao.

  Nje ya ofisi ya msimamizi wa uchaguzi, nusura vurugu zitokee baada ya wafuasi wa vyama hivyo viwili kutaka kuchapana lakini walidhibitiwa na watu waliokuwapo katika eneo hilo. Mgombea wa CUF alikabidhi fomu yake saa 8:10 mchana huku wafuasi wao na wa Chadema wakizozana nje ya ofisi ya msimamizi huyo wa uchaguzi.

  CCM, UPDP, wakabidhi kimyakimya

  Wakati vyama hivyo viwili vikionyeshana ubabe, vyama vingine vya CCM, Chausta, UPDP, AFP na SAU vilirudisha fomu zao bila mbwembwe wala maandamano yoyote.

  Mgombe wa CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu alirudisha fomu yake saa 11:00 asubuhi akiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na kusema kuwa kwa upande wake hali si mbaya na anategemea ushindi kutokana na kuwania nafasi hiyo mara tatu na kushindwa katika kura za maoni ndani ya chama hicho, hivyo kuwa na imani kuwa wananchi wengi wanamfahamu.

  “Wapiga kura wasiwe na wasiwasi wa kunichagua kwa kuwa watakuwa wamepata mbunge ambaye anafaa. Nitatoa kipaumbele kwenye maji na barabara hasa za vijijini na pia Daraja la Mbutu ni changamoto. Hayo na kilimo cha pamba na ufugaji kufanya viwe vya kisasa ni mambo muhimu.”

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu, Dk Kafumu alitaja mikakati yake kuwa ni pamoja na kuifanya Igunga kuwa na maendeleo alisema miongoni mwa mambo atakayoyapa kipaumbele katika kuijenga Igunga ni kuboresha huduma za maji, miundombinu ya barabara hadi vijijini ikiwamo inayounganisha Igunga na Manonga.

  “Baadhi ya mambo haya yameshafanywa kwa kiasi chake na mbunge wetu aliyepita, Rostam Aziz nitahakikisha kuanzia pale alipoishia na kuyaboresha zaidi," alisema.

  Kwa upande wake, Msimamizi wa kampeni za CCM jimboni humo, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba alisema Dk Kafumu ndiye mwenye majawabu ya matatizo ya wananchi wa jimbo hilo tofauti na wa vyama vingine ambao alisema vina majibu tu.

  Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye alisema atafanya kampeni za kistaarabu kwa kuwa shamrashamra zilizoonyeshwa na wananchi wa Igunga zimedhihirisha kuwa anakubalika.

  “Nitafanya kampeni za kistaarabu wana Igunga wananikubali umati huu ni mkubwa, mwenyewe umeuona hiyo inajidhihirisha yenyewe,” alisema Kashindye.

  Kuhusu CUF kuingilia msafara wao alisema: “Wananchi hawakuonyesha aina yoyote ya kutaka ugomvi lakini chama hiki (CUF) kinatuingilia wakati hata bado hatujamaliza kazi yetu. Barabarani wameingilia msafara na ofisi ya msimamizi pia wameingia wakati hatujamaliza kuwasilisha, huu si ustaarabu.”

  CUF, SAU wajinadi
  Mgombea wa CUF, Leopald Mahona alisema Wana Igunga wategemee maisha mapya ya kisiasa hasa kwa kuwa wana shida ya maji kitu ambacho ni kipaumbele cha kwanza. Pia alisema ataboresha sekta ya kilimo na mifugo kwa wakazi hao.

  Akizungumzia kuingilia msafara wa Chadema alisema haoni kama kuna tatizo kwa kuwa hizo ni mbwembwe tu za kisiasa kwa hiyo hakuna shida.. “Wasukuma ni watu wapole na hakuna anayeweza kuleta vurugu. Amani itakuwapo ila ugomvi utaletwa na watu wengine ambao wana chuki binafsi.”

  Mgombea wa SAU, John Magid alisema matarajio yake ni kuhakikisha kuwa katika kampeni anawaelimisha wananchi juu ya mabadiliko wanayoyahitaji kwani muda umewadia.

  “Huu ndiyo muda wa muafaka wa kuyafikia matarajio hayo kwa njia ya kunipigia kura ili niwe mbunge wao na niweze kukaa nao na kuangalia mbinu za kuweza kufikia mafanikio katika uchumi,” alisema.

  Sirro atua Igunga
  Mkuu wa Kikosi cha Operesheni Maalumu cha Jeshi la Polisi, Simon Sirro aliwasili hapa jana kwa ajili ya kuhakikisha kampeni za uchaguzi huo zinafanyika kwa amani.

  Sirro alisema kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kusimamia usalama katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2 mwaka huu... “Tumejipanga vizuri na kazi inaendelea vizuri, nitakuwapo muda wote kwa kuwa ndiyo kazi yangu.”

  Mbowe, Slaa kutua leo
  Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa wanatarajiwa kuwasili leo mjini hapa kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho kesho.

  Mbowe alisema jana kwamba pia watakuwapo wakurugenzi wote wa chama hicho na
  wabunge mbalimbali katika timu hiyo.

  Wakati huo huo, Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad ameishauri Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Igunga kuacha kuingilia masuala ya uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika Oktoba 2 mwaka huu ili kuepusha vurugu.

  Katibu huyo imevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Igunga kufuata taratibu na kutoingiliana katika mikutano yao ya kampeni.

  Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, alitoa kauli hiyo jana akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kiserikali katika Mkoa wa Tabora, siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo mdogo unaoshirikisha vyama tisa vya siasa.

  “Kiutaratibu, uchaguzi husimamiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo kimsingi ni huru na isiyoingiliwa na upande wowote, lakini uzoefu unaonyesha kamati ya usalama huingilia kazi za tume. Acheni kuingilia kazi za tume ili uchaguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru. Naamini hiyo pia itaepusha vurugu.”

  Alisema kwa sasa Kamati ya usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario ina kazi ngumu ya kuhakikisha uchaguzi huo unamalizika kwa amani na utulivu.

  Alisema kama tume itaachiwa ifanye kazi yake kwa uhuru na kutenda haki, itawezesha wananchi wa Jimbo hilo kusikiliza sera za vyama na kuchagua mwakilishi anayewafaa.

  Hamad alizitaka mamlaka kuachia vyama vya siasa kunadi sera zao akisisitiza kuwa hatua hiyo itawezesha wananchi kuchagua mbunge wanayemtaka. Alisema wakati mwingine uchaguzi hufanyika kwa amani na tulivu lakini tatizo huja wakati wa kujumlisha kura ambako nguvu hutumika bila sababu za msingi.

  Kampeni za uchaguzi huo zinaanza leo katika kata 26 za Jimbo la Igunga mkoani Tabora.
   
 2. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CDM ndo kidume chao hapo.
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nimeamini CUF wanapenda ugomvi inawezekana kule zenji wao ndio walikuwa wanaweka vinyesi kwenye visima na kwasingizia CCM.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ENYI WASOMI WA IGUNGA, UKOMBOZI WENU WA WALAZWAHOI IGUNGA KUPATA MWAKILISHI WAO KWA MARA YA KWANZA BAADA YA MIAKA MINGI YA ULAGHAI WA CCM NI UKOMBOZI KWA TAIFA ZIMA

  Hakika wana-Igunga tumefarijika sana kupata taarifa hizi kwamba safari hii mmeamua kuwapa nafasi vijana wenu mliowasomesha wenyewe ili wakawasaidieni kutoa dira sahihi ya upigaji kura Igunga safari hii bila rushwa wala uchakachuaji.

  Kwa kweli Msomi mmoja tu pale Igunga ana uwezo wa kuelimisha zaidi ya wapiga kura 10 kwa siku pale kijijini.

  Hivyo basi kampeni zikiendelea walau kwa siku salasini tu basi CHADEMA kinahitaji walau wasomi wa vyuo vikuu nchi 20 tu kuelimisha zaidi ya wapiga kura 600. Hiyo ni sawa na kusema kwamba endapo BAVICHA wamepeleka silaha hizo za maangamizi ya UFISADI Igunga basi capacity itakayofika pale ina uwezo wa kuelimisha mkoa mzima ndani ya mwezi tu hata kabla ya makamanda wenyewe wa ukweli hawajafika mahali pale.

  Namuona Makamanda Zitto na Lema wakiongoza mashabulizi ya nchi kavu huku, mtaalam mwenyewe wa Anga Freeman Mbowe akimsaka Rostam kijiji hadi kijiji sawa tu na NATO kwa Gaddafi huku Dokta wa ukweli akimalizia kiutaalam akiwa na Majenerali wenye kuogopwa na Mafisadi nchini; Prof Baregu, Tundu Lissu, Mabere Marando, Mzee Ndesamburo, Mchungaji Msigwa, Makamanda tishio Chiku Abwao, Halima Mdee, Selasini, Mr II, John Mnyika ... usipime!!!!!!!!!!!

  People' Powerrrrrrrrr Igunga na kiziki cha ufisadi nchi sasa kung'olewa bila utani tena!!!! Tazameni baada ya wiki mbili mje muone mziki mkubwa Igunga kiasi cha kumfanya huyo Fisadi wa Wizara ya madini kuchanganyikiwa na mwishowe kujisalimisha mwenyewe kwa Wapiganaji wa ukweli nchini.

   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mliokuwa mnamtetea Mtatiro huku jamvini mmeanza sasa kuona alichomaanisha aliposema atahakikisha chadema inakuwa ya 3 nyuma ya ccm na cuf.Kwa nini cuf ianze kuifanyia fujo chadema kama hawatekelezi mpango maalum wa siri kati ya mtatiro na nape?
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kweli kafu ni wachokozi. Wamejua watashindwa kwahiyo wameamua kufa na cdm!. Ndio maana wanasema liwalo na liwe!<br />
  Na cdm wamedhiirisha kuwa ni chama makini kwa kuwa watulivu na tolerance kubwa kuepusha vurugu. Bravo cdm. Wao wana hela, sisi tuna Mungu!
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kumbe Kafumu amegombea mara tatu akapigwa chini na wananchi wa Igunga!? Kweli ccm kazi wanayo. Mgombea wao alishakataliwa na wananchi wa Igunga tena mara tatu, halafu kwenye hatua za awali!
  Halafu utashangaa kuna watu humu wanasema eti anakubalika sana na atashinda. Kisha wanajiita GT.
  Huitaji kuwa na elimu hata ya shule ya kata kutambua kwamba huyu jamaa hakubaliki kabisa na wanaigunga na ndio maana kila alipojitokeza walimkataa kwenye kura za maoni tu!
   
 8. makwimoge

  makwimoge JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  naanza kuona ajali ya Helkopter katika anga la igunga katika hiziwiki tatu
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />


  Mkuu unajua sana kupangilia maneno'una skill ya uandishi?
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mnataka kusema igunga nzima ni wapiga kura 600 pekee?
   
 11. N

  NALO LITAPITA JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  CUF msitake kutuharibia uchaguzi!!!kuingilia msafara wa chama kingine na kupita katikati yao ni hatari kubwa!!lengo la CUF walilenga kujenga mazingira ya kuonyesha CHADEMA NDO WAANZILISHI,walipoona watu wameujua mchezo sasa wanasema lugha laini eti kuingilia msafara ni jambo la kawaida
   
 12. delabuta

  delabuta Senior Member

  #12
  Sep 7, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  People's power!!!!!!!!!!!!!! hilo jimbo mbona letu hilo wala sina wasiwasi.
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kazi kwelikweli, ngoja tuone.
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Hapa Makwanda linasifia Magamba! teh teh teh teh!!
   
 15. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  KAFU sio chama ni kikundi cha vurugu kwa kweli. Sasa waliokuwa wanatamba hapa jamvini wajibu kilichoandikwa kwenye haya magazeti yote. Kila gazeti limeandika mambo waliofanya hawa KAFU. Ninawaonea huruma wanaojiita ni KAFU.

  CHADEMA kipo juu sana kwa mapambano ya kuchukua kiti. Uzi huo huo tumeshawaacha njia panda, wingu limeshawafunika tayari wanatafutana na ndoa yao.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  teh teh teh ..... [FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot]v[/FONT][FONT=&quot][/FONT]ilaza bana
   
 17. L

  Lua JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yaani hilo jimbo na chadema. ni kama kusukuma mllevi, huyu dogo mtatiro nadhani anamatatizo kwani hata ubungo alikua hivyo hivyo, badala ya kupambana na hawa ng'umbi yeye alikua anamtusi mnyika na mwisho wa siku kaambulia nafasi ya 3 aka beki tatu. ndivyo itakavyokua igunga.
   
 18. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Kuna sehemu nimesoma kwamba Wasira anaenda kuongeza nguvu za ccm kule Igunga! Kwani keshaamka?
   
 19. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kuingilia misafara ya CHADEMA ni sehemu ya operesheni "LOLOTE NA LIWE" ya CUF.
  Hapa huyu CUF wamepewa kazi ya kuichokoza CHADEMA ili kuijengea CCM mazingira mazuri.
  Nafikiri CCM imewaahidi CUF kama mgombea wa CCM atashinda basi mgombea wao atakuwa NAIBU MBUNGE.
   
 20. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Demokrasia bongo bado.
   
Loading...