Igunga: ITV na uchakachuaji wa habari

Nilimnukuu Alfrd Masako akiripoti matukio ya wiki nami nilishangaa. maana niliona picha video za Chadema zikionesha anayehutubia bila kuonesha wanaohutubiwa. Ilipofika kwa CCM ikawa tofauti na lugha ikawa ifuatavyo. '.... maelefu na mamia ya waIgunga walifika kuhudhuria ufunguzi wa cpeni za CCM Igunga'. Huyu mzee wa hii TV ni opportunist sana. Nachooombea ile kesi anayodaiwa senti moja imrudi kisawasawa.
penye red na kupinga inamaana huyu mzee ndiye anaeongoza vipindi?we huoni watendaji wake wakuu ndo wenye matatizo?
 
Wataripoti kitu gani cha wamwagia watu tindikali na wapiga wakuu wa wilaya?
Kama we mtoto ungekuwa unajiuza ungetengeneza sana hela manake sisi wenye tamaa na vihelehele tungekuwa tunashinda kwako. Kila post unavamia umeahidiwa nini?? Nape mwenyewe aliyewaajiri saizi yuko kimya baada ya kuona Mzee Lowassa anachukua pointi kimyakimya, na juzi mzee alikuwa Zanzibar kuwatetea waliozama walipwe bima. Soma alama za nyakati bwana mdogo
 
Ahahahaaah!! Anajitahidi...
<br />
<br />
Ni kama anakazi ngumu naona kwasababu wapinzani wake wana sifa tau; kwanza, wako wengi, pili, wanafuatilia mambo yanavyokwenda katika nchi kwa hiyo wanakuwa na data nyingi na tatu, wanahasira hao!
 
Mikutano ya kampeni ya CCM inasisimua kidogo. Wanaruhusu maswali kutoka kwa wapiga kura watarajiwa. Dr Slaa bado anadhani yuko altare. Hotuba zake ni za kipadre sana.
 
kama ni nongwa tu ss wapenzi wa cdm tunaongoza mbona ITV wanaonesha habari karibu za vyama vyote
 
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikiona ITV inawapa CCM coverage kubwa ii hali vyama vingine husikii kitu. Kuna nini mbona walikuwa wazuri hawa ITV kuripoti?

Mkono wa magamba huo......
 
Juzi ITV walionyesha Chadema pekee yake, jana saa 2 usiku ilianza na CCM kupitia Wassira akijibu maswali magumu (aliripoti Novatus Makunga),ikafuata Chadema kupitia Dr Slaa na Kashindye (aliripoti Ufoo Saro), then CUF kupitia kwa Profesa Lipumba). Kwenye hili napingana na wewe Mkuu ITV wamejitahidi kuonyesha Chadema karibu kila siku isipokuwa leo asubuhi
<br />
<br />
Mkuu hata leo asubuhi ITV wameionyesha ile taarifa ambayo Wassira alikimbia swali kwahyo tuseme wanaripoti kwa usawa penye ukweli tuseme ukweli bandugu wana Cdm
 
Wana JF,
Leo siku ya tano naona kitu kipya kabisa machoni kwangu kutoka ITV, sijui ndio kukuwa kwa Demokrasia nchini au ni kitu kinafanywa kwa makusudi.
Taingia juzi kwenye taarifa za habari ya ITV walimuonyesha Dr Slaa akihutubia umati wa wafuasi wa CUF.
Jana tena niliona Prof, Lipumba akihutubia watu wapo juu ya miti.
Leo tena wameonyesha mgombea ubunge jimbo la Igunga kupitia CDM Joseph Kashindye, akihutubia umati wa CCM. Hivi ni kweli uchaguzi wa Igunga ndio upo hivyo.
Wadau naombeni mtujuze kwenye hili suala
 
ITV iko kibiashara lakini kama hawakuwa makini huu uchaguzi wa Igunda unaweza kuwaletea matatizo huko mbele ya safari. Nahisi kuna uchakachuaji wa makusudi wa picha hasa za vyama vya upinzani. Lakini kama nia kujiweka karibu au kuwafurahisha ccm basi hawana wa kumlaumu siku ya hukumu itapowadia. Biashara na siasa vinaweza kugeuka sumu. ITV wawe macho kabla wananchi hawajaanza kususia hiki kituo.
 
Mi nilivyoielewa ile taarifa ni kua wanachama na washabiki wa Chama Twawala wamechoka na siasa, ahadi feki + sera uchwara za mgombea wao asie na jipya wakaona bora waje kusikiliza Point kwa Chadema
 
....Hizi TV ngoja tuchukue nchi,tutazishughulikia perpendicular....
 
Mi nilivyoielewa ile taarifa ni kua wanachama na washabiki wa Chama Twawala wamechoka na siasa, ahadi feki + sera uchwara za mgombea wao asie na jipya wakaona bora waje kusikiliza Point kwa Chadema
kuna siku walimuonyesha Dr Slaa akihutubia nyumba za Tembe pamoja na watoto, naona wewe ujaona ndio maana unasema hivyo
 
njia mojawapo ya kukomesha upuuzi wa media zetu ni kupitia mtandao kama Jf,walioko igunga wachukue picha/video waziweke hapa bila kuedit au kuchakachua!kwa upande mwingine vyama lazima viwe na uteratibu wa kuweka kumbukumbu za mikutano yake kama vile kwenye audio au DVDs.huu ni wakati wa mapambano tuacheni kulalamika!
 
ITV ni ya mengi naye ni mchaga na chadema ni chama cha wachagga, kwahiyo hiyo ndio tabia ya ITV siku zote huwa wanachakachua picha ili kuibeba chadema ni hili wanafanya kwa maelekezo ya mchagga mengi.
 
Back
Top Bottom