Igunga: ITV na uchakachuaji wa habari

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
nakuwa siwaelewi kabisa hawa ITV kwa jinsi walivyo na akili kama za VodaCom.

Lipumba na Mtatiro wake nao ameonekana akihutubia matawi ya miti.

Mtatiro amerithi kibwagizo cha Maalim Seif cha "Sawasawa!?"
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,912
1,125
ITV wanahaki ya kurusha habari yoyote hata kama haitakupendeza lakini wengine itawapendeza, halafu swali rahisi ulijuaje kuwa walihutubia miti? Jibu baki nalo.
 

MZAWATA

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
556
94
Acha upopo,kama wewe ni magamba sis ni watanzania wenye akil timamu. Itv waache watupe taarifa hata kama Dr. Slaa hahutubii mtu,thread za ajab ajab kama hiz hatuzitak hapa,sit down and think criticaly then leta topic ya maana na si mipasho
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,036
5,965
nakuwa siwaelewi kabisa hawa ITV kwa jinsi walivyo na akili kama za VodaCom.

Lipumba na Mtatiro wake nao ameonekana akihutubia matawi ya miti.

Mtatiro amerithi kibwagizo cha Maalim Seif cha "Sawasawa!?"

Sina wasiwasi sana na hili kwani uchaguzi ni kwa ajili ya jimbo la Igunga na sio Tanzania nzima, hivyo mtu wa Mtwara asipoona ule umati wa wapiga kura haitaathiri kabisa idadi ya kura kwa mgombea yeyote ila Chama Cha Majuha (Chama Cha Mazumbukuku) watafanya hujua ili wapate ushindi kwani ushindi kwao ni ndoto. Juha au zumbukuku leo anasema kitu A ni uchwara kesho anasema tena kitu kile kile A ni safi bila kufanyiwa mabadiliko yoyote hata kidogo!!!
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,206
25,659
Sasa kama watu hamna kwenye mikutano atafanyaje? ITV mbona wanarusha habari kwa haki, wewe unataka ITV iwaletee watu mikutanoni?
 

kayumba

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
653
73
Mkuu unataka kusema wakati inaonyeshwa miti ikipokea hotuba kutoka kwa Dr. Slaa pembeni walikuwapo watu? Hiyo tena kali, ningependa kuona picha ya chombo kingine cha habari kilichoripoti mkutano huo huo niweze kujilidhisha!

Nilisikia eti katika uchaguzi uliopita vyombo vya habari vilikuwa vikitoa picha zenye kuonyesha watu wengi/wachache kwenye mikutano ya vyama vya CCM/CDM kwa makusudi na mara nyingine wakipotosha ukweli kwa sababu maalum na malengo fulani fulani hivyo sitoshangaa kwa taarifa hiyo kuwa sahihi.
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
37,258
41,287
Mi siangalii itv wala tbc naangalia tv za ughaibuni tu, bongo ni uzushi mtupu.
 

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,713
Mi siangalii itv wala tbc naangalia tv za ughaibuni tu, bongo ni uzushi mtupu.

Kama kuna TV ya ughaibuni inarusha mikutano ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa Igunga naomba unipe jina lake ili na mimi nijiunge na wewe kuangalia TV za ughaibuni.
 

MANGUNGO

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
1,536
349
Ni psychology ya mtu anayetaka kufa!magamba iko wazi wazi kuwa mnakufa huku mnajiona hata 2015 mkifika ni bahati tu,kifupi IGUNGA itabaki kuwa historia kama ilivyo NYAMAGANA na ILEMELA,ARUSHA,MOSHI,MBEYA MJINI,HAI,UKEREWE,MUSOMA MJINI na kwingineko.PRO.MAJI MAREFU HANA MSAADA TENA,MAREHEMU SHEKH YAYA ambaye ulikuwa msaada wenu alisha tangulia mbele ya haki,WASILA anasinzia tu,KOMBA anasinzia tu,kifupi ni kwishneii.Chama kizee hakiwezi kwenda na kasi ya UJANA.CHADEMA pekee wameweza na tumewaaamini kwani wametutoa kwenye ukungu.IGUNGA wametolewa kwenye ukungu tunaona kwa macho yetu na si0o ya kusimuliwa.MAGAMBA YATAVULIWA MAGWANDA YATAVALIWA.
 

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,318
Mengi tutayaona na mengi tutasikia. Lakini siku zote ukweli utadhihiri.

Tuwe na subra kusikia matokeo ya Kura na sio tambo za wanasiasa.

Kila la kheir wana Igunga.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Pamoja na kupanda punda kama Yesu bado Mh Lipumba hakupata watu wa kuhutubia? Atafute mbinu kwa Ali Choki mzee wa farasi enzi zile akiingia Diamond Jubilee kuzindua albamu za Twanga!
 

Mapujds

JF-Expert Member
May 12, 2011
1,286
127
Ndugu acha uchochezi na chuki zako zisizo na msingi.hakuna chanel yoyote tz ambayo huonesha kampeni za igunga vizuri kama itv na huwa haipendelei.

Mimi kila siku naangalia taarifa ya habari laki itv wanajitahidi.huwa wanaanza kuonyesha umati wa watu waliohudhuria mkutano then wanamuonyesha mhutubiaji,hapo huwezi juoa anayechukua video amekaa upande upi ndio maana mara nyinyi utakuta inamuonyesha mhutubiaji against miti au milima but unajua kabisa angle ilikuwa ngumu kupata picha.

Msihukumu jamani vijukwaa vyenyewe tunavijua huko vijijini.
 

Mess

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
661
180
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?
 

Mess

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
661
180
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikiona ITV inawapa CCM coverage kubwa ii hali vyama vingine husikii kitu. Kuna nini mbona walikuwa wazuri hawa ITV kuripoti?
 

Johnsecond

JF-Expert Member
May 4, 2010
1,076
211
Mimi nadhani baada ya Rostam kutoka CCM, Reginald Mengi sasa ana business conflicting interest na Mbowe
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom