IGP weka ndani Wafanyakazi BRELA

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,145
716
Jamani,

Siyo mara ya kwanza kusikia/kusoma kuwa mafaili ya makampuni yamepotea BRELA. Na kinachonisikitisha zaidi ni kuwa hayo makampuni au mafaili yanahusishwa na wizi au tuhuma nyingize za udanganyifu.

Nnavyoelewa ni kuwa kama ilishatokea huko nyuma nilitegemea kuwa BRELA wange SCAN na kuifadhi Electronic copy ya mafaili yao. Hii (ambayo kwa BRELA ni Project kwa sababu ya uelewa mdogo wao) ingesaidia sana kwani ninategemea wangekuwa na Backup ya system yao, hata nyumba nzima ikiungua una retrieve tu data kutoka kwenye backup tape.

Hali sio hii Brela. Je naomba kuchangia mawazo na wana JF, hakuna kipengele chochote kwenye sheria ya PCCB au sheria ya nchi inayoonyesha kuwa kama mtu aki poteza USHAIDI inabidi ashtakiwe?

Kama hamna hicho kipengele kwanini basi bwana Mkapa wa BRELA asiwajibike?

Jamani waTanzania wenzangu tuweni na uchungu na nchi hii. Na tunjenge sense ya responsibility.

Wasalaam

FD
 
Chuma,

Business Registrations and Licensing Agency (BRELA)
Ukitaka kuanzisha kampuni Tanzania lazima iandikishwe.

Hapo ndio unaenda kwa mwandikishaji/msajili wa makampuni.

Hivi majuzi tumesikia kuwa makampuni mawili kati ya yaliyotajwa kuhusika na wizi wa BOT mafaili yao yamepotea BRELA. Ina maana huwezi kupata nani ni mmiliki na records za kampuni kwa ujumla!

Ingawa unaweza kwenda bank na kutumia TISS uka trace hela zilienda wapi na nani ni signatory wa hiyo account iliyopokea hela..., lakini tatizo litakuja kuwa sio lazima signatories wa account ya kampuni bank wawe wamiliki!

Hapo unabakiwa na sehemu moja tu ya kumjua mmiliki nayo ni BRELA.

Umenipata ndugu yangu Mtanzania mwenzangu?
 
Nadhani hii ni point muhimu sana. Huu upoteaji wa kirahisi wa kabrasha unatia mashaka. Kwa nini hawana back-ups? Kwa mahali sensitive kama BRELA ni lazima wawe na back-ups ambazo zinatunzwa sehemu nyingine. Hii vilevile is true kwa sehemu kama Benki Kuu. Watu hawasiti kuunguza jengo (BOT, NASACO n.k.) wanapokuwa threatened.
 
Hivi majuzi tumesikia kuwa makampuni mawili kati ya yaliyotajwa kuhusika na wizi wa BOT mafaili yao yamepotea BRELA. Ina maana huwezi kupata nani ni mmiliki na records za kampuni kwa ujumla!

Nina wasiwasi inawezekana hayo mafail(official files) hayapo/hayakuwepo tangia mwanzo. Baada ya kuona soo limeibuka wamekuja na shortcut! yamepotea, si wanajua wadanganyika wataamini. Katika hali ya namna hiyo hao kina 'MKAPa???' wanatakiwa wawajibishwa kwa uzembe/kupoteza ushahidi/kuliingizia taifa hasara n.k
 
Fundi,

Ndo maana nasema inabidi watanzania tuwe na tabia ya kuwajibika. Nashangaa watu hawashikilii bango hawa jamaa.

Frankly speaking sidhani kama ni uzembe, ninaamini kabisa wanafanya hujuma!
 
Nina wasiwasi inawezekana hayo mafail(official files) hayapo/hayakuwepo tangia mwanzo. Baada ya kuona soo limeibuka wamekuja na shortcut! yamepotea, si wanajua wadanganyika wataamini. Katika hali ya namna hiyo hao kina 'MKAPa???' wanatakiwa wawajibishwa kwa uzembe/kupoteza ushahidi/kuliingizia taifa hasara n.k

Kama hayakuwepo toka mwanzo, basi inabidi sio wamtoe kafara Balali pekee yake. Inabidi bwana RELI naye aondoke maana yeye ndio mkuu wa internal control BOT.

Ilikuwaje wawalipe kampuni ambayo haina usajili wala leseni?!!!!!!

Pale BOT wamejaa wasomi, lazima walicheck vitu kama hivyo vya registrations.

Kwahiyo bado naamini Mkuu wa Brela inabidi aondoke naye!
 
kama kweli tunataka kuwa kweli upuuzi huu ushughulikiwe tokea mzizi wake.

tuun'goe mtango na mizizi sio kutania kama tunavyofanya

tuwe makini kila idara au vipi wazee?
 
Kama hayakuwepo toka mwanzo, basi inabidi sio wamtoe kafara Balali pekee yake. Inabidi bwana RELI naye aondoke maana yeye ndio mkuu wa internal control BOT.

Ilikuwaje wawalipe kampuni ambayo haina usajili wala leseni?!!!!!!

Pale BOT wamejaa wasomi, lazima walicheck vitu kama hivyo vya registrations.

Kwahiyo bado naamini Mkuu wa Brela inabidi aondoke naye!

FD,

Huwezi kufungua account ya kampuni bila kuwa na registration form ya BRELA.
Huwezi kupata leseni pia bila ya hiyo registration. Kwa mtu ambaye amewahi kufungua biashara TZ, anajua wazi haiwezekani ukafanya chochote bila ya
kuwaona kwanza BRELA.

Hayo mafile yalikuwepo ila wajanja wameyanyofoa.

Hili suala ni kubwa zaidi ya JK alivyotuambia. Labda tusubiri hao wanaochunguza na huenda wao wanashughulikia mambo mengi kuliko sisi tunavyojua.
 
Kwa hiyo kunasehemu nyingi za kupata hizi taarifa hata kama hayo mafaili yamepotea Brela? Kupotea kwake isiwe ndiyo mwisho wa mchezo.
 
Hello BRELA hata kama wamepoteza bado hata benki hufungui akaunti (kama walivyosema wakuu hapo juu) ya biashara mpaka kuwe na copy ya ile registration na pia zite articles of association (zenye details za wamiliki) sema problem kubwa ya bongo mtu anaweza kujiita leo Abdallah Masanja an kesho huyohuyo akawa John Mgeja, kazi ipo!!!!!!!!!!!! Huwa unaambiwa utaje home adress (watu wanaweka PO BOX, Mjumbe mtaani kwako kama umemsahau basi unaambiwa na wale officials andika jina lolote tu.... KUTRACE INFORMATION TANZANIA NI KAZI!!
 
Hayo mafile yalikuwepo ila wajanja wameyanyofoa.

Hili suala ni kubwa zaidi ya JK alivyotuambia. Labda tusubiri hao wanaochunguza na huenda wao wanashughulikia mambo mengi kuliko sisi tunavyojua.

Tatizo la ufisadi mkubwa kama huo lazima uguse vigogo wazito zaidi. Hao wanaochunguza sina hakika kama watafika mbali na hilo zoezi kwa kuwa akina Hoseah ni wepesi sana wa kufunika mambo na hasa wakishakosa hayo ma-file BRELA hawachelewi kutuambia kwamba kampuni hizo zilikufa na hakuna documents za kuwezesha ku-trace hayo makampuni. Hata kwenye hizi benki nako ni usanii mtupu, si ajabu unaweza kukuta hata huko documents zilishachomolewa ama file lote halipo kabisa kwa kissingizio kwamba mteja akifunga account basi na mafile yake hufungwa na kuchomwa moto.

Tuliambiwa na Dr. Slaa kuna makampuni yalifungua account NBC siku ya sikukuu, sasa hapo kweli mnategemea mpate documents kutoka kwa wasanii wenzao?

Hii skendo ya BoT ni nzito sana usanii unaanzia BRELA mpaka sehemu zote wanazopita. Unadhani kwanini Mkapa aligoma kutaja majina ya wamiliki wa firms? Maana akimtaja mmliki wa firm maana yake ni kwamba ndiyo ataenda kizimbani, lakini likitajwa jina la kampuni ni kampuni ndo itasimama kizimbani na sijui ndiyo itafungwa kampuni ama inakuwaje?

Hapa naona ni usanii kwa kwenda mbele. Majina ya Kampuni ndiyo yanatajwa, majina ya firm mnaambiwa mafaili yake yalipotea. Maana mtu akitajwa tu ni kunyea ndoo mpaka basi! No wonder hata wamiliki wa hizo kampuni hawana mashaka na sasa wataanza kuhamisha mali zao, maana wamepewa grace period ya miezi 6 kwamba hamisheni kila kitu mkisajiri kwa majina yenu binafsi with exception of assets ambazo si rahisi kuzihamisha na ikiwezekana wanaweza kuuza assets hizo na siku kampuni ikienda mahakamani wanaambiwa ilisha-wind business. Bongo tutaliwa kila siku na hawa hawa viongozi wetu wa serikalini huku wanatuchekea na kutucheka ujinga!
 
Keil,

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Unajua hili jambo sasa ni kubwa na kama kweli serikali inataka kuwashughulikia hawa watu naamini wanaweza kabisa.

Watatajana wenyewe maana kuna wafanyakazi si ajabu walipewa elfu kumi, wanagundua deal kumbe ilikuwa kubwa sana. Hapo hasira zinaingia.

Wasiwasi wangu ni juu ya hiyo amri ya JK. Kama ameitoa kwa nia ya kusafisha basi wengi watatapatikana tu, lakini kama ni usanii hapo tutasikia mengi.
 
Wasiwasi wangu ni juu ya hiyo amri ya JK. Kama ameitoa kwa nia ya kusafisha basi wengi watatapatikana tu, lakini kama ni usanii hapo tutasikia mengi.

Hiyo ndiyo hoja ya msingi na huo ndiyo wasiwasi wangu.

Radio mbao zinasema baadhi ya wamiliki wa makampuni yaliyotajwa ni maswahiba wa serikali tena wa karibu sana. Nilisoma thread moja ambayo ilikuwa inaongelea wamiliki wa hayo makampuni ilibidi nijiulize, "Hivi kweli JK ametoa amri hii akijua hayo makampuni ya akina nani?"

If the guy is serious anaweza kufanikiwa kusafisha, lakini kama ni usanii tutaishia kusikia ngonjera nyingiiiiiiii!

Kinachonifanya niamini kwamba ni usanii, kwanini wame-extract info kutoka kwenye report bila ya kuiweka report kamili? CAG alisema kwamba E&Y walipewa task ya kukagua mahesabu ya EPA na mahesabu ya mwaka wa fedha wa 2005/6, mbona press release imejikita kwenye EPA pekee? Hilo ndiyo linanipa mashaka, sina imani sana lakini tusubiri tuone mwisho wa hiyo task force.
 
Bado mimi sipati jibu kwa sababu BoT na bank Zote nchini ukitaka kufungua Account ni Lazima wala sio hiyari kupeleka MoA(Memorandum of Association), Company Registration Certificate, Board resolution iliyoafiki kufunguliwa kwa account katika bank hiyo, Majina ya signatories. So bank inaweka details zote kwenye kumbukumbu zao ikiwa ni pamoja na BoT kama mwangalizi wa account zote za watanzania.

Pia kabla bank Especially BoT kama hawajatoa malipo kwa kampuni yeyote huwa wanaomba comfirmation ya company hiyo kutoka BRELA. Je hata kumbukumbu ya comfirmation nayo imepotea?

Je katika mtiririko wote huo haikuwezekana kupatikana backups za hayo makampuni?

Basi kuna wakuuu weeeeengi sana behindi this scam(kuanzia BRELA, Commercial Banks, Serikalini, na huko BoT)
 
basi ni wape kidogo,mambo huwa hivi,
1, unapeleka maombi breal,kwa kuchagua jina la kampuni,jina likishapita kwa maana hakuna kampuni yeyote inayotumia jina hilo.
2,unapeleka vitabu vyako(m and a)kwa ajili kusajili kampuni ikiwa ni pamoja na kulipia fees.(hapa huwa hakuna picha za wamiliki zaidi ya majina na addressi zao tu.)
3,ukikamilisha hivyo vyote unapewa registration certificate of incoporation.no ....,
4,mpaka hapo kazi ya breal imekwisha,unabaki kufile return kila mwaka.

Kwa upande wa leseni.
1,kuna leseni ambazo utolewa na serikali kuu na serikali za mitaa(halimashauri husika.
2 Kwanza itakubidi uende TRA kwa ajili ya kupata TIN, Taxper identification number pamoja na kufungua file las kodi ya mapato.
a, ilikupata TIN lazima upeleke picha za wakurugenzi wa kampuni na address zao kamili.
b,kwenye file la mlipakodi napo ni vile vile lazima upeleke picha za wahusika.
c,mpaka hapo umemalizana na watu wa TRA.

Leseni,hapa baada ya kutoka tra,kama leseni yako inatolewa na serikali kuu,hapa pana ubwete huwa hawakagui sehemu ya biashara itakapo fanyika(ndio maana kagoda walipeta)
Lakini kama ni halimashauri,hawa lazima wakague sehemu ya biashara
watu wa afya ndio wanajukumu la kukagua sehemu biashara itakapofanyika kabla ya kukupitia form zako kwa ajili ya kupata leseni(lakini pia utkita kitu kidogo hiyo kazi haifanyiki na wanakupitishia maombi yako,hapa pana usumbufu kupita kiasi ilimradi huwape chochote)yote tisa nipale unapokuta bar katikati ya makazi ya kuishi watu,au vituo vya mafuta ktika makazi ya watu na biashara nyingine nyingi zipo pasipo stahili.
kazi kwisha.
sasa una
1 cerificate ya msajili wa makampuni
2,TIN
3,Leseni,

Kufungua ACCOUNT.
1,Kama ni ya kampuni ltd,
A, Certificate of incoporation kutoka breal,
b,board resolution letter.
c,leseni ya biashara,
d,picha za wakurugenzi au pamoja na vivuli vya hati za kusafiria
e,m and a,
fpamoja na form ya maombi ya kufungua account pamoja barua za wadhamini wawili ambao wanaaccount hapo kwenye bank unayofungua hiyo account.

mpaka hapo kazi kwisha na baada ya watu kuvuta mchuzi wao hivi vyote hutolewa na kuchomwa moto na hii kazi mara nyingi hufanywa na makarani kwa kupewa kitu kidogo kwa kujua au kutokujua ni nini kinaendelea hapo.
mtanisahihisha kama nikosea mahali au nimeruka kitu
 
Suala hili si dogo na kupuuzia. Yawezekana kabisa kuwa hayo makampuni Mkapa aliyosema mafaili hayaonekani hayakuwahi kusajiliwa BRELA au kupata tin kutoka TRA.

Na hoo inatokana na kukosekana kwa miondo maalum ya ku-verify validity of a company. Mfano kama BRELA na TRA wangekuwa na automated online registry, basi kila anayefanya kazi na hizi kampuni angeweza kuangalia status ya hizi kampuni online ama kupiga simu kabla ya kufungua akaunti.

Kama ni vyeti, hati na makabrasha, si vijiweni bado wanakokotoa?
 
Nikitafakari sana majibizano yenu hapo juu,ninagundua kwamba Umefika wakati sasa Tanzania kuwa na DATA PROTECTION ACT Kwani tatizo la upotezaji nyaraka Tanzania ni serious sana.Hebu oneni wenzetu wanavyowajibika juzi juzi tu hapa Uingereza zilipotea disk muhimu sana za mamlaka ya mapato na shirika la huduma za afya ilikuwa soo babu kubwa sana,watu nusura wapoteze kazi,waziri mkuu nusura ajiuzulu,lakini sisi bongo tutaishia aah zimepotea bahati mbaya basi. Tanzania hatuna sheria ya kuwawajibisha wapoteza nyaraka.Sheria tuliyonayo sasa yenyewe inalinda tu nyaraka za serikali zilizoandikwa SIRI na kuwabana waandishi au mtu yeyote atakayekamatwa na waraka wa namna hiyo.Pia tunayosheria ambayo inaanzisha kitengo cha kumbukumbu na nyaraka za taifa kilichopo chini ya waziri wa utumishi(kipo nyuma ya kisutu pale) lakini kwa document za watu zilizo katika public domain,sheria zipo kimya sana labda uzilazimishe sana.Hali ambayo matokeo yake unakosa ushahidi watu wannachiwa huru. Wee inakuwaje watu wapoteze nyaraka,zimeenda wapi,kila siku najiuliza pale ardhi,humo halmashauri,mahakamani n.k eti file limepotea mmh kivipi ukitoa 5000 ukamwambia mtu bwana jitahidi lionekane anakwambia hebu subiri kidogo nicheki vizuri utasikia limeandikwa ....Augustoons unasema eeh anakwambie hili hapa.
Unabaki umeduwaa unashindwa umfanyeje,umesota kulifatilia miezi mitatu lakini ulipotoa 5000 hata dk haikupita.Naam tunahitaji sheria ambayo itamwezesha mtu kumshtaki mtu aliyemkabidhi data zake zikapotea.Kama kuna mwandishi hapa tunaweza kuandaa makala ya namana hii nikamsaidia mawazo tukaitoa hewani. Kwa kweli uzembe wa kujitakia bongo umezidi.BOT si kwamba makampuni hayo hayakusajiliwa yalisajiliwa kwa kiini macho(temporarily) black door halafu badaye nyaraka zake zikapotezwa kwa makusudi.Namba za usajili walitoa haohao BRELA kwa hiyo mi naungana mkono na hao jamaa kuwa BRELA (MSAJILI WA MAKAMPUNI) naye awajibishwe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom