IGP weka ndani Wafanyakazi BRELA

Hao kina Maregesi ndio hao hao wa kwenye kamati za wazazi za ccm na makada wa sumaye wa longi,sijui unaaanzeje kuwashika kama sio unapiga mkwala halafu baadaye unampigia simu ukisema " mzee usiwe na shaka ule ni mkwala tu ili wananchi waone nimekemea lakini yataisha tu,hehehe..." halafu unakata simu
 
Hii issue ya nyaraka ni very serious.

Labda niwape mfano live.

Japan ilibidi mwaka jana waziri mkuu na baraza lake wote waachie ngazi, na sababu kubwa ilikuwa kupotea kwa kumbukumbu za kiinua mgongo (pension) za kipindi fulani huko nyuma.

Serikali iliyoingia madarakani hawaachiwi pumzi maana kila siku PM lazima atoelee maelezo resolve ya hilo suala imefikia wapi.

Na opposition wametahadharisha kwamba wakishindwa kuweka kumbukumbu sawa na wao watatakiwa kufungasha virago soon.

Nadhani anabidi na sisi tuanze kuwajibika kwa staili hii. Maana serikali haitakiwa kuwaacha wananchi na manung'uniko, majonzi, shida na mateso kila kukicha kama vile imekwenda likizo.
 
[

Kama hamna hicho kipengele kwanini basi bwana Mkapa wa BRELA asiwajibike?

Jamani waTanzania wenzangu tuweni na uchungu na nchi hii. Na tunjenge sense ya responsibility.

Wasalaam

FD[/QUOTE]

This fellow Andrew Mkapa is very corrupt.He is Ben Mkapas younger brother ,so what do you expect.
 
Hivi ni Kweli IGP Mwema alikua anafanya kazi BoT kabla ya kwenda Polisi? alikua na nafasu gani? Alikua shushu ndani ya BoT, au na yeye mtoto wa kigogo? Kama alikua shushu hakutakua na kazi ya kuwashughulikia mafisadi wa BoT, lakini kama aliingia BoT kwa memo basi TUMEKWISHA
 
Ni kweli Mwema aliwahi kufanya kazi BoT mwanzoni mwa miaka ya 1990. Hayo mengine sina uhakika nayo. Ingawa kitendo cha yeye kuondoka BoT hakukifurahia. Wakati Mwema yuko BoT, Ballali hakuwepo.
 
Swali langu kwenu wenzangu ni kuwa kwanini serikali haiipi kipaumbele tatizo la kupotea mafaili pale BRELA?!
 
FD,

Mafaili ni budi yafanyiwe "Communion" kwanza kabla ya viwavi kuingia........unakumbuka haya maneno.....
First you get the Money
Then the Power
Then........malizia........ndio mchezo unaoendelea

wakitaka hayo mafaili yatapatikana tu
 
Kwa sababu serikali ina hurumia wafanyakazi wake!!! ati kwa kuwa haijawapa vitendea kazi vizuri kama kompyuta!

Wakati huo huo wafanyakazi hawazitaki hizo kompyuta maana wengi itabidi waondolewe... patamu hapo!!!

Kwi kwi kwi kwi
 
Ni kweli mtia sahihi siyo lazima awe mmiliki, lakini tukijua aliyetia sahihi kwenye hundi si atatueleza hela alizipeleka kwa nani. Unapotaka kufungua account benki lazima upeleke picha za watia sahihi na barua ya kampuni inayoidhinisha sahihi hizo kutoa fedha. Hivyo sura za wahusika zinajulikana, tukamate hao kwanza nao watatueleza wahusika ni akina nani.
PENYE NIA PANA NIA.
Bado nina wasiwasi na hatua za JK kwani tunaweza kuonyeshwa usanii mwingine. Yaani wameshaona kwamba wanaweza kumtaja Balali na bado wakamsave. Tusiwe na haraka za kutoa pongezi wakati bado ni mapema mno. Tusubiri kuona hatua zitakazofuata. Rais tunaye; wakati wowote tutampongeza
 
Hivi ni Kweli IGP Mwema alikua anafanya kazi BoT kabla ya kwenda Polisi? alikua na nafasu gani? Alikua shushu ndani ya BoT, au na yeye mtoto wa kigogo? Kama alikua shushu hakutakua na kazi ya kuwashughulikia mafisadi wa BoT, lakini kama aliingia BoT kwa memo basi TUMEKWISHA

Bwana Saidi Mwema alikuwa Security Officer kutoka Polisi(kwenye directorate of National Payment System). Kazi yake kubwa ilikuwa kuwa kuongoza ile misafara ya fedha kwenda na kurudi kwenye matawi ya BOT huko Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Mtwara na Arusha. Ilibidi arudishwe polisi wakati ule Dr. Idrissa alipoukwaa uGovernor. Maana hakuona umuhimu wa kuwa na mabranch mengi ya BOT. Na akafunga Branch kama ya Mtwara na kuwapa hiyo kazi NBC na vile vile akatimua baadhi ya maofisa aliokuwa anaona hawana umuhimu. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa nadhani hawa mabwana waliopunguzwa walienda mahakamani na kushinda hiyo kesi,ila hawajalipwa mpaka leo. BOT wanaendelea kuappeal tu
 
Thanks Mbangaizaji,

Kama ni hivyo bwana IGP anauelewa kidogo angalau. Hope atasaidia.
 
Bwana Saidi Mwema alikuwa Security Officer kutoka Polisi(kwenye directorate of National Payment System). Kazi yake kubwa ilikuwa kuwa kuongoza ile misafara ya fedha kwenda na kurudi kwenye matawi ya BOT huko Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Mtwara na Arusha. Ilibidi arudishwe polisi wakati ule Dr. Idrissa alipoukwaa uGovernor. Maana hakuona umuhimu wa kuwa na mabranch mengi ya BOT. Na akafunga Branch kama ya Mtwara na kuwapa hiyo kazi NBC na vile vile akatimua baadhi ya maofisa aliokuwa anaona hawana umuhimu. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa nadhani hawa mabwana waliopunguzwa walienda mahakamani na kushinda hiyo kesi,ila hawajalipwa mpaka leo. BOT wanaendelea kuappeal tu

Unataka kuniambia IGP aliondolewa na Dr Rashid na akaenda mahakamani!!!? kazi kweli kweli!!! Lakini ni jambo jema kwamba atakua anayaelewa vyema mazingira ya ndani ya BoT
 
Unataka kuniambia IGP aliondolewa na Dr Rashid na akaenda mahakamani!!!? kazi kweli kweli!!! Lakini ni jambo jema kwamba atakua anayaelewa vyema mazingira ya ndani ya BoT

Katika orodha ya watu wanaopambana mahakamani, jina la Mwema halimo. Mwema ni mmoja wa askari waliorudishwa Jeshi la Polisi, hakufutwa kazi.

Miaka ya nyuma BoT ilichukua askari polisi kutoka Jeshi la Polisi ambao ajira zao zilihamia BoT na hivyo kuingizwa kwenye payroll ya BoT. Alichofanya Dr. Rashid ilikuwa ni kuwarejesha kule walikotoka.

Dr. Rashid aliamua kuwarejesha kule walikotoka kwa kuwa misafara ya fedha siyo kazi ya kila siku na inaweza kutokea mara moja moja, na hivyo BoT ingepunguza gharama kwa kuachana na kitengo hicho ambacho kilikuwa hapo permanently na hivyo walistahili haki zote from mshahara mpaka benefits nyinginezo zote.
 
Unataka kuniambia IGP aliondolewa na Dr Rashid na akaenda mahakamani!!!? kazi kweli kweli!!! Lakini ni jambo jema kwamba atakua anayaelewa vyema mazingira ya ndani ya BoT

Mkuu Halisi, nadhani hatujaelewana vizuri. Bwana Mwema alipelekwa BOT na mwajiri wake ambaye ni Jeshi la Polisi. Dr. Rashid alivyoingia BOT akareview utendaji wa kazi na rungu kubwa likawakumba Directorate of National Payment kwa kuwapa kazi ya cash management NBC badala ya BOT branches. Hivyo Mwema akawa hana kazi ya kufanya pale ndio akarudishwa kwa mwajiri wake(Polisi). Ila wakati huo huo maofisa wengine ambao hao walikuwa waajiriwa wa BOT nao wakatimuliwa na ndo wakaenda mahakamani kufungua hiyo kesi ya unlawful dismissal. Hivyo afande Mwema alipona kwa kuwa hakuwa muajiriwa wa BOT. nadhani sasa tutakuwa kwenye page moja.
 
Ahsante kwa ufafanuzi. Kwa kawaida usipouliza huwezi kujua na ajuae kuwa hajui ni mjuvi lakini ambaye hajui na hajui kwamba hajui, ni mshindi wa NISHANI YA JUU YA UPUMBAVU
 
Tukirudi kwenye BRELA...naomba niulize swali dogo tu. Hivi faili linawezaje kupotea? Je, ikiwa faili hakuna kuonesha kuwa kampuni X imesajiliwa, si ina maanisha hata uwepo wa kampuni X ni batili?

Kama utanielewa vizuri, ninachotaka kuonesha katika kuuliza huku ni kwamba kwanini tuwe na BRELA wakati hata kazi inayotakiwa kufanya haifanyiki? Huu uwajibikaji uko wapi? Siamini kuwa serikali na taasisi zake kama BRELA iwe inatoa majibu ya kipumbavu na yasiyoridhisha kama "faili limepotea". Hii inamaanisha Rais avunje BRELA na akiunda BRELA mpya, awape semina ya uhazili na jinsi ya kutunza mafaili kabla hawajatunza siri nyingine za serikali. Kwa kweli hata nikiwa na kampuni, nitashuku kuiamini BRELA.

Huu ni uzandiki uliokubuhu na kwa kweli sijui huyo Mkapa (whoever the hell heads BRELA) awajibishwe. Yeye binafsi au watendaji wake kamwe wasiwe na msamiati "faili halionekani". Sasa kama wewe umepewa kazi ya kufungua na kutunza faili, unataka nani alione au alitafute? Simaanishi kuwa mjuvi kung'amua kwamba ni kitu kidogo au ufisadi unaochangia kwa majibu ya kipuuzi kama hayo, kinachonikasirisha ni kwa hiyo rushwa kuwa waziwazi. Yaani, "faili limepotea" ni synonymous na "naomba rushwa" na kila asemaye hivyo, aripotiwe PCB na kufanywa kisamvu cha mboga kule Keko au Isanga.

Kwa upande mwingine, hii inadhihirisha jinsi serikali inavyohitaji kuboresha utunzwaji wa kumbukumbu. BRELA ni sehemu moja tu, lakini uzembe huu uko kila mahali; mahakamani, hospitalini, polisi, TRA, n.k. Kila taasisi ingetakiwa kuwa utunzwaji wa nyaraka za serikali mtandaoni huku kukiwa na access codes kulingana na unyeti wa nyaraka hizi. Tena hizi taasisi, ziwe zina back-up servers katika mikoa mingine ili kama uhujumu (au balaa la moto kutokea) ukifanyika kwenye sehemu moja, bado hizo nyaraka zitakuwa zimehifadhika. Mfano wa umuhimu huu ni wa Benki Kuu ya Marekani (Federal Reserve) ilivyojitayarisha kujihami siku ya Septemba 11,2001. Kwa vile New York ndio kitovu cha biashara Marekani, hususan Wall Street, data zote zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye sehemu zilizoathirika na matukio ya siku hiyo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye back-up server kwingineko (nukuu kutoka kitabu cha Alan Greenspan).

Tusingoje kwa balaa kutokea ili kurekebisha mambo. Ni vyema serikali ijihami na kuboresha mambo hayo. Hii itasaidia pia kwa vyombo vya usalama na dola (Polisi, PCB, Usalama wa Taifa,TRA,BoT nk) kushirikiana katika kutokomeza rushwa na ufisadi nchini. Ningeshauri waanzie BRELA na BoT kuonyesha mfano wakati huu ambapo habari zao bado ni za moto!
 
Mpanda Merikebu,

Kwa tanzania yetu hayo yote hayawezekani, kwasababu hata huyo Mkapa si ajabu ana uhusiano na aliyekuwa rais Mkapa (I stand to be corrected).

Sasa kuwajibisha ni kujaribu kumpinga Mkapa (former Prez)

Tanzania ni ya kulindana na kula bila kunawa...
 
Mi nadhani BRELA kwenye hili la kukosa kumbukumbu walifanya usanii tu kwa kutokuwa specific. Maana katika hali ya kawaida kampuni kama Ernest and Young walichokifanya ni kuandika barua ya kuomba Company Search, BRELA na kulipia fee yake(mara ya mwisho nilivyofanya search ilikuwa Tzs. 2,000). Baada ya hapo unasubiri majibu. BRELA wanakuandikia barua kukutajia mashareholders na percentage zao, directors, registred ofices,mpaka kama assets za kampuni zimewekwa dhamana(debenture). Maana hizi zote ni public records. Sasa inavyoelekea nikifuatilia maelezo ya Mzee Luhanjo ni kwamba BRELA hawana hizo records.

My take ni kwamba either hizo kampuni zilipresent forged docs(Mamerts na Certificate of Incorporation) fake. Yaani za kuchonga mitaa ile karibu na zamani posta club.Kama ndio hivyo ina maana hakuna usajili uliowahi kufanyika pale kwenye daftari la msajili wa makampuni. Sasa kama EPA hawakufanya Company search basi ndo imetoka hiyo, hakuna wa kumkamata.
Or
Hizi kampuni zilikwenda Brela kuomba usajli lakini hazikumalizia process, yaani walikuwa cleared kwenye business name (Registrar of Business names) na wakaambiwa sasa jamani leteni Mamerts na other information, wakaingia mtini na kwenda kuproduce Certificate of Incorporation fake, na kuendelea na mambo yao huko EPA. Scenario hii ya 2 ina maanisha msajili ana partial documentation ambazo hatoweza kutoa full company search.

Scenario ya 3 ni kuwa hizi kampuni zilikuwa full registered Brela, na watu wa ndani wameamua kuondoka na file(full records zimepotezwa kutoka kwenye registry. Sasa hapo ndo patamu,maana concrete records zinazoweka kupatikana ni kutoka kwa Registrar of Business name pamoja na accounts maana kama unasajili kampuni lazima Mamerts zile na jina la suscriber/drawer(mara nyingi huwa mwanasheria).Kwa hili sitaki kuamini kuwa BRELA watakosa records kabisa.

Udhaifu wa BRELA kwa mtizamo wangu upo kwenye uzembe wa kufuatilia going concern of the registered companies. Maana kila kampuni inahitajika ku file annual return(Form no 128 as per Section 128 of the Companies Act 2002. Lakini zaidi ya 80% ya kampuni hazifile wala BRELA hawafatilii. Sio kuwa tu wanapoteza Income(filling fees) bali hata kukiwa na any changes za directors,physical location etc, wanakuwa hawana taarifa zozote.Hapo ndo kwenye real problem, maana kama hizi data zingekuwa latest kwa haya makampuni yote yaliokula hizi hela wangeweza kuretrieve latest records including records such as jina la director lina appear kwenye kampuni gani zingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom