Wageni wanavyopata ajira za Watanzania

Wageni wanavyopata ajira za Watanzania

mzanzibara-

Senior Member
Joined
Feb 3, 2014
Posts
179
Reaction score
61
wanapenda umeneja fedha, uendeshaji na masoko,
wengi wanatoka india, kenya, china na south africa

jamani nauliza hili tatizo litaisha, limekuwa ni common hapa nchini kwetu na watu wa idara ya kazi wanaangalia tu, nimeiona hii katika gazeti la HABARI LEO
mwishowe wanasema rais kikwete kuwabana na kubadilisha sheria,
yangu macho!!
------------------------------------------------------------



t39a.jpg

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa kashikanamikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mh, Waziri wa Kazi na Ajira Mh Gaudence Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Galawa katika sherehe za Mei Mosi
UWEPO wa vyombo mbalimbali vinavyotoa kibali cha kufanya kazi
nchini, umetoa mwanya kwa wageni kuingia nchini na kuajiriwa katika Umesahau
nafasi za kazi, ambazo baadhi hata Watanzania wana uwezo wa
kuzijaza. Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa Sikukuu ya Wafanyakazi
Duniani (Mei Mosi), Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali imebaini kuwa
tatizo hilo la kutolewa kwa vibali kiholela, linatokana na vibali hivyo,
kutolewa na taasisi zaidi ya moja.

Gazeti hili limepata taarifa kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, inayoonesha
namna wafanyakazi hao, wanavyopata vibali vya kufanya kazi nchini,
jambo lililolalamikiwa na wafanyakazi kuwa baadhi ya wageni hao, wanapata ajira ambazo Watanzania wanaweza kuzijaza kwa
ufanisi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vibali vya kufanya kazi nchini kwa wageni, vimekuwa vikitolewa na Wizara ya Kazi na Ajira, kupitia
Kamati ya Utatu inayoundwa na Wizara, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) na Chama cha Waajiri nchini (ATE).

Hata hivyo, baada ya mgeni kukubaliwa kupata kibali na Wizara kupitia utatu huo, wageni hao hupata kibali kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Uhamiaji ambacho ni kibali Daraja B, kinachoruhusu wageni watakaoajiriwa kwa masharti ya
kudumu tu.


Mbali na Wizara ya Kazi na Ajira, taarifa hiyo imeeleza kuwa vibali Daraja A na C, hutolewa moja kwa moja na Idara ya Uhamiaji,
bila kupitia Wizara hiyo.
"Idara ya Uhamiaji pia ina mamlaka pia ya kutoa vibali vya muda mfupi bila kupitia Wizara ya Kazi na Ajira, mfano vibali vya miezi
mitatu mpaka sita kwa wageni ambao wanakuja kufanya kazi kwa muda mfupi," imeeleza taarifa hiyo.

Utaratibu unaotumiwa na Wizara ya Kazi na Ajira, kutoa kibali kwa mgeni kufanya kazi nchini, kwa kushirikisha ATE na Tucta,
huzingatia mambo mbalimbali. Kwanza taarifa hiyo imeeleza kuwa kibali hukubaliwa kwa kuzingatia idadi ya miradi, ambayo
kampuni husika inayo na muda ambao miradi hiyo itakamilika.

Pia, kabla ya kutoa kibali, mapendekezo ya wizara zenye dhamana ya kupendekeza waombaji huzingatiwa, mfano Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa upande wa walimu, Wizara ya Ujenzi kwa wageni katika miradi ya ujenzi na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sababu nyingine inayozingatiwa wakati wa utoaji kibali katika Wizara ya Kazi na Ajira, imetajwa kuwa
ni cheo cha muombaji, ukubwa wa kampuni na idadi ya Watanzania, walioajiriwa na kampuni husika.
Mamlaka nyingine inayohusika kutoa vibali vya ajira kwa wageni ni Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC). Kwa mujibu wa taarifa hiyo,
Sheria ya Uwekezaji ya 1997 Ibara ya 24 (1) (2), inaruhusu waombaji watano wa mwanzo katika mradi wa uwekezaji, wapewe
vibali vya kufanya kazi nchini, hata kama sifa zao Watanzania wanazo.

Mbali na waombaji hao watano wa mwanzo, Sheria hiyo
imewaruhusu pia wawekezaji, kuongeza wageni zaidi ya hao watano katika ajira wanazotoa, kulingana na umuhimu wa mtu
wanayemuombea. Nafasi zao, watokako Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchambuzi uliofanyika wizarani, umeonesha wageni wengi
wanaokuja kufanya kazi nchini, hupendelea nafasi za umeneja, ambazo ndizo zenye malipo mazuri.

"Uchambuzi unaonesha mameneja (uendeshaji, masoko, fedha na kadhalika), ndio wanaoongoza kwa idadi ya wageni
wanaokuja kufanya kazi nchini," taarifa hiyo imeeleza.
Wengine ni wataalamu, ambao hawako katika mchanganuo wa kisekta, wakiwemo mafundi mchundo katika sekta ya ujenzi,
walimu, wasimamizi, mameneja wakuu na wakurugenzi, wafanyakazi katika viwanda vya chuma, wahandisi na wanasayansi.

Nchi zinazoongoza kwa kuwa na wingi wa wageni wanaofanya kazi nchini, kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni India ikifuatiwa na China,
Kenya, Afrika Kusini, Pakistani na Uingereza.

Taarifa hiyo imekiri kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa wanaopewa vibali hivyo, ambapo baadhi ya wawekezaji wanapata vibali na kufanya kazi, ambazo hazipo katika vibali vyao.
"Wafanyabiashara ndogo hasa maduka, hawapendekezwi kupewa vibali isipokuwa kumekuwa kukifanyika udanganyifu mkubwa,mfano wanaingia nchini kama wawekezaji na nyaraka zote muhimu wanapata na wakipewa hawafanyi lengo lililowaleta. "Hii ni
changamoto kubwa kwa Wizara ya Kazi na Ajira na wadau wengine kama Wizara ya Viwanda na Biashara, Msajili wa Makampuni
(Brela) na TIC kubaini mbinu zote na kuchukua hatua kwa kuwa ili mtu afanye biashara hapa nchini, taasisi mbalimbali
zinahusika," ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika sherehe za Mei Mosi, zilizofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema
kutokana na kukithiri kwa malalamiko ya Watanzania, kuhusu kutolewa holela kwa vibali vya kazi kwa wageni, Serikali inafikiria
kurekebisha Sheria ya Vibali vya Ajira kwa Wageni, ili kudhibiti ipasavyo utolewaji wa vibali hivyo.

Alisema Serikali imebaini kuwa tatizo hilo la kutolewa kwa vibali kiholela, linatokana na vibali hivyo kutolewa na taasisi zaidi ya
moja. "Hali hii inatoa fursa kwa watumishi wasio waaminifu kutumia mwanya huo wa taasisi nyingi kuidhinisha vibali hivi na
kuvitoa hata kwa watu wasiostahili kwa kujinufaisha, hili hatuwezi kulinyamazia," alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na kukithiri kwa tatizo hilo, Serikali imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, juu ya kujaa kwa
wageni nchini, wanaofanyakazi hata zile zinazoweza kufanywa na wananchi wa kawaida, jambo linalowanyima ajira wananchi
wengi.

Aliwaahidi Watanzania kuwa Serikali imeliona tatizo hilo na iko kwenye mchakato wa kulifanyia kazi kwa kuipitia upya Sheria hiyo
na kuandaa muswada wa marekebisho katika kipengele cha vibali vya ajira kwa wageni.
Alisema moja ya mapendekezo, yanayofanyiwa kazi kwa ajili ya kurekebishwa katika sheria hiyo, ni pamoja na eneo la taasisi
zinazohusika kutoa vibali hivyo, ambapo katika marekebisho hayo, itapendekezwa iwe taasisi moja pekee.

"Tutarekebisha na kutoa fursa ya kutoa vibali hivyo kwa taasisi moja pekee na kuiongezea udhibiti, ili endapo kutatokea
wafanyakazi wasio waaminifu iwe rahisi kuwabaini na kuwadhibiti," alisisitiza.


Chanzo:Habari leo
 
Tatizo ni ofisi zetu za uhamiaji sidhani kama sheria ya kumpa mgeni work permit ipo strong au ndio ukiwa na dola zako utapata tu.
 
Nendeni kwenye migodi muone walivyojaa yani asubuhi mnapishana na wazungu kama mpo south africa, na wana roho mbaya kama wapika sumu vile

Hii nchi ilivyokaliwa na wageni ndio maana mtu akipata upenyo anachota kwa kwenda mbele. Kama wakubwa hawatujali wanatoa ajira kwa wageni. sisi ni nani tuwe wazalendo ?
 
Kuna meli wao wanaita utafiti moja ina crew 800 na ina almost kila kitu humo hospitali mpk na facility nyingine. Ajabu hakuna Mtanzania hata mmoja humo na wanabadilishwa kila mwezi hiyo meli inaitwa Discoverer Americas. Ipo chini ya Kampuni ya Statoil ina supporting vessels nyingine ndogo kwa aajili ya kuleta mahitaji ndio zinaenda pwani hasa Mtwara na kurudi huko sea. Pia inameli zingine 3 za kuilinda hilo kubwa linalochimba ajabu katika hizo ndogo ndio kuna walinzi wa kibongo tena wa mwisho. Hata wanajeshi wapo kwenye hizo meli za ulinzi lkn wanapangiwa wazungu na kutumwa kama watoto ni aibu kwa kweli. Crew wengine ni Wasouth Africa na Wakenya na Warusi. Walinzi ni Waingereza na wanamaji wachache wa Tz. Lkn nao hawaruhusiwi kupiga picha au kulisogelea meli hilo. Je tutafika?
 
Nadhani tuchukie hatu kuliko kuulizana kila siku na wao wanazidi kuingia namanga, taveta, tunduma na kwingine ila ....Niliskia waajiri wakisema watanzania ujanja mwingi.. wenzetu wapo serious na kazi thats why wanachukua kazi zetu...
 
Napenda kusema tumefika hapo kwa sabab ya uvivu na utendaji mbovu wa idara ya uhamiaji,huku kwa wenzetu yan ukitaka kuja kuomba kazi mtu wa nje utapigwa maswal na mhusika ataulizwa hivi hatuna watu wenye vigezo hivo mpaka unamleta huyu.Narudia tena tatizo ni ubovu wa uhamiaje katika kutekeleza majukumu yao,tembeleeni idara zote hadi migodini na mjue kwa nini huyu expert yuko hapa,na kwa nin wako weng na kwa nin wengi wanakuja kujifunzia kazi hapa kwetu wakati anatakiwa aje mtu comptent,narudia tena naamini magogoni wanajua yote sema ndo hivo hatuwez kufanywa chochte mana watanzania tupo tayari kufa na tai shingoni
 
Jambo la kushangaza ni kuwa Gazeti la Serikali (Habari Leo) linatoa vyeo wanavyopata na uraia wao.Ina maana serikali inawajuwa lakini haitaki au haina uwezo wa kuwashughulikia.
Vyombo vya Serikali ndiyo vinavyosaidia kupata hizi ajira. Kuanzia Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Idara ya Usalama wa Taifa (security assessment) n.k.
Waajiri wakubwa wa wageni ni Makampuni makubwa ya kigeni,Mahoteli n.k na hili Serikali inalijuwa lakini inajificha kwenye udhaifu wa sheria zetu.
 
Hali yetu imefikia pabaya. Leo hii kuna wageni wenye bachelor degrees wamejaa maofisini wakati kuna wataalam kibao hapa, tena wenye elimu na uzoefu wa kutosha wa mazingira yetu wamewekwa bench.

Serikali imeruhusu wageni watutawale maofisini wakati elimu tunalingana. Rangi yake inamfanya alipwe dola 7000 za marekani kwa mwezi wakati mzawa analipwa Tshs 800,000 kwa mwezi.
 
Wabongo wezi!Mr.Kimei tuu ndiye katutoa kimasomaso kwa kuweza kusimamia kampuni ya umma ikakua kwa ufanisi
 
Hii ni ajabu kwa serikali kulalamikia uwepo wa wageni waliochukua nafasi za watz ili hali wana nyenzo zote za kuwashughulikia. Wanatulalamikia ili tuchukue hatua gani? Hatuna polisi, uhamiaji hata magereza! Na kwa nini walalame? Wasitutege sasa wangoje 2015.
 
Rudi zako shimoni kule....Nyinyi wakenya ni wabaguzi na roho mbaya pia.....kuna hoteli huku znz inaitwa Breezes beach club....haw jamaa wanawadhalilisha wazawa kupita kiasi...siku zenu zinahisabika...endeleeni tu
 
Hali yetu imefikia pabaya. Leo hii kuna wageni wenye bachelor degrees wamejaa maofisini wakati kuna wataalam kibao hapa, tena wenye elimu na uzoefu wa kutosha wa mazingira yetu wamewekwa bench.

Serikali imeruhusu wageni watutawale maofisini wakati elimu tunalingana. Rangi yake inamfanya alipwe dola 7000 za marekani kwa mwezi wakati mzawa analipwa Tshs 800,000 kwa mwezi.
 
Tatizo kubwa naloliona ni kuwepo kwa mianya ya Rushwa serikalini,hasa katika wizara husika ya ajira. Sheria zimebainisha wazi kabisa, ila tatizo ni hao wafanyakazi wake. Akipatikana Waziri husika aliye serious, hiyo madudu yote itabaki stori.
Lakini kwa mwendo huu, hata wachoma mahindi watakuja kuwa wageni kutoka nje
 
Wabongo wezi!Mr.Kimei tuu ndiye katutoa kimasomaso kwa kuweza kusimamia kampuni ya umma ikakua kwa ufanisi

Wabongo sio wezi kaka,tatizo ni la kuwekana madarakani kwa kufahamiana ndo mana mtu anaona aibe tu mana aliemuweka si atajazia vilivopotea,hilo ndo tatzo kaka.Mbna benk ya Exim ilikua chini ya Mrs Mwambenja na imesimama mpaka leo na alikaa zaid ya miaka 4 na sasa hivi ashaondoka,aliwekwa na wahindi mana wanajua wanahitaj mtu wa aina gani sio wizara ya madini unamuweka msela wako wa education afu wizara ikifa unamlaumu wa education.Hii ni dharau ya Mkuu
 
vp kuhusu dr dau yeye nae mwizi?

Mkuu nssf hata wewe ungeweza management maana hakuna production cost pale ni kucollect pesa tuu toka kwa waajiri na ku invest basi.
 
Back
Top Bottom