IGP Sirro, Tafadhali usiligeuze jeshi la polisi kama mob

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,503
51,098
Kamanda Sirro, kuna clip inatrend kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha jeshi lako la polisi likivamia mkutano halali kabisa wa chama cha ACT wazalendo.

Mkutano wao huo wa amani na wa ndani ulikuwa ungali ukiendelea huku wananchi wakiwa wanaimba nyimbo kumkaribisha kiongozi wao wa chama, ghafla polisi wakajitokeza na kuvamia mkutano huo huku mmoja akotoa maelekezo yakionyesha Zitto aondolewe kwa nguvu.

Wakati huohuo Polisi ikiendelea kuwasumbua wapinzani kufanya shughuli zao halali zilizoko kwa mujibu wa katiba, Chama cha mapinduzi chenyewe kimeonekana kuendelea kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa na yeyote.

Tunalaani matendo haya ya polisi, ningependa kumueleza IGP Sirro, Si vizuri jeshi la polisi kufanya mambo kama Mob, tunapojaribu kujenga Taifa letu.

Vyama vya upinzani vipo kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba, na vina haki ya kufanya siasa kwa uwazi kabisa bila kubughudhiwa na Yeyote.

Kitendo cha polisi mara kwa mara kusumbuasumbua wapinzani, au kutoa matamko ya kuashiria kuwa linatumika kisiasa, ni mambo ya kihuni, aibu na hayafai hata kidogo. Hayo mambo hayawezi kuleta heshima kwa jeshi la polisi nchini.

Tunalitaka jeshi la polisi kuacha mara moja matendo haya aibu na yasiyokuwa ya kiungwana hata kidogo.

Hayo mambo hayalifai jeshi la polisi, hayo mambo hufanywa na mobs lakini si kwa jeshi la polisi linalopaswa kuheshimiwa

IGP Sirro unafeli sana kwenye angle hii, usikubali kutumika kisiasa!

Hii video ya uvamizi wa mkutano wa ACT huko Kilwa inasikitisha sana

 
Policcm! Ni jeshi lisilo na tofauti kabisa na lile la enzi za Mkoloni. Limejikita zaidi kuibeba Ccm huku likiwakandamiza wapinzani na wale wote wanao tofautiana na Ccm au Serikali ya Ccm.

Aibu kwenu Polisi! maana mnafahamu fika mnachokifanya siyo sahihi. Ila kwa makusudi kabisa mnajitoa ufahamu.
 
Kamanda siro ni mchapakazi sana,,tena wanajf ndo mlipiga debe apewe u IGP toka enzi za jk,mlitaka apewe U igp,leo munageuka tena?,,,
Chapa kazi kamanda
 
Hivi vitu mbona vipo sana Afrika huko mkuu! Sema mnakosa kumbukumbu labda,yanayofanywa na Polisi ni kua nchi imetekwa na wadhalimu,wananchi wamepokwa mamlaka na Uhuru wao. Kuna tofauti gani wakati wa ukoloni na wakati katika haki na Uhuru wa mtu mweusi apo Afrika?
 
Mie nawashangaa wale wanaoshangaa,huu n wakat wa kusifu na kuabudu co vngne, unadhn hawajui walitendalo?hakuna mkate mgumu mbele ya chai mkuuu
 
Back
Top Bottom