IGP Sirro: Mabasi ya DSM kwenda Arusha, Mwanza na Mbeya yataruhusiwa kusafiri Usiku hivi karibumi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,965
141,969
IGP Sirro amewatembelea majeruhi wa ajali ya coaster iliyotokea Mafinga na kuwatakia uponyaji wa haraka

Aidha IGP Sirro ameagiza mmiliki wa hiyo coaster akamatwe na kutoa maelekezo kwanini aliruhusu gari yake kusafirisha abiria usiku tena bila kutoa tiketi

Kamanda Sirro amesema Jeshi lake limekamilisha mazungumzo na mamlaka za Usafirishaji na hivi karibumi mabasi ya abiria yataruhusiwa kusafiri Usiku

Kwa kuanzia wataanza na route za Dar to Arusha , Dar to Mwanza na Dar to Mbeya

Chanzo: ITV
 
Usiku ndiyo hatari kabisa, ajali ya Mafinga inathibitisha na hii ni kutokana aina ya miundo-mbinu, weledi wa madereva kuzingatia mwendokasi, nini kifanyike gari lako likiwa bovu limeharibika njiani je uite askari wa usalama barabarani waweke viashiria vya kuwepo gari bovu na hatua za haraka kuita msaada wa gari bovu litolewe haraka barabarani ili lisiweze kusababisha ajali n.k

MLIMA KITONGA MTIHANI KWA MAGARI NA MADEREVA WANAOKUMBANA NA GARI LILILOHARIBIKA

HITAJI KWA JESHI LA POLISI KUJIKITA KUFANYA DORIA KUONDOA MAGARI YALIYOHARIBIKA BARABARANI

Mfano mafunzo kwa askari wa usalama barabarani na vikosi vya uokozi vya zimamoto kufika haraka eneo la tukio ili kuondoa magari yaliyoharibika barabarani ili kuzuia ajali kutokea.

Askari wa usalama barabarani walazimishwe kisheria ku patrol barabara na kuhakikisha magari yaliyoharibika barabarani yanaondolewa haraka na pia madereva kulazimika kisheria kuripoti kuhusu magari yao yaliyoharibika barabarani ili vyombo husika kama askari wa doria wa usalama barabarani/ magari ya breakdown/ zimamoto n.k wafike na kuyatoa au kuyakokota kutoka ktk barabara ili kuepusha uwezekano wa ajali iwe usiku au mchana au mvua inanyesha au jua kali lipo.

Pia kuna ulazima wa haraka bunge kuja na muswada wa dharura ili serikali kuunda kikosi maalum cha highway patrol ambacho kazi yake kubwa ni kuhakikisha usalama ktk njia zote kuu za usafiri, hiki ni tofauti na trafiki wa usalama wa barabarani katika miji.

Serikali imewekeza sana ktk miundombinu barabara za lami hivyo hitaji la kikosi cha doria cha barabara kuu ndiyo wakati umefika maana wanaotumia barabara wameongezeka na changamoto pia .

Rescue teams train to keep drivers safe by clearing accidents on AZ roads

First responders are trained to handle bad accidents quickly and safely. Here's an inside look at how rescue teams prepare for dangerous road situations.
 
Dar Sumbawanga lazima ufike saa 8 usiku au saa 9 usiku.

Kwahiyo mabasi yanasafiri usiku kama kawaida labda hiyo route ya Dar Moshi Arusha itasaidia wafanyabiashara kuingia asubuhi Dar au Arusha.
 
IGP Sirro amewatembelea majeruhi wa ajali ya coaster iliyotokea Mafinga na kuwatakia uponyaji wa haraka

Aidha IGP Sirro ameagiza mmiliki wa hiyo coaster akamatwe na kutoa maelekezo kwanini aliruhusu gari yake kusafirisha abiria usiku tena bila kutoa tiketi

Kamanda Sirro amesema Jeshi lake limekamilisha mazungumzo na mamlaka za Usafirishaji na hivi karibumi mabasi ya abiria yataruhusiwa kusafiri Usiku

Kwa kuanzia wataanza na route za Dar to Arusha , Dar to Mwanza na Dar to Mbeya

Source ITV
Hivi bado Siro haja anza kuaga kuachia ofisi zetu???
 
HITAJI KWA JESHI LA POLISI KUJIKITA KUFANYA DORIA KUONDOA MAGARI YALIYOHARIBIKA BARABARANI

Mfano mafunzo kwa askari wa usalama barabarani na vikosi vya uokozi vya zimamoto kufika haraka eneo la tukio ili kuondoa magari yaliyoharibika barabarani ili kuzuia ajali kutokea.

Askari wa usalama barabarani walazimishwe kisheria ku patrol barabara na kuhakikisha magari yaliyoharibika barabarani yanaondolewa haraka na pia madereva kulazimika kisheria kuripoti kuhusu magari yao yaliyoharibika barabarani ili vyombo husika kama magari ya breakdown/ zimamoto n.k wafike na kuyatoa au kuyakokota kutoka ktk barabara ili kuepusha uwezekano wa ajali iwe usiku au mchana au mvua inanyesha au jua kali lipo.

Rescue teams train to keep drivers safe by clearing accidents on AZ roads

First responders are trained to handle bad accidents quickly and safely. Here's an inside look at how rescue teams prepare for dangerous road situations.

bagamoyo mtu yeyote mwenye mafunzo halali ya udereva anajua gari inapoharibika njiani kitu cha kwanza kabisa ni kuweka alama kuanzia mbali ili kuonya madereva wengine wapunguze mwendo na kuwa makini. Infact unatakiwa kutembea na alama kwenye gari lako kwa tahadhari. Hata kama polisi wakifanya patrol lakini hawawezi kuwa kila sehemu gari ilipoharibika kwa wakati. Gari inapoharibika, dakika tano tu ni muhimu sana.
 
Hata kama polisi wakifanya patrol lakini hawawezi kuwa kila sehemu gari ilipoharibika kwa wakati. Gari inapoharibika, dakika tano tu ni muhimu sana.

Tujiulize nchi zilizoendelea kama za Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan, Australia na China kwa kuzitaja kwa uchache wana vikosi vya doria vya usalama wa njia kuu / highway patrol iwe vipi nchi ya Tanzania ishindwe na kukosa kuona umuhimu wa kikosi cha doria cha usalama wa barabara kuu ?

Bonus Scene : Always On Patrol I Heavy Rescue : 401

Law enforcement on the 400 series highways is a massive task. The Ontario Provincial Police responds to calls big and small - all of them vital to making the highways safer.
Source : Discovery Canada
 
Nilichokiona, ajali nyingi zinazotokea hasa highway, zinasababishwa na uoni hafifu wa madereva!
Serikali itilie mkazo kwa madereva kupimwa macho ili wale wasioona mbali wapatiwe miwani. Hii itasaidia kupunguza ajali.
 
IGP coaster haina Roadworthy, leseni na imeweza kusafiri umbali wa zaidibya 450km bila kuzuizi njiani, na wewe undamaged akamatwe owner why?,Anza kukamata traffic officers wako kuanzia ubungo hadi mafinga maana waliruhusu hii coaster kupita kwenye check points na utitiri wa road blocks, pia my IGP wangu hii T1 ondoa road blocks zote(ni vituo vya rushwa)bakisha check points only.
 
Tujiulize nchi zilizoendelea kama za Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan, Australia na China kwa kuzitaja kwa uchache wana vikosi vya doria vya usalama wa njia kuu / highway patrol iwe vipi nchi ya Tanzania ishindwe na kukosa kuona umuhimu wa kikosi cha doria cha usalama wa barabara kuu ?

Bonus Scene : Always On Patrol I Heavy Rescue : 401

Law enforcement on the 400 series highways is a massive task. The Ontario Provincial Police responds to calls big and small - all of them vital to making the highways safer.
Source : Discovery Canada

Nisome vizuri: Sijakataa kuwa na doria. Nachosema ni kuwa gari linapoharibika barabarani, wajibu wa kwanza ni kwa dereva kuweka alama za warning ASP! Haya mengine ya ndiyo yanafuatilia. BTW tatizo letu kubwa ni polisi kuendekeza rushwa na kutowajibika hivyo hata hizo patrol zinaweza kuwa kero zaidi ya kusaidia.
 
Namshukuru sana Spika Tulia kwa kuibua tena jambo hili.
1. Nashauri mabasi yaruhusiwe kuondoka wakati wowote ufaao badaa ya kulazimishwa kuondoka Dar alfajiri (saa 12).
Kwa mfano.
Mabasi yanayokwenda mikoani yakiruhusiwa kuondoka saa 6 mchana yatafika Kahama alfajiri ambapo yataendelea na safari yake.
2. Kusafiri usiku kutapunguza gharama za wasafiri.
Hivi sasa ili kuwahi stendi ya Magufuli kupanda mabasi ya alfajiri inabidi ama kulala nyumba ya wageni au kutumia usafiri wa gharama kubwa kwa kuwa ni usiku.
Safari zikianza mchana au jioni zitatuondolea adha hii.
3. Muda mwingi unapotea kwa kusubiri.
Kila ukifika usiku mabasi yanaegeshwa.
Kwa kanda ya ziwa ni Kahama.
Abiria wanatumia gharama kwa kulala safarini.
Baadhi ya abiria ni wagonjwa wanaokwenda kwenye matibabu au misiba
Hawa wanacheleweshwa.
Mabasi yakitoka Singida jioni yatafika Dar alfajiri ambapo abiria mfanya biashara ataingia kwenye manunuzi kisha jioni/usiku atapanda basi kurejea alikotoka.
Hakuna.muda wa kupotea.
4. Muda wa matengenezo utakuwapo wa kutosha.
Baadhi ya mabasi ya mikoani kama yaendayo Mbeya na Kahama yanafika usiku na alfajiri yanarudi Dar.
Matengenezo yanakuwa hafifu kwa kuwa gereji nyingi zinakuwa zimefungwa.

Hata hivyo ni LAZIMA jeshi la polisi lijiandae vema kwa ajili ya kuhakikisha usalama.wa.abiria.

Nadhani ni vema LATRA iondokane na utaratibu wa sasa wa kuondoa mabasi vituoni kwa wakati mmoja kama vile ni mashindano ya mbio kwenye riadha.

Nashauri mabasi yaanze safari kwa muda tofauti.

Asante sana Spika Tulia Ackson kwa kuchagiza hili.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom