IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

If it's true that some unruly members of the ill-disciplined police force descended on the late Hamza and forcefully took away his gold worth hundreds of millions of shillings when he was on his way to sell it, then it will be nonsensical to blame the late Hamza for his reaction.

If Sirro has failed to instill some sense of discipline to his police to have them adhere to the code of ethics guiding their job then one can say what Hamza did to them won't be the last and we should brace ourselves to witness similar "Reactions" in the future because his police force has turned into a game wardens cum poachers.

Let this incident serve as a lesson to the surviving members of this discredited force to mend their ways and abide by the police code of conduct.

Lastly, let Sirro understand that, as the police chief, he bears the responsibility for ensuring that all members of his police force are conducting their duties in line with the laid down procedures by restraining themselves from indulging in criminal acts and above all, they ought to know that, they aren't above the law.

Please Mr. Sirro come to your senses that police are not supposed to break the law but to respect the same so as to reflect on the general populace.
 
Mimi Imani yangu inakataza kulipa kisasi !

Tunatakiwa kumuachia Mwenyezi Mungu yeye ndiye anayejua jinsi ya kuwalipa uovu wao.

Allah Wakil.
Siku ya kiama kuna watu watahukumiwa kwa makosa madogo sana ya kutokujua kipi ni haki yake na kipi sio haki yake. Kisasi ni haki lakini kusamehe ni vizuri zaidi. Na hakuna sehemu ndani ya Quran inayosema mtu akikukosea sio haki yako kumlipizia, ila inahimizwa kusamehe ni vizuri zaidi.
Kasome Surah Al - Qasas
 
Kiongozi yoyote yule mkubwa katika nchi hatakiwa anapotoa kauli zake ziwe zinabase upande mmoja kwa kutetea upande huo na kulaumu upande mwingine kuwa ulichokifanya sio sahihi, kwa hili Ai jii P ameteleza kwa maana hakuna mzazi anaependa mwanawe aliyemzaa kuwa mhalifu, lakini pia hakuna mwenye guarantee ya Muumba kuwa kizazi chake hakina tabia mbaya wala miongoni mwa kizazi chake hawatotoka wahalifu bali ni Muumba mwenyewe ndio anaejua namna ya mapito na kukiongoza kizazi cha mtu.
Then watanzania tusiwe na tabia ya kumsema mtu moja kwa moja kutokana na vitendo vyake kwasababu kitendo cha kusema kuwa Hamza ni Gaidi hakuna mwenye uthibitisho (hakuna mwenye kuijua nafsi ya mtu imekumbwa na kitu gani)... Na pia ni kitu kinachojulikana kabisa hata kama polisi wakikushika ndani ya muda mfupi kitendo cha wao kuchukua chochote kwenye pochi yako ni jambo ambalo limeshazoeleka.
Alichotakiwa Ai jii P kufanya ni kutoa pole kwa familia za askari waliopoteza wapendwa wao basi na sio kuongea kauli ambazo hata yeye kama mtanzania na kama mzazi pia siku akikaa chini na kuzirudia ndipo ataona zina walakini. Kwani hata yeye sio malaika hivyo hata kizazi chake ni binaadamu na kama tunavyojua binaadamu hata baba na mama wawe ba tabia njema kiasi gani lakini watoto hawatokuwa na tabia njema kwa 100% kwani kuzaliwa wote tunazaliwa sawa lakini tabia kila mtu anakuwa na yake.
Na kama kweli moja ya mtoto wake ana tabia za ajabu..... Nampa pole sana kwa hilo maana Watanzania kila mmoja akili zake anazijua mwenyewe.
 
Huyo ni Mtoto wa Sirro anasumbua watu sana mtaani kwa ubabe wake na anavuta bangi hadharani. Muda Mwingi anashinda Chanika kwenye Bar ya Baba yake.
Anafanya yote hayo kwasababu anajua hakuna yeyote anaethubutu kumkamata wala kumfanya lolote kwani polisi wote wako chini ya amri ya baba yake. Na hili swala ni huku Africa tu! Madaraka ya baba yanagawanyika kwa mama na hata kwa watoto!!
 
Sirro tumbo Ni mithili ya shamba hutoa mazao ya Kila aina,hivyo huwezi kutukana wazazi na familiya Kisha tukupigie makofi kwa ubora wa matusi. Sirro ulichofanya Ni utoto na ulevi wa madaraka, tubu mapema. Sirro unahisi Kama kizazi chako hakifahamiki? Mbona na wewe ulizaa, kulea, na kukuza mvuta bangi anayesumbua chanika. Hotel zako za mwanza ulizijenga kwa mshahara na lesheni ya upolisi gani. Usitake tuseme yasiyotakiwa kusemwa. Kitendo Cha kudhihaki familiya HAPANA HAPANA HAPANA HAKIKUBALIKI.
JF...Tiririka Mkuu
 
Siro ukimwangalia mwonekano wake kimwili utadhani ni mtu wa kuheshimika sana!

Hapana, kuna wakati hata matamshi yake yalionekana kuwa ya mtu mwenye busara.

Haieleweki ni kitu gani hasa kimembadilisha akili kiasi hiki alivyokuwa sasa?

Unajua, inasemekana damu za binaadam zikimwagwa kwa uonevu tu, hazimwachi mtu anayesababisha zimwagike, ni lazima atadhurika tu kwa njia moja au nyingine.

Siro ni mhanga wa umwagaji wa damu za waTanzania ambao hawakustahili kuuliwa au kuumizwa.

Maisha yake ya uhai wake uliosalia yatakuwa ya matatizo tupu.

Mkuu umejiongeza mpaka umejiandika mwenyewe. Maishani mwkao umetoa au umechangia pesa au kimawazo umwagaji damu kiasi gani. Mimba changa au. Jifunze kucontrol hisia zako Fake. Siro amefanya mengi sana. Kama Askari hawezi kuwa hakosei Ila Sasa tuhuma za damu za watu wasio na Hatia na yeye wapi na wapi.
 
Mkuu umejiongeza mpaka umejiandika mwenyewe. Maishani mwkao umetoa au umechangia pesa au kimawazo umwagaji damu kiasi gani. Mimba changa au. Jifunze kucontrol hisia zako Fake. Siro amefanya mengi sana. Kama Askari hawezi kuwa hakosei Ila Sasa tuhuma za damu za watu wasio na Hatia na yeye wapi na wapi.
Kama wewe ndiwe Sirro, jitafakari, kwa sababu unayofanya sasa hayakuongezei chochote kizuri maishani mwako. Kuumiza watu wengine hakutakupa sifa nzuri. Kama wewe siyo Sirro, ila ni shabiki wake tu, mfikishie ujumbe. Anamaliza utumishi wake vibaya, na kumbukumbu zake ndani ya taifa hili zitaonyesha uongozi mbovu anaouonyesha sasa hivi. Hayo mazuri yote aliyofanya huko nyuma yatapotea, kitakachokumbukwa ni haya ya sasa ambayo siyo mazuri.

Anayofanya sasa siyo "kukosea kama binaadam" unavyotaka watu waamini. Haya ya sasa ni maksudi ya kuumiza wengine. Haieleweki kwa manufaa ya nani!

Ngoja nimalizane na wewe: Kama "hisia ni Fake," kwa nini zikuumize kama unavyoonyesha hapa!

Mchango wangu katika kuumiza, kuharibu maisha ya watu wengine hayawezi kamwe kulinganishwa kwa kiasi chochote anachokifanya Sirro wakati huu.
 
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.

"Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?". Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.

Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu, ukiwemo kupiga watu.

Je, unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
Wazee wa intelijensia bado hawajamfikishia huu uzi?
 
Upekuzi Kwaajili Ya Iigiipii Umeanza
Ikikupendeza Tafadhali Pictures Kwenye Thread
 
Back
Top Bottom