IGP mbona anashushiwa heshima!

IGP mbona anashushiwa heshima!

Usalama upi? Rejea msukuma anavyotukana wapinzani live kwenye mikutano, juzi juzi kheri james kaongea maneno ya ovyo kabisa, yule mnyeti je?
Hawa ccm na vijana wao wanaona poa tu sababu wana viposho vyao kila kukicha, ila kuna siku hasira za watu mioyoni zikifumuka kutokana na yanayoendelea wenda hata jeshi lisiingilie, maana uonevu ni wa wazi wazi.
Bora tuna jf angalau tunapashana habari maana vituo vya habari navyo vimebaki kama tbc, azam ilivyokuwa neutral wameshaifanyia figisu na bado mijitu inaona huko tunakoelea ni sawa.
Wakati ilibidi watu waogope kwa kinachoendelea, jiulize udiwani tu ni hivi, je 2020 itakuwaje?
Kweli kabisa mkuu inapaswa Taifa likombolewe kifikra.Hasa hawa Lumumba wapewe elimu ya uraia.Lakin nadhani wanaigiza tu ila wanajua kabisa kuwa tunakoenda sio kabisa kwa makusudi wanatetea uovu.Rejea zile tumbuatumbua,Makonda kuvamia clouds,makonda kutokuwa na cheti,mnyeti kusema hashirikiani na wapinzani nk.Lengo lao ni kuona ccm haichafuki ila kuna wachache wanaichafua na wao wanafunga macho makusudi kabisa
 
Usalama upi? Rejea msukuma anavyotukana wapinzani live kwenye mikutano, juzi juzi kheri james kaongea maneno ya ovyo kabisa, yule mnyeti je?
Hawa ccm na vijana wao wanaona poa tu sababu wana viposho vyao kila kukicha, ila kuna siku hasira za watu mioyoni zikifumuka kutokana na yanayoendelea wenda hata jeshi lisiingilie, maana uonevu ni wa wazi wazi.
Bora tuna jf angalau tunapashana habari maana vituo vya habari navyo vimebaki kama tbc, azam ilivyokuwa neutral wameshaifanyia figisu na bado mijitu inaona huko tunakoelea ni sawa.
Wakati ilibidi watu waogope kwa kinachoendelea, jiulize udiwani tu ni hivi, je 2020 itakuwaje?
Mimi nafikiri Zito Kabwe ana jambo la kufanya kulinda demokrasia.

Ni aibu kubwa kwa Muhimili wa dola kudharau watendaji wa muhimili mwingine kiasi hicho.
Ndugai amefanya bunge limekua chini kabisa .

Wabunge ni watu waliochaguliwa kama ilivyo Rais tofauti ni kwamba wabunge wamechaguliwa kwa kazi ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Lakini Serikali IPO kwa ajili ya kusimamia zile sheria zilizotungwa na bunge ikiwemo sheria za Uchaguzi na sheria za mfumo wa vyama vingi.

Cha ajabu wasimamizi wa sheria wanazivunja wazi wazi sio kwa sababu yoyote lakini ni woga wa kila mtu kulinda cheo chake.
Wasimamizi wa sheria wanakua wanawadharau wabunge kwa kiwango kikubwa sana.

Katika haki ya kawaida Mkuu wa wilaya ni kama mtu wa kuja kwenye wilaya lakini mbunge amechaguliwa na wananchi lakini wakuu wa wilaya na mikoa wanalinda maslahi yao kwa kuumiza watu na kuvunja sheria hata kwa mihimili mingine ambayo kimsingi inapaswa kuheshimiwa sana.
Watendaji wengi wa awamu hii wanajifanya kama miungu watu wanaotoa maendeleo kwa matakwa yao na mapenzi yao bila kuhojiwa alimradi tu watu wanashindana kwa kasi kubwa kawaumiza watu wengine na kuonyesha ukatili kwa binadamu wenzao.

Kama mtu mmoja analinda kazi yake kwa kuumiza wengine ili azidishiwe madaraka na familia yake ishibe itakuaje siku wote wakiona huo ndio mfumo bora wa kulinda maslahi.

Wakati wa mampeni lakini ni wazi Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi kama sio wote wameonekana kuwa wameshindwa kusimamia uchaguzi.
Kodi za watanzania wote zinatumika kuwaumiza wao wenyewe kwa manufaa na ubinafsi wa wachache.
 
Kama Magufuli akiwa hana dola alitumia UBABE kuhakikisha anapita bila kupingwa kwenye ubunge kwa miaka 20, vipi kuhusu URAIS

TIME WILL TELL huyu MTU hatoki ikulu hata muda wake ukiisha. Ndio maana anahangaika na wabunge wake ili ateleze kilaini kwenye chaguzi zake
Habari za jioni? Poleni na mihangaiko ya kazi.

Hivi mbona mkuu wa jeshi la polisi anashushiwa heshima kiasi hiki?

Leo tumesikia hukoTarime, mkuu wa mkoa akisema polisi wakimruhusu Zitto ahutubie, basi atafukuza kazi wote waliokuwa huko.

Hivi mamlaka ya kipolisi siku hizi inaendeshwa kwa matamko?

Hii hali isipokemewa, tutakuja pata matatizo mbeleni.

Maana alianza Kangi kumpa maagizo as if ni mtoto wake, leo huko tarime mtu anajifanya Mungu mtu, hii katiba iliyopo sijui imekuwaje mpaka sasa haijarrkebishwa.

Na kwa style hii 2020 naona damu ikimwagika katika nchi hii, maana udiwani tu watu wanatishwa hivi, je urais itakuwaje?
 
Huyohuyo Malima anaewaagiza polisi ndiob huyohuyo alitolewa SMG wakati amepack gari vibaya,akawa anawaambia nipige....nipige akalala na viatu lkn leo kasahau.
 
Habari za jioni? Poleni na mihangaiko ya kazi.

Hivi mbona mkuu wa jeshi la polisi anashushiwa heshima kiasi hiki?

Leo tumesikia hukoTarime, mkuu wa mkoa akisema polisi wakimruhusu Zitto ahutubie, basi atafukuza kazi wote waliokuwa huko.

Hivi mamlaka ya kipolisi siku hizi inaendeshwa kwa matamko?

Hii hali isipokemewa, tutakuja pata matatizo mbeleni.

Maana alianza Kangi kumpa maagizo as if ni mtoto wake, leo huko tarime mtu anajifanya Mungu mtu, hii katiba iliyopo sijui imekuwaje mpaka sasa haijarrkebishwa.

Na kwa style hii 2020 naona damu ikimwagika katika nchi hii, maana udiwani tu watu wanatishwa hivi, je urais itakuwaje?
Huko kumwaga damu imekuwa wimbo kila kukicha,si muimwage tuone. RC anatamka akiwa ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake na siyo kwamba anamdhalilisha IGP
 
Habari za jioni? Poleni na mihangaiko ya kazi.

Hivi mbona mkuu wa jeshi la polisi anashushiwa heshima kiasi hiki?

Leo tumesikia hukoTarime, mkuu wa mkoa akisema polisi wakimruhusu Zitto ahutubie, basi atafukuza kazi wote waliokuwa huko.

Hivi mamlaka ya kipolisi siku hizi inaendeshwa kwa matamko?

Hii hali isipokemewa, tutakuja pata matatizo mbeleni.

Maana alianza Kangi kumpa maagizo as if ni mtoto wake, leo huko tarime mtu anajifanya Mungu mtu, hii katiba iliyopo sijui imekuwaje mpaka sasa haijarrkebishwa.

Na kwa style hii 2020 naona damu ikimwagika katika nchi hii, maana udiwani tu watu wanatishwa hivi, je urais itakuwaje?
Police sasa kazi yao imebaki kupigana na wapinzani tu ....... hawana lingine la kunya zaidi ya hilo!!

Hata Jamvi la Habari linawashinda kwa upelelezi ............ Linajua aliyetaka kumuua Lissu wakati Police wameshindwa!!
 
Hakuna sababu kisheria ya kufukuza kazi polisi kwa ishu hiyo hats kama yeye in mwenyekiti wa kamati ya ulinzi.
Sheria haimpi hayo mamlaka,
 
Back
Top Bottom