IGP kupinga agizo la Rais, kumfokea na kumkejeli Rais -- hii ni sawa?

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,902
95,409
Kwenye hii video fupi sana hapa chini Rais Samia anaonekana kutoridhishwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini na kutoa maagizo kadhaa kwa IGP.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa Rais kwenda kwa IGP ni pamoja na IGP kuhakikisha kuwa anazuia vifo vya mahabusu, kuzuia matumizi ya nguvu kupindukia kwa raia na kadhalika.

Lakini kama video hii inavyoonekana, IGP aliibuka baadae kupinga maagizo yale, kuyabeza, kumfokea Rais na kumkejeli.

Haya yote yanaibua maswali muhimu sana kwa watanzania. Je,Taifa lina Rais mwenye mamlaka? Kuna watu nchini wameamua kuwa Marais? Rais tulienae ni Rais dhaifu sana? Kuna kundi Serikalini linampinga Rais?Kwa nini Rais hafukuzi hawa wateule wake wanaomdharau?Ni nini hatima ya Taifa hili kama mambo yataendelea kuwa hivi?

Lakini pia katika mazishi ya Polisi waliouawa na Bwana Hamza tulimsikia IGP akitoa kauli za ajabu, zenye utata mwingi,zisizo za kisheria, za kugandamiza na kadhalika.

IGP alisikika akilaumu ndugu wa marehemu kana kwamba ndugu hawa walishirikiana na Bwana Hamza katika kufanya uhalifu ule. Lakini pia IGP alisikika akiwaambia wananchi kuwa wakizubaa zubaa watakuwa wanachezea risasi za Polisi na kadhalika.

My take:
Haya yote yanathibitisha kuwa Taifa lipo chini ya mgogoro mkubwa wa viongozi wasio na uwezo wala hekima za kuongoza na muda wowote ule kuanzia sasa hivi Taifa litatumbukia katika migogoro ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa maoni yangu haya ni matokeo ya kuongozwa na chama kilichopora chaguzi na ambacho hakina kibali cha wananchi kwani kupora chaguzi husababisha watu wenye uwezo wa kuongoza kuwekwa kando katika kuliongoza Taifa.

 
Watz bhana... IGP alikuwa anawaambia wananchi kuwa mara zote huwasema polisi.
 
Back
Top Bottom