IGP kupandishwa vyeo askari kuendane na utaratibu wa zamani wa sasa unakwaza

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Hivi sasa wameonekana askari wenye elimu kama Diploma na degree kwenda kusomea cheo wengine wa zamani walio kaa sana wana miaka zaidi ya 8 hawajawahi pandishwa cheo wakiwa wanakidhi vigezo vyote na ni watiifu wamebaki, vijana walio ingia kabla yao na ambao hawana vigezo vya muda wa kukaa kazini wameanza kupelekwa kwenda kusomea vyeo.

Swala hili limeonekana kuwakwaza askari baadhi na wamekaa kimya, fikiria swala hili rudisha mfumo wa zamani kwamba yazingatiwe miaka ya kuwepo kazini kupandishwa vyeo nidhamu na kadhalika. hao wanao pelekwa kwenye vyeo wengine hata kazi za CRO hawazijui, wanakua hawajui kufungua file aibu maana hawajui aina ya kesi inayotakiwa kufunguliwa na hawajui maswala ya ma faili.

Nipendekeze tu kuwa utaratibu wa zamani wa watu kupitia CRO na kupata uzoefu ni muhimu sana, wenye uzoefu mkubwa na walio kaa sana bila kupandishwa vyeo wakiwa wamekidhi vigezo iwe priority ya kwanza, kwa sasa wapo walio kata tamaa ya kupandishwa vyeo namba zikiwa ni kubwa, waone na uwatimizie ahadi ya mkataba kama barua ya ajira katika jeshi la polisi inavyoeleza.
 
Itakua ana mtoto wake wa juzi kaamua kumpandsha kwa mgongo wa wengi
 
Mkuu uende uongeze shule kabla ya kuomba kuongezewa cheo, hao unaowasema kuwa wamekaa mda mfupi kazini na wao wamesota sana huko shule na pia wengi wao wamekaa jkt miaka mingi kabla ya kupata nafasi ya kuja hapo polisi.
 
Nyie maaskali na ndugu zenu walimu kwa kinachoendelea Ni bora tu kaeni kimya kabisa.

Nyie ndio mmetufikisha hapa, mnacholalamika Ni Nini sasa?

Si mtulie ili dawa iwaingie vizuri.

Au mlijua hii mitano ya Moto itakua ya wapinzani peke yao?

NA BADO minne, Na ndo kwanzaa picha limeanza.

TUTAHESHIMIANA TU
 
Tatizo hao ambao hawataki kujiendeleza wanatumia vyeti vya ndugu na kazi wanafanya kwa mazoea na kukalili ikija changamoto nje ya kukalili hawawezi kuitatua na ndo wagumu kuelekeza wenzao Ili wasijue vitu vya kawaida, Kama huamini angalia vyeti vyao vya form na six jinsi walivyofaulu ujiulize kwanini hawataki kujiendeleza? Ndo hivyo wenye vyeti vyao wamejiendeleza navyo.
 
TPDF Haina kulilia cheo huko ..
Mwendo chibubu!!! Muda ukifika 6yrs ata kama una Elimu!!!.

Oder inakutema nenda kaumie Ulud Na Cheo!!

Hakuna figisu!!! Labda uwe juniour sana!!!! Lakin cheo kinakuja kwa jasho la damu
 
Shule ni muhimu sana pamoja na taratibu zingine za upandishaji vyeo kama vile kwenda kozi mbalimbali fupi na ndefu za weledi nk
 
Tuwe wavumilivu, Vyeo kwa sasa havipandishwi ovyo tuna kazi za Kitaifa za kujenga SGR
 
Back
Top Bottom