Ifunda Tech yafungwa kwa muda usiojulikana

Ifunda Tech yafungwa kwa muda usiojulikana

Malolella

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
366
Reaction score
114
Hii imetokea leo Shule ya Sekondari Ifuunda Tech iliyoko mkoani Iringa majira ya saa nane mchana baada ya wanafunzi kuvunja baadhi ya samani za shule ikiwemo vioo na kuiba kengele na kuificha kusikojulikana.

Chanzo cha fujo hizo inasemekana ni walimu kuwachapa viboko zaidi ya 15 kwa wanafunzi waliochelewa kufika parade. Inasemekana maji yalikatika hivyo wanafunzi kulazimika kufuata maji mbali kidogo na shuleni hivyo kuwafanya wachelewe parade.

Hiyo ndio sababu kuu iliyowafanya waibe kengele na kufanya uharibifu na uongozi wa shule kwa kushirikiana na afisa elimu kuifunga shule hiyo na wanafunzi walipewa nusu saa wawe wameondoka eneo la shule vinginevyo polisi waliokuwa wamesheheni silaha na gari za washawasha wangewashugulikia.
 
Kufuata maji mbali kidogo na shule? Mimi nimesoma Ifunda tech nilipokuwa 4m 5. Ni kwel kuna changamoto ya maji lakini huwa yanatoka asubuh then mchana yanazingua. Vyanzo vingine vya maji haviko mbali na shule hata kidogo. Hao watakuwa na sababu nyingine. Kikubwa kinachoisumbua shule ni kupinga utawala wa shule. Wakati naingia 4m 6 uongozi wa serikal ya walimu ulisambaratishwa wote. Kutakuwa na changamoto nyingne juu ya hao vijana sio hio inayotajwa.
 
Wafunge mpaka siku ya mtihani wa mwisho ndiyo waje shule pumbavu zao bangi zao wasituharibie shule yetu.

Unaporomoka hivo hivi unajua Ifunda ya sasa inakabiliwa na uovu gani uliokithiri kiasi cha hayo yote kutokea? Fikiri upya alafu jutia kauli yako
 
Jamani hivi Ifunda Technical School kuna form six siku hizi??. Nimemaliza hapo form mwaka 1986. Ni kweli kulikuwa na changamoto za maji kwa kiasi fulani. Yakikatika tulikuwa tunaoga katika mto LYANDEMBELA.
 
sitausahau mgomo wa tosamaganga 2011 tulipigika sana
 
Jamani hivi Ifunda Technical School kuna form six siku hizi??. Nimemaliza hapo form mwaka 1986. Ni kweli kulikuwa na changamoto za maji kwa kiasi fulani. Yakikatika tulikuwa tunaoga katika mto LYANDEMBELA.

Ifunda Tech siku hizi ina form one mpaka form six. Wanafunzi wa Ifunda Tech ni watundu mno hasa form four. Kuna binti anasoma Ifunda Girls High School ambayo inapakana na Ifunda Tech anasema wanafunzi wa Ifunda Tech huwa wanaruka fensi ya ifunda girls na kuwaibia vifaa vyao mbali mbali. Na wameshazoea kuibiwa hasa mabweni yaliyopo karibu na fensi hiyo
 
Unaporomoka hivo hivi unajua Ifunda ya sasa inakabiliwa na uovu gani uliokithiri kiasi cha hayo yote kutokea? Fikiri upya alafu jutia kauli yako
Sema sasa shida n nn!? Ukiacha viulizo husaidii mtu
 
dah nilisoma ifunda olevel pale vurugu sana tu hadi nilitamani miaka minne iishe tu, pale shida ya maji ipo but sio sanaa mara nyingi ni wakati wa kiangazi but maji yakikosekana wanafunzi huenda kuchota ifunda girls ambapo ni karibu tu so sio tatizo la umbali, sema iyo shule migogoro tu watakuwa na sababu zao zingine, mwaka jana academic office iliungua na vyeti vyote vya wanafunzi waliomaliza miaka ya nyuma viliungua ikiwemo na changu sasa sijui waliunguza wanafunzi ama nini maana chanzo cha moto hata hakikujulikana...
 
Hata hivyo hapo wanachapa sana, shemeji yangu alimaliza advance mwaka jana aliwahi kuchapwa fimbo zaidi ya 16 tena ni wakike. Serikali iangalie vzr ila ni kweli wanachapa sana na malalamiko yanatolewa ila hayafanyiwi kazi.
 
Hata hivyo hapo wanachapa sana, shemeji yangu alimaliza advance mwaka jana aliwahi kuchapwa fimbo zaidi ya 16 tena ni wakike. Serikali iangalie vzr ila ni kweli wanachapa sana na malalamiko yanatolewa ila hayafanyiwi kazi.

yeah kuchapwa sana tu nakumbuka kulikuwa na ticha wa mazingira ye watu wakimuona anakuja kalass kila mtu mbio, sasa nyie atakao wakuta class ndo mtabeba mzigo wa waliokimbia, utasikia anawaambia kwahiyo nyie ambao hamjakimbia ndo hamuniogopi baada ya hapo fimbo kwenda mbele, sie wengine wapole pale tulipata shida aisee
 
Polen xana ifunda mara vitabu vimeungua, mmetafta kwa shda mwaharibu wenyw, ni sheeeeda! I thank God hapo iringa girls ni raha tupu, adabu kwa wanafunz na walmu, mkipata shida mnashirikiana kutatua igen hapo bas hzo vurugu mwajiharibia wnyw, hayo ni maisha yenu co walm! By 4m six leaver iringa girls 2014!
 
Back
Top Bottom