Ifikie mahali African Union (AU) isimame na kutoa matamko dhidi ya mataifa makubwa na Jumuia zao kama wao wanavyofanya dhidi ya mataifa ya Afrika

chagonjam

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
354
418
Nimetafakari kwa kina Juu ya mustakbali na kazi za African Union (AU) katika mashirikiano yao kama wanavyojiita ila binafsi nimebaini, bado muungano huo hauna tija ya maana miongoni mwa mataifa yanayounda muungano huo.

African Union (AU) wanapaswa kukaa pamoja kuangalia upya maana halisi ya muungano nini, wanaunganishwa na nini, faida za hayo watakayo unganishwa nayo ni nini kwa kila mmoja,mikutano yao katika namna ya dharura kujibu matamko nyeti itakuaje.

Mimi nijuavyo muuungano kujibizana na muungano inaleta tija kuliko nchi fulani kujibizana na muungano, hasa majibizano ya kutokukubaliana. Nimesema hili kutokana na wenzetu wenye mataifa makubwa kutumia miungano yao kuchapia nchi za afrika hali ya kuwa muungano wa afrika uko kwa ajili ya kushauriana baina ya viongozi na si kujibu hoja za miungano mingine inayowachapa kila kukicha.

Nimeshwashika kusema hili hasa kutokana na asilimia zaidi 95% ya nchi za afrika kukataa ushoga kimoyo moyo hali ya kuwa asilimia zaidi ya 95% ya nchi za ulaya kuhalalisha ushoga katika, aidha nchi za ulaya zinatumia muungano wao (EU) kulazimisha nchi za afrika kukubali ushoga kutokana na wao kukubaliana katika hilo. Ila kwa nchi za afrika inakuwa kinyume kutokana na kushindwa kutumia umoja wao (AU) kuonyesha kutokukubaliana na (EU) katika hilo.

Endapo EU ingesema ushoga ni halali naamini tija ingepatikana tuu endapo AU ingesema ushoga si halali, wanachofanya wenzetu ni kushikamana na kisha kutukaba mmoja mmoja. Na hata mnapokataa wanawatengenezea karatasi la kusaini mmoja mmoja, nadhani ikifika mahali AU ikaanza kutoa matamko ya kujibu miungano sambamba na kuwekeana taratibu za kuwa na msimamo mmoja ambao itamlazimu kila mwanachama kuuheshimu naamini muungano wa AU ungekuwa na tija kubwa kwa africa.

African stand up! You should know and use the power of AU!

Dawa ya kumtibu EU ni AU na dawa ya kumtibu AU ni EU but EU dhidi ya nchi ni rahisi kwa EU kushinda na vilevile AU dhidi ya nchi ni rahisi kwa AU kushinda. To try your power against country simply stand as AU and say we don’t want England commodities in Africa you will see power of you!


Mungu Ibariki Africa.
 
African Union nao ni vibaraka tu, wa hao hao unaotaka wakemewe. Ni sawa na MTOTO kumfokea BABA.

Halafu msitusahaulishe, tunasubiri mtoe tamko lenu kama "mtatimiza au mtafanya jeuri" juu ya WITO waliotoa EU na USA.

Tujikumbushe maombi yao yalikua;

● Bashite na wahusika wengine wafikishwe mbele ya mikono ya sheri.

● Sheria za mitandao, habari, uchambuzi wa statistics zibadilishwe.

● Wafungwa wote gerezani wa KISIASA waachiwe huru mara moja.

● Upelelezi binafsi ufanyike dhidi ya matukio yote yaliofanyika (Wanahabari kupotea, Wanasiasa kupotea, Majaribio ya kuuliwa wanasiasa, Waandishi wa habari kukamatwa, Raia kupotea na kutekwa) kisha wahusika nao wafikishwe mbele ya mikono ya sheria.

***Swala la ushoga hatutaki hata kulisikia, hio laana hatuitaki kabisa***

NB Ili tujue mapema, kama ndio raia tuanze kutafuta machimbo ya nchi jirani, kabla hao jamaa hawajatuma DRONES zao kujakui DECORATE magogoni. Sisi wengine hatupendi vita/machafuko/ugomvi/vikwazo/shida/chuki. Tunapenda AMANI na HAKI itawale milele daima nchini Tanzania.
 
Una maanisha hii AU ambayo moja wapo ya wanachama wake Niger hana chakula cha kutosheleza raia wake? Makao makuj yao paleAdis yamejengwa na China...Au kuna AU ingine unaiongelea?
 
Umejaribu kulinganisha vitu viwili tofauti kabisa. Huwezi kamwe kuilinganisha Africa Union(AU) dhidi ya European Union(EU). Huwezi kuwalinganisha watu wenye akili za mtindio na Werevu..

African Union ni genge la madikteta, maskini na vibaraka watupu. Hawawezi kujisimamia, kuzimamia nchi za Afrika na hawana mwelekeo. Wapo pale kupotezeana muda tu.

Kwa sasa kila nchi ya kiafrika ipambane na hali yake tu.
 
Back
Top Bottom