Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,470
- 38,207
Pamoja na kukipamba sana bado hakistahili kubebwa na Boeing 787 Dreamliner. Dreamliner ilipaswa ibebe kitu unique na kikubwa kwa sababu ni ndege ya masafa marefu. Rubondo ingekuwa kwenye Bombardier ingekuwa sawa kabisa.
Watanzania bado tuna tatizo kwenye branding and promotion. Ninachikiona ni kufanya matangazo ya kumridhisha Rais kwa vile anatoka kanda hiyo.
Hakuna mtalii atakayetoka India au Guangzhou kwa ajili ya kwenda Rubondo kuja kuviona hivyo vitu ulivyo vitaja mtoa mada.
Tuendelee kupaza sauti ya kuitangaza Kilimanjaro, Ngorongoro na Serengeti. Ni kweli Kilimanjaro nalo limeandikwa, ila badala ya Rubondo basi tungeendelea kuandika vilele vya Mawenzi au Kibo.
Ushauri; ATCL ihusishe Wizara ya Utalii au taasisi zilizo chini yake kama TTB au TANAPA kwenye branding.
Mkuu umenifilisi maneno .Ni ajabu sana kuacha mbuga za maana na zenye majina makubwa kama Ruaha,Mkomazi ambako wapo Faru wengi kuliko mbuga zote Tanzania,Ngorongoro,Katavi,Tarangire..... eti Rubondo ambayo inatembelewa na Wageni wachache na ni mbuga ndogo hata 2% ya wageni hawafiki.