SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Ndege yetu mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakayowasili mchana wa leo imepewa jina la kisiwa cha Rubondo 'Rubondo Island'. Hii ni ndege ya nane mpya katika ya 11 zilizonunuliwa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe MAGUFULI kwa lengo la kuimarisha shirika letu na ndege (ATCL).
Nimeona nikufahamishe kidogo juu ya kisiwa hiki kilichopewa hadhi ya hifadhi ya Taifa. Moja ya faida ya kumiliki shirika imara la ndege ni pamoja na kuutangaza utalii wetu ili watalii wengi zaidi waje nchini. Kuzipa ndege majina ya vivutio vyenu vya utalii ni njia moja wapo ya kuutangaza utalii wenu.
Sasa fahamu machache juu ya kisiwa hiki cha Rubondo:-
1. Kisiwa hiki waliishi wakazi waliojulikana kama Banyarubondo hadi kati ya mwaka 1964-1965 serikali ilipolazimika kuwaondoa kwa kuwalipa fidia na kisiwa hiki kutangazwa pori la akiba mnamo mwaka 1966 na baadae kupandishwa daraja kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 1977. Kisiwa cha Rubondo kipo kusini magharibi mwa ziwa Victoria.
2. Kisiwa cha hifadhi ya Taifa Rubondo kina ukubwa wa kilomita za mraba 457 ambazo kati yake 237 ni nchi kavu na 220 ni maji. Hifadhi hii ipo jirani na visiwa 11 vya makazi ambavyo ni Mizo, Nyamitundu, Chitende, Katera, Iroba, Chambuzi, Munyila, Makosi na Izilambula.
3. Kisiwa cha hifadhi ya Taifa Rubondo ndio pekee hapa nchini na Afrika vinavyopatikana katika makazi ya maji ya ziwa.
4. Rubondo ina wanyama wa asili na waliopandikizwa. Mnyama wa asili ni nzohe ambaye anapatikana katika hifadhi hii pekee. Wapo vile vile tembo, sokwe mtu, pongo, mamba, viboko, fisi maji, ngedere, kenge, ndezi, vicheche, nguchiro, ndege aina 400, samaki aina 13, misitu minene mikubwa ya asili ya Kongo, fukwe zilizojaa rasilimali za uoto wa asili wenye harufu nzuri ya kipekee na eneo zuri la kulala watalii.
wafanyakazi wengi wa migodi mikubwa na viwanda vikubwa kanda ya ziwa, raia wa kigeni wanaokuja kufanya tafiti pia hupendelea kwenda kupumzika katika kisiwa hiki kwani kinavutia na kinautulivu wa hali ya juu. Panga kukitembelea.
#TanzaniaUnforgettable
#MabadilikoBora #MabadilikoYaKweli #MabadilikoTuliyoyataka #ChaguaCCMKaziIendelee