Ifahamu dhambi ya mtu mmoja ilivyoiangamiza familia nzima

Yaani agizo la kuangamiza kila kitu hata binadamu wenzako, ila vito vya thamani uvihifadhi? Huu ni uongo wa bible, Mungu hana ubaguzi. Munguni wa upendo na wa haki
 
Mji wa kwanza kutekwa na Waisraeli baada ya kuuvuka mto Yordani ulikuwa Yeriko.
Na Mungu aliwaagiza kuwa kila watakapouvamia mji wa Kaanani ni sharti waangamize vyote watakavyovikuta kwenye miji isipokuwa vito vya thamani ambavyo sharti ilibidi viwekwe kwenye hema ya kukutania.


Kwa kutii agizo hili mji wa Yeriko ulianguka na Waisraeli kushinda kirahisi.


Mji uliofuata kuvamia ulikuwa ni mji mdogo wa Ai.

Yoshua akiamini kuwa atashinda kirahisi alituma jeshi dogo la Waisraeli 2000 ambao waliishia kutwangwa na kupepetwa na Waisraeli 36 kufariki hapohapo.
Ilipopitishwa sensa ya kubaini chanzo cha kushindwa vita,ikaonekana kuwa kuna mtu aliiba vito mjini Yeriko.Mtu huyo alikuwa Akani,ambaye ilibidi auwawe yeye na familia yake.

TUNAJIFUNZA NINI?
Kuna mikosi,laana,na shida ambavyo vinatukabili leo kutokana na dhambi za ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hivyo tujifunze kumuuliza roho mtakatifu kila tunaposhindwa kufanikiwa ili tujue kama chanzo ni siye,Mungu,Shetani au ndugu zetu

REFFERENCES
YOSHUA 7
Ndio maana Mh Rais anapambaana na aina hii ya Laana..
 
umande

Ukute hujawahi soma kitabu hata kimoja cha Agano la Kale.

Ebu funua Yoshua 6 uisome mpaka saba kisha urudi hapa.
 
Mmh! Hapo sasa ni suala la imani sio tena kutaka kujua ukweli au uwongo Wa kitu.
Ndiyo maana nimetangulia kwa kusema "if u believe" kama unaamini imani nyingine sawa ijaribu kama itakusaidia well & good.
 
Mkuu na hapa je Ezekiel 18:18-20

18 Kwa habari za yule baba yake, kwa sababu aliwaonea watu kwa ukali mwingi, na kumnyang?anya ndugu yake mali yake kwa nguvu; na kuyatenda yasiyo mema kati ya watu wake, tazama, atakufa katika uovu wake.
19 Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi.
20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.
22 Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi

Wagalatia 6:5


5 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.

Hapo je
 
Na hapa mkuu je Yeremia 31:29-32

Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.
30 Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi.
 
Back
Top Bottom