Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Ninakiri kwamba nimekutana na uzi wa mwana-JF, “King Mufasa” leo ukihoji uaminifu walio nao mapadri wa Kanisa Katoliki,mintarafu utunzaji wa siri za mambo yanayojiri wakati sakramenti ya Upatanisho.

Kimsingi ukisoma katikati ya mistari ya mtoa uzi, utagundua kwamba mtoa mada ni Mkatoliki bandia, ndio kusema ni mprotestanti lakini kwa kuwa bila kujua yeye ameamua kutoa nafasi ya wakatoliki kuonyesha kwamba huwa hawafanyi mambo kwa kurupuka,nimeamua kujibu hoja yake “kwa nini maungamo yanafanyika kwa Padri” kwa uzi kamili.

Awali ya yote naomba kutoa tafsiri ya maneno makuu ambayo nimeyatumia katika Kichwa cha mada hii: Mosi,Mpinga Kristo ni mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapingana na sehemu au mafundisho yote ya Yesu Kristu na ya Mitume ambao ndio Yesu aliwakabudhi mamlaka ya kuliendesha Kanisa.Pili, Na Mtu anayesoma mambo kwa kuruka ruka ni yule ambaye anavamia machapisho na kuanza kuyasoma bila kufuata misingi na kanuni za usomaji na uchakataji maudhui husika.

Ni hivi, suala la kuungama watu dhambi kwa Padri lina teolojia yake kutoka katika kisa cha kutano la Zakayo na Yesu kule Yeriko.Katika kutano hilo,kuna mambo mengi sana ambayo Kanisa Katoliki tunachota na mojawapo ni hilo la kuungama dhambi kwa Mungu, tena kwa sauti, kupitia mwakilishi wa Yesu,ambaye ni Padri.Tunasoma hivi:

“1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. 2 Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. 3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. 4 Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. 5 Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” 6 Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” 8 Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” 9 Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu. 10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” 11 Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, ufalme wa Mungu ungefika.”

Kwa mjibu wa nukuu hiyo, ni kwamba tunatafakarishwa kuungama dhambi na kurudisha mali zote ambazo tunakuwa tumezipata kwa njia ovu kama ambavyo Zakayo alikuwa amejipatia kwa njia zisizo halali.

Katika muktadha huo wa Kisa cha Zakayo na Yesu tunaangaziwa mambo matatu:

  • kuumia au kujutia dhambi tunazozitenda
  • kuungama dhambi mbele ya Yesu Kristu
  • kufanya malipizi ya dhambi zetu.
Mwandishi Luka katika kisa hiki hatuonyeshi Zakayo aliungama dhambi zake kimoyokimoyo bali kwa sauti tena mbele ya Yesu na wala Yesu hasikiki kumkemea Zakayo kwa kitendo chake hicho cha kutaja dhambi zote alizopata kuzitenda kwa sauti na wala Yesu hasikiki kumkataza Zakayo aache kurejesha vile alivyokwisha kujipatia kwa njia ya udanganyifu. Kumbe ni kutokana na muktadha huo, Kanisa Katoliki pamoja na mambo mengine liliamua kuendeleza utaratibu huo wa kuungama dhambi kwa sakramenti ya Upatanisho.

Baadhi ya Wakristu wakatoliki hawaipendi hii Sakramenti kwa sababu ya kulishwa sumu na waumini wa madhehebu ya kiprotestanti kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuwafanya mapadri kama Mungu, wa kwenda kuelezwa dhambi. Tena katika mstari huo huo, wanahoji kwa nini kama mtu unaona unahitaji kutubu dhambi zako usifanye hivyo moja kwa moja kwa Yesu mwenyewe kwa sababu kwa madai yao, yeye ndiye mpatanishi wetu kati ya Mungu na wanadamu? Kumbe, suala linalowasumbua sio kuungama dhambi,bali kile kitendo cha kujinyenyesha mbele ya Padri na kumueleza dhambi zako.

Kumbe, waprotestanti hao hao wanashindwa kufahamu fundisho lililolala katika kisa hiki cha Zakayo. Wakosoaji kama hao ”Wanapotea maboya” kwa kutokuelewa kwamba ingali Yesu angetaka kufundisha kwamba dhambi ziungamwe kwa Mungu kimyakimya, basi angalifanya hivyo kwa Zakayo kama ambavyo alisahihisha mambo mengine, ambayo yalikuwa na hitilafu katika jamii ya Kiyahudi.Kumbe,badala yake anaweka msisitizo katika fundisho ambalo lilikuwepo hata wakati wa Agano la Kale kama tunavyosoma Kutoka 22:1-17,Mambo ya Walawi 6:1-7 na Hesabu 5:1-10.

HOJA YA KIMANTIKI INAYOUNGA MKONO KUUNGAMA DHAMBI KWA PADRI

Kabla hatujaanza kuzama sana katika maandiko matakatifu katika kujibu hoja hiyo, naomba nami nitumie hoja ya kimantiki tu katika kuijibu hoja hiyo ya kiprotestanti.Hoja hiyo inajengwa na maswali yafuatayo:

  • Je, kuna mahali popote katika mafundisho yake Yesu Kristu alizuiwa watu kuungama dhambi zao mbele ya binadamu wenzao?
  • Hivi katika maisha yetu ya kawaida hata katika familia au jumuia zetu, inakuwaje pale unapomkosea mwenzako na ukahitaji usamehewe?
  • Je, huwa hatuwaelezi tuliowakosea hatua kwa hatua makosa yetu kabla kuwaomba msamaha?
  • Au vile vile, pale tunapotaka tupitie kwa marafiki au ndugu zetu ili watuombee msamaha kwa tuliowakosea, je hao tunaokuwa tumewakusudia watuombee msamaha wao huwa hawatuhitaji kwanza tuwaeleze jinsi tulivyowakosea wahusika?
KUMBE, haya mambo ya kuelezana jinsi tulivyokosa sio mambo mageni kabisa katika jamii zetu.Ni mambo tumeyazoea sana kiasi kwamba:

  • Mume na mke wanafanya;
  • mtu na ndugu zake wanafanya, hivyo hivyo.
  • Makazini ndiyo usiseme, mpaka wakati mwingine tunaambiwa tuandike barua za kujieleza ili kupima kama kosa lenyewe linahitaji msamaha au kufukuzwa kazi.
MASWALI MENGINE YA KIMANTIKI NI HAYA:

  • Inakuwaje kufichua dhambi zetu kwa wanadamu wenzetu lionekane jambo la kawaida ila inapokuja katika muktadha wa imani, ndio watu wengine wang’ake?
  • Kama tunaona ni jambo jema kuungamiana mke na mume makosa; ndugu na ndugu,rafiki na rafiki,kwa nini tupate soni na aibu kuungama mbele ya Mungu,muumba wetu?

HISTORIA YA MAUNGAMO YA DHAMBI KATIKA AGANO LA KALE

Kitabu cha Mambo ya Walawi 19:1-22, tunaelezwa na mwandishi jinsi ambavyo Musa alikuwa anaeleza aina ya dhambi ambazo wana wa Israel hawakupaswa kuzitenda na iwapo ingetokea wakakosa basi, alitoa utaratibu jinsi ambavyo dhambi za mtu huyo zingeondolewa:

“20 Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru. 21 Mwanamume huyo ataleta mbele ya hema la mkutano sadaka yake ya kondoo dume ya kuondoa hatia na kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. 22 Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.”

Kumbe, MUSA katika Agano la Kale, alikuwa amewaagiza wana wa Israel kwamba wanapomkosea Mungu, Kuhani ndiye anachukua nafasi ya upatanishi kati ya Mungu na mhusika baada ya mtenda dhambi husika kuwa amewasilisha mbele ya hema ya Mkutano, kondoo dume kwa ajili ya upatanisho.Lakini najua unaweza kujiuliza kuwa mbona Musa hakuelekeza kwamba mtu huyo anapowasilisha kondoo huyo kwa ajili ya kuondolewa dhambi,basi ni lazima pia aseme dhambi zake kwa kuhani huyo?Jibu la swali kama hilo ninalo na nakupatia sasa hivi.Ni kwamba katika mantiki ya kawaida haingwezekana Kuhani akawa akiona tu kondoo dume mlangoni, basi yeye anafanya kazi ya kumuombea huyo mtu mdhambi kwa Mungu, ili ziondolewe bila kuhafahamu ni dhambi zipi hizo zinaombewa msamaha. Basi, tunasoma hivi katika kitabu hicho cha Kutoka 5:1-6:

“1 Kama mtu yeyote akitakiwa kutoa ushahidi kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kulisikia naye akakataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atauwajibikia. 2 Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia. 3 Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia. 4 Au, kama mtu akiapa kufanya chochote kile, chema au kibaya, kama wafanyavyo watu bila kufikiri, atakapojua atakuwa na hatia. 5 Basi, mtu akiwa na hatia kuhusu mambo hayo lazima akiri dhambi yake aliyotenda 6 na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.”

Aya ya 5, katika nukuu hiyo hapo juu, inatoa sharti la mtu aliyekusudia kupatanishwa na Mungu kupitia Kuhani kuungama dhambi zake kwa Kuhani kwanza kabla ya kuombewa msamaha.

Mpaka hapo sasa nadhani tumeelewana.Au bado unataka kuniuliza swali kwamba hata kama wakati wa Agano wa Kale Kuhani ndiyo alikuwa anaelezwa dhambi za mtu kuna haja gani ya kufanya hivyo wakati huu wa Agano Jipya kwa sababu Yesu kristu alikwishakufa msalabani kwa ajili hiyo? Ndio kusema, Yesu ndiye Kuhani Mkuu. Kama hiyo, ndio hoja basi, fuatana nami kwa taratibu sana.

NJIA ZA KUONDOA DHAMBI ZA MWANADAMU
Ni kweli kwamba msamaha wa dhambi kwa mwanadamu kimsingi unatokana na kazi ya Yesu msalabani.Lakini swali linakuja msamaha huo unapatikanaje kwa kila mmoja wetu?Je, Kristu alituachia njia yoyote ndani ya Kanisa ya kuondolea dhambi?

Kwa mjibu wa mafundisho ya Kanisa Katoliki, Yesu Kristu alituachia njia mbili:

1. Ubatizo kwa ajili ya kutuondolea dhambi ya asili (original sign) ambayo hurithiwa tokea kwa wazazi wetu wa kwanza,Adamu na Hawa, na zile ambazo tunazitenda kabla ya kupewa huo ubatizo.Dhambi tunazozitenda baada ya ubatizo zinaitwa dhambi halisi(Actual sin).Dhambi zote tuzitendazo baada ya kubatizwa zinaitwa dhambi halisi kwa sababu ndio dhambi ambazo zinatokana na matendo yetu wenyewe.

2. Kwa sababu ya asili ya udhaifu wa mwanadamu, basi hata baada ya ubatizo hujikuta anaendelea kumkosea Mungu.Kumbe ni katika mazingira kama hayo Yesu Kristu alituachia njia ya pili ya kutuondolea dhambi.Ukweli ni kwamba dhambi zinatutenganisha na Mungu na kwa dhambi hakuna anayeruhusiwa kukanyaga Mbinguni.Kumbe ukitafakari kwa undani kabisa kuhusu mpango wa Mungu kumfanya mwanadamu aingie Mbinguni akiwa hana dhambi, haukukomea katika mateso,kifo cha ufufuko wake Yesu Kristu bali ni jambo ambalo ni endelevu kwa wanadamu vizazi kwa vizazi.

Ni lazima kila mwanadamu aangukapo dhambini atubu na kuazimia kuachana na dhambi ili kuweza kuingia Mbinguni.Kumbe,ni kwa kutokana na kufahamu kwamba licha yeye Yesu kuturudishia mahusiano kati ya Mungu Baba na wanadamu ambayo yalifungua tena njia ya wanadamu kufika Mbinguni,lakini pia kwa kufahamu kuwa hata baada ya kutupatanisha na Mungu bado wanadamu tungaliendelea kuwa tukianguka dhambini,Yesu basi aliamua kutuwekea utaratibu wa kuondolewa dhambi zetu.

Basi,kumbe ukimakinika sana utagundua kuwa Mungu aligawanya mkakati wa kumuondolea mwanadamu dhambi katika vipindi vitatu:

  • Kabla ya yeye kufika duniani(ndio kile kipindi ambacho makuhani walikuwa wakifanya kazi ya upatanishi.
  • Wakati yeye akiwapo hapa duniani.
  • Baada ya kuondoka hapa duniani na kuwaachia Mitume na mahalifa wao kazi hiyo.Sasa hebu nifuatilie ili tukitalii kipindi hiki cha awamu ya tatu cha mwanadamu kuondolewa dhambi.
Yesu na ukasimishaji mamlaka ya kuwaondolea watu dhambi

Neno kukasimu katika Kamusi Kuu ya Kiswahili (ya BAKITA) ina maana ya kumuagiza,kumtuma mtu mwingine;kuhamishia mamlaka ya kufanya jambo fulani kwa niaba yako.Na katika kufanya hivyo,mtu huyo anayeagizwa au kutumwa akifanya lolote itahesabiwa wewe uliyemuagiza ndiwe umefanya.

Katika maisha yetu ya kila siku kwa namna moja au nyingine tunakasimu baadhi ya majukumu yetu.Tunakasimu sehemu ya wajibu wetu kwa baadhi ya wanafamilia,maofisi ya Serikali au sekta binafsi.

Ukasimishaji una malengo mawili tu: mosi, kuleta ufanisi hasa pale inapokuwa inatoa nafasi kwa kazi husika kuhamishiwa kwa watu wenye ujuzi ambao unaendana na kazi iliyokusudiwa kufanyika.Pili, kuleta maendeleo.

Katika kuleta ufanisi na maendeleo, ukasimishaji una hatua zipatazo kama sita hivi ambazo zinapaswa kufuatwa: mosi, maandalizi. Pili, uteuzi wa wakasimiwa.Tatu, kuthibitisha uelewa wa majukumu.Nne,kuthibitisha kama mhusika ameyakubali majukumu.Tano,kuepuka kubatilisha ukasimishaji.Sita, kusimamia utekelezaji.

Mambo hayo sita, wengi wetu ndio tunayafanya kila mara,iwe katika familia au maofisini kabla ya kufikia kusema mtu fulani akasimiwe majukumu kadhaa.Hali kadhalika, ndiyo mambo aliyazingatia Yesu Kristu kabla ya kuwakasimisha Mitume mamlaka ya kuwaondolea watu dhambi zao mara angeondoka duniani.

Mwinjili Yohana katika sura ya 20:9-23, anatupasha ukweli huo nilioueleza hapo awali kwamba Yesu baada ya kufufuka ndio aliona inafaa awakasimishe Mitume wajibu huo wa kuwaondolea watu dhambi:

“19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20 Alipokwisha sema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. 21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”

Kuna mambo matatu, Yohana anayaeleza ambayo yanaambatana na mamlaka haya ya kuondolea watu dhambi:

1. Kwamba Mungu Baba alikuwa amemuagiza Yesu Kristu kuja kuwaondolea wanadamu dhambi.Dhambi zinazoongelewa hapa ni zile zilizoondolewa kwa damu ya Yesu kumwagika msalabani na yeye akishakumaliza kazi hiyo anawatuma na Mitume wakafanye kazi hiyo ya kuondolea watu dhambi zinazotendwa baada ya damu yake kuwa imemwagika msalabani: “21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.”

2. Kwamba ili Mitume waweze kuifanya kazi hiyo ya kuondolea watu dhambi,Yesu anawapatia nguvu na uwezo wa kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi:” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu.” Kumbuka katika maandiko Matakatifu, mahali pengine pekee ambako Mungu anampulizia mwanadamu pumzi ya uhai (sawa na wakati huu wa kuwapeni mamlaka na nguvu ya kuondoa dhambi) ni wakati ule wa uumbaji mwanadamu.Tunasoma Mwa 2:7 hivi:
“ 7 Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa.

Kumbe, Yesu kwa kuwapulizia Mitume Roho Mtakatifu ni kama anafanya uumbaji mpya sawa na vile alivyofanya wakati ule wa uumbaji ulimwengu.Tendo hili linaashiria ni nini kwa Mitume? Wakati ule wa uumbaji, Mungu katika nafsi tatu alifanya uumbaji na hivi kumbe katika tendo hili la Mitume kuwaondolea watu dhambi anadhihirisha kwamba jukumu hilo analowapatia Mitume ni Mungu mwenyewe katika nafsi zake tatu anafanya kazi hiyo ya kuwaondolea watu dhambi na kwamba Mitume watakuwepo kwa niaba yake katika kuifanya kazi hiyo.Ndio kusema kwamba kazi ya kuwaondolea wanadamu dhambi kwa asili yake ni kazi yake yeye Mungu mwenyezi aliyewaumba wanadamu.

Mtakatifu Cyril wa Alexandria (376 – 444), anasema maneno “akawapulizia” yanaeleza kile ambacho wazazi wetu wa kwanza bustanini Edeni walichokipoteza mara baada ya kuruhusu nafsini mwao mawazo ya kutaka kuwa na hadhi ya Umungu (dhambi ya asili) na kwamba huyo Roho Mtakatifu wanayepewa Mitume ni kielelezo kwamba kwa huyo Roho Mtakatifu, wanadamu watakuwa na maisha sawa ya yale ya mwanzo, wangali Adamu na Hawa hawajatenda dhambi.(Rejea Mtandao wa Sapienta, Genesis 2:7 & the Meaning of 'Life' in Cyril of Alexandria's Theology | Henry Center)

Jambo la tatu katika ukasimishaji huo wa maondoleo ya dhambi ni masharti ya mtu katika kuondolewa dhambi.Sawa na Kisa za Zakayo kwamba ilibidi aeleze dhambi mbele ya Yesu, ndivyo Yesu anavyowaelekeza Mitume kwamba mtu atahesabiwa amesahemewa dhambi zake Mbinguni ikiwa ameweza kuzisema dhambi zake. Ni maneno “…msipowasamehe, hawasamehewi” ndiyo yanatoa picha kwamba mtu anayetaka kuondolewa dhambi zake, analazimika kuzieleza dhambi zake nje ya moyo.

MANTIKI YA WAKATOLIKI KUUNGAMA DHAMBI KWA PADRI

Kanisa Katoliki, linaazima maelekezo ya kuungama dhambi kwa Padri kutoka maneno ya Yesu mwenyewe. Yesu angalimaanisha mtu kuungama dhambi zake bila kuzieleza basi, kusingalikuwa na uwezekano wa kushindwa watu wengine kusamehewa dhambi zao. Kwa mantiki ya kawaida, huwezi kumkatalia mtu jambo au ombi ambalo hulijui ni nini? Mantiki Ya pili, ya kulazimika wadhambi kusema au kutaja dhambi zao mbele ya Mitume,ni kwa sababu Mitume kama binadamu hawakuwa uwezo wa kusoma mioyo ya waungamaji na kuona humo dhambi zao ili waweze kusamehewa.

Kumbe, kwa maneno “…msipowasamehe, hawasamehewi”, Yesu anawaelekeza Mitume kwamba baada ya kusikiliza dhambi za waungama, kuna mazingira dhambi husika zinaweza zisiondolewe na mara watakapofanya hivyo, basi Mungu naye anakuwa ameridhia maamuzi hayo.

HITIMISHO

Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba Mitume walipewa uwezo huo wa kuondolea watu dhambi na kwamba wakifanya hivyo au wasipofanya hivyo basi dhambi zinakuwa zimeondolewa au hazijaondolewa mtawalia.

Na kwa misingi hiyo, wale waprotestant wanaokubali kwamba Mitume walipewa uwezo huo ni lazima waonyeshe uwezo huo wa Mitume uliishia kwa Mitume tu au uliendelea?.Na ili kuondoa mashaka kabisa pale watakapojenga kwamba uwezo huo hauendelei hadi kwa mapadri tokea hapo, basi lazima waonyeshe na mambo mengine mawili au matatu ambayo waliagizwa Mitume pekee na hivi kwamba waliowarithi hawakustahili kuhusika na maagizo hayo.

Jambo hili la kuungama dhambi ni pana lakini itoshe tu kusema kwamba, tunaweza kunyumbulisha faida kama kumi na tisa hivi hivi(19) za kwa nini tunapaswa kuungama dhambi:

1. Mungu alituamuru tuungamiane dhambi zetu.

2. Ni njia nyepesi kuwezesha dhambi zetu kuondolewa kwa sababu ukiwa mbele ya padre utajua kama dhambi zako zimeondolewa au la tofauti na vile ambavyo ingefanyika kwa Mungu moja kwa moja(kuungama kimoyokimoyo).

3. Tunapokea Neema inayotusaidia kuzishinda dhambi kupitia Sakramenti ya Kitubio.

4. Tunajifunza kuwa wanyenyekevu kwa kuungama dhambi zetu kwa wenzetu kama ambavyo Zakayo alivyokuwa mnyenyekevu kwa kushuka mtini na kukubali kusema dhambi zake mbele ya Yesu.

5. Kuungama kunatujengea moyo wa kuwajibika.

6. Mahusiano yetu na Kanisa yanahuishwa au yanaponywa.

7. Kwa kuungama tunapokea na ushauri nasaha toka kwa Padri.

8. Tunaweza kupokea faraja kupitia maneno ya Ondoleo la dhambi.

9. Dhambi zetu zote pamoja na zile zinazokuwa zimesahaulika huondolewa.

10. Kitubio kinatusaidia nguvu ya kuwasamehe na wenzetu wanaokuwa wametukosea.

11. Haidhuru chochote kwa sababu dhambi za mhusika haziwezi kusemwa kwa yeyote Yule baada ya maungamo.

12. Kitubio kinatusaidia kuzama ndani kabisa ya mioyo yetu na hivi kuona namna tunavyoweza kuimarika kuepuka dhambi.

13. Kwa kitubio tunajiona jinsi tulivyo wadhambi na kuwa na saburi kwa wenzetu wanaotukosea.

14. Tunabakia na amani mioyoni kwa sababu tunao uhakika tunachokisema pakuungamia (confessional) kwamba hubakia hapo hapo.

15. Mioyoni mwetu dhamiri haitusuti tena.

16. Tunaandaliwa vyema kupokea Ekaristi Takatifu

17. Msamaha wa dhambi ni sehemu muhimu katika kuwa watakatifu

18. Dhamiri zetu zinajengwa vizuri zaidi kupitia kitubio

19. Kwa dhambi za mauti,Kitubio kinatuunganisha tena katika familia ya Mungu na Kanisa pamoja na kurejeshewa Neema ya utakaso.

Kwa haya maelezo haya nawakaribisha kwa michango ya kimantiki na kiteolojia,mintarafu waprotestanti na wakatoliki wapinzani wa sakramenti ya Upatanisho.
 
Asante kwa Somo Zuri. Mwenye Masikio Atasikia, mwenye Macho atasoma, na mwenye Uelewa ataelewa!

Pale mwisho ungeongezea namna ya Maungamo na hatua zake.
 
Walokole wanawazungumzia wanaoenda mbele ya padri (mmoja). Sasa je huko kwa Waprotestanti unapotaja dhambi zako hadharani huku TV ikirusha matangazo? Huwa nawashangaa Waprotestant, wanakuwa wakipinga jambo fulani la RC, lakini kwa mlango wa pili wanalitekeleza. Mtu unashika microphone unaongea katika LIVE TV broadcasting mbele ya ulimwengu jinsi ulivyokuwa malaya, ulikuwa jambazi, ulikuwa mchawi ukasababisha ajali ishirini za magari, ulikuwa mlevi wa kupindukia, ulikuwa unakashifu Roho wa Bwana, je, vyote hivyo kuviongea mbele ya madhabahu huku TV ikikurusha LIVE duniani kote, halafu unakuja kumshangaa Mkatoliki anavyoungama dhambi zake mbele ya padri! Maajabu hayatawaisha Waprotestanti!
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote
 
wakati tunasoma kulikuwa Na shamba la kanisa la Karanga wanafunzi wakawa wanaenda kuiba padri akawa analalamika sana siku hiyo kijana mmoja akaenda kuungama kwa padri Dhambi ya kuiba Karanga za kanisa.Padri akaenda kumchongea shuleni .Hiyo jumatatu akaitwa mbele ya wanafunzi akacharazwa viboko vya uhakika akataja wezi wenzie nao wakacharazwa viboko vya uhakika.Karanga za kanisa hazikuibiwa tena Na sehemu ya kuungama nayo ikakosa wanafunzi wa kwenda kuungama Dhambi kwa padri
 
Ninakiri kwamba nimekutana na uzi wa mwana-JF, “King Mufasa” leo ukihoji uaminifu walio nao mapadri wa Kanisa Katoliki,mintarafu utunzaji wa siri za mambo yanayojiri wakati sakramenti ya Upatanisho.

Kimsingi ukisoma katikati ya mistari ya mtoa uzi, utagundua kwamba mtoa mada Mkatoliki bandia, ndio kusema ni mprotestanti lakini kwa kuwa bila kujua yeye ameamua kutoa nafasi ya wakatoliki kuonyesha kwamba huwa hawafanyi mambo kwa kurupuka,nimeamua kujibu hoja yake “kwa nini maungamo yanafanyika kwa Padri” kwa uzi kamili.

Awali ya yote naomba kutoa tafsiri ya maneno makuu ambayo nimeyatumia katika Kichwa cha mada hii: Mosi,Mpinga Kristo ni mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapingana na sehemu au mafundisho yote ya Yesu Kristu na ya Mitume ambao ndio Yesu aliwakabudhi mamlaka ya kuliendesha Kanisa.Pili, Na Mtu anayesoma mambo kwa kuruka ruka ni yule ambaye hana anavamia machapisho na kuanza kuyasoma bila kufuata misingi na kanuni za usomaji na uchakataji maudhui husika.

Ni hivi, suala la kuungama watu dhambi kwa Padri lina teolojia yake kutoka katika kisa cha kutano la Zakayo na Yesu kule Yeriko.Katika kutano hilo,kuna mambo mengi sana ambayo Kanisa Katoliki tunachota na mojawapo ni hilo la kuungama dhambi kwa Mungu, tena kwa sauti, kupitia mwakilishi wa Yesu,ambaye ni Padri.Tunasoma hivi:

“1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. 2 Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. 3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. 4 Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. 5 Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” 6 Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” 8 Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” 9 Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu. 10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” 11 Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, ufalme wa Mungu ungefika.”

Kwa mjibu wa nukuu hiyo, ni kwamba tunafakarishwa kuungama dhambi na kurudisha mali zote ambazo tunakuwa tumezipata kwa njia ovu kama ambavyo Zakayo alikuwa amejipatia kwa njia zisizo halali.

Katika muktadha huo wa Kisa cha Zakayo na Yesu tunaangaziwa mambo mawili:

  • kuumia au kujutia sababu dhambi tunazozitenda
  • kuungama dhambi mbele ya Yesu Kristu
  • kufanya malipizi ya dhambi zetu.
Mwandishi Luka katika kisa hiki hatuonyeshi Zakayo aliungama dhambi zake kimoyokimoyo bali kwa sauti tena mbele ya Yesu na wala Yesu hasikiki kumkemea Zakayo kwa kitendo chake hicho cha kutaja dhambi zote alizopata kuzitenda kwa sauti na wala Yesu hasikiki kumkataza Zakayo aache kurejesha vile alivyokwisha kujipatia kwa njia ya udanganyifu. Kumbe ni kutokana na muktadha huo, Kanisa Katoliki pamoja na mambo mengine liliamua kuendeleza utaratibu huo wa kuungama dhambi kwa sakramenti ya Upatanisho.

Baadhi ya Wakristu wakatoliki hawaipendi hii Sakramenti kwa sababu ya kulishwa sumu na waumini wa madhehebu ya kiproetestanti kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuwafanya mapadri kama Mungu, wa kwenda kuelezwa dhambi. Tena katika mstari huo huo, wanahoji kwa nini kama mtu unaona unahitaji kutubu dhambi zako usifanye hivyo moja kwa moja kwa Yesu mwenyewe kwa sababu kwa madai yao, yeye ndiye mpatanishi wetu kati ya Mungu na wanadamu? Kumbe, suala linalowasumbua sio kuungama dhambi,bali kile kitendo cha kujinyenyesha mbele ya Padri na kumueleza dhambi zako.

Kumbe, waprotestanti hao hao wanashindwa kufahamu fundisho lililolala katika kisa hiki cha Zakayo. Wakosoaji kama hao ”Wanapotea maboya” kwa kutokuelewa kwamba ingali Yesu angetaka kufundisha kwamba dhambi ziungamwe kwa Mungu kimyakimya, basi angalifanya hivyo kwa Zakayo kama ambavyo alisahihisha mambo mengine ambayo yalikuwa na hitilafu katika jamii ya Kiyahudi.Kumbe,badala yake anaweka msisitizo katika fundisho ambalo lilikuwepo hata wakati wa Agano la Kale kama tunavyosoma Kutoka 22:1-17,Mambo ya Walawi 6:1-7 na Hesabu 5:1-10.

HOJA YA KIMANTIKI INAYOUNGA MKONO KUUNGAMA DHAMBI KWA PADRI

Kabla hatujaanza kuzama sana katika maandiko matakatifu katika kujibu hoja hiyo, naomba nami nitumie hoja ya kimantiki tu katika kuijibu hoja hiyo ya kiprotestanti.Hoja hiyo inajengwa na maswali yafuatayo:

  • Je, kuna mahali popote katika mafundisho yake Yesu Kristu alizuiwa watu kuungama dhambi zao mbele ya binadamu wenzao?
  • Hivi katika maisha yetu ya kawaida hata katika familia au jumuia zetu, inakuwaje pale unapomkosea mwenzako na ukahitaji usamehewe?
  • Je, huwa hatuwaelezi tuliowakosea hatua kwa hatua makosa yetu kabla kuwaomba msamaha?
  • Au vile vile, pale tunapotaka tupitie kwa marafiki au ndugu zetu ili watuombee msamaha kwa tuliowakosea, je hao tunaokuwa tumewakusudia watuombee msamaha wao huwa hawatuhitaji kwanza tuwaeleze jinsi tulivyowakosea wahusika?
KUMBE, haya mambo ya kuelezana jinsi tulivyokosa sio mbo mageni kabisa katika jamii zetu.Ni mambo tumeyazoea sana kiasi kwamba:

  • Mume na mke wanafanya;
  • mtu na ndugu zake wanafanya hivyo hivyo.
  • Makazini ndiyo usiseme mpaka wakati mwingine tunaambiwa tuandike barua za kujieleza ili kupima kama kosa lenyewe linahitaji msamaha au kufukuzwa kazi.
MASWALI MENGINE YA KIMANTIKI NI HAYA:

  • Inakuwaje kufichua dhambi zetu kwa wanadamu wenzetu lionekane jambo la kawaida ila inapokuja katika muktadha wa imani, ndio watu wengine wang’ake?
  • Kama tunaona ni jambo jema kuungamiana mke na mume makosa; ndugu na ndugu,rafiki na rafiki,kwa nini tupate soni na aibu kuungama mbele ya Mungu,muumba wetu?

HISTORIA YA MAUNGAMO YA DHAMBI KATIKA AGANO LA KALE

Kitabu cha Mambo ya Walawi 19:1-22, tunaelezwa na mwandishi jinsi ambavyo Musa alikuwa anaeleza aina ya dhambi ambazo wana wa Israel hawakupaswa kuzitenda na iwapo ingetokea wakakosa basi, alitoa utaratibu jinsi ambavyo dhambi za mtu huyo zingeondolewa:

“20 Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru. 21 Mwanamume huyo ataleta mbele ya hema la mkutano sadaka yake ya kondoo dume ya kuondoa hatia na kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. 22 Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.”

Kumbe, MUSA katika Agano la Kale, alikuwa amewaagiza wana wa Israel kwamba wanapomkosea Mungu, Kuhani ndiye anachukua nafasi ya upatanishi kati ya Mungu na mhusika baada ya mtenda dhambi husika kuwa amewasilisha mbele ya hema ya Mkutano, kondoo dume kwa ajili ya upatanisho.Lakini najua unaweza kujiuliza kuwa mbona Musa hakuelekeza kwamba mtu huyo anapowasilisha kondoo huyo kwa ajili ya kuondolewa dhambi,basi ni lazima pia aseme dhambi zake kwa kuhani huyo?Jibu la swali kama hilo ninalo na nakupatia sasa hivi.Ni kwamba katika mantiki ya kawaida haingwezekana Kuhani akawa akiona tu kondoo dume mlangoni, basi yeye anafanya kazi ya kumuombea huyo mtu mdhambi kwa Mungu, ili ziondolewe bila kuhafahamu ni dhambi zipi hizo zinaombewa msamaha. Basi, tunasoma hivi katika kitabu hicho cha Kutoka 5:1-6:

“1 Kama mtu yeyote akitakiwa kutoa ushahidi kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kulisikia naye akakataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atauwajibikia. 2 Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia. 3 Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia. 4 Au, kama mtu akiapa kufanya chochote kile, chema au kibaya, kama wafanyavyo watu bila kufikiri, atakapojua atakuwa na hatia. 5 Basi, mtu akiwa na hatia kuhusu mambo hayo lazima akiri dhambi yake aliyotenda 6 na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.”

Aya ya 5, katika nukuu hiyo hapo juu, inatoa sharti la mtu aliyekusudia kupatanishwa na Mungu kupitia Kuhani kuungama dhambi zake kwa Kuhani kwanza kabla ya kuombewa msamaha.

Mpaka hapo sasa nadhani tumeelewana.Au bado unataka kuniuliza swali kwamba hata kama wakati wa Agano wa Kale Kuhani ndiyo alikuwa anaelezwa dhambi za mtu kuna haja gani ya kufanya hivyo wakati huu wa Agano Jipya kwa sababu Yesu kristu alikwishakufa msalabani kwa ajili hiyo? Ndio kusema, Yesu ndiye Kuhani Mkuu. Kama hiyo, ndio hoja basi, fuatana nami kwa taratibu sana.

NJIA ZA KUONDOA DHAMBI ZA MWANADAMU
Ni kweli kwamba msamaha wa dhambi kwa mwanadamu kimsingi unatokana na kazi ya Yesu msalabani.Lakini swali linakuja msamaha huo unapatikanaje kwa kila mmoja wetu?Je, Kristu alituachia njia yoyote ndani ya Kanisa ya kuondolea dhambi?

Kwa mjibu wa mafundisho ya Kanisa Katoliki, Yesu Kristu alituachia njia mbili:

1. Ubatizo kwa ajili ya kutuondolea dhambi ya asili (original sign) ambayo hurithiwa tokea kwa wazazi wetu wa kwanza,Adamu na Hawa, na zile ambazo tunazitenda kabla ya kupewa huo ubatizo.Dhambi tunazozitenda baada ya ubatizo zinaitwa dhambi halisi(Actual sin).Dhambi zote tuzitendazo baada ya kubatizwa zinaitwa dhambi halisi kwa sababu ndio dhambi ambazo zinatokana na matendo yetu wenyewe.

2. Kwa sababu ya asili ya udhaifu wa mwanadamu, basi hata baada ya ubatizo hujikuta anaendelea kumkosea Mungu.Kumbe ni katika mazingira kama hayo Yesu Kristu alituachia njia ya pili ya kutuondolea dhambi.Ukweli ni kwamba dhambi zinatutenganisha na Mungu na kwa dhambi hakuna anayeruhusiwa kukanyaga Mbinguni.Kumbe ukitafakari kwa undani kabisa kuhusu mpango wa Mungu kumfanya mwanadamu aingie Mbinguni akiwa hana dhambi, haukukomea katika mateso,kifo cha ufufuko wake Yesu Kristu bali ni jambo ambalo ni endelevu kwa wanadamu vizazi kwa vizazi.

Ni lazima kila mwanadamu aangukapo dhambini atubu na kuazimia kuachana na dhambi ili kuweza kuingia Mbinguni.Kumbe,ni kwa kutokana na kufahamu kwamba licha yeye Yesu kuturudishia mahusiano kati ya Mungu Baba na wanadamu ambayo yalifungua tena njia ya wanadamu kufika Mbinguni,lakini pia kwa kufahamu kuwa hata baada ya kutupatanisha na Mungu bado wanadamu tungaliendelea kuwa tukianguka dhambini,Yesu basi aliamua kutuwekea utaratibu wa kuondolewa dhambi zetu.

Basi,kumbe ukimakinika sana utagundua kuwa Mungu aligawanya mkakati wa kumuondolea mwanadamu dhambi katika vipindi vitatu:

  • Kabla ya yeye kufika duniani(ndio kile kipindi ambacho makuhani walikuwa wakifanya kazi ya upatanishi.
  • Wakati yeye akiwapo hapa duniani.
  • Baada ya kuondoka hapa duniani na kuwaachia Mitume na mahalifa wao kazi hiyo.Sasa hebu nifuatilie ili tukitalii kipindi hiki cha awamu ya tatu cha mwanadamu kuondolewa dhambi.
Yesu na ukasimishaji mamlaka ya kuwaondolea watu dhambi

Neno kukasimu katika Kamusi Kuu ya Kiswahili (ya BAKITA) ina maana ya kumuagiza,kumtuma mtu mwingine;kuhamishia mamlaka ya kufanya jambo fulani kwa niaba yako.Na katika kufanya hivyo,mtu huyo anayeagizwa au kutumwa akifanya lolote itahesabiwa wewe uliyemuagiza ndiwe umefanya.

Katika maisha yetu ya kila siku kwa namna moja au nyingine tunakasimu baadhi ya majukumu yetu.Tunakasimu sehemu ya wajibu wetu kwa baadhi ya wanafamilia,maofisi ya Serikali au sekta binafsi.

Ukasimishaji una malengo mawili tu: mosi, kuleta ufanisi hasa pale inapokuwa inatoa nafasi kwa kazi husika kuhamishiwa kwa watu wenye ujuzi ambao unaendana na kazi iliyokusudiwa kufanyika.Pili, kuleta maendeleo.

Katika kuleta ufanisi na maendeleo, ukasimishaji una hatua zipatazo kama sita hivi ambazo zinapaswa kufuatwa: mosi, maandalizi. Pili, uteuzi wa wakasimiwa.Tatu, kuthibitisha uelewa wa majukumu.Nne,kuthibitisha kama mhusika ameyakubali majukumu.Tano,kuepuka kubatilisha ukasimishaji.Sita, kusimamia utekelezaji.

Mambo hayo sita, wengi wetu ndio tunayafanya kila mara,iwe katika familia au maofisini kabla ya kufikia kusema mtu fulani akasimiwe majukumu kadhaa.Hali kadhalika, ndiyo mambo aliyazingatia Yesu Kristu kabla ya kuwakasimisha Mitume mamlaka ya kuwaondolea watu dhambi zao mara angeondoka duniani.

Mwinjili Yohana katika sura ya 20:9-23, anatupasha ukweli huo nilioueleza hapo awali kwamba Yesu baada ya kufufuka ndio aliona inafaa awakasimishe Mitume wajibu huo wa kuwaondolea watu dhambi:

“19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20 Alipokwisha sema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. 21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”

Kuna mambo matatu, Yohana anayaeleza ambayo yanaambatana na mamlaka haya ya kuondolea watu dhambi:

1. Kwamba Mungu Baba alikuwa amemuagiza Yesu Kristu kuja kuwaondolea wanadamu dhambi.Dhambi zinazoongelewa hapa ni zile zilizoondolewa kwa damu ya Yesu kumwagika msalabani na yeye akishakumaliza kazi hiyo anawatuma na Mitume wakafanye kazi hiyo ya kuondolea watu dhambi zinazotendwa baada ya damu yake kuwa imemwagika msalabani: “21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.”

2. Kwamba ili Mitume waweze kuifanya kazi hiyo ya kuondolea watu dhambi,Yesu anawapatia nguvu na uwezo wa kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi:” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu.” Kumbuka katika maandiko Matakatifu, mahali pengine pekee ambako Mungu anampulizia mwanadamu pumzi ya uhai (sawa na wakati huu wa kuwapeni mamlaka na nguvu ya kuondoa dhambi) ni wakati ule wa uumbaji mwanadamu.Tunasoma Mwa 2:7 hivi:
“ 7 Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa.

Kumbe, Yesu kwa kuwapulizia Mitume Roho Mtakatifu ni kama anafanya uumbaji mpya sawa na vile alivyofanya wakati ule wa uumbaji ulimwengu.Tendo hili linaashiria ni nini kwa Mitume? Wakati ule wa uumbaji, Mungu katika nafsi tatu alifanya uumbaji na hivi kumbe katika tendo hili la Mitume kuwaondolea watu dhambi anadhihirisha kwamba jukumu hilo analowapatia Mitume ni Mungu mwenyewe katika nafsi zake tatu anafanya kazi hiyo ya kuwaondolea watu dhambi na kwamba Mitume watakuwepo kwa niaba yake katika kuifanya kazi hiyo.Ndio kusema kwamba kazi ya kuwaondolea wanadamu dhambi kwa asili yake ni kazi yake yeye Mungu mwenyezi aliyewaumba wanadamu.

Mtakatifu Cyril wa Alexandria (376 – 444), anasema maneno “akawapulizia” yanaeleza kile ambacho wazazi wetu wa kwanza bustanini Edeni walichokipoteza mara baada ya kuruhusu nafsini mwao mawazo ya kutaka kuwa na hadhi ya Umungu (dhambi ya asili) na kwamba huyo Roho Mtakatifu wanayepewa Mitume ni kielelezo kwamba kwa huyo Roho Mtakatifu, wanadamu watakuwa na maisha sawa ya yale ya mwanzo, wangali Adamu na Hawa hawajatenda dhambi.(Rejea Mtandao wa Sapienta, Genesis 2:7 & the Meaning of 'Life' in Cyril of Alexandria's Theology | Henry Center)

Jambo la tatu katika ukasimishaji huo wa maondoleo ya dhambi ni masharti ya mtu katika kuondolewa dhambi.Sawa na Kisa za Zakayo kwamba ilibidi aeleze dhambi mbele ya Yesu, ndivyo Yesu anavyowaelekeza Mitume kwamba mtu atahesabiwa amesahemewa dhambi zake Mbinguni ikiwa ameweza kuzisema dhambi zake. Ni maneno “…msipowasamehe, hawasamehewi” ndiyo yanatoa picha kwamba mtu anayetaka kuondolewa dhambi zake, analazimika kuzieleza dhambi zake nje ya moyo.

MANTIKI YA WAKATOLIKI KUUNGAMA DHAMBI KWA PADRI

Kanisa Katoliki, linaazima maelekezo ya kuungama dhambi kwa Padri kutoka maneno ya Yesu mwenyewe. Yesu angalimaanisha mtu kuungama dhambi zake bila kuzieleza basi, kusingalikuwa na uwezekano wa kushindwa watu wengine kusamehewa dhambi zao. Kwa mantiki ya kawaida, huwezi kumkatalia mtu jambo au ombi ambalo hulijui ni nini? Mantiki Ya pili, ya kulazimika wadhambi kusema au kutaja dhambi zao mbele ya Mitume,ni kwa sababu Mitume kama binadamu hawakuwa uwezo wa kusoma mioyo ya waungamaji na kuona humo dhambi zao ili waweze kusamehewa.

Kumbe, kwa maneno “…msipowasamehe, hawasamehewi”, Yesu anawaelekeza Mitume kwamba baada ya kusikiliza dhambi za waungama, kuna mazingira dhambi husika zinaweza zisiondolewe na mara watakapofanya hivyo, basi Mungu naye anakuwa ameridhia maamuzi hayo.

HITIMISHO

Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba Mitume walipewa uwezo huo wa kuondolea watu dhambi na kwamba wakifanya hivyo au wasipofanya hivyo basi dhambi zinakuwa zimeondolewa au hazijaondolewa mtawalia.

Na kwa misingi hiyo, wale waprotestant wanaokubali kwamba Mitume walipewa uwezo huo ni lazima waonyeshe uwezo huo wa Mitume uliishia kwa Mitume tu au uliendelea?.Na ili kuondoa mashaka kabisa pale watakapojenga kwamba uwezo huo hauendelei hadi kwa mapadri tokea hapo, basi lazima waonyeshe na mambo mengine mawili au matatu ambayo waliagizwa Mitume pekee na hivi kwamba waliowarithi hawakustahili kuhusika na maagizo hayo.

Jambo hili la kuungama dhambi ni pana lakini itoshe tu kusema kwamba, tunaweza kunyumbulisha faida kama kumi na tisa hivi hivi(19) za kwa nini tunapaswa kuungama dhambi:

1. Mungu alituamuru tuungamiane dhambi zetu.

2. Ni njia nyepesi kuwezesha dhambi zetu kuondolewa kwa sababu ukiwa mbele ya padre utajua kama dhambi zako zimeondolewa au la tofauti na vile ambavyo ingefanyika kwa Mungu moja kwa moja(kuungama kimoyokimoyo).

3. Tunapokea Neema inayotusaidia kuzishinda dhambi kupitia Sakramenti ya Kitubio.

4. Tunajifunza kuwa wanyenyekevu kwa kuungama dhambi zetu kwa wenzetu kama ambavyo Zakayo alivyokuwa mnyenyekevu kwa kushuka mtini na kukubali kusema dhambi zake mbele ya Yesu.

5. Kuungama kunatujengea moyo wa kuwajibika.

6. Mahusiano yetu na Kanisa yanahuishwa au yanaponywa.

7. Kwa kuungama tunapokea na ushauri nasaha toka kwa Padri.

8. Tunaweza kupokea faraja kupitia maneno ya Ondoleo la dhambi.

9. Dhambi zetu zote pamoja na zile zinazokuwa zimesahaulika huondolewa.

10. Kitubio kinatusaidia nguvu ya kuwasamehe na wenzetu wanaokuwa wametukosea.

11. Haidhuru chochote kwa sababu dhambi za mhusika haziwezi kusemwa kwa yeyote Yule baada ya maungamo.

12. Kitubio kinatusaidia kuzama ndani kabisa ya mioyo yetu na hivi kuona namna tunavyoweza kuimarika kuepuka dhambi.

13. Kwa kitubio tunajiona jinsi tulivyo wadhambi na kuwa na saburi kwa wenzetu wanaotukosea.

14. Tunabakia na amani mioyoni kwa sababu tunao uhakika tunachokisema pakuungamia (confessional) kwamba hubakia hapo hapo.

15. Mioyoni mwetu dhamiri haitusuti tena.

16. Tunaandaliwa vyema kupokea Ekaristi Takatifu

17. Msamaha wa dhambi ni sehemu muhimu katika kuwa watakatifu

18. Dhamiri zetu zinajengwa vizuri zaidi kupitia kitubio

19. Kwa dhambi za mauti,Kitubio kinatuunganisha tena katika familia ya Mungu na Kanisa pamoja na kurejeshewa Neema ya utakaso.

Kwa haya maelezo haya nawakaribisha kwa michango ya kimantiki na kiteolojia,mintarafu waprotestanti na wakatoliki wapinzani wa sakramenti ya Upatanisho.
 
Kwa hiyo nikitubu dhambi bila kwenda kwa padri siwezi kusamehewa?

Kama umesoma uzi vizuri utabaini kwamba uwezekano huo ungalikuwapo basi Yesu Kristu asingaliweka miundo mbinu hiyo ya Upatanisho.Kwa kuwa Yesu ni Mungu alijua watu kwa kujiungamia wenyewe wangaliishia kufanya sarakasi tu.Kuungama dhambi kunahusisha kufanya malipizi,waaidha kurudisha ulivyochukua kama alivyofanya Zakayo.

Ni kwamba tunalazimika kuungama dhambi ili mahusiano yetu na Mungu yawe mazuri.Dhambi ina madhara yafuatayo:mosi,inaleta mahusiano mabaya kati ya mwanadamu na Mungu.Pili,kati ya mtu mmoja na mwingine na tatu, kwa mtu mwenyewe.

Kumbe tofauti na Wakristu wengine wanavyoelewa, dhambi haiharibu tu mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu, bali pia kati ya wanadamu na wanadamu.Mt.Paulo anatueleza mara nyingi sana katika barua zake kuwa sisi ni viungo katika mwili wa Kristu na kwamba yeye (nafsi ya Pili) na Mungu baba ni wamoja Rejea Warumi 12:5):

“Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.”

Kwa hiyo, ni mantiki hiyo kwamba kwa sababu sisi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake,basi dhambi ya mtu mmoja haiishii katika kumuumiza mhusika pekee, bali madhara yake lazima yamguse na mwingine katika mnyororo ule ule unaotuunga kwa Kristu.(Rejea 1 Kor 12:26):

“26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.”

UNACHOONGELEA WEWE UNAMAANISHA KUTUBU

Injili ya Marko 1:1-5, nayo inatueleza kuwa watu walikuwa wanamwendea Yohana Mbatizaji wakishakutubu na wakishaungama dhambi zao, walibatizwa ili kupokea ondoleo la dhambi zao:

“4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani”.

Katika ya aya 4 na 5 ya Injili hiyo ya Marko, tunapata maneno mawili “Kutubu” na “kuungama” ambayo yana maana tofauti.

Na mwinjili Marko, anapotuandikia hivyo anamaanisha kwamba kulikuwa na mambo mawili yanafanyika kwa mtaka ubatizo kabla hajabatizwa.Mosi, kutubu dhambi na pili,kuungama dhambi.

KUTUBU, kunatofuatiana na KUUNGAMA kwa sababu, kutubu ni hali ya kuugua moyoni.KUTUBU ni kitendo cha kujutia tendo fulani.Kutubu hufanyika moyoni, wakati kuungama kunafanyika nje ya nafsi ya mtu.

Kuungama ni kusema nje ya moyoni na mbele ya mtu mwingine kuwa umekosa.Kumbe, Marko anapotumia maneno hayo mawili sio kama anataka kutueleza maana ile ile moja ya kujutia dhambi moyoni bali kuweka wazi hizo dhambi zenyewe.

Yakobo naye katika 5:14-15, anatupatia picha halisi ya maana ya neno kuungama anapotumia neno “ungamianeni” dhambi zenu.Ikiwa Yakobo alitaka kumaanisha mtu kusema dhambi zake kimoyokimoyo, basi angalitumia neno jingine na wala sio ungamieneni:

“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.”
 
Walokole wanawazungumzia wanaoenda mbele ya padri (mmoja). Sasa je huko kwa Waprotestanti unapotaja dhambi zako hadharani huku TV ikirusha matangazo? Huwa nawashangaa Waprotestant, wanakuwa wakipinga jambo fulani la RC, lakini kwa mlango wa pili wanalitekeleza. Mtu unashika microphone unaongea katika LIVE TV broadcasting mbele ya ulimwengu jinsi ulivyokuwa malaya, ulikuwa jambazi, ulikuwa mchawi ukasababisha ajali ishirini za magari, ulikuwa mlevi wa kupindukia, ulikuwa unakashifu Roho wa Bwana, je, vyote hivyo kuviongea mbele ya madhabahu huku TV ikikurusha LIVE duniani kote, halafu unakuja kumshangaa Mkatoliki anavyoungama dhambi zake mbele ya padri! Maajabu hayatawaisha Waprotestanti!

Mlokole mdhambi kuungama dhambi kwenye Luninga mbashara lakini akaona mdhambi mwenzie Mkatoliki kufanya hivyo mbele ya Padri kuwa noma ndio kusoma maandiko matakatifu kwa kuruka ruka na hivi kushindwa kuchakata maudhui stahiki.
 
Kama umesoma uzi vizuri utabaini kwamba uwezekano huo ungalikuwapo basi Yesu Kristu asingaliweka miundo mbinu hiyo ya Upatanisho.Kwa kuwa Yesu ni Mungu alijua watu kwa kujiungamia wenyewe wangaliishia kufanya sarakasi tu.Kuungama dhambi kunahusisha kufanya malipizi,waaidha kurudisha ulivyochukua kama alivyofanya Zakayo.

Ni kwamba tunalazimika kuungama dhambi ili mahusiano yetu na Mungu yawe mazuri.Dhambi ina madhara yafuatayo:mosi,inaleta mahusiano mabaya kati ya mwanadamu na Mungu.Pili,kati ya mtu mmoja na mwingine na tatu, kwa mtu mwenyewe.

Kumbe tofauti na Wakristu wengine wanavyoelewa, dhambi haiharibu tu mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu, bali pia kati ya wanadamu na wanadamu.Mt.Paulo anatueleza mara nyingi sana katika barua zake kuwa sisi ni viungo katika mwili wa Kristu na kwamba yeye (nafsi ya Pili) na Mungu baba ni wamoja Rejea Warumi 12:5):

“Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.”

Kwa hiyo, ni mantiki hiyo kwamba kwa sababu sisi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake,basi dhambi ya mtu mmoja haiishii katika kumuumiza mhusika pekee, bali madhara yake lazima yamguse na mwingine katika mnyororo ule ule unaotuunga kwa Kristu.(Rejea 1 Kor 12:26):

“26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.”

UNACHOONGELEA WEWE UNAMAANISHA KUTUBU

Injili ya Marko 1:1-5, nayo inatueleza kuwa watu walikuwa wanamwendea Yohana Mbatizaji wakishakutubu na wakishaungama dhambi zao, walibatizwa ili kupokea ondoleo la dhambi zao:

“4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani”.

Katika ya aya 4 na 5 ya Injili hiyo ya Marko, tunapata maneno mawili “Kutubu” na “kuungama” ambayo yana maana tofauti.

Na mwinjili Marko, anapotuandikia hivyo anamaanisha kwamba kulikuwa na mambo mawili yanafanyika kwa mtaka ubatizo kabla hajabatizwa.Mosi, kutubu dhambi na pili,kuungama dhambi.

KUTUBU, kunatofuatiana na KUUNGAMA kwa sababu, kutubu ni hali ya kuugua moyoni.KUTUBU ni kitendo cha kujutia tendo fulani.Kutubu hufanyika moyoni, wakati kuungama kunafanyika nje ya nafsi ya mtu.

Kuungama ni kusema nje ya moyoni na mbele ya mtu mwingine kuwa umekosa.Kumbe, Marko anapotumia maneno hayo mawili sio kama anataka kutueleza maana ile ile moja ya kujutia dhambi moyoni bali kuweka wazi hizo dhambi zenyewe.

Yakobo naye katika 5:14-15, anatupatia picha halisi ya maana ya neno kuungama anapotumia neno “ungamianeni” dhambi zenu.Ikiwa Yakobo alitaka kumaanisha mtu kusema dhambi zake kimoyokimoyo, basi angalitumia neno jingine na wala sio ungamieneni:

“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.”
Mkuu hivi kweli Biblia unaijua au ndo unaandika tu?.UNAIJUA MAANA YA KUUNGAMANIANA KWELI?.sio kwenda kwa padri bali ni kuomba ya ajili ya makosa ya watu wengine(hata kama wew huusiki).Na katika kutubu au kuomba hatutubu mbele ya wazee wa kanisa wala padri bali MBELE YA MUNGU.
IMG_20180829_175928.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na nafikiri kwenye uzi ule kuna baadhi ya watu waliowahi mwanzo walihoji kwa nini na niliwapa jibu na wala hakuna mtu aliyezuiliwa kwenda kuomba msamaha kwa Mungu kupitia mapadri. Ila si mapadri wote siku hizi wanatenda kazi zao katika maadili yanayokubalika. Mengi nilieleza ndani ya uzi ule kwa walionihoji hivyo siwezi kurudia hapa maana si muda muhafaka kwa hilo. Kila mkatoliki ana haki ya kwenda mbele ya padri kwa maungamo ila mtu huwezi kwenda pale huku ukiwa unakumbuka kitu kilichowahi tendeka nyuma na padri mwenzie ukaondoka kwenda kwenye malipizi ukiwa bado una wasiwasi. Binafsi siwezi sijagusia mtu mwingine.
 
Mkuu umewahi kusoma kisa cha watu wawili walioenda hekaluni,mmoja aliungama dhambi zake kwa kunyenyekea mbele ya Mungu na mwingine alijivuna kwa wema wake,na Yesu akasema yule aliyenyenyekea alipata msamaha wa dhambi zake.Mbona alisamehewa bila kwenda kwa padri?
 
Back
Top Bottom