Ifahamu: Ajali mbaya na kubwa zaidi ya ndege iliyowahi kutokea duniani iliyoua watu 583

big dreamer

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
398
1,059
Tarehe 27/03/1977 kwenye visiwa vya Hispania katika uwanja wa ndege wa Tenerife ndege mbili kubwa ulimwenguni kwa wakati huo #Boeing 747 moja ikiwa ya Shirika la #KLM ya #Uholanzi na nyengine PanAm ya Marekani ziligongana kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege Runway na kupoteza maisha ya watu 583.

66264450_454336508681464_4083816258368176128_n.jpg

66120886_454336558681459_3323359923147898880_n.jpg

Ajali hiyo iliyosababishwa na mtiririko wa matukio tofauti ikiwemo Tukio la Ugaidi lililotokea katika viwanja vingine vya ndege, Mawasiliano duni, Hali ya
hewa ya ukungu mzito na makosa ya marubani.

Ndiyo ajali inayoshikilia rekodi kubwa katika usafiri wa anga kwa kupoteza maisha ya abiria wengi kwa wakati
mmoja kwa kuhusisha ndege mbili za kampuni ya Boeing 747 #JumboJet zilizoshikilia rekodi ya ukubwa
duniani kwa miaka zaidi ya 30 (Kabla ya kuundwa kwa Airbus380 na #Antonov225).

Ndege hizo zilitua kiwanjani hapo kwa dharura kwakuwa viwanja vilivyo takiwa kutua kulikuwa na na tishio kuwepo kwa ugaidi hivyo

hivyo ikatakiwa kutua kiwanja hicho kidogo Tenerife kwa dharura kwa saa kadhaa mpaka polisi walipojiridhisha hali ni shwari ndipo wakaruhusiwa ku departure kiwanjani hapo na kuelekea kwenye miji yao wanayotakiwa kwenda

ikumbukwe kiwanja cha Tenerife kilikuwa ni kidogo na hakikiwahi kupokea ndege kubwa kama hizo na kwa wakati mmoja

baada ya kupewa 'go ahead' hali ni shwari wanakotakiwa kwenda,,,,picha likaanza hivi

Pakiwa na ukungu mzito uwanjani hapo uliosababisha kutokuona kilicho umbali mfupi mbele yako, Rubani wa KLM alianza kuchochea kasi ya kwenda kuruka pasipo amri kutoka kwa muongozaji ndege #Air Traffic Controller wakati huo huo Rubani wa ndege ya PanAm alipewa amri ya kuingia kwenye njia ya mchepuko ya karibu #TaxiWay mara baada ya kutua
lakini nae alipitiliza na kuingia njia inayofuata.
Marubani wa KLM huku ndege yao ikiwa imeanza kushika kasi ya kwenda kupaa njiani waliweza kuiona kwa mbali ndege ya PanAm njiani ikiwa inakata kona ya kutoka nje ya "Runway" ambapo Rubani mkuu wa KLM alijaribu kunyanyua ndege yake ili kupaa mapema kuepuka kukutana na PanAm lakini kwa bahati mbaya ilikuwa haijafika kasi ya kutosha kuweza kupaa hivyo kuishia kunyanyuka mbele huku nyuma ikiburuza mkia wake kwenye "Runway" na kuivaa ndege ya PanAm juu
ubavuni na zote kuishia katika mzinga mkali na milipuko ya moto.

Jumla ya abiria 583 walipoteza maisha na wengine 61 kunusurika huku wakiwa na majeraha makubwa.
Abiria wote 61 walionusurika ni kutoka katika ndege ya
PanAm akiwemo Rubani wake ambaye alifariki dunia
mwaka 2017.
Hata hivyo bado wanasema kuwa ndege hizo hazikujaa abiria inavyotakiwa pengine watu wengi zaidi wangepoteza maisha.
Screenshot_20221107-103440_1.jpg
Screenshot_20221107-104305_1.jpg
Screenshot_20221107-104816_1.jpg
Screenshot_20221107-104758_1.jpg
Screenshot_20221107-103549_1.jpg
Screenshot_20221107-104430_1.jpg
Screenshot_20221107-103620_1.jpg
Screenshot_20221107-103452_1.jpg
Screenshot_20221107-103600_1.jpg
 
Tarehe 27/03/1977 kwenye visiwa vya Hispania katika uwanja wa ndege wa Tenerife ndege mbili kubwa ulimwenguni kwa wakati huo #Boeing 747 moja ikiwa ya Shirika la #KLM ya #Uholanzi na nyengine PanAm ya Marekani ziligongana kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege Runway na kupoteza maisha ya watu 583.

View attachment 2409109

View attachment 2409110

Ajali hiyo iliyosababishwa na mtiririko wa matukio tofauti ikiwemo Tukio la Ugaidi lililotokea katika viwanja vingine vya ndege, Mawasiliano duni, Hali ya
hewa ya ukungu mzito na makosa ya marubani.

Ndiyo ajali inayoshikilia rekodi kubwa katika usafiri wa anga kwa kupoteza maisha ya abiria wengi kwa wakati
mmoja kwa kuhusisha ndege mbili za kampuni ya Boeing 747 #JumboJet zilizoshikilia rekodi ya ukubwa
duniani kwa miaka zaidi ya 30 (Kabla ya kuundwa kwa Airbus380 na #Antonov225).

Ndege hizo zilitua kiwanjani hapo kwa dharura kwakuwa viwanja vilivyo takiwa kutua kulikuwa na na tishio kuwepo kwa ugaidi hivyo

hivyo ikatakiwa kutua kiwanja hicho kidogo Tenerife kwa dharura kwa saa kadhaa mpaka polisi walipojiridhisha hali ni shwari ndipo wakaruhusiwa ku departure kiwanjani hapo na kuelekea kwenye miji yao wanayotakiwa kwenda

ikumbukwe kiwanja cha Tenerife kilikuwa ni kidogo na hakikiwahi kupokea ndege kubwa kama hizo na kwa wakati mmoja

baada ya kupewa 'go ahead' hali ni shwari wanakotakiwa kwenda,,,,picha likaanza hivi

Pakiwa na ukungu mzito uwanjani hapo uliosababisha kutokuona kilicho umbali mfupi mbele yako, Rubani wa KLM alianza kuchochea kasi ya kwenda kuruka pasipo amri kutoka kwa muongozaji ndege #Air Traffic Controller wakati huo huo Rubani wa ndege ya PanAm alipewa amri ya kuingia kwenye njia ya mchepuko ya karibu #TaxiWay mara baada ya kutua
lakini nae alipitiliza na kuingia njia inayofuata.
Marubani wa KLM huku ndege yao ikiwa imeanza kushika kasi ya kwenda kupaa njiani waliweza kuiona kwa mbali ndege ya PanAm njiani ikiwa inakata kona ya kutoka nje ya "Runway" ambapo Rubani mkuu wa KLM alijaribu kunyanyua ndege yake ili kupaa mapema kuepuka kukutana na PanAm lakini kwa bahati mbaya ilikuwa haijafika kasi ya kutosha kuweza kupaa hivyo kuishia kunyanyuka mbele huku nyuma ikiburuza mkia wake kwenye "Runway" na kuivaa ndege ya PanAm juu
ubavuni na zote kuishia katika mzinga mkali na milipuko ya moto.

Jumla ya abiria 583 walipoteza maisha na wengine 61 kunusurika huku wakiwa na majeraha makubwa.
Abiria wote 61 walionusurika ni kutoka katika ndege ya
PanAm akiwemo Rubani wake ambaye alifariki dunia
mwaka 2017.
Hata hivyo bado wanasema kuwa ndege hizo hazikujaa abiria inavyotakiwa pengine watu wengi zaidi wangepoteza maisha.
View attachment 2409111View attachment 2409112View attachment 2409113View attachment 2409116View attachment 2409117View attachment 2409118View attachment 2409119View attachment 2409120View attachment 2409121
Hii niliifatilia kwny kipindi cha aircraft investigation kupitia discovery channel ya Canada
 
Natumaini kwa ajali hiyo walijifunza mengi kiasi haitatokea ajali yenye mazingira kama hayo,na hata ikitokea haitakua na athari kubwa namna ile.
Huku kwetu ni tofauti kabisa, hakuna tunachojifunza kutokana na makosa, hatuwezi kuzuia makosa moja kwa moja ila tunapaswa kujifunza kutokana na makosa hayo.

Kosa litakua kosa ikiwa litarudiwa.
 
Tarehe 27/03/1977 kwenye visiwa vya Hispania katika uwanja wa ndege wa Tenerife ndege mbili kubwa ulimwenguni kwa wakati huo #Boeing 747 moja ikiwa ya Shirika la #KLM ya #Uholanzi na nyengine PanAm ya Marekani ziligongana kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege Runway na kupoteza maisha ya watu 583.

View attachment 2409109

View attachment 2409110

Ajali hiyo iliyosababishwa na mtiririko wa matukio tofauti ikiwemo Tukio la Ugaidi lililotokea katika viwanja vingine vya ndege, Mawasiliano duni, Hali ya
hewa ya ukungu mzito na makosa ya marubani.

Ndiyo ajali inayoshikilia rekodi kubwa katika usafiri wa anga kwa kupoteza maisha ya abiria wengi kwa wakati
mmoja kwa kuhusisha ndege mbili za kampuni ya Boeing 747 #JumboJet zilizoshikilia rekodi ya ukubwa
duniani kwa miaka zaidi ya 30 (Kabla ya kuundwa kwa Airbus380 na #Antonov225).

Ndege hizo zilitua kiwanjani hapo kwa dharura kwakuwa viwanja vilivyo takiwa kutua kulikuwa na na tishio kuwepo kwa ugaidi hivyo

hivyo ikatakiwa kutua kiwanja hicho kidogo Tenerife kwa dharura kwa saa kadhaa mpaka polisi walipojiridhisha hali ni shwari ndipo wakaruhusiwa ku departure kiwanjani hapo na kuelekea kwenye miji yao wanayotakiwa kwenda

ikumbukwe kiwanja cha Tenerife kilikuwa ni kidogo na hakikiwahi kupokea ndege kubwa kama hizo na kwa wakati mmoja

baada ya kupewa 'go ahead' hali ni shwari wanakotakiwa kwenda,,,,picha likaanza hivi

Pakiwa na ukungu mzito uwanjani hapo uliosababisha kutokuona kilicho umbali mfupi mbele yako, Rubani wa KLM alianza kuchochea kasi ya kwenda kuruka pasipo amri kutoka kwa muongozaji ndege #Air Traffic Controller wakati huo huo Rubani wa ndege ya PanAm alipewa amri ya kuingia kwenye njia ya mchepuko ya karibu #TaxiWay mara baada ya kutua
lakini nae alipitiliza na kuingia njia inayofuata.
Marubani wa KLM huku ndege yao ikiwa imeanza kushika kasi ya kwenda kupaa njiani waliweza kuiona kwa mbali ndege ya PanAm njiani ikiwa inakata kona ya kutoka nje ya "Runway" ambapo Rubani mkuu wa KLM alijaribu kunyanyua ndege yake ili kupaa mapema kuepuka kukutana na PanAm lakini kwa bahati mbaya ilikuwa haijafika kasi ya kutosha kuweza kupaa hivyo kuishia kunyanyuka mbele huku nyuma ikiburuza mkia wake kwenye "Runway" na kuivaa ndege ya PanAm juu
ubavuni na zote kuishia katika mzinga mkali na milipuko ya moto.

Jumla ya abiria 583 walipoteza maisha na wengine 61 kunusurika huku wakiwa na majeraha makubwa.
Abiria wote 61 walionusurika ni kutoka katika ndege ya
PanAm akiwemo Rubani wake ambaye alifariki dunia
mwaka 2017.
Hata hivyo bado wanasema kuwa ndege hizo hazikujaa abiria inavyotakiwa pengine watu wengi zaidi wangepoteza maisha.
View attachment 2409111View attachment 2409112View attachment 2409113View attachment 2409116View attachment 2409117View attachment 2409118View attachment 2409119View attachment 2409120View attachment 2409121
Ipo youtube
 
Back
Top Bottom