If no dirty tricks, what is wrong with independent tallying for verification?

If no dirty tricks, what is wrong with independent tallying for verification?

Okay, tufanye kulikuwa na center za kuhesabia mikoa yote Tanzania na UKAWA wakamaliza kuhesabu na kupata jumla yao terehe 26 jioni - unadhani NEC ndio wangekubaliana na hesabu ya CHADEMA na kumpa urais Lowassa? either way hili lingeendelea kuwa tatizo kama ilivyo huko Zanzibar hii leo. Cha msingi ni kuwa wamoja na tujadiliane jinsi ya kubadilisha haya.

Kwani hesabu ya kujumlisha jibu si lazima liwe moja tu? Kinachoweza kuwa siyo sawa ni zile namba zinazojumlishwa. Namba za kujumlisha zipo wazi kwa kila mtu. Ukawa ni lazima waseme ni namba zipi ndiyo zenye matatizo.
 
that is the problem

but we have a very BIG problem here!!

which is this swali I asked

Hivi raia wa TZ ukikamatwa nchi kama chinna au N.Koreea unafanya talling ya matokeo ya uchaguzi MKUU kwa moja ya vyama vya siasa kwenye nchi zao, unadhani adhabuyake inaweza kuwa ni nini??

Wana very addvanced systems za tallying, wewe mtanzania huhitajiki kwenda kufanya tallying, na hata ukiamua kufanya tallying kwao sio issue wapo transparent sana sio kama huku kwenu mabonde kuinama
 
Kama vyama kupitia mawakala wake, wote wanazo nakala halisi za matokeo, sasa kuna ubaya gani vyama vikajumlisha, na kuiambia NEC kuwa haya ndio matokeo halisi, sasa hayo ya NEC yanatoka wapi wakati kila chama kina nakala za matokeo halisi ya vituoni?!.

Kwa maana nyingine, baraza la mtihani litoe mtihani wa form six, then wanafunzi waruhusiwe kusahihisha mtihani huo na kutoa majibu kwa baraza la mtihani, then hilo baraza litangaze matokeo kwa kuangalia majibu ya marks walizopeana wanafunzi....
So funny bro!!
 
Wanabodi,

Sheria ya uchaguzi imeruhusu vyama vyote kuweka mawakala wake kwenye kila kituo!, matokeo yakitoka kila wakala anapewa anasaini na kupewa nakala yake yenye matokeo halali ya kila kituo, kisha matokeo hayo ndio yanabandikwa vituoni!.

Sasa kuna ubaya gani kama mawakala wayayatuma matokeo hayo kwenye vyama vyao, na vyama vikafanya an independent tallying, ili kuverify matokeo yanayotolewa na NEC ndio matokeo halisi na sii matokeo ya kupikwa?!.

Sheria inatamka ni NEC pekee ndio wenye mamlaka ya kutangaza matokeo, lakini sio NEC pekee ndio wenye mamlaka ya kujumlisha hizo kura!.

Kama vyama kupitia mawakala wake, wote wanazo nakala halisi za matokeo, sasa kuna ubaya gani vyama vikajumlisha, na kuiambia NEC kuwa haya ndio matokeo halisi, sasa hayo ya NEC yanatoka wapi wakati kila chama kina nakala za matokeo halisi ya vituoni?!.

If there is nothing to hide, kwa nini serikali ikawakamata wataalamu wa Chadema wanaofanya independewnt tallying?!.

Japo I smell something fishy!, naomba Lowassa asikilizwe ana hoja za msingi, na kiukweli baadhi ya wafuasi wake, ni watu waliopigika sana kimaisha, the have a very thin line between kuendelea kuishi au kuamua kufa na Lowassa, hivyo at this juncture, Lowassa must be handled with extra care, and if possible contained for the sake of national interests, if let loose na yeye akawacha wafuasi wake to get loose, kuipigania haki yao walioaminishwa imepokwa!, kiukweli Tanzania hapata kalika!.

Pasco

Mkuu acha vitisho kama vya kingunge alivyoitisha ccm ikae na lowassa baada ya kumkata.hii ni mbinu yenu maarufu ya kutaka huruma.
Ujue pia kuna watu wapo tayari nao kufanya lolote shauri ya ccm.
Election mechanism ya lowassa ilifeli katika nyanja nyingi.nguvu kubwa ilitumika ngazi ya taifa na mgombea wa urais huku wagombea ubunge na udiwani wakiachwa watembelee nyota zao au umaarufu wa mgombea urais.
Mikutano iliishia makao makuu ya wilaya au mikoa.vijijini ilikua nadra mgombea urais wa ukawa kupita.
Kuhusu IT wa lowassa state inajua sana kuliko mimi na wewe hususan kilichofanyika pemba.
Mshaurini mzee akubali aanze kujipanga upya naamini akifanyia kazi mapungufu hayo na kama ccm wakilala kura 2020 kura zitamtosha tu.
 
Wakala yeye anahusika kura za kituo chake tu. Hausiki na kujumlisha kura za vituo vingine. You are so yestarday! Kwani kupata mahesabu ya kura kituo a, f , r, n,.... nilazima uwe ilo jimbo au mkoa?

Dhumuni mojawapo la kuwa na Tallying centre ni kupata jumla ya kura kwa muda mfupi. Kusubiri mawakala watoke vijijini lingechukuwa muda na gharama na inabidi uwalipie usafiri, chakula na malazi ni gharama zisizo na ulazima.

Hayo ya maeneo tofauti nani wangepataje jumla yake?! Ingebidi kuwa na Tallying Centre nyingine ya kupata jumla ya hayo maeneo tofauti. Sio cost effective, ingechukuwa muda na gharama.

Kuna kitu ambacho huenda mimi sikielewi kabisa. Hesabu za nani ameshinda kiti cha ubunge kwenye jimbo fulani nani alifanya? Hesabu za nani ameongoza kura za Urais kwenye jimbo fulani ni nani alifanya?
 
Mkuu acha vitisho kama vya kingunge alivyoitisha ccm ikae na lowassa baada ya kumkata.hii ni mbinu yenu maarufu ya kutaka huruma.
Ujue pia kuna watu wapo tayari nao kufanya lolote shauri ya ccm.
Election mechanism ya lowassa ilifeli katika nyanja nyingi.nguvu kubwa ilitumika ngazi ya taifa na mgombea wa urais huku wagombea ubunge na udiwani wakiachwa watembelee nyota zao au umaarufu wa mgombea urais.
Mikutano iliishia makao makuu ya wilaya au mikoa.vijijini ilikua nadra mgombea urais wa ukawa kupita.
Kuhusu IT wa lowassa state inajua sana kuliko mimi na wewe hususan kilichofanyika pemba.
Mshaurini mzee akubali aanze kujipanga upya naamini akifanyia kazi mapungufu hayo na kama ccm wakilala kura 2020 kura zitamtosha tu.

Na mimi ndio nawataka hao wa CCM walioko tayari.Jipangeni tusubiri Lowasa afungue pambano
 
that is the problem

but we have a very BIG problem here!!

which is this swali I asked

Hivi raia wa TZ ukikamatwa nchi kama chinna au N.Koreea unafanya talling ya matokeo ya uchaguzi MKUU kwa moja ya vyama vya siasa kwenye nchi zao, unadhani adhabuyake inaweza kuwa ni nini??
Wewe ni zoba la kutupwa. Unafikiri ni kila nchi inaendeshwa kifala kifala kama hii yetu! Unafikiri uchaguzi kwao utaona ujinga uliouona hapa kwetu. Tembea uone upanue mawazo wacha kufikiri kama uko Magu unakula mlenda
 
Wanabodi,

.....
If there is nothing to hide, kwa nini serikali ikawakamata wataalamu wa Chadema wanaofanya independewnt tallying?!.

Japo I smell something fishy!, naomba Lowassa asikilizwe ana hoja za msingi, na kiukweli baadhi ya wafuasi wake, ni watu waliopigika sana kimaisha, the have a very thin line between kuendelea kuishi au kuamua kufa na Lowassa, hivyo at this juncture, Lowassa must be handled with extra care, and if possible contained for the sake of national interests, if let loose na yeye akawacha wafuasi wake to get loose, kuipigania haki yao walioaminishwa imepokwa!, kiukweli Tanzania hapata kalika!.

Pasco

Pasco ni wewe ndio unatoa ushauri huu?

Wewe huelewi kuwa UKAWA ndio wamelinda/ wamezuia isitokee fujo na maafa mpaka muda huu baada ya uharamia uliofanywa na NEC?
Kweli miaka yote huelewi Tanzania imekuwa na utulivu kwa sababu tu, viongozi wa upinzani wamekuwa wastaarabu kupita kiwango kinachotakiwa kwa viwango vya kimataifa? Upinzani wangefanya kama "Polisi" yetu inavyopokea maelekezo kutoka kwa Chai Chapati Maharage hali ingekuwaje?

Who should contain Lowassa?

Watanzania watu wa ajabu kweli, unaweza kusema pia ni watu wa hovyo tu kama Mkapa anawaita, wapumbavu na malofa.

Haki inaminywa na anaepiga kelele kusema haki inamwinywa unataka awe "contained?"

Tafadhali tuambie awe "contained" vipi?
 
Toa Ushahidi kwamba wali hack system ya NEC.

Na kwa taarifa yako hauwezi kuhack system ambayo haina Link sharing status ya Information. Savers zinazotumika kutunza matokeo ni storage only na hakuna anywhere unaweza ukaingilia coz hazina public link ya mtu kuweza Ku retrieve info Kutoka kwenye hizo saver.

Nenda kasome IT then urudi na majibu sahihi.

Kama issue ni tallying kwann wahusika watoka nje ya nchi?hakuna watz ambao wangeweza kufanya hiyo tallying?kama ni kweli unachokisema basi wale jamaa walikua kazi kubwa zaidi ya hiyo tallying.
 
Kwa mjibu wa Nec kila mgombea/chama ana haki ya kuweka wakala wake kuanzia ngazi ya kituo cha kupigia kura,kuhesabu kura na kutangaza matokeo kwa ngazi ya kituo,kata na jimboni tu.

Lakini ni kosa la jinai kwa ngazi ya taifa kwa wakala wa chama/mgombea kushuhudia matokeo yake toka majimboni yakijumlishwa na kutangazwa?

Tume inataka kuaminiwa wakati yenyewe haiamini baadhi ya vyama/wakala?

Mbona hesabu za majimbo yote ya Tanzania zilikuwa zinawekwa wazi na NEC na kila mtu alikuwa huru kuzijumlisha? Ukawa ilitakiwa waseme ni hesabu za majimbo gani zimekosewa. La sivyo wakae kimya.
 
Kwa maana nyingine, baraza la mtihani litoe mtihani wa form six, then wanafunzi waruhusiwe kusahihisha mtihani huo na kutoa majibu kwa baraza la mtihani, then hilo baraza litangaze matokeo kwa kuangalia majibu ya marks walizopeana wanafunzi....
So funny bro!!

Katiba Mbovu au tuseme isiyokidhi mahitaji ya siasa za ushindani inazuia kupingwa matokeo ya Urais Mahakamani. Hii ni kubaka demokrasia. NEC ikifanya uharamia ndio basi watanzania wanatawaliwa na Rais ambaye hata kama upo ushahidi kuwa alipachikwa tu kwa utashi wa NEC na CCM na sio kutokana na kupata kura nyingi huwa ndio imetoka. wadanganyika inabidi wavumilie maumivu;"maisha bora" kwa miaka zingine 5. na zingine 5 kila duru ya uchaguzi inapofika.
So funny bro!!
 
Kama issue ni tallying kwann wahusika watoka nje ya nchi?hakuna watz ambao wangeweza kufanya hiyo tallying?kama ni kweli unachokisema basi wale jamaa walikua kazi kubwa zaidi ya hiyo tallying.

Kazi ya kujumlisha inaweza kufanywa hata na mtoto wa shule ya msingi. Hakuna utaalam wowote unahitajika
 
Mbona hesabu za majimbo yote ya Tanzania zilikuwa zinawekwa wsxi na NEC na kila mtu alikuwa huru kuzijumlisha? Ukawa ilitakiwa waseme ni hesabu za majimbo gani zimekosewa. La sivyo wakae kimya.
Hili unalosema ndio muhimu. UKAWA kama wana ushahidi wameibiwa watoe ushahidi sasa isiwe kuaminisha umma tu kuwa wameibiwa. Ushahidi wa kuibiwa uko wapi?

Kama wamekusanya nakala za vituoni zionesheni kwa umma. Kule Zanzibar Seif amewabana ZEC-CCM mapema mpaka wamechanganyikiwa.
Ile kitu ZEC-CCM imefanya mwaka huu; kutomtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi itakuwa ni maajabu ya 9 ya dunia. CCM inalalamika imeibiwa, haijapata kutokea!
 
Upinzani wa nchi hii ni bogus tu hauna plan wala strategy; hawakuwa wamejipanga kupata idadi ya kura zao na nadhani sehemu nyingi hawakuwa na wakala na sehemu zingine hawakuwa na wagombea wa ubunge wa kuweza kuwarushia data. Kura za raisi hazikuwa na figisu huko majimboni na ingekuwa rahisi kabisa mgombea ubunge kuzirusha haraka na zikaweza kujumlishwa kura za majimbo 256 ndani ya lusiku mmoja na siku ya pili kila kitu kikawa wazi; tatizo hawa watu ni wababaishaji ndio mana hawawezi kusema kura zimeibiwa ngapi na wapi na wapi

Mkuu hapa nakubaliana na wewe 100%. It is as if Ukawa walikurupuka na hawakuwa na mkakati madhubuti wa kuzuia wizi wa kura! Kwa mfano inavyoonekana hawakuwa na plan B baada ya watu wao wa IT kukamatwa. Ingetakiwa wawe na backup centre nyingine ambayo ingeendelea na kazi ya tallying kama kawaida ili Ukawa waweze kujua haraka ni kituo au jimbo gani wamechakachuliwa.! Hapa sasa hivi wanasema matokeo yamechakachuliwa lakini hawako specific ni wapi na kwa kiasi gani. Ni malalamiko ya jumla jumla tu . Too sad!
 
Wewe ni kati ya wazalendo wa kweli waliobaki.
raided kama tahadhari?
Ndio mahali Tanzania imefika,polisi wana raid kama tahadhari?
Ni kwa kiwango gani hii raided kama tahadhari inaweza kufanyika,hii raided kama tahadhari ni maarufu sana kwenye nchi za kidictator.Na sheria za mkononi kama hizi zinaita sheria za mkononi kutoka upande wa pili.Kwa mfano,kwa hichi ulichoandika mimi sioni kama unastahili kuwa hai,lakini naheshimu sheria,naumia,naumia sana lakini namezea na maji navumilia,msichukulie uvumilivu wetu kama alama ya ujinga,sisi sio wajinga haki ya Mungu nakuhakikishia.

Na ukitaka kujua sio wajinga,subiri Lowasa atoe Tamko!
 
Kwa maana nyingine, baraza la mtihani litoe mtihani wa form six, then wanafunzi waruhusiwe kusahihisha mtihani huo na kutoa majibu kwa baraza la mtihani, then hilo baraza litangaze matokeo kwa kuangalia majibu ya marks walizopeana wanafunzi....
So funny bro!!
Nimeipenda hii, tatizo hakuna kitufe cha like
 
Pasco nimesoma uzi wako na comments za watu naona hasira inazi kupanda!!! Acha niachie hapa!!! ILA NI LINI WATANZANIA TUTAJIVUNIA KUWA WATANZANIA???
 
Last edited by a moderator:
Leo umeandika vitu vya msingi,two days before ulikuwa unafanya spinning, huwezi kaa kimya wakati unadhulimiwa.I'm distressed immesuarably
 
Back
Top Bottom