Ielewe orodha ya matajiri duniani

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Habari za Asubuhi;

Wote tumezoea kusikia habari matajiri wa dunia na kiwango chao cha utajiri.Kuna ambao huwa tunafikiri hawa matajiri wana vyumba vimejaa minoti,wanamiliki hekari na hekari za plots, mashamba, majumba, ng'ombe na labda wanamiliki viwanda etc.

Hali imefanya wengi wetu tupata ugumu wa kujua hasa utajiri wao unamaanisha ni nini na inawezekanaje mtu aingize utajiri wa Bilioni 1 kwa siku moja ambayo ni pesa nyingi kuliko hata makusanyo ya kodi ya Tanzania.

Kwanza kabisa napenda tufahamu kwamba ili uingie katika orodha rasmi ya matajiri wa dunia ni lazima uwe tayari kuweka taarifa zako zote wazi na kufuatiliwa kwa ukaribu.

Ni lazima uweke taarifa za Assets zako, Liabilities zako kwa uwazi kabisa.Ninaposema kuweka wazi simaanishi kwa dunia nzima bali kwa wale ambao wanafuatilia hizo takwimu na taarifa.

Kuna vyanzo vingi vya taarifa za ukwasi wa watu matajiri duniani baadhi ya vyanzo hivyo ni:
  1. Taarifa za umiliki wao katika masoko ya hisa duniani.Katika soko la hisa bei ya hisa hupanda na kushuka kila mara.Iwapo bei za hisa ya kampuni inayomilikiwa na tajiri ikipanda basi kiwango chake cha utajiri kinapanda na ikishuka kiwango cha utajiri kinashuka.Thamani ya hisakatika soko la hisa inapanda na kushuka kwa kutegemea utendaji wa kampuni na mahitaji katika soko la hisa.Hisa za kampuni zikihitajika sana(High demand) basi zitapanda bei ila zikiuzwa kwa wingi basi zitashuka bei.Ni kama tu mazao yanavopanda bei wakati wa kiangazi na kushuka bei wakati wa mavuna(Demand and Supply).Hizi sio sababu pekee lakini ndio zenye impact kubwa zaidi katika kuonesha mabadiliko katika utajiri au umaskini wa Bilionea
  2. Chanzo cha pili ni marejesho ya kodi au malipo ya kodi.Hizi ni taarifa za kikodi za tajiri husika ambazo huonesha kiwango cha kodi anacholipa.kadiri anavolipa kodi kubwa basi ujue pia faida yake na mapato yake ni makubwa.Sasa hizi taarifa hupewa hawa waandaaji wa orodha ya matajiri ni kisha huzihakiki ili kupata thamani ya mapato ya tajiri kwa kipindi husika.
  3. Chanzo cha tatu ni Rasilimali ziszohamishika kama majengo na ardhi zinazomilikiwa na muhusika.Mfano kama tajiri anamiliki majengo basi yatafanyiwa valuation kujua thamani yake nayo itajumlishwa katika Assets zake.
Swali la kujiuliza je madeni ya hawa matajiri yanatolewa katika kukotoa kiwango chao cha utajiri?Siwezi kuwa na jibu la uhakika ila kwa mtazamo wangu jibu ni Hapana.

Kwa kiasi kikubwa hawatazami kiwango cha madeni yao mpaka pale ambapo yanakuwa significant kuweza kuathiri mwenendo wao wa kibiashara.

Je tunaweza kuwa na orodha yetu ya matajiri wa Tanzania?Ndio ila kwanza ni lazima tuhamasishe wamiliki wa Biashara kupeleka kampuni zao katika soko la HISA lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima tuhamasishe watu wapende kwenda kwenye SOKO la hisa kuwekeza,lakini kabla ya kufanya hivyo lazima watu wapate elimu sahihi juu ya huduma na soko la fedha.

Tujadili zaidi namna tunaweza kuongeza idadi ya matajiri Duniani.
 
Hii nchi yetu ikiweza kuwaandalia wakulima mazingira mazuri ya kufanya hyo shughuli yao kama kuwapatia mbolea na madawa kwa bei nafuu tunaweza kutengeneza matajiri wengi sana.
 
Back
Top Bottom